NSSF... Sikujua kama Shirika hili lipo hivi!!!!!

Hapo pamejaa udini balaa, na kama we ni 'kafir' ndo utaipatapata!.
 
Yaani inaudhi sana lazima ifikie mahali useme yatosha. Mimi minaushahidi wakusumbuliwa na Tanesco wakitaka kula rushwa kunipa haki yangu lakini moyoni nilishaahidi lazima wanipe haki yangu bila malipo. nilipoona Longo Longo nyingi niliwapa dead line baada ya hapo ningepeleka madai yangu vyombo vya juu hata ikinigharimu. Nakuambia siku hiyo hiyo walinishughulikia. Lazina ifike wakati tuichukie rushwa tusiendelee kuipalilia.
 
wasikuzingue nenda makao makuu watu wa pale wamestaarabika ingawa kuna mapepe wachache pia ikiwezekana watoe kwenye vyombo vya habari ingawa vingi huwa haviripoti kwa kuogopa kukosa matangazo kitu kingine wakikulipa hakikisha wanakulipa na riba yako ambayo ni1.8% kwa mwaka mara nyingi huwa wanapiga watu bao
 
Wewe kama wanakuomba rushwa waambie sawa, nenda Takukuru watakupa njia za kufanya kuwanasa hao waomba rushwa.

Tatizo ukienda takukuru wakakupa maelekezo wanawapigia simu nssf na kuwaeleza tumewawekea mtego tunakuja nchi hii imeshaaribika
 
Tanzania bila rushwa haiwezekani,kuwakomesha hao wafanyakazi wasio waaminifu mchukue mwanasheria wako,ndugu yako kama shahidi na askari m1 ndio muende takukuru kutoa taarifa!!! Siri ikivuja mnawafungulia kesi takukuru,mnachunguza simu zote zilizoingia kutoka takukuru na zilizoingia nssf.
 
Tatizo ukienda takukuru wakakupa maelekezo wanawapigia simu nssf na kuwaeleza tumewawekea mtego tunakuja nchi hii imeshaaribika

Usikate tamaa kabla hujafanya hiyo si sawa. Fanya kwanza halafu ndio useme kuwa imekuwa hivyo.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom