Nusu Karne na CCM?

[ Hivyo wananchi wa vijijini wanapigwa kweli kweli na maisha. Serikali ya CCM labda inashindwa kuelewa kuwa baada ya Ndugu Benjamin Mkapa kujenga misingi imara ya uchumi mkubwa (macro) , hii ya Ndugu Kikwete ilipaswa kutafsiri uimara wa misingi hii kwa maisha ya wananchi wa kawaida wanaotegemea kilimo.

]​


Kwa kweli kwa kuliona hilo tuu,sasa naamini CHADEMA kuna vichwa.Hapa nilipo natafuta kijikadi chao CCM walichonitumia eti cha kufungulia matawi hapa ughaibuni nikipige mkasi.Hebu ngoja nikitafute haraka ili nikichane haraka kabla sijasahau........Yaaani inasikitisha mimi baada ya kwenda majita na kuona niliyojione.Kuanzia Kamnyonge (Majita road) hadi bukumi hali inatisha SANA.Wakondya Zitto​
 
Tanzania sio Kenya kama vile ilivyo kuwa Tanzania sio Zambia

...tatizo ni kuwa CCM haina nusu karne toka izaliwe, sasa sijui imekuwa vipi madarakani kwa nusu karne! vinginevyo nusu karne siku hizi ina maana nyingine, na 2008 kutoa 1977 unapata miaka 50.

mtasema, "oooooh kinachojalisha ni ujumbe"!! sawa, hata mie naukubali...lakini usahihi usio doa wa ujumbe pia ni nyeti, @least ktk dunia yangu.:(

chinks!!
 
Wana JF,

Ninaomba kuwashirikisha katika makala yangu hii kuhusiana na hali ya nchi yetu. Nimeandika kufuatia kauli ya Chiligati kuwa nchi ipo shwari na nini nimeona katika Mkoa wa Kwanza wa Operesheni Sangara.

Tujadiliane



-----------------------------------------------

Nikiwa Mjini Mugumu Serengeti katika ziara ya kikazi ya viongozi wote wa CHADEMA katika kujenga chama chetu, ninapata taarifa ya mkutano wa waandishi wa habari ambao Katibu Mwenezi wa CCM ndugu Kapteni John Chiligati amekanusha kwamba nchi imekosa mwelekeo. Alikuwa akijibu hoja ya Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kwamba kwa hali ya sasa ya nchi Rais Jakaya Mrisho Kikwete hapaswi kupewa kipindi cha pili cha utawala. Chiligati anasema nchi imetulia, ni shwari kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Chiligati aling'aka na kuanza kutoa matusi yasiomithilika dhidi ya ndugu Mbowe kana kwamba ndugu Mbowe alimtukana ndugu Kikwete. Mbowe hakumtukana Rais Kikwete. Mbowe alisema Uongozi umemwelemea Kikwete na hivyo asipewe kipindi kingine cha uongozi.

Nilikaa na kutafakari kwa kina sana kwa nini Chiligati amesema maneno ambayo hayaendani na taswira yake kama mtu mpole na mwungana? Mimi ninamwona Chiligati hivyo. Sikumjua kabla sijawa Mbunge, nimemjulia Bungeni tena baada ya kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati huo wizara hiyo ilikuwa imebakia na vitengo vya Magereza, Uhamiaji na Zimamoto. Haikuwa Wizara kubwa sana, lakini wizara muhimu kwa usalama wa nchi. Nilimwona ni mtu mwungana, alikuwa akishirikiana kwa karibu sana Waziri wetu kivuli katika Wizara hiyo ndugu Mhonga Ruhwanya. Nilishangazwa sana alipoamua kutoka kwenye hoja na kuamua kumtukana ndugu Mbowe!

CHADEMA imezindua kampeni maalumu ya kuimarisha chama katika maeneo ya vijijini. Operesheni hii tumeiita ‘OPERESHENI SANGARA'. Kwa nini Sangara? Kwa kweli wala hatukufikiria kwa kina sana kuna nini katika jina hilo, tuliamua kutafuta kitu kinachowaunganisha wananchi wa mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mwanza na Mara. Tulitafuta kitu ambacho kinahusiana na maisha ya wananchi ya kila siku. Tukakuta Sangara ni jina murua kwani ni samaki alie katika ziwa Viktoria na ni samaki ambae analiingiza Taifa mapato mengi sana. Takwimu za Hali ya Uchumi wa Taifa zinaonesha kuwa Samaki wa Ziwa Viktoria wanachangia takriban asilimia 8 ya mauzo yetu nje ya nchi. Thamani ya mauzo ya samaki kutoka Ziwa Viktoria ni karibia Tshs. 150 Bilioni kwa mwaka. Hata hivyo sehemu kubwa ya fedha hizi zinabaki kwa wawekezaji wachache na Taifa halipati kiasi kinachostahili cha mapato yake kutokana na utajiri huu. Vilevile wananchi wanalalamika kuwa kitoweo cha samaki kimekuwa ghali sana kufuatia samaki wote kuuzwa nje na wao kubakia na Mapanki. Jina hili lilitosha kuwa sehemu ya kampeni ya uimarishaji wa chama katika Kanda ya Ziwa Viktoria.

Nimepata fursa ya kutembelea majimbo yote ya Mkoa wa Mara isipokuwa Jimbo la Musoma Vijijini. Musoma Vijijini nimewahi kwenda; Butiama katika misa ya Baba wa Taifa kwa mwaliko maalumu wa Mbunge wa Jimbo hilo na Buhemba kwa ziara ya Kamati ya Rais kuhusu Mikataba ya Madini. Ninaamini kabla hatujaenda Mkoa wa Mwanza kuendelea na Operesheni mnamo tarehe 11 Novemba, tutapata fursa ya kupita katika Jimbo la Musoma Vijijini ili kuongea na wananchi na kuimarisha chama chetu cha CHADEMA.

Ziara hii imenifumbua macho ya maisha ya Watanzania. Nilipomsikia Chiligati anasema hali ni shwari, kisha nikaangalia maisha ya wananchi wa Buhare (Musoma Mjini), Bukura (Rorya), Nyanungu (Tarime), Muriba (Tarime), Nansimo (Mwibara), Hunyari (Bunda) na Nyamuswa (Bunda), nikasema kweli viongozi wetu hawapo na wananchi (out of touch). Nikachunguza mara ya mwisho ndugu Chiligati alikwenda kutembelea wananchi wa vijijini lini toka amekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, nikapata taarifa kuwa hajawahi hata siku moja. Nikathibitisha kuwa sio tu Chiligati alipaniki ‘panick' bali yeye na wenzake wapo ‘out of touch'! Wanajifungia katika maofisi yao yenye viyoyozi Dar es Salaam na kuitisha ‘press conferences' na kusema nchi ipo shwari.

Hali ya nchi sio nzuri hata kidogo, nitatumia mifano halisi niliyoiona katika vijiji vya mkoa wa Mara na kuihusanisha na takwimu za Serikali kujenga hoja zangu kwamba CCM imeshindwa kuongoza Taifa letu, imebaki inatawala na ndio maana wao wenyewe wanapenda kujiita ‘Chama Tawala'. Kwa maoni yangu, hatupaswi kuruhusu CCM kutimiza nusu karne katika Utawala, kwani mwaka 2011 tunatimiza miaka 50 ya Uhuru wa upande mmoja wa Taifa letu (Tanzania Bara). Wazalendo wote wa Taifa hili wanapaswa kujiandaa na kuizuia CCM kutufikisha nusu karne kwani kwa hali ya sasa CCM ni hatari kwa usalama na ustawi wa Taifa letu. Nitajieleza!

Mwaka 2005, wakati wa Kampeni za Uchaguzi CCM waliahidi katika Ilani yao ya uchaguzi kuwa ifikapo mwaka 2010 watakuwa wamepunguza umasikini wa Watanzania kutoka asilimia 38 ya Watanzania mpaka asilimia 19. Mwaka 2005 kulikuwa kuna Watanzania Masikini takribani milioni 11. Hapa tafsiri ya Masikini ni wale watu wote ambao kipato chao kwa mwezi ni chini ya shs 14,000, yaani chini ya sh 400 kwa siku. Hiki ni kiwango cha chini sana kwani kufuatia kupanda bei kwa bidhaa na hasa chakula, hata mwenye kipato cha shs 30,000 kwa siku bado ni mtu masikini tu.

Mnamo tarehe 3 Oktoba, Waziri wa Fedha ndugu Mustafa Mkulo alitangaza takwimu mpya za hali ya Umasikini nchini. Takwimu hizo zimefuatia utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu nchini na utafiti huo unaitwa kwa kimombo ‘Household Budget Survey'. Takwimu hizi mpya zinaonesha kuwa Watanzania walio masikini wa kutupwa sasa wamefikia Milioni 12.7. Hii inaonesha kuwa Serikali ya CCM ya awamu ya nne katika kipindi cha miaka 3 ya utawala wake badala ya kupunguza umasikini miongoni mwa Watanzania, imeongeza masikini zaidi ya Milioni 1. Hii imetokana na ukweli kwamba chama hiki kimekuwa ‘nzee', kimechoka na hakina mawazo mapya. Chama hiki tukikiacha madarakani, tena kikiwa na ukiritimba wa Bunge ambao hivi sasa CCM inao, kitaingiza watu wengi zaidi katika dimbwi la umasikini.

Njia mojawapo ya kuokoa Taifa letu, ni kutoruhusu CCM kuuunda serikali tena ifikapo mwaka 2010. Ikitokea hivyo, basi CCM isiwe na ukiritimba Bungeni kama ilivyo sasa ambapo asilimia 86 ya wabunge wanatoka chama hicho kimoja. Hii ndio mantiki ya Mbowe kusema tusimruhusu JK kuchukua muhula wa pili. Mbowe hakuwa na maana ya Kikwete kama mtu binafsi bali CCM. Kwani ikiwa ni suala la Kikwete kama mtu binafsi, CCM watabadili mtu na hivyo kuendelea kutawala. Tunachosema, CCM ya awamu ya nne haistahili kupewa muhula wa pili kwani wamechoka na hawana mawazo mapya ya kuondoa umasikini wa Watanzania.

CCM ya sasa haina idara ya sera wala utafiti na hivyo, hawaongozi tena sera za serikali wanayoongoza bali wanategemea serikali kutengeneza sera na wao wanazikariri katika ilani zao. Lengo la kupunguza umasikini kutoka asilimia 38 mpaka asilimia 19, lilikuwa lengo la MKUKUTA ambapo CCM kwa kutaka kura tu, waliamua kukariri MKUKUTA na kuuweka katika kitabu cha kijani na kicha kuiita ilani.

Watu wa Gazeti la The Economist waliwahi kuita ilani ya CCM kuwa ni ‘wishlist'. Sasa imedhirika kuwa lengo hili kubwa la kupunguza umasikini, limeshindikana. CCM wataweza nini?
Leo CCM imetengeneza mataifa mawili ndani ya Taifa moja la Tanzania. Hivi sasa kuna Taifa la Masikini na Taifa la Matajiri. Masikini wana shule zao zinazoitwa Sekondari za Kata. Matajiri wana shule zao zinazoitwa ‘Academies au English Medium'. Watoto wa masikini katika Sekondari za Kata wanasoma katika mazingira magumu sana. Shule hazina walimu, madarasa hayana madirisha na hata vitabu hakuna.

Nilipokuwa Wilaya ya Rorya nilitembelea Kata ya Bukura. Pale Bukura nilipata bahati ya kutembelea shule ya Kata na kuzungumza na wanafunzi. Shule hii inayoitwa Shule ya Sekondari ya Bukura ina kidato cha Kwanza na cha pili. Shule ya Sekondari Bukura ina Walimu 4 tu na wanafunzi waliniambia walimu wote ni wa masomo ya sanaa. Hakuna Mwalimu wa Sayansi. Shule ya Sekondari Bukura haina uhakika kama mwakani wataweza kuingiza kidato cha kwanza kwani wao wamejenga madarasa mpaka uwezo wao, lakini msingi wa darasa la kidato cha tatu bado upo chini kabisa. Hawana msaada wa serikali.

Nimejionea madarasa ambayo hayana madirisha wala milango. Kuna watoto wanatembea kilometa nane kufika shule na matokeo yake katika kipindi cha mwaka huu peke yake, watoto wa kike 5 walipata uja uzito.

Wanafunzi wa Bukura, wanaonekana ni wenye akili sana, waliniambia kwa nini vyama vya siasa tunapewa ruzuku badala ya ruzuku hiyo kujenga miundombinu ya shule zao. Niliwaeleza umuhimu wa vyama vya siasa katika uongozi wa nchi. Nikawaambia lazima vyama viendeshwe na bila ruzuku matajiri wachache watamiliki vyama. Wakaniambia mbona tayari vyama vimeshikwa na matajiri? Wakanisuta na kuniambia mbona ninyi wabunge hamshindi bila kutoa takrima? Wakaniambia mbona wameona rushwa katika uchaguzi wa viongozi wa CCM katika ngazi ya Kata na Tawi?

Niliwaangalia watoto wale na kukumbuka takwimu za serikali kuhusu elimu. Kwamba hivi sasa kila mwalimu mmoja anafundisha watoto 65 (Rejea PHDR 2007), kwamba watoto 20 wanachangia kitabu kimoja shuleni, kwamba wakati uandikishaji wa watoto umeongezeka na kuvuka malengo ya MKUKUTA, hakuna ufuatiliaji kujua watoto wanasoma nini shuleni. Kata ya Bukura yenye vijiji vya Nyambori, Bwiri, Thabache na Bubombi wananchi wake wanaweza kusema kweli hali nchini ni shwari wakati watoto wao hawapati elimu wanayostahili kama Raia wa Taifa Huru? Hivi Chiligati alipokuwa anamtukana Mbowe kuwa ni muhuni alikuwa anaelezea kadhia hii ya Elimu?

Lakini Chiligati anajua fika kwamba, fedha zilizoibwa Benki Kuu kwa akaunti ya EPA peke yake zingeweza kujenga madarasa 24,000. Madarasa 24,000 ni sawa na madarasa 2 kila Kijiji maana Tanzania ina vijiji 12,000. Hivyo kama mafisadi wasingefisadi fedha hizi, watoto wa Bukura wasingekuwa wanamlalamikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini kuhusiana na vyumba vya madarasa. Kama fedha za EPA zingejenga vyumba za Walimu, zingejenga nyumba 19,000. Lakini CCM iliona ni bora ichukue michango ya watu waliokwapua fedha za EPA ili wanunue fulana na kofia za kampeni kuliko kutunza fedha hizi ziweze kujenga mashule.

Chiligati anasema nchi ipo shwari, itakuwaje shwari wakati Serikali ya CCM imeshindwa kutunza hazina yetu? Kama wameshindwa kuaminika kwa hazina yetu na kupata tamaa kuchota fedha za kampeni zao 2005, tuwaamini kweli waendelee kuangalia hazina yetu mpaka 2015? Tunaposema wasipewe miaka mingine 5 tuna maana kuwa CCM haiaminiki tena kutunza fedha zetu za kodi. Hawana ujasiri wa kutochota kidogo waende kupigia kampeni.

CCM na viongozi wake hawajui kuwa kila saa inayopita kuna mwanamke mmoja wa Tanzania anafariki dunia kwa matatizo ya uzazi (Maternal Mortality). Taarifa ya Hali ya umasikini nchini ya mwaka 2007, inaonesha kuwa katika kila Watanzania wanawake 100,000, wanawake 578 wanapoteza maisha kwa ukosefu wa huduma nzuri za afya kwa kina mama. Hii ni sawa na kupoteza Mtanzania mwanamke 1 kila saa. Miaka 47 baada ya uhuru, tunashindwa kulinda afya ya kina mama zetu! Tunajiita Taifa huru na kwamba Taifa hili halina matatizo. Lazima Chiligati anaota! Haiwezekani hali ya Taifa ikawa nzuri ilhali tunapoteza mwanamke mmoja kila saa kwa matatizo ya uzazi.

CCM kwa uchovu wake imeshindwa kuona ya kwamba kuna chumi mbili nchini na uchumi mmoja unakua na mwingine umedumaa. Uchumi wa mijini (Urban Economy) unakua na kukuzwa na sekta za madini, ujenzi, mawasiliano na utalii. Sekta hizi ndizo sekta zinazokua kwa kasi ikiwemo pia sekta ya fedha kama mabenki na bima. Wenye kushika sekta hizi ni matajiri wenye fedha. Kwao hali ya uchumi ni shwari sana.

Uchumi wa Vijijini (Rurak Economy) umedumaa. Uchumi huu unaendeshwa na sekta ya Kilimo ambacho ukuaji wake umebakia asilimia 4 tu kwa takribani miaka 3. Hivyo watu wa vijijini hali zao zimekuwa mbaya sana kwani wanauza bidhaa zao kwa bei za vijijini na wananunua bidhaa kama mafuta, sukari nk kwa bei za mijini. Hivyo wananchi wa vijijini wanapigwa kweli kweli na maisha. Serikali ya CCM labda inashindwa kuelewa kuwa baada ya Ndugu Benjamin Mkapa kujenga misingi imara ya uchumi mkubwa (macro) , hii ya Ndugu Kikwete ilipaswa kutafsiri uimara wa misingi hii kwa maisha ya wananchi wa kawaida wanaotegemea kilimo.

Nilitaraji hii ndio ilikuwa kazi ya msingi ya serikali ya CCM ya awamu ya nne. Imeshindikana miaka 3 ndani ya utawala. Ndio maana tunasema hawastahili kupewa kipindi kingine. Kwa kweli kama chama upinzani, hatuna lingine la kusema. Nchi imekosa mwelekeo.

Wiki ijayo....... Rushwa, Madini, Uaminifu na uchambuzi zaidi wa umasikini.

Mheshimiwa Zitto,

Nimependa uchambuzi wako na inaonyesha munaanza kujifunza kwa kwenda vijijini.

Nimeguswa na baadhi ya mambo, kwanza umeongelea sana umaskini wa wilaya za Mara, je hivi kule Kigoma ni tofauti? Mimi kila wilaya niliyowahi kupita vijijini ni hoi bin taabani. Kuna jamaa yangu mmoja alipita Kigoma juzi juzi tokea Dar, akasifia ardhi ilivyo mzuri lakini umaskini wa kutisha. Binafsi nilifikiri kwa kuzunguka wilaya za Kigoma tayari unakuwa na picha kamili juu ya jinsi nchi ilivyo nyuma.

Pili mtafanya la maana kama zile wilaya ambazo mnaongoza halmashauri mtazitumia kama show case, kwa maana ya kwamba hizo wilaya zitakuwa na maendeleo makubwa kuliko wilaya za CCM.

Tatu, watu wengi sasa wanajua makosa ya CCM, kinachowasumbua watu ni huo upande wa pili, je nyie mkipata madaraka mtafanya nini? Naona katika mijadala yenu hicho ndio kinakosekana, sawa ni vizuri kukosoa lakini pia ni vizuri zaidi kuja na solutions.

Mafanikio mema kwa mwaka 2010.
 
Zitto; Umenena; kazi nzuri sana; naona mwanga ( light)

Nakuhakikishia na ninaamini mpaka sasa WATZ vijana wasomi karibu wote wako pamoja na chama kama hiki; kwa mitizamao na mikakati ya kisayansi; ila sasa kwa kutumia wasomi inabidi tutafute namna rahisi ya kuwafikishia ujumbe wa namna hii mhimu kwa mstakabali wa taifa letu watu wale uliowataja Mil 12.7 maskini wa kutupwa kwa sasa; maana wale ndio wanaohongwa Tshirt/kofia/khanga/chumvi nk na kudanganyika na kumbuka hawajaeleimika vema; ujumbe wa operation Sangara ni vema ulenge maeneo maalumu; ukisema uzunguke nchi nzima mafuta yataisha na ujumbe hautafika sawa sawa; mfano kuweka mkakati wa kuhakikisha kanda ya ziwa yote inakuwa himaya maalumu ya Chadema; maanake mnawekeza mawazo na mkakati huko mpaka kieleweke kwanza; na kuwa na uhakika kabisa kwa asilimia 80 wa ushindi majimbo yote hayo; then mnatafuta strategic area nyingine; nasema hata siasa za marekani zina maeneo maalumu ya kuanzia kabla hujaenda eneo jingine; maeneo yawe defined ya kuanzia mkakati kama mlivyoanza na kila sehemu ina slogani yake;na mkipeleka operation iishi huko kimkakakati; mambo yakienda sawa; maeneo mengi yatakubalika na kufuata; nashauri msilazimishe kuzunguka nchi nzima; let be strategic maana unaweza kuzunguka nchi nzima then watu wasielewe vema na mwisho wa siku usiambulie chochote; Wabunge zaidiya 150 wanahitajika toka Chadema by 2010; sasa nini kifanyike; ni strategy kama hizo; define area and concetrate

Yangu ni hayo leo

Malunde
 
Mweshimiwa nakubaliana na wewe mia kwa mia;kwamba ccm haina hadhi ya kupewa kipindi kingine cha miaka 5, ila na nyie inabidi muwaeleze wananchi mtafanya nini kama mtapewa nafasi kwa mfano kwenye afya, elimu,miundombinu nk.
Na siyo kubakia nayo kwenye katiba au ilani ya chama tu, kwani si wote wenye uwezo wakupa hizo katiba na ila.
Yote katika yote nakupa big up mkubwa.
 
Asante sana Mheshimiwa Zito,
Tulio wengi tumeshangazwa na Matamshi ya Chiligati, kwamba, kama mwenyekiti wa chama cha chadema au chama chochote cha siasa anaambiwa 'yeye ni nani?' itakuwaje kwa wakulima na wananchi masikini kabisa, siwataminywa ili wafie mbali.

Asante kwa makala yako imekaa makini sana ukizingatia imetoa data kusapoti maelezo yako.

BigUP!

cheers,
 
This country has ceased to be the land of opportunities where the rich and the poor kids share the same desk at school and the rich and poor woman meet at the same clinic.

Are we being judged according to the content of our characters or according to the zeros in our bank accounts?

Zitto:Hongereni sana kwa kazi nzuri!.Fanyeni mambo yenu tofauti na CCM ili muwe kweli chama mbadala!.
 
...tatizo ni kuwa CCM haina nusu karne toka izaliwe, sasa sijui imekuwa vipi madarakani kwa nusu karne! vinginevyo nusu karne siku hizi ina maana nyingine, na 2008 kutoa 1977 unapata miaka 50.

mtasema, "oooooh kinachojalisha ni ujumbe"!! sawa, hata mie naukubali...lakini usahihi usio doa wa ujumbe pia ni nyeti, @least ktk dunia yangu.:(

chinks!!

Chinkala,

Utawala wa CCM unaanzia TANU na ASP. Ni hawahawa wapo madarakani toka 1961 na 1964
 
Mhe. Zitto; hivi tatizo la Tanzania ni kuelewa kiini na kina cha hali ngumu ya maisha ya watu wetu? Au unataka kudokezea kuwa hizo sehemu ulizopita na kuona adha na hali ngumu ya maisha ya watu CCM hawajaona kabisa au hawataki kuona? Yawezekana tatizo letu siyo kuona na kuelewa ugumu wa hali ya maisha?

Kuna ripoti nyingi kuanzia zile za kimataifa na hizo ulizodokezea na nyingine kwenye poverty reduction programs. Yawezekana tatizo letu ni zaidi ya namba na idadi?
 
Mhe. Zitto; hivi tatizo la Tanzania ni kuelewa kiini na kina cha hali ngumu ya maisha ya watu wetu? Au unataka kudokezea kuwa hizo sehemu ulizopita na kuona adha na hali ngumu ya maisha ya watu CCM hawajaona kabisa au hawataki kuona? Yawezekana tatizo letu siyo kuona na kuelewa ugumu wa hali ya maisha?

Kuna ripoti nyingi kuanzia zile za kimataifa na hizo ulizodokezea na nyingine kwenye poverty reduction programs. Yawezekana tatizo letu ni zaidi ya namba na idadi?

Upo sahihi kabisa................ Ningependa uniite Zitto, achana na maneno mheshimiwa kaka. Ukipenda Prefix, ndugu is better kwangu
 
Inauma sana tena mno.
Wachache ndo wananufaika sana tena sana.
Wakati umewadia wa kuyapunguza matumbo yao.Angalia wenzetu Zambia Satta anaongoza kwa kura 40,000... za awali Banda yupo nyumba mbali mno ana kura 20,000..
 
Wildcard, mikakati na sera za upinzani zinatatua vipi tatizo lilipo sasa? Ili kuweza kuja na mapendekezo ya uhakika na ambayo yanawezekana la kwanza ni kutambua tatizo na kina cha tatizo hilo. Siyo tu kulitambua lakini kuweza hata ikibidi kulichambua katika sehemu zake ndogondogo.

Katika makala hiyo ya Zitto hapo juu ninachoona ni jinsi gani daktari mpasuaji anapomuandaa mgonjwa kwa upasuaji mkubwa na kabla ya kuanza upasuaji au kukusanya timu ya upasuaji maandalizi ya kulielewa tatizo yanafanyika. Hivyo mazungumzo na mgonjwa, x-rays, c-scans n.k n.k

Tusipolielewa tatizo kiusahihihi ni rahisi kwa watu kuja na mapendekezo ya "Aspirin"!
Umenikumbusha kauli za mwenyekiti wa CCM na Rais wetu aliyesema kuwa Hajui kwa nini Tanzania ni Maskini. Huyo ni Rais anayesema hivyo
 
Zitto,
Nimeziona sera zenu kule kwenye tovuti ya CHADEMA. Ni nzuri ingawa nyingi kama sio zote ni hizi za CCM. Mlichokifanya ni kukosoa au/na kutoa suluhuhisho pale walipokwama wao. Tatizo kubwa kwa sasa katika Nchi yetu ni UONGOZI. Bahati mbaya kabisa CHADEMA mnao baadhi VIONGOZI wanaoabudu MALI kama ilivyo kwa CCM.
 
Umegusia vema sana matatizo ya taifa letu.
Cha msingi kwa sasa tuunganishe nguvu kwa kuwaelimisha watu zaidi umuhimu wa kubadili utawala uliopo. Ninaamini kwa dhati ccm haistahili tena kututawala kwa sasa. Lazima tujiunge pamoja kuwabadili.

Ninaamini kwenye grass root movement tunaweza kabisa kufikia malengo yetu. Vipi suala la kuwezesha kampeni hizi, chadema ikafungua akaunti watu wakaruhisiwa kuchangia kwa uwezo wao?? Hebu tujaribu tuone kwani rasilimali fedha ni muhimu kufikia watu wengi hasa ukichukulia ubovu wa miundo mbinu yetu.

Watu wa mijini sielewi kwa nini muamkoo wetu uko chini hasa kwa vitendo? Mfano dsm tunaongoza kuwa na wabunge dormant kabisaaaaaaaaaaaaaaa.....
 
ZITTO,
Big up tuko pamoja.
`SLAA FOR PRESIDENCY 2010'.

Ukitaka kupima ukomavu wa kisiasa wa CHADEMA, basi hapo ndipo penye mtihani mkubwa! Slaa can make a better president for this country than Mbowe!

Ila kwa kuwa kuna tabia za ubinafsi kwa wanasiasa wetu, yaani mtu kama Mbowe hawezi kuelewa kabisa mkimwambia hilo!

SLAA FOR PRESIDENCY 2010
 
www.chadema.net

Zitto;

Excuse me plz, huyu jamaa alieuliza hili swali huenda anawatu anawakilisha wewe unasema aende kwenye Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Sawa mimi nitaenda, Je

Hivi wananchi wako wote kule kigoma kaskazini wanapata huu mtandao?

Hvi ni wananchi wangapi wana acess na internet?

Hivi internet ni nani anaeijua zaid yangu mimi na wewe?

Inawezekana mimi na wewe tunajuana lakini nijibu kama hatujuani ili ukomavu wa kisiasa uonekane basi.

ahhaaaaaaaaa
 
Ukitaka kupima ukomavu wa kisiasa wa CHADEMA, basi hapo ndipo penye mtihani mkubwa! Slaa can make a better president for this country than Mbowe!

Ila kwa kuwa kuna tabia za ubinafsi kwa wanasiasa wetu, yaani mtu kama Mbowe hawezi kuelewa kabisa mkimwambia hilo!

SLAA FOR PRESIDENCY 2010

Tusibadili mwelekeo wa mada jamani, na pengine tusimsemee Mbowe kwamba hawezi elewa, kwani naamini si yeye anaye jipendekeza kusimama nafasi ya uraisi nadhani kuna mfumo huru wa kupata mgombea ndani ya Chadema, na kama tunaona Slaa anafaa wajibu wetu ni kumsahauri achukue fomu na sisi tumpe sapoti.

Back to the issue, Zitto huu ni mwanzo mzuri, tuna amini 2010 mabadiliko makubwa yatatokea ikiwa ni matunda ya juhudi hizi.
 
Nani amekudaganya kwamba vyama vya upinzani vichochee mabadiliko ya kiuchumi??

wewe hujui Sera ya upinzani TZ uchochezi wa uchumi ni lazima wapewe u Rais na serikali??

Hapo ndipo tatizo kubwa lilipo, na hapo ndipo wanaponifanya nikose imani nao hawa wapinzani. Wao sio malaika, wanaweza kuingia madarakani wakaishia kuwa mafisadi tu. Kama kweli wana nia njema na nchi hii, wawe na njia mbadala ya kupunguza matatizo ya Watanzania.Badala ya kutumia mamilioni kukodishia ma-helkopta, watumieni hizo pesa kuwajengea wananchi, hasa wa vijijini nguvu za kiuchumi.

Wanaweza kuanza kwa kanda, kama vile hiyo kanda ya Ziwa. Kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutumia rasimali zilizopo kwenye maeneo wanayoishi kutawafanya wasirubuniwe na khanga, pilau, fulana na vijirushwa wakati wa uchaguzi. Lakini ukienda na sera tu kwa watu ambao hata mlo mmoja kwa siku wanaupata kwa tabu, hawawezi kukuelewa, watamwelewa yule aliyekuja na burungutu la pesa!

Hebu jiulizeni, kwanini mkoa wa Dar es Salaam hauna mbunge hata mmoja wa upinzani wakati ndiko kwenye mwamko mkubwa zaidi wa kisiasa? Wapiga kura walio wengi wa Dar es Salaam ni watu wa kipato cha chini, na hakika nawaambia wanarubuniwa kwa pesa, vitenge, fulana na khanga kama wale wa vijijini tu!

Jipangeni kwa kuanzia kwenye kiini cha tatizo! Kujaza watu kwenye mkutano wa kampeni kwa sababu umekwenda na helkopta halafu ukaondoka na kuwaachia "SERA" huku wakiwa bado wanalala na njaa ni kujidanganya mwenyewe!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom