Wanaforum kuna hii kitu inaniumziga kichwa kuhusu hawa ppf na nssf ni kwa nini wanashindwa kutoa mikopo kwa wanachama wake na badala yake wanakazi ya kutoa mikopo kwa serikali na wafanyabiashara wakubwa huku ikiwaacha wanachama wake wakiwa masikini.na wengi wao masikini ya mungu hawana sifa ya kupata mikopo kwenye mabenki.kwa mfn unakuta anamichango yake nssf au ppf nk ml 7 kwanini huyu mtu asiitumie hiyo pesa yake kama dhamani akaweza kupata mkopo kwny mfuko husika akafungua hata biashara ambayo itakuwa msaidia kuongeza kipato chake hapo ndiyo ile kauli ya tuna ya jenga maisha yako ya baadaye ita leta maana.maisha ya uzeeni yana jengwa ujanani.maana tunaona hao waliostafu jinsi wanavyo taabika