Nssf/tra/wanasheria/wanajf; msaada katika hili!!!!

Speedo

Member
Feb 15, 2011
70
19
Mimi ni mwajiriwa katika kampuni moja jijini/mjini Arusha (jina kapuni), pamoja na wenzangu kama sita (6) hatujalipwa mishahara yetu tangu October 2010. Juzi (juma lililopita) tumelipwa mshahara wa mwezi mmoja tu tena umeandikwa ni wa January 2011.
Niliona ni vizuri kutafuta kazi nyingine wakati nasubiri kulipwa mshahara wangu mwingine uliobaki kwani tunaelezwa kuwa tutalipwa ila kwa sasa kampuni haina pesa.

Jana nimepokea statement yangu ya NSSF na kukuta kuwa michango yangu haijapelekwa tangu May 2010 - sijui kwa wenzangu.

Ninamkataba wangu wa ajira unaisha (expire) August 2011.

Wana JF naomba ushauri katika hili.
 
Aise pole sana ndugu yangu. Kimsingi mi navyojua unapaswa kulipwa mshahara wako kila mwezi na mwajiri anapaswa kupeleka mchango wako NSSF kila mwezi.

Kuhusu statement ya NSSF unatakiwa uinagalie vizuri kwani huwa wanachelewa kupdate hata kama michango ishapalekwa ila kama haijapelekwa kweli unapaswa kufika idara ya kazi watakusaidia kuongea na mwajiri apeleke lichango yako na akupe mishahara yako pia

Pia nakushauri ufikirie kupata kazi nyingine ambayo itakuwa na tija kwako

Pole sana once again
 
Toa taarifa NSSF watakwenda hapo mara moja na mambo itakuwa safi...
 
Toa taarifa NSSF watakwenda hapo mara moja na mambo itakuwa safi...

Asante kwa ushauri.
Hata hivyo naomba kufahamishwa kuhusu hili la kutokulipwa mshahara. Kuna mahali naweza kulichukulia kisheria zaidi au?

Hawa jamaa naamini watakuwa na makosa kibao km;
hawajalipa michango ya NSSF, hivyo hata kodi zingine km. SDL nawasiwasi hawajalipa. mishahara ya wafanyakazi wamechelewesha ila production bado inaendelea.

Kidogo tu tutasikia wameondoka nchini maana sio watanzania.
 
Back
Top Bottom