Nukuu Sita za Nyerere ambazo CCM hawana budi kuzitafakari kwa makini sana leo hii

  1. Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?
  2. Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.
  3. Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?
  4. Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.
  5. Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili.
  6. Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe....

Na ya saba ambayo aliitoa siku nyingi sana;

7.
“Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika” –Mwalimu Nyerere (Januari, 1966)


Wanafunzi wa kike wanaobeba mimba huki wakiwa masomoni wana vihelehele...J.M. Kikwete
 
Ni kweli kabisa maneno yake. Utulivu unaonekana sasa siyo kuwa wananchi wanaridhika na jinsi mambo yanavyokwenda. Ni dalili tosha kuwa ndani yake watu wanakataa tamaa na kuvunjika mioyo taratibu. Mioyo ikashaanza kuvunjika taratibu kisha huja wakati ambapo mioyo hiyo huvunjika kabisa. Mioyo iliyovunjika kabisa huwa haisikii la mtu ikishaamua jambo. Kama wasemavyo watu wa siku hizi LIWALO NA LIWE. Naisikitikia sana nchi yangu kwani tuliowapa dhamana watuongoze, kwa makusudi kabisa wameamua kuivunja mioyo yetu. Ipo siku inakuja, ama kwa hakika hiyo siku haipo mbali sana.
 
Inatia kinyaa eti mahakamani unatakiwa wewe ndo ukathibitishe basipo shaka kuwa rostam azizi, chenge, lowasa, mkapa, ridhiwani etc.. ni mafisadi. Enzi za mwalimu ujinga kama huo kamwe haukuwepo.
 
Kwa nukuu hizi utaambiwa Mwalimu aliwachukia matajiri. Mwalimu alitaka mtu atajirike KIHALALI. Alitaka pia matajiri wahangaike na utajiri. Wakae mbali na utajiri wao wakitaka kuwaongoza watu. Hatukumwelewa. Mwalimu alitaka akikuuliza utajiri umeupataje using'ate ulimi kutafuta maelezo. Alikuwa na sheria nzuri sana ya kupambana na kuzuia rushwa. Ikachakachuliwa mwaka 1997 na 2007. Sasa hauwezi kumsimamisha mtuhumiwa yeyote mahakamani akueleze vijisenti na mali nyingine alizonazo kazipataje. Sheria inakulazimisha wewe unayemtuhumu ndio utafute ushahidi!
Tunakoelekea kubaya.


Hii nukuu ya Wild cat imekaa bomba sana...
 
Ungeziboresha kidogo kwa kuweka semi za kufunga na kufungua. Pia ungeweka tarehe/mwaka na ikiwezekana mahali alikotoa hizo semi. Asante

Mkuu shukuru hata kwake yeye kuziweka hapa maana wengine hata tusingekuja kuziona milele hayo masuala ya koma sijui na nini ni mambo ambayo hayana uzito kama ujumbe wenyewe ambao umeuelewa
 
R. I. P mwalimu huko uliko usilisahau taifa lako linaloangamia
 
Nimekuwa nikifuatilia hotuba nyingi za viongozi wetu: wa serikali, chama tawala na pia wa vyama vya upinzani. Pamoja na kuwa sina takwimu sahihi lakini kwa haraka haraka ni viongozi wachache sana (kama wapo) wa serikali na chama tawala ambao wana nukuu maneno au sehemu ya hotuba za marehemu Mwl Nyerere ukilinganisha na viongozi wa vyama vya upinzani! Mfano mzuri ni hotuba za kambi ya upinzani bungeni, karibu hotuba zote zina nukuu mbali mbali za maneno ya Mwl Nyerere lakini si kwa viongozi wa serikali na chama tawala. Je hii ina maana gani? Nawakilisha!
 
Kwasababu kila wanalofanya na wanalofikilia linakinzana na aliyoyataka na kuyatenda Mwl.Nyerere

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Wamekuwa si wazalendo tena wameweka mbele maslahi binafsi badala ya watanzania kwanza. Ndo maana wako kimakundi ya mafisadi na wanaosema si mafisadi katik chama kimoja.
 
sio lazima kila hotuba iwe na nukuu za maneno ya mwl JK,kwani maneno mengine hakuna!?
 
Nukuu ni jambo jema kuelezea unachoamini ili watu wajue kuwa mawazo yako yanaungwa mkono na watu fulani maarufu. Kwa mfano, Godbless Lema anapenda kunukuu wanafalsafa ambao ni revolutionists. CCM ya sasa hivi haifanyi yale ambayo Mwalimu Nyerere angefanya kwa sababu sio wazalendo hata kidogo, kwa hiyo usitegemee kiongozi wa CCM akanukuu maneno ya Mwalimu Nyerere. Sijui watanukuu yapi, ni ngumu sana. Watasutwa na hayo wanayonukuu
 
Mwl. JK. aliongea maneno yanayoishi mpaka leo, aliyo yakataa ndiyo magamba wanayotenda! Wanajuwa wakiyafuata maneno ya Mwl. yatawanyima fursa ya kufanya ufisadi.
 
Nukuu ni jambo jema kuelezea unachoamini ili watu wajue kuwa mawazo yako yanaungwa mkono na watu fulani maarufu. Kwa mfano, Godbless Lema anapenda kunukuu wanafalsafa ambao ni revolutionists. CCM ya sasa hivi haifanyi yale ambayo Mwalimu Nyerere angefanya kwa sababu sio wazalendo hata kidogo, kwa hiyo usitegemee kiongozi wa CCM akanukuu maneno ya Mwalimu Nyerere. Sijui watanukuu yapi, ni ngumu sana. Watasutwa na hayo wanayonukuu

Agreed! Scientifically unapo nukuu au kutoa reference kwa kitu unachokisema au ulichokiandika inaonyesha kuwa umefanya homework ya kutosha na unachokisema ni kitu credible sio kimetoka hewani. Inatia mashaka sana pale unaposhindwa kutoa reference au hata nukuu hasa kama una repoti ya zaidi ya kurasa 10 na hauna reference au hata nukuu moja!
 
Wakuu, katika kipindi kuelekea uchaguzi, si vibaya leo hii tukarudi kwenye hii thread...ina mambo ya msingi sana.
 
Kwa kukumbushia tu.....


  1. "Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?"
  2. "Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii."
  3. "Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?"
  4. "Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga."
  5. "Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili."
  6. "Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe...."

Na ya saba ambayo aliitoa siku nyingi sana;

7.
“Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika" - Mwalimu Nyerere (Januari, 1966)

Na nyingine ya nane;

8. “Kwani fursa iko mbele yetu na inategemea kama tuna ujasiri wa kuichukua. Kwani uchaguzi uliopo siyo kati ya kubadilika au kutobadilika; uchaguzi kwa Afrika ni kati ya kujibadilisha au kubadilishwa – kubadilisha maisha yetu wenyewe kwa mwongozo wetu, au kubadilishwa na matokeo ya nguvu zilizo nje ya udhibiti wetu.. .Tunapendelea kushiriki katika kutengeneza hatima yetu sisi wenyewe” –MwalimuNyerere (Januari, 1966)

Nukuu hizi zimo katika kitabu kinachoitwa : Reflections on leadership in Africa: forty years after independence : essays in honour of Mwalimu Julius K. Nyerere, on the occasion of his 75th birthday ' , by Haroub Othman, VUB University Press, 01 Jul 2000.
 
Kwanza kabisa naungana na familia ya mwl Nyerere na taifa kwa ujumla katika kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha mpendwa wetu baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kumbukumbu hii inatufanya sote kuenzi kwa kutambua, kuheshimu na kuthamini mchango wake katika ujenzi na ustawi wa taifa letu heshima iliyopelekea yeye kuwa ndiye baba wa taifa hili. Ningeomba leo hii nishee na nyie baadhi ya nukuu za baba wa taifa kama ishara ya kumuenzi mwasisi huyu.

1. Tunataka kuona katika taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini, si vijana waoga, akina ndiyo bwana. Tunataka vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania..... J.K Nyerere

2. Chama mimi si mama yangu wala si baba yangu, kwangu mimi chama ni sera. Chama kile kikiziacha shabaha zile na mimi natoka. Mimi si mwenzenu tena, leo nawaeleza ukweli tu...... J. K Nyerere

3. Uongozi unaweza ukawa mzuri au mbaya au usiojali lakini kama watu wanajitambua wenyewe, kutoshirikishwa kwa mawazo na tabia ya jamii hakutaendelea kwa muda mrefu..... J. K Nyerere

4. Kukubali kufanywa vikaragosi vya viongozi ni dalili ya woga na si dalili ya heshima. Hatuwezi kuuachia utamaduni wa woga ukawa mbinu au sifa mpya ya uongozi...... J. K Nyerere

5. We have no alternative but to apply ourselves scientifically and objectively to the problems of our country . We need to think; and then act on our thinking. We have to recognize poverty, the ignorance and the disease, the social altitudes and the political atmosphere which exist, and in that context think about what we want to do and how we can move from existing situation towards one which we like better...... J. K Nyerere

Ni dhahiri kwamba wakati tulionao kama taifa tunahitaji "mabadiliko" hivyo naamini kufuatia nukuu hizo chache unaweza ukajifunza jambo jipya na hatimaye kupata msukumo mpya wa kifikra, kimtazamo na kimaamuzi kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.
 
"Serikali ni Serikali.Serikali haiwezi ikapendeza kwa watu wakati wote.Haiwi Serikali.Itakuwa ni Serikali ya ajabu sana ikiwa itapendeza watu tu wakati wote.Hata Serikali ya Mwenyezi Mungu mimi sidhani kama inafanya hivyo maana kuna siku zingine kunatokea mafuriko haya yanatia misukosuko kwa watu"
 
Back
Top Bottom