Nakubali kuwa Tanesco ina matatizo mengi, na hata wizara ya madini inayo matatizo mengi, lakini nisichokubali hata kidogo ni kuwa mtu wa kukabiliana na matatizo hayo ni huyu Ngeleja. Huyu bwana hana uelewa achilia mbali mbinu za kutatua matatizo ya umeme Tanzania. Hana.
Hata hivyo, mimi simlaumu Ngeleja, kwa sababu sijui aliyempa nafasi ya kuongoza wizara hii nyeti alimpa 'job descriprition' gani. Ya kuhakikisha nchi inakuwa gizani? Na kama siyo inakuwaje nchi iko kwenye giza lakini uliyempa madaraka ya kuleta mwanga anabakia ofisini?