NSSF versus PPF

Tores

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
551
475
Wadau!

Kwa sasa nimerudi nyumbani TZ, baada ya kufanyakazi kwa muda mrefu nje ya nchi.....Na kwa bahati nzuri nimepata kazi katika kampuni ya utafiti wa madini kanda ya ziwa, maana mimi mwenyewe ni mtaalamu wa utafiti wa madini na mafuta.

Mwajiri wangu ameniambia ni lazima kujiunga na shirika mojawapo kati ya PPF au NSSF. Sasa nipo kwenye dilema..naomba msaada wenu wa kimawazo lipi shirika zuri (huduma nzuri,masharti nafuu na faida nzuri kwa mwanachama) kati ya haya niliyoyataja?
 
Ungemuuliza HR wa hapo ofisini kwako ungepata jibu. Lakini pia uki-google nssf, na ppf utapata web pages zao na kuangalia benefits to members. In a nutshell pamoja na benefits zingine, ppf wewe unakatwa 5% ya mshahara wakati ukiingia mpango wa nssf wewe utakatwa 10%.
 
FYI,
NSSF ina mafao mengi zaidi kuliko PPF; PPF huwezi kupata matibabu (health benefit) lakini NSSF utapata health benefit pamoja na maternity benefit kwa mkeo

NSSF ina matawi mengi mkoani in case ukastaafu mikoani si lazima ufuate mafao hadi Dar unlike PPF..

chungulia brochures za ppf na nssf ziko online linganisha mwenyewe
 
Asante sana wadau kwa ushauri wenu mzuri,.....King'asti, Kipanga kampiga mkoloni na topical......ushauri wenu nitauzingatia accordingly!
 
Mbwembwe za NSSF zinawakimbiza. HIvi kama mkeo hazai au hashiki mimba what will you do? JAMANI MWEEEE, PPF is the best GO for it.
 
NSSF kupata hicho kibinua mgongo ni ndoto! Nilishawasusiaga pensheni yangu, manake unaifukuzia kama unafukuzia mchumba wa JF!
 
Kwa usala wa mafao yako hamia NSSF. hujusikia professor anayechangia PPF akistaafu cummulative pension yake anazidiwana mwlimu wa shule ya msingi?. PPF ukiacha kazi kupata hela yako utatembea mpaka usamehe. Tumepambana nao wabadili kanuni ya kukokotoa mafao hawataki. Kwa sasa kuna mamlaka ya udhibiti imeundwa inaitwa SSRA wako katika mchakato wa kuhuisha hizi kanuni za mifuko ya pension. Lakini hii itachukua mda. Nakushauli uende NSSF maana sijasikia ikilalamikiwa kama PPF.
 
Kwa wanaojua kuhusu hii mifuko miwili ya jamii,ni mfuko upi bora hasa kwa mwaajiriwa mpya hasa PRIVATE SECTOR?
 
Kuna mtu anayefahamu fomula ya kukokotoa mafao kati ya PPF na NSSF
 
Wanakwambia siku kumi! Then ukienda wakwambia siku kumi tena! Mpaka sasa mwez wa tatu! Sielewiiiiiiiiiiiiiii!
 
NSSF kupata hicho kibinua mgongo ni ndoto! Nilishawasusiaga pensheni yangu, manake unaifukuzia kama unafukuzia mchumba wa JF!

Hawako mbali na LAPF, wanawalea wajiiri wasiopeleka michango hat zaidi ya mwaka! Mwajiri akisema ana financial crisis tu, wala hawamsumbui!
 
vp fao la kujitoa nssf? nampango wa kuacha kazi na kuwa mjasiliamali kuanzia january mwakani...ntapata fao langu baada ya mda gani?
 
NSSF niBora zaidi. Kwa nini? Wana mafao mengi kama walivyoeleza watu hapo juu..ina network kubwa kuliko mfuko wowote mwingine..kuhusu kuchangia sasa hivi sheria inaruhusu mwanachama kukatwa 5% au 10%. So it is your choice.

Nssf ina reserve ratio kubwa kuliko mfuko mwingine wowote mwingine afrika mashariki na kati...yaani hata watu wakiacha kuchangia leo 'as a worst case scenario' nssf inaweza kulipa mafao yake mfululizo kwa miaka 7. Lakihi pia ina actuarial surplus ya kuweza ku-usustain mpaka miaka 50 ijayo. (Wakati mfuko kama Pspf ina Aftuaria deficit hadi serikali imeamua kuikopa bn 50 kwa mwaka ili kulipa mafao....na haya ndiyo yanaelekea kwa LAPF na PPF)

Pia sasa hivi NSSF inaelekea kuwa Certified na ISO 9001:2008 ili kuboresha huduma zake ambazo kwa sasa zinasua sua. Ila kwa ninavyoijua ISO..hqikupatii certification mpaka uchange kweli kweli. Na mimi nategemea positives.

MWISHO: USidanganyike, mifuko mingine yooote inacopy na kupaste mambo ya NSSF. Kwa kifupi NSSF ni baba lao wengine wanafuata.
 
Mifuko yote inaharibiwa na Serikali na hakuna mfuko unaotoa mafao ya mhimu kama fao la kupoteza kazi. ukiajiriwa mwaka mmoja na ukapoteza kazi utasubiri ufikishe miaka 55 na hapo ndo utajuuta kuwajua NSSF watakaposema hawaoni michango yako wakati mwajiri kishasepa!! nasikia wanalazimisha kuipitisha sheria ya kukaa na pesa za watu hadi 55yrs.
 
Back
Top Bottom