Nukta 3 za ccm ndio zimeibua mgomo wa mabasi moshi.

MsakaGamba

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
392
141
Barua ya ccm wilaya ya Moshi mjini ya tarehe 8/7/2012 yenye kumb na CCM/MOS/VOL.102/FOLIO 230/2012 inasema
YAH: MGOMO WA USAFIRISHAJI ABIRIA KUANZIA TAREHE 9/7/2012
Rejea makubaliano ya kikao chetu kilicho kaa siku ya jumamosi mchana tarehe 7/7/2012 katika ofisi zetu za ccm ikiwa ni muendelezo wetu wa kupinga kupanda kwa ushuru wa mabasi madogo kutoka 1000/= hadi 15000/=.

Katika kikao tulianzimia yafuatayo:-

1. Kwamba kuanzia siku ya jumatatu 9/7/2012 kusimamisha shughuli zote za usafirishaji wa abiria hadi halmashauri watakapo koma kupanga ushuru kama wanavyo taka wenyewe.

2. Kwamba chama kitatumia safi yake ya upambanaji kuandaa kikundi cha vijana wa Greenguard ili kuhakikisha kinafanya fujo zenye lenye lengo la kuishinikiza halmashauri irejee maamuzi yake.

3. Chama kitahakikisha kwamba wote watakao shiriki katika mgomo watalindwa dhidi ya mkono wa sheria. Hakuna hata mmoja atakae kamatwa na kushtakiwa kwenye operesheni yetu hii. Hata kama atakuwa amesababisha maafa.

Ili kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanyika kwa ufanisi chama kitato fedha taslimu TSH 30,000 kwa kila mshiriki.

Kwa barua hii tuna wataarifu wale wote waliohudhuria kikao chetu cha jumamosi tarehe 7/7/2012 wafike ofisi ya chama wilaya saa 2:00 asubuhi wakiwa na bendera za chama walizo gaiwa kwa ajili ya kupokea fedha na kuhakiki kufungwa kwa bendera hizo kwenye magari na kusubiri maelekezo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nami kwa namba 0713 002800

Alu Sigamba
KATIBU (W)

Nakala kwa:
. Mkuu wa mkoa - kilimanjaro
. Mh Nape Mnauye - katibu wa Nec itikadi na uenezi CCM Taifa
. Usalama wa taifa (kikosi maalum kudhibiti CHADEMA/WANAHARAKATI)

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

*Barua hiyo hapo juu imetoka uk wa 3 wa gazeti la Mwanahalisi julai 11 - 17, 2012. Nimeikopy ili iwafikie wengi wa mitandaoni na kuibua mijadala hasa katika NAKALA kwa usalama wa taifa kitengo maalumu kudhibiti Chadema/Wanaharakati.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom