Japhari Shabani (RIP)
R I P
- Jan 16, 2007
- 721
- 176
kutokana na umuhimu wake katika taifa letu, nimeamua kutundika hotuba iliyotolewa na Mheshimwa Mkuchika Huko Busanda kwenye kampeni za uchaguzi kwenye jimbo hilo. Ni hotuba inayohitaji tafakuri ya kina sana.hotuba hii nimeitoa kwenye gazeti la leo la Nipashe.
Mapema jana asubuhi Mkuchika aliwacharukia waandishi wa habari wanaoripoti habari za vigogo wa CCM kuzomewa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Zakaria, Mkuchika alisema CCM ina nguvu na inakubalika ila waandishi ndio wanaifitini.
Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyine wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu,alifoka Mkuchika.
Jamani huyu ndiyo waziri wa habari ambaye moja ya kazi zake ni kuhakikisha wananchi wana uhuru na uwezo wa kupata habari.Kama hayo haliyoyasema ndivyo basi hastahili kuwa waziri wa habari.kukosa umeme,kukosa habari hii nimja ya sababu ambayo imeifanya serikali ya CCM kuwa madarakani kwa muda mrefu.Kama walalahoi ambao idadi kubwa hawapati habari kupitia katika vyombo vya habari mbali mbali wengu hawafahamu madudu yanayofanywa na hao wanaowajihita viongozi.Sasa naanza kuelewa kwanini vyombo vingi vya habari vya serikali Radio Tanzania TBC ,television havina hata website kwani vyombo hivi vemelenga kuwadumaza walalahoi kwa propoganda za CCM na viongozi wao.Habari zao zikiingia katika mtandao na kusomwa au kutizamwa na watanzania wengi waishio nje ya nchi ni wazi watapata challenge kubwa.Kitu kingine ambacho najiuliza hivi hao viongozi wa CCM na serikali uwa wanaandaa hotuba zao au wanakurupuka tu na kuoanda majukwaani!CCM SIKIO LA KUFA ALISIKII DAWA MUNGU IBARIKI TANZANIA.