NSSF to erect ultra-modern multi-storey building in Nairobi

Mbona hawa NSSF hawajengi kwenye ile plot yao katika makutano ya Mtaa wa India na Azikiwe karibu na Haidary Plaza? nasikia mchoro ulikuwa tayari kabla ya Mustafa Mkullo kuachia ngazi pale. Nini kimemfanya Dau ashindwe kuingiza pesa sehemu nzuri ile ya biashara?
 
Ingekuwa vizuri, wadau wakaambiwa pia. Lakini faida hii huenda ikawa inawafaidia hao wanaofanya kazi huko nssf na si watanzania kwa ujumla.
je ni kweli hakuna nafasi ya kuwekeza hapa bongo mpaka waende kenya?? mfarakano wowote na nairobi inakuwaje????????? Nadhani ilihitaji kuangaliwa zaidi.
 
Hiyo ndo ajabu yenyewe! SI hivyo, NSSF wanawaibia sana wanachama wao, pamoja na uwekezaji huo feki (ulaji) utashangaa kuona faida wanayotoa kwa mtu mwenye michango ya milioni nane ni elfu 9 kwa mwaka.

Baba yangu ameamua kususia mafao ya NSSF baada ya kukuta akiba zake wakati anastaafu hazifiki hata laki 5 kwa miaka karibu 35 alofanya kazi (1966-2000)! Wakati anaanza kazi makato ya shs tano yalikuwa makubwa sana, leo NSSF wanamuhesabia shilingi tano ya 1966 kuwa sawa na shilingi tano ya mwaka 2000! Wizi mtupu!

NSSF wangeiga mfano wa PPF kwa kuwekeza kwenye nyumba za gharama nafuu ambazo wanawauzia wanachama wao kwa mkopo; huo ndo uwekezaji wenye akili wenye kumnufaisha mteja badala ya kujinufaisha wenyewe.


Kwa kweli huu ni wizi mtupu!
nadhani kuna haja ya wafanyakazi nasi kuanzisha movement ya kugomea pesa zetu kukatwa halafu zinaishai kusaidia wengine wasio husika, wafanyakazi tunaambualia patupu, hata walau wangetuanzishia mikopo nafuu!


Halafu ambalo huwa sielewi? watu gani wana qualify kwenda kukpoa huko NSSF? huwa nasikia tu wadiwa, walikopaje mbona huwa haijulikani ili nasi tukakope?
 
Poa tu, kuliko zile zilizipotea na Manji ya Quality Group!

Biashara ya real estate Nairobi inalipa kuliko Dar!

Nauliza: hivi Tz tuna vitega uchumi gani vingine Kenya?

Nashangaa kwa nini hatupeleki angalao bia ya safari Kenya ikashindane na Tusker? Jenog la ghorofa 26 downtown Nairobi ni mradi mzuri ingawa nina wasiwasi na 'political stability' ya Kenya kama itaweza kusustain 'economic achievement' ya nchi hiyo.

Chokochoko za kisiwa cha migingo peke yake zinaashiria machafuko katika nchi hiyo pindi Raila akibahatika kuiongoza Kenya na M7 akifanikiwa kutetea ufalme wake. Isitoshe uzoefu unaonyesha kuwa utawala wa falme nyingi duniani hauvuki miongo minne, sembuse M7? Nahisi anapalilia mwisho wa ufalme wake kwa kugombana na waJaluo kama Idd Amini alivyopalilia mwisho wake kwa kugombana na waTanzania...
 
You dont invest in a politically unstable country unless you are insane. all the odds will be against you. Period
 
Baba yangu ameamua kususia mafao ya NSSF baada ya kukuta akiba zake wakati anastaafu hazifiki hata laki 5 kwa miaka karibu 35 alofanya kazi (1966-2000)! Wakati anaanza kazi makato ya shs tano yalikuwa makubwa sana, leo NSSF wanamuhesabia shilingi tano ya 1966 kuwa sawa na shilingi tano ya mwaka 2000! Wizi mtupu!

Mkuu, nadhani hiyo ni challenge ya pension funds zote Tanzania. Basically, they are ought to adjust benefits to inflation level. However, one would argue, 'how can I do that while salaries are not adjusted to the same tune?' This is obviously lausible argument especially to Tanzanian environment. May be we bame the whole system, otherwise these Funds' will collapse.

NSSF wangeiga mfano wa PPF kwa kuwekeza kwenye nyumba za gharama nafuu ambazo wanawauzia wanachama wao kwa mkopo; huo ndo uwekezaji wenye akili wenye kumnufaisha mteja badala ya kujinufaisha wenyewe.

Nadhani NSSF walikuwa wakwanza kujenga nyumba za aina hiyo Kinyerezi. nasikia wanajenga tea Mtoni kijichi. Tatizo hizi nyumba sidhani kama zinastahiri kuitwa 'low cost housing' the costs are on the higher sider and the approach is not consistent with low cost housing scheme. however, they provide flexible payment arrangements.
 
Dar es Salaam, Nairobi, Kampala, Bujumbura na Kigali in some years to come will be just like Mwanza, Arusha etc. Hili hatuna nguvu ya kulizuia, kama sisi hatutapata bahati ya kuona hivyo basi vizazi vyetu vitayaona hayo. Eneo la Afrika Mashariki halitaweza kuvutia wakazi wake kiuchumi na kupata maendeleo kama litaendelea kuwa hivi kwa miaka mingine mingi ijayo.
Uwekezaji katika Kenya na Uganda hauwezi kuzuilika unless tuwaachie wakenya waendelee kukamata usukani. unapowekeza katika nchi nyingine ni wazi kuwa unapanua soko lako kwa kuongeza mapato.
Kwa mfano, katika kila nauli ya safari ya ndege ya Precision Air utayofanya ndani ya Tanzania, 49% ya faida huenda Kenya, maana halisi nchi ikiwekeza katika nchi nyingine inavuna na kupeleka nchini kwake faida inayopatikana.
Upande mwingine hebu angalia hii:
Makampuni yanayokuja kuwekeza hapa from SA karibuni yote yanaweka fedha zao katika benki za SA zilizopo hapa Tanzania, kwanini? Je kwa kufanya hivyo Tanzania kama nchi inafaidikaje na uwekezaji huo as far as benki ambazo si za SA zinahusika?
Nakubaliana na mchangiaji mmoja hapo juu kuwa NBC na CRDB zilipaswa kuwa zimewekeza ndani Kenya ama Uganda. Uwekezaji wa NSSF utasaidia Benki zetu nazo kuvuka mpaka kwani mteja/wateja wakuanzia wa uhakika watakuwepo na hatimaye kuimarisha vitega uchumi vingine.
Ni wazo zuri la uwekezaji wa NSSF
 
Back
Top Bottom