Nssf...!!!!

MJINI CHAI

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
2,198
1,226
Heshima wakuu
Naombeni munisaidie, hivi mfanyakazi akisha achishwa/kufukuzwa kazi na baada ya miezi sita kulipwa na NSSF michango yake ambayo aliwekeza NSSF, je hasitahili kulipwa gawio la faida ya vitega uchumi ambavyo NSSF wamewekeza? kwani ni pesa za michango ya mfanyakazi ambazo wametumia bila ridhaa nina ndugu yangu anataka kuwashitaki na ameniomba ushauri, sasa wana JF nimshauri vipi? maana mimi si mtaalamu wa Sheria
 
mkuu ... kwani mkataba wako na NSSF unasemaje ...usiende kinyume na compliance ya agreement .... hayo mengine ni ujanja wanaoufanya bila wanachama kujua ..pia pesa lazima ziwe dynamic
 
mkuu ninacho kifahamu hata mimi nahitaji sasa kwenda NSSF kucheki kama kuna mkataba ambao niliingia nao kwani wakati naajiriwa sikuona mkatamba wowote zaidi ya kuelezwa kuwa utakatwa asilimia 10 ya mshahara wangu na mwajiri atachangia kiasi hicho hicho lakini sikuambiwa kuwa pesa zangu zinaenda kufanyiwa biashara. ingawa kwa huyu ndugu yangu sijui kama aliingia mkataba na NSSF
 
Sasa Mkuu hapo kwenye Red, je haifai sasa kuwatoa 'Bangi' hawa jamaa wa NSSF? na swala la pesa kuwa Dynamic its ok, ndio maana jamaa yangu anataka apewe gawio sasa
 
[/COLOR]

Mifuko yote ya mafao ya TZ ni ya kifisadi. Wachangiaji (wafanyakazi) hawapati chochote kutokana na uwekezaji wa michango yao. Badala yake wanaifaidi vigogo wa mifuko, serikalini na wafanyabiashara. Wafanyakazi hawana usemi juu ya mifuko kwa sababu wajumbe wengi wa Bodi zao wanachaguliwa na serikali. Uwakilishi wa wafanyakazi ni kidogo. Kuna haja ya wafanyakazi kudai mifuko yao waisimamie wenyewe. Mgaya wa TUCTA akomalie hilo.
 
mkuu ... kwani mkataba wako na NSSF unasemaje ...usiende kinyume na compliance ya agreement .... hayo mengine ni ujanja wanaoufanya bila wanachama kujua ..pia pesa lazima ziwe dynamic
Hakuna mkataba na NSSF. Unapojiunga unajaza mafomu fulani wanayokuletea. Hayo hayaweki wazi haki na wajibu wa kila mdau.
 
mkuu ninacho kifahamu hata mimi nahitaji sasa kwenda NSSF kucheki kama kuna mkataba ambao niliingia nao kwani wakati naajiriwa sikuona mkatamba wowote zaidi ya kuelezwa kuwa utakatwa asilimia 10 ya mshahara wangu na mwajiri atachangia kiasi hicho hicho lakini sikuambiwa kuwa pesa zangu zinaenda kufanyiwa biashara. ingawa kwa huyu ndugu yangu sijui kama aliingia mkataba na NSSF

Hapo kwenye red,,,ni sawa na kuuziwa 'mlio wa mbuzi kwenye gunia'. Ukweli ni kwamba mikataba haiko wazi ndio maana inakuwa taabu ifikapo kipindi ukachukue mafao yako ETI UNAAMBIWA MWAJIRI WAKO HAKUWA AKIPELEKA GAWIO HIVYO ENDELEA KUSUBIRI AU TUMFUNGULIE MASHITAKA.
 
Angalizo pia kwa walio wanachama wa NSSF. Usisubiri ustaafu ndiyo ujue salio lako. Michango inayoenda NSSF huchakachuliwa. Unaweza leo ukaweka laki nne wewe na mwajiri wako kwa mwezi halafu NSSF wakakuandikia elfu 10 katika baadhi ya miezi. Ukiomba full statement kwenye matawi tangu ulipojiunga hawakubali wanakupa ya miezi kiduchu then wanakueleza uende makao makuu. Pia ukiingia kwenye website yao, huwezi kupata statement hadi ujiunge na utakaa unasubiri jibu la kukbaliwa kujiunga hata miezi mitatu itapita. Ukishakuwa sasa umejiunga na hiyo website, ukiomba statement wanakupa inayoishia miaka mitano ya nyuma, huwezi kupata current. Hivyo ikitokea ukafa na hukupata nafasi ya kufuatilia wakati ukiwa hai basi ujue warithi wako watalipwa mchakachuo. Kwa hivyo hata kabla hujajiuliza kuhusu utakavyofaidika na huo uwekezaji wa majumba ya NSSF na daraja la Kigamboni, kwanza angalia kama hata hicho ulichokichangia utakipata chote. Kama huamini haya na wewe ni mwanachama, basi jaribu kufuatilia then uje hapa utujuze yatakayojiri.
 
Mifuko yote ya mafao ya TZ ni ya kifisadi. Wachangiaji (wafanyakazi) hawapati chochote kutokana na uwekezaji wa michango yao. Badala yake wanaifaidi vigogo wa mifuko, serikalini na wafanyabiashara. Wafanyakazi hawana usemi juu ya mifuko kwa sababu wajumbe wengi wa Bodi zao wanachaguliwa na serikali. Uwakilishi wa wafanyakazi ni kidogo. Kuna haja ya wafanyakazi kudai mifuko yao waisimamie wenyewe. Mgaya wa TUCTA akomalie hilo.

Big up Mkuu nami naunga mkono 100% na nipo tayari kwenda kumuona Bwana Mgaya juu ya jambo hili, wanatudhulumu haki yetu au vinginevyo isiwe lazima kujiunga na NSSF
 
Mimi mwaka 2003 nilikuwa nachangia Tsh. 80,000/= amayo iliweza kununua mifuko 10 ya cement, nikiacha au kuachishwa kazi watanilipa ile ile Tsh. 80,000/= ambayo sasahivi itanunua mifuko 4 tu ya cement.

Jameni huu si ujambazi wa nguvu kabisa-TUNAHITAJI MABADILIKO kama noma na iwe noma!
 
Mimi mwaka 2003 nilikuwa nachangia Tsh. 80,000/= ambayo iliweza kununua mifuko 10 ya cement, nikiacha au kuachishwa kazi watanilipa ile ile Tsh. 80,000/= ambayo sasahivi itanunua mifuko 4 tu ya cement.

Jameni huu si ujambazi wa nguvu kabisa-TUNAHITAJI MABADILIKO kama noma na iwe noma!

Umesema ukweli kabisa, niliwahi kuchukua mafao yangu 2006, baada ya kuchangia 6 years, yaani huwezi amini wakaniambia hakuna Interest baada ya kuhangaika sana kufuatilia hiyo michango, na nikagundua kama laki mbili zimepungua, kwa taabu niliyopata wakati wa kufuatilia niliamua kuacha.
Sasa angalia vigogo wanavyojikopesha hizo hela, yaani ni upuuzi mtupu hii mifuko,wafanyakazi ambao ndio wadau wakubwa hawafaidiki chochote.
At least wangekuwa wanakopesha hao wafanya kazi, mimi nadhani haya ndio mambo ambayo vyama vya wafanyakazi wangefuatilia kusaidia wanachama.

matokeo yake wanaishia kukopesha wanasiasa na vyama vya siasa.
Hiyo website ndio uozo mtupu mwezi wa sita sasa kila siku najiunga napata password, nikitaka statement naambiwa nijuinge tena, yaani upuuzi mkubwa.
Nilienda kwenye tawi lao moja na card yangu nikaulizia statement baada ya kuwa mwanachama kwa mwaka mmoja nikaambiwa eti bado haiko tayari nisubiri miezi sita.
 
Wakulu- kwa mnaoingia kazini sasa, ni vzuri kuuliza mfuko upi angalu chongo kati ya vibofu.

Niataarifa kwamba LAPF ndo inalipa poa kuliko mifuko mingine. Nitakuja angusha jamvini formular zake. Nasikia LAPF inatoa X3 zaidi ya mifuko mingine.

It is better ukaudhur
 
Nimekuwa nikujiuliza hili suala siku nyingi sana....
Pesa zetu wanazi-invest, kwa nini tusipate interest kila mwezi?
Kwa kweli NSSF ni wezi
 
Wakulu- kwa mnaoingia kazini sasa, ni vzuri kuuliza mfuko upi angalu chongo kati ya vibofu.

Niataarifa kwamba LAPF ndo inalipa poa kuliko mifuko mingine. Nitakuja angusha jamvini formular zake. Nasikia LAPF inatoa X3 zaidi ya mifuko mingine.

It is better ukaudhur

Lakini NSSF ni lazima kwa kila mfanyakazi? au mi ndo sielewi
 
Mifuko yote ya mafao ya TZ ni ya kifisadi. Wachangiaji (wafanyakazi) hawapati chochote kutokana na uwekezaji wa michango yao. Badala yake wanaifaidi vigogo wa mifuko, serikalini na wafanyabiashara. Wafanyakazi hawana usemi juu ya mifuko kwa sababu wajumbe wengi wa Bodi zao wanachaguliwa na serikali. Uwakilishi wa wafanyakazi ni kidogo. Kuna haja ya wafanyakazi kudai mifuko yao waisimamie wenyewe. Mgaya wa TUCTA akomalie hilo.

Kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii, hapo kwenye red sii sahihi, maana inafanya kazi za jamii nyingi tu NSSF ni mmoja wao, kuchangia ni sharti unapoajiriwa unaelezwa kama unakubali masharti ya ajira yako kwanza ndio unaanza, na unachangia asilimia kumi tu au tano kutegemea na mfuko husika. na mwajiri anakuchangia asilimia kumi au kumi na tano ili iwe 20% ambayo utapewa ukistaafu, ukifa(warithi wako), au ukiachishwa kazi!! mifuko ya hifadhi ya jamii ipo dunia nzima, sii TZ pekee na haina uhusiano na siasa wala vyama vya wafanyakazi sii jukumu lao, maana pesa unayoweka sii ya kutumia wakati wa neema!! ni ya wakati wa dhiki yaani ukistaafu, ukifa (warithi wako), au ukiachishwa kazi!!!!. ukipatwa na lolote kati ya hayo unapoteza sifa ya kuwa mfanyakazi hivyo TUCTA wala haihusiki na haitakusaidia kwa lolote hapa. Wakati ukiwa kazini una asilimia tisini (90%) au tisini (95%) na tano ya mshahara wako kufanyia kila utakacho. kuwekeza ni lazima ili pesa isipoteze dhamani, huwezi kuziweka kama mayai!!! na hifadhi ya jamii sii benki ni kitu kingine kabisaa!!

Mgaya wa wa TUCTA hana utaalam wa mambo ya hifadhi ya jamii na hii sii deci.Hifadhi ya jamii kwa maana ya mifuko iki crash, uchumi wa nchi kwisha na akiba ya wafanyakazi itapotea hamna cha pensheni wala nini!!

Watanzania tubadilike si kila kitu ni siasa, elimu tumeifanya siasa sasa tunakoenda siko!! mbona elimu inatolewa kila siku kuhusu hifadhi ya jamii hatuelewi tu.
 
Mkuu, hapo kwenye Pink mbona hueleweki? kwani wewe Mshahara wako hufanyii kitu unachotaka? na kwenye Blue sipingani na wewe ila kinachotokea ni kuwa baada ya mfanyakazi (mchangiaji) kupatwa na matatizo analipwa kiasi kilekile cha mwaka '47' bila kujali kama pesa wanayolipa imeshuka thamani na vilevile hapewi gawio la faida la vitega uchumi vilivyowekezwa na NSSF kwa nini wasiwakopeshe wanachama wao kwa masharti nafuu ili nao wafaidike?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom