Nusu Karne na CCM?

Mhe. Zitto; hivi tatizo la Tanzania ni kuelewa kiini na kina cha hali ngumu ya maisha ya watu wetu? Au unataka kudokezea kuwa hizo sehemu ulizopita na kuona adha na hali ngumu ya maisha ya watu CCM hawajaona kabisa au hawataki kuona? Yawezekana tatizo letu siyo kuona na kuelewa ugumu wa hali ya maisha?

Kuna ripoti nyingi kuanzia zile za kimataifa na hizo ulizodokezea na nyingine kwenye poverty reduction programs. Yawezekana tatizo letu ni zaidi ya namba na idadi?

Correct Mwanakijiji,

We need views like these.
 
Ndugu Zitto,

Nawapongeza kwa mkakati wenu huo wa operesheni sangara.

Naomab kuuliza je kwenye huu mkakati mnahimiza watu wajiandikishe kwenye daftari la wapiga kura?

Maana kuwaelemilisha wana nchi au kuwafungua macho ni jambo moja na kujiandikisha na kupiga kura ni jambo lingine.

Naomba muweke msisitizo ktk swala zima la kujiandikisha na kupiga kura.

Mimi ni mfano sijawahi kupiga kura(31yrs old) na nimeiga kwa mama yangu hii tabia yake hakuelewi ukimueleza. Ana sababu zake kuwa viongozi wanahidi halafu utekelezaji sifuri.

Naamini kuna watanzania kama hawa wengi tu. Wanakuja kwenye kampeni lakini hawakujiandikisha.

rgds
 
Nani amekudaganya kwamba vyama vya upinzani vichochee mabadiliko ya kiuchumi??

wewe hujui Sera ya upinzani TZ uchochezi wa uchumi ni lazima wapewe u Rais na serikali??



Mkuu,

Hivi haya mawazo unayatoa wapi?
 
Nijibu swali langu mimi mwenyewe.

Tatizo la Tanzania si kuelewa kiini na kina cha umaskini. Watanzania kwa hakika wanajua hali yao na ugumu wa maisha yao na vile vile wanajua potential ya mafanikio yao. Tunafahamu sisi ni 'maskini' na pia tunafahamu sisi ni 'matajiri'.

Umaskini sitaufafanua sana maana imeshaelezwa vya kutosha; hebu nizungumzie utajiri.

Kuna watu Tanzania ambao wamekuwa na utajiri kwa miaka mingi kabla hata ya sera hizi za ubepari. Namkumbuka mzee mmoja alikuwa na duka lake pale Dongobesh (Mbulu) na lilikuwa ni kama supermarket ya kijiji. Kwenye hilo duka viliuzwa vitu vyovyote ambavyo vingeweza kuingia. Kulikuwa na vitu vya nyumbani, baskeli, vipuri vya baskeli na pembeni yake alikuwa na kijimgahawa pia. Maduka ya namna hii ungeweza kuyaona haata kwenye vijiji vingine vingi ambapo yamekuwa kama vituo vya kufanyia biashara.

Nakumbuka wakati tukienda kwenye minada na kuona jinsi watu wanaleta vitu mbalimbali kwa kuuza kila jumatano au jumamosi. Minada ile ilikuwa ni ya kuuza kitu chochote ambacho kingeweza kuhamishika, kuanzia mbuzi, baskeli, kuku, ng'ombe na vitu vya matumizi ya nyumbani. Kwa wale wanaokumbuka ndio kile tulichokuwa tunakiita wakati huo "gulioni". Najua hivi bado vinaendelea.

Nikija siku hizi naangalia "matamasha" ya Jirambe Fiesta, na matamasha kibao yanayofanywa na wasanii mbalimbali. Naangalia jinsi mashindano ya urembo yapo hadi kwenye mtaa. Ninaangalia jinsi gani wananchi na hasa vijana walivyo na hela mfukoni kwenda kujistarehesha kila juma. Kuna watu ambao wanaenda pale Mlimani City kila mwisho wa Juma, na kuna watu ambao hawakosi kwenye vijiwe vya nyama choma wakiteremshia na moja moto na moja baridi. Haya hayakuanza leo. Kwa watu wa pwani tunafahamu vizuri sana vile tunavyoviita "baraza" ambapo watu walikuwa wanapata gahwa kwenye vile vijikombe vidogooo tena kahwa kali inayoteremshiwa na kashata.

Kuna watu ni wanachama wa kudumu maeneo hayo na baraza halinogi hadi wawepo. (hawa nawazungumzia watu wa kawaida tu). Tukija kwa watu wa kima cha kati na cha juu kuna sehemu ambazo hawa wamekuwa wakifurahia maisha na kutumia fedha yao katika kila aina ya anasa. Kuna hiyo Leaders Club, nakumbuka pale Officer's Mess O'bay, na hata ile ya Jeshi na maeneo mengine kama kule Ukonga, na pale Tanga kuna "Police Club".

Kwa wanaokumbuka kulikuwa na maeneo kama pale Ubungo (ukumbi ule siku hizi nasikia uligeuzwa kanisa) n.k Sasa hawa ni wa mjini, lakini kule kijijini kulikuwa na burudani zake pia. Karibu kila kijiji kuna mahali ambapo watu wanaenda kunywa vya "kienyeji" na hata nyama choma. Sehemu hizi ziko wazi karibu 7 days na kuna sehemu (niliwahi kuona kule Songea) ambapo vilabu hivyo viko wazi masaa 24, ni ulanzi ulanzi ulanzi! Ukija wakati wa mavuno na hasa wakati wa mauzo tu kwa chama cha Ushirika au siku hizi wanunuzi mbalimbali wananchi wana fedha nyingi mfukoni.

Hawa utaona siku hizi wanamudu kutumia fedha hizo kwa vitu vingi vya kila aina. Jana katika pita pita yangu nilisikia mdogo wangu mtawa (huko Ndanda) na yeye anataka simu ya mkononi! Ka mpwa kangu nako kako Ifunda girls na kenyewe kanasema "Uncle ninunulie simu" wote kwa sababu ati "wengine nao wanazo".

Mara mbili nimefuatilia IPO za makampuni mbalimbali. Mwanzoni ilikuwa ni CRDB iliponivutia na mimi miaka ile na nikanunua hisa za kutosha na hivi majuzi zimelipa. Vikaja vya Umoja Fund na ile ya kina Mzee Mosha. Mifuko hiyo miwili kwa pamoja ilipoweka IPOs zao ziliweza kukusanya shilingi bilioni 100 kutoka kwa Watanzania!! Tunapoangalia majengo yanayojengwa na NSSF na taasisi nyingine wananchi hawahusishi kuwa hizo fedha zinazotumika kujenga majengo hayo ni michango ya wafanyakazi wa Tanzania!

Kwa hiyo utaona kuwa tunapozungumzia umaskini kimsingi tunamaanisha utajiri tusioutumia na siyo ufukara (kitu tusichokuwa nacho) au ulemavu wa kukosa kiungo fulani na hivyo to impair our ability to live a productive and sufficient life. Sisi siyo fukara kwa kipimo chochote kile na umaskini wetu siyo wa vitu au fedha. Hilo la kwanza. Kumbuka hapa sijazungumzia utajiri wetu wa mali asili ambao kila Mtanzania tayari anaujua upo bwelele.

La pili ni kuwa kwa vile sisi siyo maskini na watu wetu siyo fukara basi tatizo letu sisi ni zaidi ya vitu au fedha. Nimeonesha kwa kiwango kidogo tu kuwa watu wetu wanazo fedha, na nchi yetu siyo MASKINI. Lakini cha pili hapa ninachotaka kusema kuwa tatizo la kwanza la Tanzania ni KURIDHIKA.

Watanzania kwa ujuma wetu kama Taifa (siyo mtu mmoja mmoja) tumeridhika na hali ilivyo (status quo). Siyo kwamba tunafurahia na kukubali kuwa inapaswa kuwa hivyo bali tumeipokea kuwa "ndivyo ilivyo". Nitakupa mfano mzuri hapa. Kati ya vitu ambavyo vinanishangaza sana kuhusu JIji la Dar na nadharia nzima ya uongozi ni jinsi gani watawala wetu (kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu) wanavyoshughulikia suala la mitaro ya maji machafu Dar (najua ningeweza kutumia mifano ya miji mingine).

Sote tunajua kuwa Dar ni mji tambarare (siyo kwa uzuri bali kijiografia yake) na meza ya maji (water table) iko karibu sana. Na wote tunafahamu kuwa Dar iko pembezoni mwa bahari. Sote tunafahamu kuwa mvua ikinyesha Dar kunatokea mafuriko ya ajabu ambayo yanakera watu. Lakini tumeweza kuishi na mafuriko na kuridhika kuwa ndivyo yalivyo. Hivyo utaona kwa mtu mgeni anaweza kushangaa akipita wakati wa ukavu akaona nje ya nyumba fulani kuna matofali yamepangwa kwa hatua hatua hadi upande wa pili. Au nje ya ofisi fulani kuna matairi ya magari yamewekwa na watu wanayapita kama vitu vya kishirikina.

Ikija mvua hata hivyo utona maana yake. Matairi na matofali yale yanatumika kama vivukio wakati wa mafuriko. Utaona watu waliovaa suti zao nzuri, utaona watu ambao wanafanya kazi kwenye ofisi ya mipango mijini na wataalamu wa Chuo kikuu wote wakiruka maji hayo na wengine kubebwa mgongoni kukwepa mafuriko hayo. Wadada wazuri wenye kupendeza na vijana watanashati wanavua viatu na kuvishika mkononi wakitembea kwenye maji machafu. Kwanini?

Leo hii tutajenga shule nzuri kijijini katika mpango wa kuendeleza shule zetu, tukaweka matofali ya kuchoma, madirisha mazuri, milango na mabati, baada ya muda utaona milango inaanza kutoweka mmoja baada ya mwingine na usipoangalia na mabati nayo yakaanza "kutoweka" kama kwa mazingaombwe. Wananchi watapita na kuona hali hiyo na wengine wanaweza hata kujua ni wapi madirisha na vitu hivyo vinatumiwa kumalizia nyumba ya nani.

Hata kwenye maeneo hasa ya mijini (na hili nalizungumzia kutoka katika mang'amuzi yangu) wataweka nguzo ya taa ya usiku mtaani. Watoto na hata watu wazima watachukua manati na kuanza kuirushia ila balbu kuipopoa. Mifano iko mingi ya jinsi gani kuna vitu tumevizoea kiasi kwamba kufikiri nje yake ni vigumu.

Kwa hiyo utaona kuwa tumeridhika na vitu vilivyopo na mambo yalivyo na jaribio lolote la kubadilisha linakutana na upinzani mkubwa. Na hii ndiyo sababu naamini kama kuna mchango wowote nilioufanya kwa Taifa langu ni uthubutu wa kusema hadharani na kwenye kurasa za magazeti kile ambacho watu wengi wanakifikiria au wanazungumzia kijiweni. Tulichoweza kufanya ni kuleta public discussion to the public. Na mwanzoni tulikutakana na upinzani mzito kwani waandishi wengi na watoa maoni walikuwa wanapenda kuzunguka mbuyu, JK alikuwa haguswi na watawala walikuwa hawapingwi hadharani namna hiyo. Tukautingisha huu mbuyu na kuna watu hawako comfortable.

Ndugu Zitto mwenyewe ni mfano. Kwenye suala la Buzwagi mwaka jana kitabu kinasema alipoambiwa na Bunge kuwa amesema uongo alitakiwa aombe radhi na kusalimu amri na kufanya mambo yaendelee jinsi yalivyo kuwa (status quo) yeye hakukubali bali alisimamia kile anachoamini na kukijua. Akaamua kuitikisa boti aliyokalia. Matokeo yake sote tunayajua.

Jambo la tatu na la mwisho (angalau kwa wakati huu) ni kuwa zaidi ya kuridhika na tatizo la status quo (hali ilivyo) suala jingine linaloihusu Tanzania ni uwezo wa kutamani kilicho bora kama mastahili yetu na siyo hisani. Bado watu wetu hawajaona haja ya kuwa na maisha bora (affluent life) bila ya kulazimika kuwa "mzungu" au kujifanya uonekane "mzungu". Miaka ile iliyopita niliwahi kufika kijiji kimoja huko Nzega katika pita pita yangu na jambo kama hilo nililiona pia Bariadi (kwa Fr. Gappa) na hata maeneo ya Misungwi Mwanza, au maeneo ya Dodoma (kikosi cha Rada pale). Na nina uhakika hata mijini unaweza kuona. Kuna watu ambao wanatunza nyumba nzuri, wanabustani nzuri nje, wanafagia (japo baraza ni vumbi tupu), wanaamka asubuhi na mapema kumwagilia maua yao n.k Nyumba hizi kijijijini zinapendeza na mazingira yake ni mazuri kweli wakati mwingine kushinda mjini. Watu hawa wakati mwingine wanaonekana wanapenda kuishi kizungu.

Pale Tanga eneo la Mwamboni kulikuwa na mzee mmoja wa kipogoro ambaye aliwahi kuishi ughaibuni kwa muda na aliporudi nyumbani nyumba yake ndani ilikuwa ni kama ya Ulaya (usiniulize nilijuaje). Wenyewe tulikuwa tunapenda kutembelea kuona vitu alivyo navyo ndani na kutufanya tutamani kwenda huko majuu na sisi. Baada ya kukaa hapa kwa muda kidogo nikagundua kuwa "siyo maisha ya uzunguni" bali wenzetu hawa wanataka maisha affluent na maisha affluent hayaonekani kwa magari, simu, nguo, elimu n.k (nitazungumzia hili siku moja).

Wananchi wetu wanahitaji kuona kuwa na wao wanastahili (kama vile ni haki yao) maisha mazuri na maisha mazuri siyo uzungu. Miaka ile ya sabini tuliwahi kuwa na kampeni ya "Ujenzi wa Nyumba Bora". Tulisema wakati huo nyumba bora iweje. Nakumbuka nilifika kijiji kimoja huko Kusini kinaitwa Njalamatata maeneo ya Mkongo (songea) na kulikuw na mstari wa nyumba za udongo wa kuchoma na mabati yanayong'aa na kile nyumba ilikuwa na choo cha shimo nje ya nyumba hiyo na zilikuwa zimepangwa vizuri kabisa. Watu walikuwa wanaitikia wito wa ujenzi wa nyumba bora. Kuna maeneo kama Kashoro, au huko Machame n.k ambapo watu walianza kujenga nyumba bora zamani tu. Siyo tu nyumba bora lakini pia tulikuwa na kile tulichokiita "Chakula Bora". Nakumbuka wimbo wa mzee Mwinamila (Kuleni kuku, mayai, mboga, samaki maziwa, na kujenga nyumba safi pa kulala pawe bora) kuhamasisha affluent life.

Ni lazima tufanya maisha bora kuwa ni ya kiafrika na tusiridhike na tulipo. NI lazima tutamani more than we have na ikibidi kutikisa mtumbwi tunaokalia. Walichofanya wazee wa EAC ni kutikisa boti, walichofanya vijana Mwanjelwa ni kutikisa boti, na muda si mrefu huu mtikisiko utaendelea taratibu na wananchi watajua kuwa vile vilivyo, sivyo vinavyopaswa kuwa.

Kiufupi, tatizo letu ni kukosa maoni ya nini tanzania iwe na kuanza kuitengeneza Tanzania tuitakayo na badala yake tumeacha mambo yatokee kwa nasibu. Na hata yale tunayoyapanga tunayachukulia kama mambo ya kawaida not urgent. Hebu jiulize:

a. Wananchi wangapi leo wanajua ulikofikiwa mpango wa MKUKUTA?
b. Wananchi wangapi wanajua mafanikio ya MKURUBITA
c. Wananchi wangapi wanajua mafanikio ya MMES na MMEM
d. Wananchi wangapi wanajua MFURUKUTWA (I have no idea what this is! I probably made it up)

Tumeacha kulijenga Taifa na sasa tunazungushana kwenye mti wa ufisadi. Tunatenda kana kwamba tumeshalijenga Taifa na sasa tunalitumikia. Leo hii Rwanda na Burundi wanaanza kufanya kile ambacho sisi tuliacha kukifanya; kulijenga Taifa. Tunajaribu kuishi kana kwamba sisi ni Taifa lililoendelea na kwamba tunakwama "kidogo" tu na tukibonyeza kitufe hiki au kile mambo yatakuwa ni pouwa. TUnasahau kuwa sisi bado ni taifa changa, kiuchumi ni insignificant, na mchango wake duniani ni negligible. Wenyewe tunafurahia kupigiana kelele kwenye simu, kuvaa nguo za kuagiza toka majuu, kuagiza hadi maziwa na nyama, tunaingiza bado mchele kutoka ng'ambo n.k

Hatutaki tena kujenga Taifa na sasa tunatenda kana kwamba tumeshajenga Taifa. Tumeacha vya msingi na kukumbatia vya sekondari, tumeacha kumalizia msingi na sasa tunataka kuezeka! NI watu wa ajabu sisi!

Well I didn't mean to write this much...
 
Bil. 350/- kubadili Dar

na Edward Kinabo


INAKADIRIWA kuwa kiasi cha dola milioni 350 (zaidi ya sh bilioni 350), kinapaswa kuwekezwa katika Jiji la Dar es Salaam kila mwaka, kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya, ili kulibadili jiji hilo.

Hayo yalibainishwa jana na Mtaalamu wa Maendeleo ya Miji wa Benki ya Dunia, Mathew D. Glasser, wakati akitoa muhtasari wa matokeo ya utafiti kuhusu ‘mabadiliko ya miji Tanzania’ kwa waandishi wa habari na wawakilishi kutoka Asasi Zisizo za Kiserikali (AZISE), katika ukumbi wa mikutano wa benki hiyo, Dar es Salaam.

Alisema kiasi hicho kinapaswa kuwekezwa katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, nishati, maji na usafi wa jiji.

Alisema Jiji la Dar es Salaam na miji mingi inayotambuliwa kisheria na Mamlaka za Serikali za Mitaa, imekuwa ikikosa mapato ya kutosha kuweza kujiendesha na kukarabati miundombinu ukiachilia mbali haja ya kujenga miundombinu mipya kwa kuzingatia ukuaji wa idadi ya watu.

Alisema kwa ujumla matokeo ya utafiti huo yanakadiria kuwa kiasi cha dola milioni 880 (zaidi ya sh bilioni 880), kinahitajika ili kuwekezwa katika majiji yote nchini, kwa lengo la kutoa huduma kwa wakazi wapya.

Alisema kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo, uwekezaji katika ujenzi miundombinu mipya ni moja kati ya mambo matatu ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya baadaye ya ukuaji wa miji nchini.

Aliyataja mambo mengine kuwa ni uendelezaji wa maeneo ya pembezoni mwa miji na kuwa na mfumo mzuri wa usimamizi wa ardhi.

Akizungumzia uendelezaji wa maeneo ya pembezoni mwa miji, alisema karibu nusu ya ukuaji wa miji ya Tanzania unatokea nje ya mipaka ya kisheria ya miji na hakujawa na mipango wala uwekezaji unaotakiwa.

Alisema hali hiyo inatokana na uwekaji wa mipaka ya miji chini ya sheria ya mamlaka za Serikali za Mitaa, kutoendana na hali halisi ya ukuaji wa idadi ya watu katika maeneo husika.

Check:

Hii hii taarifa ilihitajika? Itakuwa na nguvu kwa sababu imefanywa na WB?
 
Jitihada za Chadema kutaka kuliongoza taifa letu zinaonekana. Operesheni Sangara na zinginezo zitakazokuja, zije, maana ndiyo demokrasia. Lakini operesheni hizo lengo lake ni nini? Kuwaelimisha wananchi juu ya ufisadi na uovu mwingine wa Chama Tawala na Serikali yake ili hatimaye wananchi wakipe CHADEMA ridhaa ya kuliongoza Taifa?

Kama alivyosema Wildcat ni mikakati gani ambayo CHADEMA wameiandaa ya kutuvusha kutoka hapa tulipo? CHADEMA watueleze, tukiwapa ridhaa ya kuliongoza Taifa letu uongozi wao utakuwaje na utatufanyia nini? Tunahitaji kuwa na picha ya viongozi watarajiwa ili tuweze kuwapima tujiridhishe kwamba Chama hicho kinao viongozi wanaoweza kutuvusha kulingana na matarajio. Tunahitaji kuwapima ili wakati ukifika tusijeuziwa mbuzi kwenye gunia. Twataka tupitishe hukumu mapema wasijeshindwa mbele ya safari, tukaulalamikia uongozi huo kama unavyolalamikiwa uongozi wa CCM hivi sasa.

2010 ni miaka miwili tu ijayo. CHADEMA wamejipanga vipi na watajipanga vipi katika kipindi cha miaka miwili kuweza kupata viongozi thabiti watakaoweza kuiendesha nchi kwa mafanikio? Au watatutaka “tuwajaribu” tu? Viongozi wa CHADEMA tunaowafahamu, wanaosikika na kueleweka (miaka miwili kabla ya uchaguzi) ni viongozi wa Kitaifa tu wa chama hicho e.g. Mbowe, Slaa, Zitto, Mnyika na wabunge wachache wa chama hicho. Viongozi wa Chama wa mikoa na wilaya ni kama hawapo. Hawafanyi juhudi yoyote ya kutaka tuwasikie tuwajue. Wapo wana-CHADEMA wachache makini kama akina Prof. Baregu, MMKijiji (ambaye anafaa kuwa Rais na sijui kama ni mwanaCHADEMA!) ambao sidhani kwamba idadi yao inaweza kufikia kuunda Baraza zuri la Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Wakuu wa Mikoa na Wilaya n.k., watakaoweza kutuletea Tanzania mpya tunayoitaka. Itabidi CHADEMA wafanye kazi ya ziada kushawishi watu makini, wazalendo wenye uchungu na nchi yetu wajiunge na chama hicho ili azma ya kutaka kuwepo na uongozi makini na bora iweze kufanikiwa. Hata kama wapo, inabidi wasikike mapema.

Pia, nakubaliana na maneno ya MASAKI. “Wao (CHADEMA) sio malaika, wanaweza kuingia madarakani wakaishia kuwa mafisadi tu. Kama kweli wana nia njema na nchi hii, wawe na njia mbadala ya kupunguza matatizo ya Watanzania…..” Kabla ya kuwapa uongozi tunahitaji sana kujua watakavyopambana na ufisadi na watatumia njia gani mbadala kupunguza matatizo nchini mwetu.

‘Rais wangu MMKijiji’ amefafanua kwa kina hali halisi ya Tanzania yetu na Watanzania wenyewe jinsi tulivyoridhika na hali hiyo. CHADEMA wana mikakati gani ya kuiondoa hali ya kuridhika, hali ya ‘mazoea’ iliyojengeka kwenye vichwa vya wananchi wa mijini na vijijini, mazoea ya kukipigia kura CCM kwa kuwa tu ni Chama kilichozaliwa na TANU iliyotuletea Uhuru ama chama cha Nyerere, bila kuangalia utendaji wake katika zama hizi.

CHADEMA watafanya mbinu gani kujaribu kurejesha uzalendo ili wananchi wasiangalie umaskini walionao ambao huwashawishi baadhi yao kupokea takrima na kuwapa kura viongozi wabovu. Tutakapowapa CHADEMA uongozi, watatumia njia gani kuwadhibiti matajiri ambao wametawaliwa na uroho wa mali kiasi cha kuiibia serikali na kutowaonea huruma wananchi wanaonyonywa ili wao watajirike.

Wananchi walishatangaziwa kauli mbiu ya “maisha bora kwa kila Mtanzania” na kauli hiyo ndiyo inayotumika sana majukwaani na vijiweni kudhihirisha kushindwa kwa Serikali ya CCM kutekeleza wajibu wake. CHADEMA wanapaswa kutuwekea wazi mikakati ya muda mfupi na mrefu kuhakikisha kwamba maisha bora kwa kila Mtanzania yanapatikana. Tovutini haitoshi. Viongozi kuhamia vijijini na kuchanganyika na wananchi wa kawaida ni muhimu sana - mpaka kieleweke!

CHADEMA, waje na operesheni zao wakijua kwamba si kazi rahisi kuchukua uongozi mwaka 2010. Mbali ya kukikosoa CCM majukwaani, magazetini, vijiweni, vilabuni n.k., wapiga kura wako vijijini. Wanahitaji na wanapaswa kuelezwa kwa lugha wanayoweza kuielewa kuwafanya waachane na kupiga kura kwa mazoea ama takrima. Wananchi wote watataka kujua ni kwa namna gani Taifa litaweza kusonga mbele na hali zao kuwa bora ili wajiridhishe kwamba CHADEMA ni ‘chama cha ukombozi’ na si chama badala ya CCM.

Wapo akina Mzee Makamba, Tambwe Hiza n.k. ambao watapita kufukia nyayo za CHADEMA kwa maneno ya propaganda kali! Kazi kubwa itakuwepo.

Mwisho, nawapongeza viongozi wa CHADEMA kwa kulitumia ipasavyo jina la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika operesheni/kampeni zao. Bila shaka wanafanya hivyo kwa kumuenzi Mwalimu kwa dhati. Nawapongeza kwa sababu, inasemekana baadhi ya viongozi wa CCM wanalionea soni jina la Baba wa Taifa, ama wanashindwa kulitaja na kulitumia kwa sababu dhamira zao zinawasuta.

Zidumu Fikra …………….!
 
Mh. Zito nashukuru sana kwa makala yako nzuri. Ila nachelea kidogo kusema kuwa, je upo ukweli kuwa uchumi wa vijijini umekuwa kwa asilimia 4? au ulikuwa unamaanisha -4% (yaani unashuka kwa 4%)? Nasema hivi kwa sababu, uweza wa wanakijiji umekuwa ukipungua kila mwaka, huko tulikotoka wanakulima walikuwa na uweza wa kununua japo mbegu, mbole na madawa, siku hizi hawawezi. Sina hakika kuwa kilimo cha pamba, korosho, tumbaku kimeongezeka vipi tukilinganisha na miaka ya nyuma na wakulima wameweza kujitegemea zaidi kwa asilimia 4? Kilimo cha mazao kama kahawa ndio usiseme, kwani tangu mkapa alipoingia madarakani ndio wakulima walizikwa, mtakumbuka hata wakati wakulima walipopewa fedha za ruzuku na EU, serikali kupitia waziri wake wakati huo "Keenja", waliwanyima wakulima kwa kisingizio kuwa fedha hizo zingeingizwa kwenye ujenzi wa miundombinu, mpaka kesho (Nadhani walikuwa wanatafuta fungu la ushindi wa kimbunga).

Nasikitika kuwa kuna umasikini wa kutisha mno vijijini, Watu wanapata shida sana kupata mlo mmoja wa ugali kwa mchicha, watu wakiona nyama, MACHO yanatoa machozi ya damu. Maisha yamewafanya wakulima wengi mno wamekata tamaa, na sasa wameamua kunywa GONGO kwa kwenda mbele, sijui ni maneno ya mithali kuwa "MPE KILEO ALIYE MASKINI ILI ALEWE AISAHAU SHIDA YAKE"

Inasikitisha, ile wenye mustakabali wa nchi yetu ni sisi watanzania wenyewe.

Kama Marekani inakaribia kutawaliwa na mtu mweusi, iweje watanzania kuwa wagumu kuruhusu watanzania wenzetu wa mrengo mwingine kutawala nchi?

Sijui, kwa nini watanzania tunaendelea kuwa wazito, tubadilike?

ukipita maeneo mengi ya vijijini hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha. naunga mkono hoja yako kuwa uchumi unashuka badala ya kupanda. ZITTO keep it up
 
Mwanakijiji,
Tatizo ni sisi wenyewe, Hatutaki kuelewa kuwa hatuna viongozi..
Tofauti na Zitto nitasema hivi, mara nyingi viongozi wa nchi huwa wana uchungu na nchi zao, uchungu na maslahi ya Taifa, uchungu na Muskabali wa nchi unapohusika lakini wengi hushindwa kutekeleza kwa sababu huwa - Out of touch!
Tofauti na nchi hizo, Tanzania viongozi wetu sio kwamba wako Out of Touch isipokuwa hawana uchungu na nchi, hawana uchungu na wananchi, hawana uchungu na maslahi wala Mustakabali wa Taifa..
Siamini kabisa kwamba Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata huyo Chiligati wote hawa were/are out of touch kwani report za hali mbaya zipo mezani kwao na kila siku hotuba zao huzungumzia Umaskini wetu, licha ya hivyo wao wenyewe wametokea huko..
Mimi nafikiri hakuna kitu zaidi ya maskini akipata makalio hulia mbwata!..
 
mkandara, tatizo ni kuwa wanajua tumeridhika nao.. tumeridhika na wao kuwa out of touch.. tumeridhika na status quo. Ndio maana sasa hivi kijasho kinawatoka wanapoona wazee wanalala barabarani, wanakimbilia kwenda mahakamani wanaposikia walimu wanaenda kuandamana ingawa hawakukimbilia mahakamani kuhusu EPA, Richmond, Rada n.k !

Wakati wowote jamii inapoanza kuonesha kuwa hairidhiki ndio mwanzo wa mabadiliko.
 
Ukisoma post ya Zitto utadhihirisha yale ambayo tumekuwa tukijadili kila siku humu. Tanzania sisi ni masikini wa kutupwa!


Opereshen sangara ni mwanzo mzuri. Upinzani unahitaji moyo. ndo maana kila siku nasema kwa wale ambao tunaogopa kuweka mchanga kwenye vitumbua vyetu kwa kuonekana kussuport upinzani..tukae pembeni wenye moyo huo watakomboa nchi na sisi tutasherehekea. I can assure you hata wananchi sasa vijijini WAMECHOKA na usanii wa CCM! I have proved this and as time goes by wanajua kabisa CCM ni chama ambacho hakina jipya! Ndo maana mimi naamini wale wote wanaonzisha matawi ya CCM huko UGHAIBUNI siyo kwa sababu wana mapenzi mema na Tanzania. No way..wanataka wapate opportunity ya kuiba wakirudi nyumbani. na watu kama hao INABIDI TUWAOGOPE KAMA UKOMA WAKIRUDI HAPA NYUMBANI! Hivi kweli lets be real kwa hali tuliyonayo watanzania kwa sasa, na huu umasikini wakutupwa bado tunaamini kwamba CCM means well for our country?

Swala la kuikomboa Tanzania siyo la Chadema peke yake ni swala la WATANZANIA WOTE! its wrong kuinyoshea kidole chadema as if wao ndo wana hilo jukumu. Tanzania ni yetu sote. Ndo maana aliyeipigia kura CCM na ambae hakuipigia kura wote tunaumia tuu! (trust me wanaofaidi ni wachache mno). Kwa hiyo kila mtanzania ajiulize nini nafasi yake katika kuleta mabadiliko katika nchi. Its not ALL about Chadema Its about TANZANIA. Kwani nini maana ya uchaguzi? tukiwapa ridhaa Chadema wakaboronga..we kick them out! tuweke chama mbadala! Tusiogope mabadiliko! Its inevitable!

Its easy to accuse Mbowe "eti mpiga disco" hawezi kuwa kiongozi. But deep down jiulize..what Mbowe has done atleast kuwaweka mafisadi on guard! Ni upinzani huu ambao unafichua kila kukicha madhambi ya CCM...but watanzania wachache wanao appreciate juhudi za hawa jamaa! Lets judge Mbowe as any other human being. He is a politician but he needs to make a living and he has his history too! tusipoteze agenda kwa kuangalia vitu ambavyo havina uzito kwa maisha yangu na yako! Personally I have nothing with Mbowe being mpiga dansi!. Naangalia uwezo wake wa kukata issue. And looking at what we have in the country..he is far far better than Kikwete or Mvungi!

Wapinzani wanaweza kuwa hawana experience ya kuongoza nchi, lakini ni CCM hiyo hiyo na experience yake waliotufikisha hapa! sasa ni sisi kuchagua...either tuendelee na CCM yenye experience ya kuiba na ambayo haina mwelekeo au tutafute viongozi mbadala!

Watanzania wenzangu tunaonekena punguani tunaposema eti "Chadema ni chama kizuri lakini hakina watu wengi wa maana kwa hiyo hata tukiwapa nchi itawashinda kuongoza" Sasa watu wazuri ni sisi tulio busy tuki-criticize Chadema..why not join them? au unafikiri watu wazuri wa kujiunga na Chadema watatoka sayari ya Mars? ni mimi na wewe! Ni sisi inaobidi tuingie kwenye mapambano. Its really unfair kudelagate wajibu wako wa kutafuta mabadiliko kwa Zitto! You cant delegate your right and duty to be at the battle front!

Chadema or CUF OR ANY OTHER POLITICAL PARTY with genuine interests to rid Tanzania of our current ENEMY who is CCM deserve our assistance!

Jamani nyumba inaungua...huu siyo mda wa kuulizana nani kachoma nyumba..ni mda wa kuzima moto! nani kachoma..tutajua baadaye moto ukizimwa!
 
Operesheni Sangara hoyee!!! Kuweni makini na mikakati ya CCM ya kutumia viongozi wachache wadhaifu wa upinzani kubomoa upinzani. Otherwise, you guys rock.
 
Kukaa sana jikoni mambo mengi yananipita. Naomba kuuliza. Niliwahi kusikia kwamba gazeti la Sauti ya Watu, Tanzania Daima ni la CHADEMA ama mmiliki wake ni kiongozi wa CHADEMA.

Gazeti la leo la Sauti ya Watu, likielezea hotoba ya Rais wetu lina kichwa cha habari kisemacho "Kikwete akata mzizi wa fitina." Shoga yangu wa jikoni mwenzangu ambaye ni shabiki wa CHADEMA aliposoma akaguna na kusema: "Fitina gani? Mwandishi anataka kutuambia kwamba wanaonung'unikia jinsi suala la fedha za EPA linavyoendeshwa ni wafitini? Huyu mwandishi keshanunuliwa!"

CHADEMA, kazi mnayo!
 
Ndugu Zitto,

Kwanza shukrani sana kwa kurudi ukumbini na kutupa hali halsi ya yanayotokea huko vijijini.

Naomba nirudi kwenye zile hoja za Chadema must Reform, Focus 2010, Marshall Plan ya Mchungaji, CCM Adui wa Maendeleo na Dynamic Productivity.

Katika mada/hoja hizi, nimeongelea mara nyingi umuhimu wa kuanza kulifundisha Taifa letu njia bora za kujitegemea na hivyo kuwa na jamii iliyo na uhuru wa kweli wa fikra ambao utamsaidia Mtanzania aachane na umasikini, unyonge na maradhi na zaidi utegemezi.

Ukirudia hotuba ya Kikwete iliyotolewa jana, kuna kitu kimoja kimejitokeza tena anapoongelea masuala ya uchumi. Analaumu kuyumba kwa uchumi wa duni ana nchi tajiri na kuonyesha hofu kuwa Afrika itakosa pesa za misaada kwa kuwa Serikali ya nchi tajiri zinajiokoa.

Kama Mzee Mwanakijiji alivyobainisha, tayari tunajua umahiri wa Umsikini wetu na hadithi kutuonyesha jinsi tulivyo masikini si tija tena. ama tunajua kuwa CCM ni mbaya, lakini inabidi kauli zetu zisiwe kulaumu tuu, bali kufundisha Watanzania waachane na kuitegemea CCM kwa kila kitu.

Juzi mgombea wa Urais wa Marekani, Bw. Barack Obama akihojiwa alizungumzia umuhimu wa Serikali inayokuja ya marekani kuwekeza (invest heavily) kwenye miundo mbinu, kuanzia barabara, reli, bandari, maji, mifereji, mitandao ya brodibendi na giridi mpya za Umeme kutumia umeme wa nishati safi kama upepo na jua.

Nikajiuliza, hivi si kitu hiki hiki ndicho tunahitaji si kukisikia kwa kauli bali kwa vitendo kutoka Serikali yetu?

Nimeleta nukuu ya kilio cha Kikwete kwa nchi wahisani kupunguza misaada kwa kuwa CCM imeegemea sana kuogopa kujituma na kutumia pesa zetu wenyewe kwa ajili ya shughuli iwe ni maendeleo au matumizi mengine.

Bajeti yetu nzima inategemea 40% ya misaada kutoka kwa nchi wahisani! Kila shughuli au mipango ya maendeleo nchini Tanzania inategemea kwanza ifanyiwe utafiti na uchambuzi nwa Wafasdhili, kisha kigharamiwe na Watanzani.

Ni tabia hii Tegemezi ambayo Mwalimu Nyerere aliipiga vita na hata kutungiwa tenzi ndani ya Azimio la Arusha.

Kinachohitajika kutoka kwenu Chadema ni kutueleza Watanzania, ni vipi mtalijenga Taifa letu liachane na Umasikini, Ujinga na Maradhi? Ni vipi mtalijenga Taifa letu liwe hru lenye kujitegemea kiuchumi na kurudia kile kiti cha uongozi si kisiasa na kimapinduzi dhidi ya Ukoloni na Ubeberu bali ni kiuchumi?

Ni vipi Chadema itabadilisha kaulimbiu yake kutoka kulaumu na kulaani mabaya ya CCM na kuanza kuongoza kwa mfano chanya wa kujenga Taifa imara lenye watu wenye fikra pevu za kimapinduzi, wenye kuthamini kazi na muda (time), lililo na watu mahiri wa maarifa, wenye juhudi, tija mwamko na uadilifu?

Mna miezi 24 kabla ya uchaguzi mkuu 2010, je Chadema itatupa sera na sura gani tuamue kuwa tunakokwenda ni kwema?
 
Wana JF,

Ninaomba kuwashirikisha katika makala yangu hii kuhusiana na hali ya nchi yetu. Nimeandika kufuatia kauli ya Chiligati kuwa nchi ipo shwari na nini nimeona katika Mkoa wa Kwanza wa Operesheni Sangara.

Tujadiliane



-----------------------------------------------

Nikiwa Mjini Mugumu Serengeti katika ziara ya kikazi ya viongozi wote wa CHADEMA katika kujenga chama chetu, ninapata taarifa ya mkutano wa waandishi wa habari ambao Katibu Mwenezi wa CCM ndugu Kapteni John Chiligati amekanusha kwamba nchi imekosa mwelekeo. Alikuwa akijibu hoja ya Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kwamba kwa hali ya sasa ya nchi Rais Jakaya Mrisho Kikwete hapaswi kupewa kipindi cha pili cha utawala. Chiligati anasema nchi imetulia, ni shwari kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Chiligati aling'aka na kuanza kutoa matusi yasiomithilika dhidi ya ndugu Mbowe kana kwamba ndugu Mbowe alimtukana ndugu Kikwete. Mbowe hakumtukana Rais Kikwete. Mbowe alisema Uongozi umemwelemea Kikwete na hivyo asipewe kipindi kingine cha uongozi.

Nilikaa na kutafakari kwa kina sana kwa nini Chiligati amesema maneno ambayo hayaendani na taswira yake kama mtu mpole na mwungana? Mimi ninamwona Chiligati hivyo. Sikumjua kabla sijawa Mbunge, nimemjulia Bungeni tena baada ya kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati huo wizara hiyo ilikuwa imebakia na vitengo vya Magereza, Uhamiaji na Zimamoto. Haikuwa Wizara kubwa sana, lakini wizara muhimu kwa usalama wa nchi. Nilimwona ni mtu mwungana, alikuwa akishirikiana kwa karibu sana Waziri wetu kivuli katika Wizara hiyo ndugu Mhonga Ruhwanya. Nilishangazwa sana alipoamua kutoka kwenye hoja na kuamua kumtukana ndugu Mbowe!

CHADEMA imezindua kampeni maalumu ya kuimarisha chama katika maeneo ya vijijini. Operesheni hii tumeiita ‘OPERESHENI SANGARA'. Kwa nini Sangara? Kwa kweli wala hatukufikiria kwa kina sana kuna nini katika jina hilo, tuliamua kutafuta kitu kinachowaunganisha wananchi wa mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mwanza na Mara. Tulitafuta kitu ambacho kinahusiana na maisha ya wananchi ya kila siku. Tukakuta Sangara ni jina murua kwani ni samaki alie katika ziwa Viktoria na ni samaki ambae analiingiza Taifa mapato mengi sana. Takwimu za Hali ya Uchumi wa Taifa zinaonesha kuwa Samaki wa Ziwa Viktoria wanachangia takriban asilimia 8 ya mauzo yetu nje ya nchi. Thamani ya mauzo ya samaki kutoka Ziwa Viktoria ni karibia Tshs. 150 Bilioni kwa mwaka. Hata hivyo sehemu kubwa ya fedha hizi zinabaki kwa wawekezaji wachache na Taifa halipati kiasi kinachostahili cha mapato yake kutokana na utajiri huu. Vilevile wananchi wanalalamika kuwa kitoweo cha samaki kimekuwa ghali sana kufuatia samaki wote kuuzwa nje na wao kubakia na Mapanki. Jina hili lilitosha kuwa sehemu ya kampeni ya uimarishaji wa chama katika Kanda ya Ziwa Viktoria.

Nimepata fursa ya kutembelea majimbo yote ya Mkoa wa Mara isipokuwa Jimbo la Musoma Vijijini. Musoma Vijijini nimewahi kwenda; Butiama katika misa ya Baba wa Taifa kwa mwaliko maalumu wa Mbunge wa Jimbo hilo na Buhemba kwa ziara ya Kamati ya Rais kuhusu Mikataba ya Madini. Ninaamini kabla hatujaenda Mkoa wa Mwanza kuendelea na Operesheni mnamo tarehe 11 Novemba, tutapata fursa ya kupita katika Jimbo la Musoma Vijijini ili kuongea na wananchi na kuimarisha chama chetu cha CHADEMA.

Ziara hii imenifumbua macho ya maisha ya Watanzania. Nilipomsikia Chiligati anasema hali ni shwari, kisha nikaangalia maisha ya wananchi wa Buhare (Musoma Mjini), Bukura (Rorya), Nyanungu (Tarime), Muriba (Tarime), Nansimo (Mwibara), Hunyari (Bunda) na Nyamuswa (Bunda), nikasema kweli viongozi wetu hawapo na wananchi (out of touch). Nikachunguza mara ya mwisho ndugu Chiligati alikwenda kutembelea wananchi wa vijijini lini toka amekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, nikapata taarifa kuwa hajawahi hata siku moja. Nikathibitisha kuwa sio tu Chiligati alipaniki ‘panick' bali yeye na wenzake wapo ‘out of touch'! Wanajifungia katika maofisi yao yenye viyoyozi Dar es Salaam na kuitisha ‘press conferences' na kusema nchi ipo shwari.

Hali ya nchi sio nzuri hata kidogo, nitatumia mifano halisi niliyoiona katika vijiji vya mkoa wa Mara na kuihusanisha na takwimu za Serikali kujenga hoja zangu kwamba CCM imeshindwa kuongoza Taifa letu, imebaki inatawala na ndio maana wao wenyewe wanapenda kujiita ‘Chama Tawala'. Kwa maoni yangu, hatupaswi kuruhusu CCM kutimiza nusu karne katika Utawala, kwani mwaka 2011 tunatimiza miaka 50 ya Uhuru wa upande mmoja wa Taifa letu (Tanzania Bara). Wazalendo wote wa Taifa hili wanapaswa kujiandaa na kuizuia CCM kutufikisha nusu karne kwani kwa hali ya sasa CCM ni hatari kwa usalama na ustawi wa Taifa letu. Nitajieleza!

Mwaka 2005, wakati wa Kampeni za Uchaguzi CCM waliahidi katika Ilani yao ya uchaguzi kuwa ifikapo mwaka 2010 watakuwa wamepunguza umasikini wa Watanzania kutoka asilimia 38 ya Watanzania mpaka asilimia 19. Mwaka 2005 kulikuwa kuna Watanzania Masikini takribani milioni 11. Hapa tafsiri ya Masikini ni wale watu wote ambao kipato chao kwa mwezi ni chini ya shs 14,000, yaani chini ya sh 400 kwa siku. Hiki ni kiwango cha chini sana kwani kufuatia kupanda bei kwa bidhaa na hasa chakula, hata mwenye kipato cha shs 30,000 kwa siku bado ni mtu masikini tu.

Mnamo tarehe 3 Oktoba, Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo alitangaza takwimu mpya za hali ya Umasikini nchini. Takwimu hizo zimefuatia utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu nchini na utafiti huo unaitwa kwa kimombo ‘Household Budget Survey'. Takwimu hizi mpya zinaonesha kuwa Watanzania walio masikini wa kutupwa sasa wamefikia Milioni 12.7. Hii inaonesha kuwa Serikali ya CCM ya awamu ya nne katika kipindi cha miaka 3 ya utawala wake badala ya kupunguza umasikini miongoni mwa Watanzania, imeongeza masikini zaidi ya Milioni 1. Hii imetokana na ukweli kwamba chama hiki kimekuwa ‘nzee', kimechoka na hakina mawazo mapya. Chama hiki tukikiacha madarakani, tena kikiwa na ukiritimba wa Bunge ambao hivi sasa CCM inao, kitaingiza watu wengi zaidi katika dimbwi la umasikini.

Njia mojawapo ya kuokoa Taifa letu, ni kutoruhusu CCM kuuunda serikali tena ifikapo mwaka 2010. Ikitokea hivyo, basi CCM isiwe na ukiritimba Bungeni kama ilivyo sasa ambapo asilimia 86 ya wabunge wanatoka chama hicho kimoja. Hii ndio mantiki ya Mbowe kusema tusimruhusu JK kuchukua muhula wa pili. Mbowe hakuwa na maana ya Kikwete kama mtu binafsi bali CCM. Kwani ikiwa ni suala la Kikwete kama mtu binafsi, CCM watabadili mtu na hivyo kuendelea kutawala. Tunachosema, CCM ya awamu ya nne haistahili kupewa muhula wa pili kwani wamechoka na hawana mawazo mapya ya kuondoa umasikini wa Watanzania.

CCM ya sasa haina idara ya sera wala utafiti na hivyo, hawaongozi tena sera za serikali wanayoongoza bali wanategemea serikali kutengeneza sera na wao wanazikariri katika ilani zao. Lengo la kupunguza umasikini kutoka asilimia 38 mpaka asilimia 19, lilikuwa lengo la MKUKUTA ambapo CCM kwa kutaka kura tu, waliamua kukariri MKUKUTA na kuuweka katika kitabu cha kijani na kicha kuiita ilani.

Watu wa Gazeti la The Economist waliwahi kuita ilani ya CCM kuwa ni ‘wishlist'. Sasa imedhirika kuwa lengo hili kubwa la kupunguza umasikini, limeshindikana. CCM wataweza nini?
Leo CCM imetengeneza mataifa mawili ndani ya Taifa moja la Tanzania. Hivi sasa kuna Taifa la Masikini na Taifa la Matajiri. Masikini wana shule zao zinazoitwa Sekondari za Kata. Matajiri wana shule zao zinazoitwa ‘Academies au English Medium'. Watoto wa masikini katika Sekondari za Kata wanasoma katika mazingira magumu sana. Shule hazina walimu, madarasa hayana madirisha na hata vitabu hakuna.

Nilipokuwa Wilaya ya Rorya nilitembelea Kata ya Bukura. Pale Bukura nilipata bahati ya kutembelea shule ya Kata na kuzungumza na wanafunzi. Shule hii inayoitwa Shule ya Sekondari ya Bukura ina kidato cha Kwanza na cha pili. Shule ya Sekondari Bukura ina Walimu 4 tu na wanafunzi waliniambia walimu wote ni wa masomo ya sanaa. Hakuna Mwalimu wa Sayansi. Shule ya Sekondari Bukura haina uhakika kama mwakani wataweza kuingiza kidato cha kwanza kwani wao wamejenga madarasa mpaka uwezo wao, lakini msingi wa darasa la kidato cha tatu bado upo chini kabisa. Hawana msaada wa serikali.

Nimejionea madarasa ambayo hayana madirisha wala milango. Kuna watoto wanatembea kilometa nane kufika shule na matokeo yake katika kipindi cha mwaka huu peke yake, watoto wa kike 5 walipata uja uzito.

Wanafunzi wa Bukura, wanaonekana ni wenye akili sana, waliniambia kwa nini vyama vya siasa tunapewa ruzuku badala ya ruzuku hiyo kujenga miundombinu ya shule zao. Niliwaeleza umuhimu wa vyama vya siasa katika uongozi wa nchi. Nikawaambia lazima vyama viendeshwe na bila ruzuku matajiri wachache watamiliki vyama. Wakaniambia mbona tayari vyama vimeshikwa na matajiri? Wakanisuta na kuniambia mbona ninyi wabunge hamshindi bila kutoa takrima? Wakaniambia mbona wameona rushwa katika uchaguzi wa viongozi wa CCM katika ngazi ya Kata na Tawi?

Niliwaangalia watoto wale na kukumbuka takwimu za serikali kuhusu elimu. Kwamba hivi sasa kila mwalimu mmoja anafundisha watoto 65 (Rejea PHDR 2007), kwamba watoto 20 wanachangia kitabu kimoja shuleni, kwamba wakati uandikishaji wa watoto umeongezeka na kuvuka malengo ya MKUKUTA, hakuna ufuatiliaji kujua watoto wanasoma nini shuleni. Kata ya Bukura yenye vijiji vya Nyambori, Bwiri, Thabache na Bubombi wananchi wake wanaweza kusema kweli hali nchini ni shwari wakati watoto wao hawapati elimu wanayostahili kama Raia wa Taifa Huru? Hivi Chiligati alipokuwa anamtukana Mbowe kuwa ni muhuni alikuwa anaelezea kadhia hii ya Elimu?

Lakini Chiligati anajua fika kwamba, fedha zilizoibwa Benki Kuu kwa akaunti ya EPA peke yake zingeweza kujenga madarasa 24,000. Madarasa 24,000 ni sawa na madarasa 2 kila Kijiji maana Tanzania ina vijiji 12,000. Hivyo kama mafisadi wasingefisadi fedha hizi, watoto wa Bukura wasingekuwa wanamlalamikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini kuhusiana na vyumba vya madarasa. Kama fedha za EPA zingejenga vyumba za Walimu, zingejenga nyumba 19,000. Lakini CCM iliona ni bora ichukue michango ya watu waliokwapua fedha za EPA ili wanunue fulana na kofia za kampeni kuliko kutunza fedha hizi ziweze kujenga mashule.

Chiligati anasema nchi ipo shwari, itakuwaje shwari wakati Serikali ya CCM imeshindwa kutunza hazina yetu? Kama wameshindwa kuaminika kwa hazina yetu na kupata tamaa kuchota fedha za kampeni zao 2005, tuwaamini kweli waendelee kuangalia hazina yetu mpaka 2015? Tunaposema wasipewe miaka mingine 5 tuna maana kuwa CCM haiaminiki tena kutunza fedha zetu za kodi. Hawana ujasiri wa kutochota kidogo waende kupigia kampeni.

CCM na viongozi wake hawajui kuwa kila saa inayopita kuna mwanamke mmoja wa Tanzania anafariki dunia kwa matatizo ya uzazi (Maternal Mortality). Taarifa ya Hali ya umasikini nchini ya mwaka 2007, inaonesha kuwa katika kila Watanzania wanawake 100,000, wanawake 578 wanapoteza maisha kwa ukosefu wa huduma nzuri za afya kwa kina mama. Hii ni sawa na kupoteza Mtanzania mwanamke 1 kila saa. Miaka 47 baada ya uhuru, tunashindwa kulinda afya ya kina mama zetu! Tunajiita Taifa huru na kwamba Taifa hili halina matatizo. Lazima Chiligati anaota! Haiwezekani hali ya Taifa ikawa nzuri ilhali tunapoteza mwanamke mmoja kila saa kwa matatizo ya uzazi.

CCM kwa uchovu wake imeshindwa kuona ya kwamba kuna chumi mbili nchini na uchumi mmoja unakua na mwingine umedumaa. Uchumi wa mijini (Urban Economy) unakua na kukuzwa na sekta za madini, ujenzi, mawasiliano na utalii. Sekta hizi ndizo sekta zinazokua kwa kasi ikiwemo pia sekta ya fedha kama mabenki na bima. Wenye kushika sekta hizi ni matajiri wenye fedha. Kwao hali ya uchumi ni shwari sana.

Uchumi wa Vijijini (Rurak Economy) umedumaa. Uchumi huu unaendeshwa na sekta ya Kilimo ambacho ukuaji wake umebakia asilimia 4 tu kwa takribani miaka 3. Hivyo watu wa vijijini hali zao zimekuwa mbaya sana kwani wanauza bidhaa zao kwa bei za vijijini na wananunua bidhaa kama mafuta, sukari nk kwa bei za mijini. Hivyo wananchi wa vijijini wanapigwa kweli kweli na maisha. Serikali ya CCM labda inashindwa kuelewa kuwa baada ya Ndugu Benjamin Mkapa kujenga misingi imara ya uchumi mkubwa (macro) , hii ya Ndugu Kikwete ilipaswa kutafsiri uimara wa misingi hii kwa maisha ya wananchi wa kawaida wanaotegemea kilimo.

Nilitaraji hii ndio ilikuwa kazi ya msingi ya serikali ya CCM ya awamu ya nne. Imeshindikana miaka 3 ndani ya utawala. Ndio maana tunasema hawastahili kupewa kipindi kingine. Kwa kweli kama chama upinzani, hatuna lingine la kusema. Nchi imekosa mwelekeo.

Wiki ijayo....... Rushwa, Madini, Uaminifu na uchambuzi zaidi wa umasikini.

Kwanza kabisa natoa hongera zangi kwa chama chako na viongozi wenu wote pamoja na wewe mwenyewe katika jitihada zenu za kupigania maslahi ya Tanzania. Pili natoa hongera nyingi sana kwa hizi safari mnazozifanya kutembelea wilaya mbali mbali za nchi yetu ili kukitangaza chama chenu, kusikia maoni mbali mbali ya Watanzania waishio katika wilaya hizo na pia kujionea hali hali ya maisha ya Watanzania walio wengi.

Tatu mmekuwa na ushirikiano wa karibu na vyama vingine visivyokuwa madarakani ambao uliingia dosari kufuatia kifo cha Mbunge Wangwe, na sijui sasa hivi ushirikiano huo ukoje ukoje. Pamoja na Watanzania wengi kufurahia kuona vyama visivyo madarakani kushirikiana lakini hilo la kushirikiana pekee halitoshi, bali Watanzania wengi tungependa kuona vyama vyenu vinaungana na kuunda chama kimoja chenye nguvu.

Maoni kuhusu umuhimu wa kuungana yametolewa na Watanzania mbali mbali katika kila kona ya nchi yetu na pia Watanzania wanaoishi nchi za nje, lakini kwa mshangao wa wengi hakuna juhudi zozote za wazi tulizoziona ambazo zinaonyesha kwamba mmesikia kilio hicho cha Watanzania katika umuhimu wa kuungana. Hapa JF pia mara nyingi watu wametoa maoni yao kuhusiana umuhimu wa kuungana na hata Waziri Mkuu wa Kenya mheshimiwa Odinga katika kikao chake na viongozi mbali mbali wa vyama visivyo madarakani aliwaambia umuhimu wa nyinyi kuungana ili kuing'oa CCM madarakani.

Watanzania hatuelewi tatizo nini hasa linalowafanya mshindwe kusikia vilio vya Watanzania chungu nzima na kulipa kipaumbele hilo suala la kuungana. Tanzania ni nchi kubwa sana kama mkiungana basi wale wote ambao ni viongozi wa juu watapata nafasi mbali mbali katika serikali yenu.

Umefika wakati tuambiane ukweli kuhusu hili labda kuna tatizo kubwa sana ambalo limekuwa kikwazo katika kutimiza ombi la Watanzania la vyama vyenu kuungana. Uchaguzi wa 2010 hauko mbali na kwa maoni yangu bado kuna muda wa kutosha kabisa wa kuungana tayari kwa uchaguzi huo ili kuhakikisha mnaing'oa CCM madarakani. Mmeshashindwa katika chaguzi tatu za vyama vingi 1995, 2000 na 2005 je, mnataka mshindwe chaguzi ngapi ndiyo muone umuhimu wa kuyafanyia kazi maoni ya Watanzania kuhusu kuungana? Ni nini pingamizi kubwa la vyama vyenu kuungana?

Kwa heshima na taadhima nawaombeni mlipe hili suala la kuungana umuhimu unaostahili ili katika uchaguzi wa 2010 kuwe na chama kimoja chenye nguvu ambacho kitaweza kushindana na CCM katika majimbo yote ya uchaguzi nchini. Uchaguzi ujao una umhimu mkubwa sana katika future ya nchi yetu ambayo sasa hivi imetekwa na mafisadi. Kushindwa kwa CCM tu ndiko kutaweza kuwang'oa mafisadi na kuhakikisha rasilimali zetu zinakuwa na manufaa kwa Watanzania wote badala ya mafisadi wachache na wageni. Mimi naamini kabisa Tanzania isiyo na mafisadi inawezekana baada ya kuing'oa CCM madarakani. UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.
 
Makala kama hii inaandikwa na mtu mjasiri kabisa. Kitu gani cha kuogopwa wakati watawala wanazidi kulididimisha taifa. CHADEMA wajaribu sana kushirikiana na wezao kusudi kuiondoa CCM madarakani. Bila CCM kung'atuka, Tanzania ni taabu sana kuona maendeleo ya kweli.
 
Rev. Kishoka,

Mkuu nakuaminia sana ktk maswala haya na hakika mada zako zote hizo Ulizotaja hapo juu ni uthibitisho mkubwa wa jinsi ulivyobobea ktk maswala haya..

Mkuu kuna kitu kimoja ambacho mimi nimekiona nacho ni kwamba pengine nchi yetu inahitaji sio tu Kiongozi msomi lakini pia amewahi kuishi nchi za nje (Ulaya) kwa zaidi ya miaka 10...
Nasema hivi kwa sababu ukimsikiliza Kikwete na pengine marais wote waliotangulia, miaka yote wamekuwa wakifikiria kwamba mafanikio ya kiuchumi yanaweza kutoka nje..Na kwamba pengine nchi tajiri duniani zinaweza ku spread Utajiri wa dunia hii ili nchi zote ziondokane na Umaskini..Jambo ambalo haliwezekani kabisa..
Marekani kiongozi yeyote akisema anataka ku spread Utajiri kwa masikini hata iwe ndani ya nchi hiyo tayari utakuwa amepoteza support ya wananchi..Obama katika mazungumzo yake na Joe - the Plumber, aligusia kitu kama hicho pamoja na kwamba hakuwa na maana hiyo hata kidogo lakini imekuwa sababu kubwa ya kuonyesha hofu ya wananchi wake..
Sasa ikiwa Marekani wenyewe ndani ya nchi yao wanapinga ku spread Utajiri wao kwa raia wao maskini iweje sisi tufikirie kwamba hao hao Marekani wanaweza kutusaidia kuondokana na Umaskini wetu..

Nilishangaa sana kumsikia Kikwete akidai kwa nini nchi za Kiafrika hazikuhusishwa ktk mkutano wa dharura nchi za G8 uliofanyika Marekani!.. Na wala sio yeye wa kwanza nimeona viongozi wengi wa nchi maskini wakijaribu kuomba nafasi ya nchi za maskini ktk mikutano ya kiuchumi ya G8..nguvu nyingi zimetumika ktk swala ambalo haliwezekani..WHY?... pengine ni kutofahamu system nzima ya nchi matajiri hasa za Ulaya.

Na wala sishangai kwa nini Kikwete anapoteza muda mwingi kwenda nchi za Ulaya kujaribu kuvuta lisilowezekana. Ni sawa na maskini ombaomba anayekwenda kupanga mstari msikitini siku za Ijumaa akitegemea kwamba kuna siku ataondokana na umaskini huo bila kufikiria kwamba fedha anazopewa pale haziwezi kuwa mtaji wa maisha bora..

Kwa kumalizia tu nasema hivi Operation Sangara inaweza kuwa na mvuto lakini muhimu zaidi ya yote ni maelezo yako ya mwisho..

I quote:- Ni vipi Chadema itabadilisha kaulimbiu yake kutoka kulaumu na kulaani mabaya ya CCM na kuanza kuongoza kwa mfano chanya wa kujenga Taifa imara lenye watu wenye fikra pevu za kimapinduzi, wenye kuthamini kazi na muda (time), lililo na watu mahiri wa maarifa, wenye juhudi, tija mwamko na uadilifu?
 
Ilani ya CHADEMA Uchaguzi Mkuu 2005

Hii ni ilani ya uchaguzi 2005. Sio kweli kuwa sisi tunalalamika tu. Tuna malengo. Tatizo ni kuwa hivi sasa hali ya sasa inatufanya tuongelee zaidi matatizo ya chama tawala. Lakini tunazungumza kuhusu siis tungefanya nini
kwa ufupi.....

Lengo la Serikali itakayoongozwa na CHADEMA ni kuunda Taifa la watu walio huru lenye kuzingatia misingi ya utawala bora na linalotoa fursa kwa wananchi wake kuboresha maisha yao

Tanzania Tunayoitaka


Ilani: Uchumi wenye ajira
 
Tulikuwa na mpango hata wa mwaka na tuliuweka katika ilani. Suala laweza kuwa 'content' ya mpango huo. Lakini kwamba sisi ni kulalamika tu sio kweli. Tupo wachache lakini tunajitahidi kuweka siasa za issues katika Taifa letu. Soma hapa chini

Mwaka mmoja tangu kuingia madarakani
Serikali ya CHADEMA ina ahidi kufanya yafuatayo:


Elimu

Bajeti ya elimu kuongezeka kutoka 18% hadi 35%, kuongeza ajira za waalimu na kuboresha mishahara ya waalimu.


Afya

Kufuta VAT kwenye huduma na vifaa vya kina mama waja wazito na watoto.

Madawa ya kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kugawiwa kwa wote walioathirika.

Kupandisha mishahara ya madaktari na wauguzi.


Kilimo

Kufuta kodi zote pamoja na VAT kwa pembejeo za kilimo.

Kuweka mpango thabiti wa kutofautisha ardhi kwa ajili ya umwagiliaji.


Uchumi

Bajeti 2006/07 kupunguza VAT iwe 16%.

Kufanya mapitio ya mikataba yote ya uwekezaji na ubinafsishaji.

Tanzania kujiunga upya na COMESA.

Kutengeneza ajira milioni moja kwa kufanya mabadiliko makubwa katika sekta za madini, utalii, ujenzi na huduma za jamii.


Mfumo wa Utawala Bora

Kurudisha serikalini mali zote zilizochangwa na wananchi na kuhodhiwa na CCM kama viwanja vya mpira na majengo yanayotumiwa na CCM n.k.

Kupiga marufuku uuzaji wa nyumba za Serikali na kurejesha zilizokwisha uzwa kiupendeleo.

Kuvunja PCB na kuweka majukumu yote ya kupigana na rushwa chini ya Mkurugenzi wa makosa ya Jinai (DCI).

Kuboresha maisha ya kina mama kwa kuwawezesha kielimu na kuwapa nafasi katika utawala.
 
Hii ndio misingi ya itikadi yetu na hivyo imani za mwana CHADEMA. We are not an ampty party. Tatizo laweza kuwa 'communication strategy'! Lakini ataanza kusikiliza itikadi hizi katika masakata yote haya ya EPA. MEREMETA, Mikataba ya Madini nk?

Itikadi ya Chama

CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).


CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.


CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.


CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.


CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.


CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.


CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.


CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii.


CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.


CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.


CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.


CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom