Nukuu takatifu ya Mkuchika!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
kutokana na umuhimu wake katika taifa letu, nimeamua kutundika hotuba iliyotolewa na Mheshimwa Mkuchika Huko Busanda kwenye kampeni za uchaguzi kwenye jimbo hilo. Ni hotuba inayohitaji tafakuri ya kina sana.hotuba hii nimeitoa kwenye gazeti la leo la Nipashe.

Mapema jana asubuhi Mkuchika aliwacharukia waandishi wa habari wanaoripoti habari za vigogo wa CCM kuzomewa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Zakaria, Mkuchika alisema CCM ina nguvu na inakubalika ila waandishi ndio wanaifitini.

“Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyine wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu,”alifoka Mkuchika.
 
............“Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyine wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu,”alifoka Mkuchika.

Hwana umeme, kwa nini? Magazet hayafiki, kwa nini? Hawana uwezo wa kununua magazeti, kwa nini? Nani kawaweka wananchi katika haya mazingira hata hawawezi kuwa na TV, Umeme wala kusoma gazeti? Kwani aliyesababisha haya yote hajulikani? Uwiiiiii
 
Huyu jamaa ni kumn'goa ubunge tu.

Hivi huyu jamaa ni mbunge wa wapi???

Tusuburi 2010, kila mmoja kivyakevyake, Hakuna kupeleka timu nzima kupigia kampeni mtu mmoja. Hakuna cha tingatinga wala baba yake tinga tinga. Hapo ndipo mchezo utakaponoga.
 
Mbunge wa Manyoni.
 
Mapema jana asubuhi Mkuchika aliwacharukia waandishi wa habari wanaoripoti habari za vigogo wa CCM kuzomewa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Zakaria, Mkuchika alisema CCM ina nguvu na inakubalika ila waandishi ndio wanaifitini.

“Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyine wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu,”alifoka Mkuchika.

Jamani CCM ni la kuvunda.. yaani hata wanayo yasema hayaeleweki, sasa hiyo ni speech ya kumnadi mgombea mbele ya wapiga kura? yaani kuwadhalau hivo? mhh...
 
Naomba resume ya huyu Mkuchika pia kama kunamtu anajua uchapaji wake wakazi atutokezee, hawa ndio wanaopata vyeo kwa uchawi kwani hawana lolote ni mpuuzi.
 
Wangeandika Mkuchika kashangiliwa huku ukweli alizomewa angewapongeza hao waandishi? Hii si kauli ya kutamkwa na mtu ambaye ana dhamana ya uwaziri wa nchi, hata kama ni kada wa chama. Inawezekana kuwa waziri katika nchi hii si lazima uwe na akili timamu au siyo kigezo muhimu.
 
.................
“Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyine wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu,”alifoka Mkuchika.

Duu! anajikaanga mwenyewe kwa mafuta yake!! hivi aliyoyasema si kuwakebehi na kuwatukana watu wa Busanda? aliyesababisha haya ni nani si utawala wa CCM? soma - Chukua Chao(wananchi) Mapema. Na kama naibu katibu mkuu anakili kuwadhoofisha kiuchumi wana Busanda kuna haja tena kuwapa ubunge waendelee kudhoofisha? GOD FORBID!

Tumefisadiwa kiasi cha kutosha
Tumepuuzwa kiasi cha kutosha
Tumenyonywa kiasi cha kitosha
Utawala dhalimu wa ccm ndiyo uliotufikisha hapa
 
Kazi kwelikweli. Tatizo tanzania kuchaguana kwenye hii serikali yetu. Hakuna kujali mtu huyu anauwezo gani,je yupo kwaajili ya maslai ya taifa/binafsi? Majibu yote 2010 wataita press tena tuone.
 
kutokana na umuhimu wake katika taifa letu, nimeamua kutundika hotuba iliyotolewa na Mheshimwa Mkuchika Huko Busanda kwenye kampeni za uchaguzi kwenye jimbo hilo. Ni hotuba inayohitaji tafakuri ya kina sana.hotuba hii nimeitoa kwenye gazeti la leo la Nipashe.

Mapema jana asubuhi Mkuchika aliwacharukia waandishi wa habari wanaoripoti habari za vigogo wa CCM kuzomewa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Zakaria, Mkuchika alisema CCM ina nguvu na inakubalika ila waandishi ndio wanaifitini.

“Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyine wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu,”alifoka Mkuchika.

Hapo alikuwa na maana kwamba wananchi wakipata uwezo wa kununua Tv na kupata pesa ya kununua magazeti watajua mengi wasiyotakiwa kuyajua na hivo wanaweza kuipiga ccm chini,masikini wadanganyika,halafu wa huko vijiji wanatia huruma kwasababu ni wapole na wanyenyekevu wenye ukarimu. Wa Tarime ni tofauti kidogo,wa Busanda sijui,tusubiri tuone,lakini kama hayo aliyoyasema ni ukweli na wananchi hao wameyasikia na bado wakaichagua ccm,then hapo tutajua kuwa umasikini na ujinga ni utamaduni wetu na kwamba nothing else can be done in this generation if we are to preserve peace.
 
kutokana na umuhimu wake katika taifa letu, nimeamua kutundika hotuba iliyotolewa na Mheshimwa Mkuchika Huko Busanda kwenye kampeni za uchaguzi kwenye jimbo hilo. Ni hotuba inayohitaji tafakuri ya kina sana.hotuba hii nimeitoa kwenye gazeti la leo la Nipashe.

Mapema jana asubuhi Mkuchika aliwacharukia waandishi wa habari wanaoripoti habari za vigogo wa CCM kuzomewa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Zakaria, Mkuchika alisema CCM ina nguvu na inakubalika ila waandishi ndio wanaifitini.

"Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyine wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu,"alifoka Mkuchika.

Kumbe CCM sera yao ni kudumaza watu wamaeneo fulani ili wasiwe na akili ya kujua mambo, na badala yake waipigie CCM, ndio maana nashanga miaka 48 ya uhuru Songea Umeme wa Kubabaisha, Lindi Mtwara Hivyo Hivyo, Shinyanga Tabora, Rukwa, Mwanza, Singida , Dodoma na Mlogolo ( Morogoro) Hivyo Hivyo, ili watu wasielemike usiwape umeme na barabara. Tosha, na hata Adam Lusekelo aliandika kwenye makala zake mojawapo, tafsiri ya kudumaza elimu tanzania
Hii inaitwa weapons of Mass Destruction, huji cha afya wala cha nini ni kuwa Mtumwa wa mawakala wa Pamba kwa kwenda Mbele
 
Ina maana kuipigia kura CCM ni kuafiki na kukubali hiyo hali iendelee - wananchi wazidi kukaa gizani ili wezi waendelee kuiba. Nilijua tu kuwa hawana mkakati zaidi ya huo lakini na sisi wengine twasema - tutawamulika tu hata kwa vigenge vya moto !!
 
“Nyie andikeni mnavyotaka, hata kwenye TV onyesheni, kwanza watu wa huku TV hawana kwa vile hata umeme hawana! Hizo TV zenu watazitazamia wapi. Na nyine wenye magazeti kwanza huku hayafiki na hata yakifika wananchi hawana uwezo wa kuyanunua, watasomea wapi hizo fitina zenu. Hayo mnayoandika yanabakia kuwa yenu na wamiliki wa vyombo vyenu,” alifoka Mkuchika.

!!!!!! t.uc g..cuf a tahw
 
Kumbe CCM sera yao ni kudumaza watu wamaeneo fulani ili wasiwe na akili ya kujua mambo, na badala yake waipigie CCM, ndio maana nashanga miaka 48 ya uhuru Songea Umeme wa Kubabaisha, Lindi Mtwara Hivyo Hivyo, Shinyanga Tabora, Rukwa, Mwanza, Singida , Dodoma na Mlogolo ( Morogoro) Hivyo Hivyo, ili watu wasielemike usiwape umeme na barabara. Tosha, na hata Adam Lusekelo aliandika kwenye makala zake mojawapo, tafsiri ya kudumaza elimu tanzania
Hii inaitwa weapons of Mass Destruction, huji cha afya wala cha nini ni kuwa Mtumwa wa mawakala wa Pamba kwa kwenda Mbele

CCM's weapons of mass Destruction kudumaza elimu tanzania
 
Hwana umeme, kwa nini? Magazet hayafiki, kwa nini? Hawana uwezo wa kununua magazeti, kwa nini? Nani kawaweka wananchi katika haya mazingira hata hawawezi kuwa na TV, Umeme wala kusoma gazeti? Kwani aliyesababisha haya yote hajulikani? Uwiiiiii

TAKATAKA MKUBWA HUYU TENA ANGETAKIWA ATUPWE SELO KWA KAULI ZA KASHFA VILE

KAMA HAWANA UMEME,,MAGAZETI HAYAFIKI,HAWANA PESA YA KUNUNUA,HAWANA UWEZO WA KUSIMA MAGAZETI,CCM IMEKALIA JIMBO LILE MIAKA YOTE,

THEN TAKATAKA ZA CCM ZINAENDA KUFANYA NINI...CI WAACHIE WENYE KULETA UMEME WENYE KULETA ELIMU....SHAME MKUCHIKA N FAMILY

BUSANDANIAN
 
Iwapo tutaendelea kuwa na viongozi wenye dharau na maneno ya kashfa kama aliyotoa huyo waziri Mkuchika.....basi hatutakuwa na maendeleo.
 
HAYA NDIO MAISHA ANAYOFURAHIA WAZIRI MWENYE MAMLAKA KUWAHUDUMIA WATANZANIA ATI NI MWANAJESHI SIJUI ALIKUWA ANATUMIKIA JESHI LIPI .WANAJESHI WOTE WANA HURUMA YA MWENNYEZ MUNGU HUYU ANAFURAHIA WENZAKE MABAYA LOH

Upungufu wa chakula watishia vijiji Dodoma

Vijiji vya Chikola, Kigwe, Nholi, Mwitikira, Mchito na Zanka wilayani Bahi mkoani Dodoma vimetajwa kuwa na hali mbaya ya upungufu wa chakula. Upungufu wa chakula umevikumba vijiji hivyo tangu Aprili mwaka huu na kuwafanya baadhi ya wananchi kusaidiwa chakula na serikali ya kijiji.

Akizungumza katika kikao cha ushauri cha wilaya hiyo kilichofanyika juzi wilayani hapa, Ofisa Kilimo wa Wilaya, Sylvester Kashaga alisema hali hiyo imesababishwa na maeneo hayo kukosa mvua kabisa katika kipindi cha msimu wa mvua uliopita.

Kashaga alisema kwa mujibu wa tathmini ya hali ya mavuno shambani na upatikanaji wa chakula iliyofanywa katika vijiji, kata na tarafa zote za Wilaya ya Bahi kuanzia Machi 10 hadi 28, mwaka huu, ilibaini kuwapo kwa upungufu wa tani 51,093.46.

Alisema mahitaji halisi ya chakula katika Wilaya ya Bahi kwa mwaka ni tani 61,172.77 kutokana na hali ya ukame ambapo mavuno tarajiwa ni tani 10,079.31 hivyo kusababisha upungufu wa tani 51,093.41. Ofisa Kilimo huyo alisema katika vijiji hivyo, tayari upungufu wa chakula umeshajitokeza tangu Aprili na katika vijiji vilivyobaki upungufu huo utajitokeza kuanzia Juni.

Baadhi ya watendaji wa kata waliohudhuria kikao hicho, walimueleza Mkuu wa Wilaya hiyo, Betty Mkwasa kuwa hali ni mbaya sana katika maeneo yao na hivyo kuomba utaratibu ufanywe kuwanusuru. Watendaji walioomba kusaidiwa chakula haraka ni wa kata za Lamaiti, Bahi, Kigwe na Chipanga ambao walisema tayari serikali za vijiji zimekuwa zikisaidia baadhi ya familia ambazo hazina kabisa chakula.
 
Uhalisia wa viongozi wa CHICHIEMU ndio huo na wala hakuwa anatania bali ni kutoka moyoni mwake, akiwasemea na wenzie wana CCM "WACHACHE" narudia WACHACHE... wasiotaka kuuona ukweli, wasioamini kuwa kuna watu wengine wanaweza kuongoza vizuri kuliko wao, Mkuchika anakata tamaa lakini bado anaamini kuwa atashinda kwa mbinu anazojua yeye na si kwa kutumia media kwani nyenzo hizo hazifanyi kazi vijijini na ana mbadala wake moyoni ambao wengi tunahisi lakini 24/05/09 itatupa jibu
 
Back
Top Bottom