NUCLEAR KWA UMEME WA TANZANIA LINI? uranium si tunayo!

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,538
6,456
Wajameni, ni lini Tanzania tutakuwa na umeme wa nuclear, kwasababu tunazo resources zake yaani uranium ya kumwaga huko Ruvuma na Mtwara, mbona tungepata umeme mwingi sana tuwauzie hata hawa wakenye jamani?

halafu, umeme wa bwawa mto Rufiji, lini? utagarimu hela ngapi na unaanza lini? angalia Brazil wanazo Kw kama 12,000, na Brazil hawana tatizo la umeme na wanauza karibia kwa latin america yote...maji ya Rufiji yanaenda tu baharini, watz wanaanglia tu hawana lolote, tutajikomboa lini wajameni?
 
Binafsi siungi mkono umeme wa urani, kwa uzembe tulionao tunaweza teketea wooote, hebu angalia mabomu yalivo ua mbagala na gongo la mboto kwa sababu ya uzembe
 
Ili kuweza kutoa umeme kutoka nguvu za nuklia, inabidi uwe na wanasayansi waliobobea na wana physikia si chini ya elfu tano (Scientists). Pia uwe na angalau bilioni mbili za dola.....kuanzia tu.
Kama wanasayansi si wako, gharama itakuwa mara tano ya hapo.
Nadhani tungeanz na umeme wa kinyesi ingekuwa inaelekea!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom