Nukta za Zitto kuhusu vurugu za wana-uamsho Zanzibar

I think you are totally out of order and i am sorry but this is rubbish.

Jussa knows my stand on Union and on his outbursts. I send the message to the public and Jussa is a non issue here. I dont discuss people, but issues. If Jussa is wrong i tell him publicly and thats me. Dont distract people to discuss issues and start discussing Jussa.

Who is Jussa? My concern is peace of our country. These people who burn Churches have been handled with kidgloves. We must not only condemn them but show them that it is unacceptable in any civil society.

rounding this to Jussa persona is totally rubbish

Trust me Zitto, I am not blubbing when I say you should send a message to Jussa. You know pefectly well his 'influence' in that part of the country is up there. You also know his views about Muungano, so let's not make a three course meal for a well known subject.

Now, as a politician, a very experienced politician, I would like to believe that you are very conversant about the different ways of communicating effectively: You can either communicate through people who command some sort of influence in thier communities, or you can give public statement and hope everyone will be 'touched' by it. You can ofcourse use both options but the first option (influence people) may bring in better results than just issueing a public statement.

So, when I say contact your friend Jussa, I know his status in his community and I am also looking at the most efffective way for your message to have an impact. The current situation in Zanzibar needs intervention beyond a 'statement'. Remember, there are people in Zanzibar right now living in great fear, fear of not knowing what will happen to them and thier properties. For them a statement isn't enough.

Your position Zitto in this (my view) is unique becuase you have a direct access to someone who is 'influential, someone who can calm down the situation and help formulate a way foward. I am saying this taking into account your earlier initiative to meet (Mzee Warioba & Dr Salim) during the muswada wa katiba fiasco. That 'direct contact worked, and I believe it can work for Zanzibar, at least for now.
 
Last edited by a moderator:
1 .Vurugu za Zanzibar ni 'unwanted distractions' katika mchakato wa kuandika katiba mpya.

2. Hakuna namna vitendo hivyo vinaweza kuhalalishwa na kutetewa lakini ni matokeo ya muda mrefu ya 'superficial attempts at dealing against groups with ulterior motives.

3. Rais Ali Mohamed Shein aunde kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti vurugu hizo, na kuanza mzungumzo na pande zote. Hiki sio kitendo cha kudharau kabisa

4. Muungano wetu ni sacred na tumetoka mbali kushindwa sasa kuulinda, 'not when we are so close at having an everlasting formula'

5. Waliochoma nyumba za ibada wasakwe na kufikishwa mbele ya sheria mara moja. Tusiruhusu hata kidogo wapuuzi wachache
kutuingiza katika vurugu za kidini ili kufikia malengo yao ya kisiasa.

6. Zanzibar Political leaders and public opinion makers must engage the Zanzibaris into a serious and objective dialogue about the future of Zanzibar within or outside the Union.

I concur with Zitto on this issue!!
 
Jibu lako ni rahisi sana.
Makanisa yamepelekwa zenj na muungo.
Kabla ya muungano zenj haikuwa na utitiri wa mabaa na makanisa.:banghead:

Kwa hiyo tatizo ni utitiri wa makanisa na bar? au watanganyika? au nini hasa?
 
Kwa bahati siajwahi kuona Picha ya zitto akiwa katika nyumba ya Ibada ya waislam , sijabahatika kuona akisalimiana na viongozi wa dini ya kiislam. Siamini kama zitto ana ushawishi ktk jamii ya kiislam. kwa picha ya mbali zitto nawezza kumuona zitto ni muislam Jina. hata harusi yake hatujui itafungwa kwa madhehebu gani

Kama Zitto ni muislam jina so what??? unafurahia kanisa na mali za mchungaji kuchomwa moto????? Unamaanisha kuwa waislamu swafi kama wewe (unavyojidhania) mnasherehekea tukio hili?
 
Trust me Zitto, I am not blubbing when I say you should send a message to Jussa. You know pefectly well his 'influence' in that part of the country is up there. You also know his views about Muungano, so let's not make a three course meal for a well known subject.

Now, as a politician, a very experienced politician, I would like to believe that you are very conversant about the different ways of communicating effectively: You can either communicate through people who command some sort of influence in thier communities, or you can give public statement and hope everyone will be 'touched' by it. You can ofcourse use both options but the first option (influence people) may bring in better results than just issueing a public statement.

So, when I say contact your friend Jussa, I know his status in his community and I am also looking at the most efffective way for your message to have an impact. The current situation in Zanzibar needs intervention beyond a 'statement'. Remember, there are people in Zanzibar right now living in great fear, fear of not knowing what will happen to them and thier properties. For them a statement isn't enough.

Your position Zitto in this (my view) is unique becuase you have a direct access to someone who is 'influential, someone who can calm down the situation and help formulate a way foward. I am saying this taking into account your earlier initiative to meet (Mzee Warioba & Dr Salim) during the muswada wa katiba fiasco. That 'direct contact worked, and I believe it can work for Zanzibar, at least for now.

Well said Mkuu. I conquer with you 100%
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: FJM
Naamini waandishi hawakumwelewa Katibu Mkuu. Mkataba wa Muungano upo. Ni moja ya hati za makabidhiano kwa kila Katibu wa Bunge na Dkt. Slaa amekuwa Mbunge muda mrefu na hawezi kusema walichoandika waandishi. Mkataba wa Muungano ulijadiliwa katika Bunge la Tanganyika na Hansard zipo kila mahala. Mkataba wa Muungano sio jambo la siri hata kidogo na wala haliwezi kuwa jambo la siri.

Ni kweli wananchi hawaujui muungano. Hii ni kutokana na watawala kutotaka tuujue muungano. Lakini kutoujua hakutun yimi haki ya kuujadili muungano na kuamua hatma yake.

You seem to be too cautious in your responnses and dialogues to raise eyebrows! One can remotely,due to your over cautiousness fit a hiden goal, a hiden mission,a hiden agenda which might not be existing. This in my view might alianate you from the peole! Otherwise you r very right but...tht overcautiousness of yours is what what worries me! Between your lines!
 
kama zitto ni muislam jina so what??? unafurahia kanisa na mali za mchungaji kuchomwa moto????? unamaanisha kuwa waislamu swafi kama wewe (unavyojidhania) mnasherehekea tukio hili?
hapa nakmbuka mauaji ya mwembechai kanisa likapongeza. Kumbe inauma?
 
Mkuu hapa CUF unawabebesha zigo lisilowahusu. Wa kulaumiwa hapa ni Nchimbi kama waziri wa mambo ya ndani ambaye wizara yake ni ya muungano, kuruhusu polisi kuanzisha vurugu hizi.

Hakukuwa na haja ya kukamata watu usiku kama majambazi na kuanza kupiga risasi wakati historia ya Zanzibar inajulikana wazi tangu uchaguzi wa mwaka 1995. Busara ingetumika, badala ya kutumia coercion wangetumia engagement. Huwezi kuulinda muungano kwa mabomu bali kwa majadiliano na maelewano. Yeyote atakeyepoteza maisha anatakiwa kuondoka na Nchimbi kama waziri mwenye dhamana ya polisi.

Lakini pia Dr Shein na wenzake wanatakiwa kuwa huru kutoa maamuzi yao si kila kitu wafuate CCM inawaambia nini. Hawa Uamsho hawahitaji kuwa contained bali kuwa unleashed. Suala la dini ni very sensitive, ukitumia nguvu kuwadhibiti unawafanya hata wale ambao wasiowafuata hawa uamsho kuaona kuwa nao wanatakiwa kufanya kitu kwani dini yao ya kiislam inasema 'ndugu wa muislam ni muislam'. Hii ni test ya kwanza ambayo CCM wasipoangalia wata-fail vibaya sana kuelekea mchakato wa katiba. Huwezi kuwawekea watu mipaka katika kujadili mustakabali wa maisha yao.

Lakini inashangaza kuuvamia upande Wa dini flani eti ndio attacking point... Hapana haitakuwi kuwaruhusu wafikie huko maana huo uamsho utaamsha amsha kweli mambo mazito, VITACHOMWA VITU VINAVYOWAHUSU UNNADHANI ITAKUWAJE?
Ustaarabu huushinda Ujinga Mara nyingi ingawa si Mara zote.. TUWE WASTAARABU, ANDAMANA UJUMBE UFIKE(ZINGATIA UTARATIBU NA SHERIA) LAKINI DINI Z WENGINE ZIHESHIMU KAMA UPENDAVYO YAKO IHESHIMIWE(je lolote kwingineko mf. Mby ikachomwa moto misikiti Kwa kisasi , je itakuwaje?)
MUNGU IBARIKI TANZANIA, WAPE HEKIMA YAKO WALIYOIKOSA MAANA UMETUAGIZA UPENDO NA SI SHARI...
 
Sijabahatika hata siku 1 kumuona Zitto msikitini, hata picha 1 ya zitto kusalimiana na viongozi wa dini ya kislam. Ni wazi ni muislam Jina. hana uchungu kabisa na uislam na waislam wa tz. kauli hii ingalitolewa na akina Abdalla safari ningalishtuka, lkn Zitto uislam wake unamashaka. ndio maana hadi leo ndoa yake haiujlikani kama itafungwa kiislam au mahakamani
kwanini awe na uchungu na waislamu wakati kimbunga cha maisha magumu,kimbunga cha fursa sawa kwenye elimu/ajira/biashara kinatupiga watanzania wote wa kawaida kwa namna moja? uvivu wako ndiyo unakufanya utake kuhurumiwa...mwenzako kichwani mwake hana hiyo mentality ya unyonge/kuonewa huruma/kupewa misaada nk ndiyo maana amefika hapo alipo...
 
Kama Zitto ni muislam jina so what??? unafurahia kanisa na mali za mchungaji kuchomwa moto????? Unamaanisha kuwa waislamu swafi kama wewe (unavyojidhania) mnasherehekea tukio hili?

Hakika ustaarabu kwingineko hakuna , mtu anashereheke na manaake mi huku Mbeya nichome moyo misikiti ??? Maana huku hiyo kwanza ndio siku hizi tunaijua b4 hatukuwa nayo ni ile ya mjini sokomatola na mwanjelwa but kwingineko hadi unasema nenda pale Kwa muislam alf kushoto ndio utakuwa umefika Kwa Christian mtoto Wa Mariam...
Si sawa kuchoma kanisa maana huchochea upuuzi....
 
Hadidu za rejea na maelekezo ya Rais kwa tume ni kwamba Muungano usijadiliwe, lakini yanayoendelea Zanzibar wote tunayaona. Ni wazi kuwa sasa mantiki ya kutokuujadili Muungano ni ya kiwenda wazimu au ya kipofu. Sasa tume inarudi kwa Rais wenyewe wana uwezo wa kwenda kinyume na hadidu rejea na maelekezo ya Rais?
 
SIUNGI MKono kuchomwa kanisa lkn nakumbuka siku kama nne zilizopita kuna padri kaitaka serekali idhibiti UWAMSHO TAASISI YA KIISLAM na wazanzibar 99% ni waislamu .serekali ya muungano imeitika wito wa padri kwa kumkamata shehe musa msikitini zanzibar unategemea nn kitokee kwa wazanzibar kufatwa misikitini na SMT tusitegeme kupanda mgomba tukavuna embe polisi wa smt ndio chanzo

So do you mean huyu Padri alishaona, na kuwaeleza serikali.Ila intelligensia ilikuwa na ganzi?CCM should give this country mapema si lazima wasubiri kutolewa au uchaguzi ujao kwani wanazidi ozesha na kutia ajisi kila kitu
 
sioni sababu ya waislam kuchoma makanisa kwa vile yanaibuka mengi, hata bara kuna miskiti ya misaasa ilijengwa kwa fujo na kuwa wakristu walihofu ktk maeneo yao ila hawathubutu iharibu.Ila iliachwa mingine haijulikani km in waumini au lah.

Same could happen with makanisa, yakiibuka km uyoga km hayana wafuasi yatapotea, km yanatumia njia haramu kulazimisha waumini sheria itawatafuna, km wanwahadaa waumini basi nao baada ya muda wanaojitoa wakigundua kweli na kweli iwaweke huru.

Sasa wa kuofia makanisa kuongezeka wangeangalia wanoongezeka ni akina nani,km ni waumini wao basi wajitazame kwa undani ni sababu.Kuchoma makanisa ni kukata tamaa kiimani na kushindwa kushawishi.
 
Kitendo cha kuchomwa kwa kanisa kinabidi kilaaniwe na kila mtu mwenye akili timamu, ila kitendo hiki kisitufanye tuache kujadili matatizo sugu yanayougusa u-muungano. Mimi nadhani wakati umefika ifanywe referendum na wananchi Waamue kama wanataka kuwa na muungano. Na kama watasema wanataka muungano uendelee basi waamue ni muungano gani wanautaka. Haya Wakina JK wameshazeeka na wanataka kuendelea kulea matatizo ambayo yatakuwa na athari kubwa kwa watoto na wajukuu zetu.
 
Kama Mhe. Zitto unasema Mkataba wa Muungano uko katika Hansard, Ninakuomba kama MwanaJF uuweke hapa kila MwanaJF ausome.

Atakachoweza kutuletea Mhe. Zitto kutoka hansard ni sheria ya kuridhia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyopitishwa na Bunge la Tanganyika na sio ule mkataba uliowekwa sahihi ya Nyerere na Karume.

Hiyo hati atakayoileta akipata muda, unajua wanasiasa huwa hawapi muda, hawana muda, itakuwa imebeba sahihi ya Pius Msekwa au Mzee Mkwawa. Huu United Republic of Tanzania: Union of Tanganyika and Zanzibar Act, 1964

Sheria kama hiyo ya kuridhia Muungano ilipasa pia kupitishwa katika Baraza la Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar lakini huko hakuna kumbukumbu inayoonesha kuwa Zanzibar walipitisha sheria /waliunda sheria ya kuridhia Muungano.

Ukigoogle unaweza kupata huu unaosema kuwa Baraza la mapinduzi pia liliridhia. lakini hauna sahihi.
Article of the Union between Tanganyika and Zanzibar

Madudu ya Muungano/ Kero za Muungano zilianza tokea ulipoanzishwa na sasa Muda wa mtoto kumwambia mfalme kuwa anatembea bila nguo (uchi) umefika.

Nafasi ya kuunda katiba mpya ya Muungano(jamhuri) ambayo inatoa masharti kuwa muungano ni off-limit ni siasa za mfumo wa chama kimoja.CCM na serikali zake bado wanaamini kuwa Tanzania ni nchi ya ujamaa na kujitegemea na Chama kinashika hatamu. Usanii uliotukuka(Upimbi).

Nyenzo zaidi. http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=179&Itemid=27

Review: The creation of Tanzania

http://www.zaoerv.de/66_2006/66_2006_1_b_215_234.pdf
 
I don't want to say much on this, however, let's every one be him/herself. This hypocricy behaviour will lead our country into disasters. Zitto, why so emotional? Are you trying to seek public sympathy while actually people know you more than you think? Please be your self. The future will tell the truth. Every thing will be open and you will be shocked and ashamed.
 
Naamini waandishi hawakumwelewa Katibu Mkuu. Mkataba wa Muungano upo. Ni moja ya hati za makabidhiano kwa kila Katibu wa Bunge na Dkt. Slaa amekuwa Mbunge muda mrefu na hawezi kusema walichoandika waandishi. Mkataba wa Muungano ulijadiliwa katika Bunge la Tanganyika na Hansard zipo kila mahala. Mkataba wa Muungano sio jambo la siri hata kidogo na wala haliwezi kuwa jambo la siri.

Ni kweli wananchi hawaujui muungano. Hii ni kutokana na watawala kutotaka tuujue muungano. Lakini kutoujua hakutun yimi haki ya kuujadili muungano na kuamua hatma yake.

Hapo kwenye red vipi ulijadiliwa pia na bunge la Zanzibar na kuridhiwa?
 
Nafikiri tusichanganye dini na mambo ya Muungano kwakuwa makubaliano ya muungano hayakufanyika kanisani wala msikitini, hivyo ni busara kupeleka hukohuko mikataba ilipofanyikia.

Nafikiri huu ulikuwa ni wakati muhimu na mzuri sana kwa jumuia ya uhamsho kutoa elimu kwa ufasaha juu ya muungano na ubaya wake kusudi wananchi watoe maoni yao kwenye mchakato wa katiba mpya, sasa wanapoamasha vurugu wakikamatwa na kuwekwa ndani maoni watatoa vipi?.

WANZANZIBAR WANAPASWA KUFIKIRIA KWA MAKINI SANA JUU YA MAMBO WANAYOFANYA JUU YA WATANGANYIKA WALIOPO ZANZIBAR, WATANGANYIKA WALIOPO ZANZIBAR HAWAZIDI HATA 6000 JE HUKU BARA KUNA WAZANZIBAR WANGAPI?, JE HUKU TANGANYIKA NAO WAKIJIBU MAPIGO NANI ATAKAOATHILIKA ZAIDI?..
 
Zanzibar hakuna udini na wala ukristo si adui wa wazanzibar. Asilimia 99 kwa chini ya asilimia moja- uadui unatoka wapi. Bora waliosema waarabu wanataka kurudi Zanzabar wana mashiko.

Hata waliosema CUF ni chama cha udini (uislam) walikuza hilo kisiasa japo lilikuwa justified na waislam wengi hasa wa ukanda wa pwani kuingia CUF kwa ushabiki wa kidini. Tatizo la zanzibar ni Uuunguja na Upemba; sasa waunguja ni waislam na wapemba waislam- udini unatoka wapi. Wazanzibar walibaguana kwa "wale CUF wapemba" na "wale CCM waunguja". Lakini wote hawa ni waislam na hamuwezi kuwatoa huko kwani hicho ndicho kilichowaunganisha.

Wanapotumia uislam wanapata support kutoka vyama vyote, ccm na cuf. SASA KWANINI WANACHOMA MAKANISA - NI VYEMA UCHUNGUZI UFANYWE KUJUA SABABU. Wakristo waliopo zanzibar kwa uchache wao hawana nguvu ya kisiasa kuzuia jambo lolote litakalokusudiwa na waislam walio wengi hivyo, hakuna haja ya kuwabagua wala kuwatisha.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom