NSSF na Infrastructure Investment: Kigamboni Bridge, IPP, Road Construction.. ???

Mdondoaji mkuu wangu, kwa nini nichangie pesa zangu kwenye mfuko kwa lazima na sina access nao?
 
Mzee Mwanakijiji,

Nimezisoma zote hizo mbili za mwanzo kwakweli hakuna cha muhimu kilichozungumziwa zaidi ya siasa tu. Kama alivyosema Gurudumu at least hii ya mwisho ya Pension Watch imezungumzia zaidi but haijachambua vya kutosha kwani Pension funds and Other thrift institutions zimekuwa zikijiingiza si tu katika infrastructure bali hata kwenye financial markets particularly kuwekeza katika makampuni makubwa kwa kununua shares na kukopesha kwenye bond markets.

Tuje katika madai ya kwamba hakuna misingi ya kuregulate hizi thrift institution hilo sio kweli na infact mnaosema hili hamjafanya your homework vizuri. Banking and Financial Institution Act ya mwaka 1991 ilikuja kufungua mianja ya sekta ya fedha na ikaweka misingi ya vp hiyo sekta iendeshwe. Vile vile Bank of Tanzania Act ya mwaka 1995 iliweka misingi ya vipi hizi sekta za fedha ziwe zinasimamiwa. Pia katika industry husika (social security) kuna Act mbali mbali zilianisha utaratibu wa kuendeshwa kwa hizo sekta. National Provident Fund of 1964 amended in by the Nationa Social Security Act of 1997, Parastatal Pension Fund of 1978 , Public Services Retirement Benefit Act of 1999 and National Health Insurance Act of 1999 na LAPF Act of 2000. Hivyo wanandugu framework zipo na zimekaa vizuri kwani mfumo wake hauna tofauti sana na uliopo katika nchi za Marekani na UK.

Kuhusu lack of regulator of these pension funds and insurance companies at the moment Bank of Tanzania ndio msimamizi wao mkuu but serikali iko katika mchakato wa kuanzisha hilo nadhani walianzisha Social Security Regulatory Authority Act 2008 . Nadhani mwaka jana walikuwa wako mbioni kwani walikuwa wanatafuta Director General wa Regulator. Nakumbuka tarehe 2 January 2011 walitangaza kuwa itakuwa operational this September 2011. Kwahivyo serikali inajiandaa kulitekeleza hilo but Bank of Tanzania still ina perform function ya kuregulate.

Ijapokuwa hiyo Authority haijawa operational hakumaanishi ya kwamba hizi Thrift institutions zisijipanue. Basle 2 ilipokuja iliweka kiwango cha mwisho hizi financial institutions zinatakiwa ziwe na pesa katika balance sheet zao ili kuziwezesha ziweze kuwekeza katika sekta mbali mbali. Hili lilifanywa kwasababu ilionekana hizi institutions zinahela nyingi but zimebanwa mno na usimamizi. Ndio maana ukaona PPF, NSSF zikaanza kujitanua kuwekeza katika majengo na sekta zenginezo. Nia na madhumuni kwanza kupunguza hizi institutions kukaa na pesa nyingi katika mifuko yao (kitu kinachoweza kuchochea ufisadi na mifano ipo kuna thread humu DG wa PPF anatuhumiwa kuiba milioni 500 unadhani chanzo kikuu nini?) , Pili hizi sekta zikikaa na pesa nyingi zinakuwa hazitanuki kimaendeleo na matokeo ni kuwa poor services na kadhalika. Tatu zikitanuka zinachochea maendeleo katika jamii.

Sio kila kitu waungwana muweke conspiracy theory kuna vitu vengine acheni taaluma za watu zifanye kazi zao kwani wanajua wanachokifanya. Moja ya watu wanaojua nini wanafanya ni Dr Dau and I support him kwani it makes sense anachokifanya sio yule anayepita akihonga akina mama na kuzila pesa hovyo!!!!

Mkuu mdondoaji, inawezekana unayosema ni sahihi lakini naomba uniruhusu nisikubaliane na wewe bila kutoa sababu tu sina muda wa kubandika bandua sasa hivi. Lala salama mkuu
 
Mkuu, wamesema wataweka vituo vya kukusanya pesa kwenye barabara mpaka pesa zao zitakaporudi then wanakabidhi barabra hiyo kwa serikali. Kwahiyo ukipita na gari lako sehemu watakakojenga barabra unalipia.

Wakiwakopesha serikali ni wazo zuri ila wakiendesha wao wenyewe mh nadhani ni akili za unazi una hakika na hizi taarifa maana navyojua mie NSSF wanawajengea serikali hivyo ni mkopo wa masharti nafuu kwa serikali. Maana sijui wanacharge bei gani maana wakicharge 10,000 kwa kila gari nadhani nitaliweka limkweche wangu ndani na kutembea kwa miguu ninakotaka kuenda haina maana.
 
Mdondoaji mkuu wangu, kwa nini nichangie pesa zangu kwenye mfuko kwa lazima na sina access nao?

Mkuu,

Unapoumia na kupata ajali ukalipwa je huoni kuna faida pale. Vile vile unapotibiwa kama una bima ya afya je zile pesa zinatoka wapi?
 
Kwa kiwango kukubwa sana nakubaliana na Mwanakijiji katika hili.

Ingawa, kunaweza kuwepo utetezi wa kusema wanaepuka hasara ya ‘Mayai mengi kwenye kapu moja”; kasi na kiwango cha uwekezaji huu wa mtapakao (diversification) unaofanywa na NSSF sasa nashauri uangaliwe kwa umakini sana.
Madhara ya mtapakao unaokithiri kiuchumi na kihuduma huwa ni kuanza kutoa bidhaa au huduma hafifu na wakati mwingine hasara ya miradi mingine kuanza kuathiri maendeleo ya miradi mingine hasa shughuli ya msingi ya kutoa huduma za hifadhi kwa Wananchi.

Aidha, nashauri badala ya kujiingiza katika ujenzi, uzalishaji wa umeme (maendeo wasiyo na uzoefu nayo) n.k warejee kibarua chao ambacho hawajakifikisha tunapotaka, hivyo ,

1. WAENDELEE KUTANGAZA KWA KUELEZA KINAGAUBAGA (bila kumungúnya maneno) MAANA NA NAMNA UTOLEWAJI WA MAFAO YAO MENGINE MF. YA AJALI, UZAZI, MAZISHI, ULEMAVU N.K

2. WATANUWE WIGO WA HUDUMA YA MAFAO YA UZEENI (PENSION) IWE KWA WATUMISHI WOTE WA NGAZI ZOTE WA UMMA NA SEKTA BINAFSI. KWA NINI WENGI WALIPWE KAFUNGU KANAKOISHA BAADA YA MUDA MFUPI WAKATI KUNA KUNDI KA WATEULE WACHACHE WANALIPWA MPAKA KUFA BAADA YA KUSTAAFU?

3. KAMA UWEZO UNARUHUSU, KWA NINI MSIANZE KUSAIDIA (HATA KWA KIWANGO KIDOGO) MAELFU YA WATANZANIA WENYE UMASKINI ULIOKITHIRI AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE (MF. KUTOKANA NA ULEMAVU ULIOKITHIRI N.K) WAMESHINDWA KUFANYA KAZI YA KUJIPATIA KIPATO?
 
Unajua kilichoua Tanzania Housing Bank? Unajua kilichotaka kuiua NBC mpaka ikawa split into Two? Hao international consultancies wanaokuja kufanya utafiti wengi wanaogopa kusema ila ndio linalochangia kufa kwa financial institutions nyingi nalo ni ufisadi na kukosekana kwa uwajibikaji kwenye Bank na Financial Institutions. Umesahau lile scandal la Mkulo pale NSSF? Sasa hivi tuna Scandal ya Erio sijui Urio wa PPF yote inachangiwa na systemic risk iliyopo katika financial institutions ambayo ni bad governance.

Tunatakiwa kuamini kuwa NSSF itakuwa na good governance muda wote? Ni kitu gani kitazuia wanasiasa kuingilia kati mambo ya NSSF either kwa uteuzi unaofanywa na Rais au teuzi zinazofanywa na Waziri?
 
Tunatakiwa kuamini kuwa NSSF itakuwa na good governance muda wote? Ni kitu gani kitazuia wanasiasa kuingilia kati mambo ya NSSF either kwa uteuzi unaofanywa na Rais au teuzi zinazofanywa na Waziri?

Kwa Tanzania hii tuliyoitengeneza, lazima tutatengeneza kashfa kubwa sana kutokana na hizi projects. Kwa bahati mbaya hata haya majengo yaliyojengwa kuna baadhi yalihusishwa na rushwa kubwa tu kwenye awards za makandarasi mpaka zikatenguliwa. Sasa leo hii nini kimebadilika kuondoa mfumo uliokuwepo?
 
Being a specialist in electricity sector...I will speak only of their move to generate as IPP...

they initially engaged non engineers to design project just because they sawa power generation deficit...
After I had a chance to see the proposal...oh! Salale!

Do you mind sharing with us exactly who or what these "non-engineers" might be?
 
MMKJJ: Mimi nimtaalam katika nyanja ya Investments tena katika miradi mikubwa ya maendeleo, tume-outsource na ku-plan miradi mikubwa sana EU, Middle east na UK kwa kifupi hapa umegusa eneo langu la kujidai.

Ila sitaweza kuongelea hili la NSSF kiufasaha zaidi mpaka tupate vitu muhimu vitatu (3)


  1. "Project Appraisal"; Hapa tutajua huo mradi hasa wa Barabara na Madaraja inategemea nini katika kurudisha fedha zinazochotwa NNSF, maana mradi unaofadhiliwa laziwa uwe na-return wenyewe kama mradi kama hauwezi ni batiri na wizi wa mchana maana hizo fedha haziwe kurudi, kama wamekosa leo na hawaonyeshi kesho watapata vipi unaamini vipi kuwa kesho watapata, kinacho-wafanya wakose leo ndio kitawanya wakose pia kesho; siyo kusema kuwa wewe fadhili tu nitakulipa fedha zako bila mradi kujionyesha kuwa unaweza kurudisha fedha wenyewe na kwa muda muhafaka.
  2. "Feasibility Study"; Hapa tutajua kitu muhimu sana, mradi unasukumwa na utashi gani? Utashi wa siasa? Utashi wa mahitaji ya Umma yaani ndio First Priority problem ya wenye fedha na Umma unaowazunguka? ndipo linapokuja suala unalosema kuwa kwanini wasiwekeze katika labda kusomesha watoto wa wanachama, au Hospital, au Nyumba za wanachama wake kwa bei nafuu nk, study lazima iwe imeenda mbali kiasi cha kuonyesha hasara gani watapata wanachama iwapo fedha zitachewa kurudishwa kwa mwaka mmoja, miwili nakuendela, Study pia lazima iseme miradi itasimamiwa vipi na itakarabatiwa vipi, mara nyingine study inaweza kumtaka mkopeshwaji kuweka Bima ya Mradi na pia kama wanachama walishirikiswa maana hata hata ni Nchni hisiyo na sheria lazima wanachama washirikiswe iliuwe mradi endelevu maana inaweza kuanzisha migomo ya wanachama kutaka kujito nk nk
  3. Mkataba kati ya Serikali na NSSF; Lazima uwepo, uonyeshe wanategemea kutumia kiasi gani na ni % ngapi ya mapatato yao, jinsi ya kurudisha fedha,nini nia ya serikali katika kushirikisha hilo shirika katika hiyo miradi (Kwanini imechaguliwa Particularly Mradi A nasio H; kwanini wasijenge Lindi na ikawa Tanga na serikali imeweka wapi wakati huo, ni kama nipe nikupe; kuwa wewe nunua mboga mi nitanunua ugali; nk

Tukipata angalao hizo nyaraka tatu tutaweza kujua kilichomo na kuchangia vyema zaidi, ila kwa haraka haraka kutokana na Taaarifa ulizotoa hapa mi naona matatizo makubwa manne (4)

  • NSSF Haiwezi kuwekeza Katika miradi chini ya PPP, kwasababu hizi fedha ni za Security ya Wafanyakazi, na NSSF siyo Private Partiner kwa Serikali. ni Kama serikali inataka kukopa fedha za Wafanyakazi bila ridhaa yao, Risk yake ni hatari sana, Tunaaamini katika kugawana Risk kati ya Umma na Wafanyabiashara (Private); ni vyema kila mtu akajua NSSF siyo Private Entity ya kufanyabiashara, hakuna watu wamewekeza mitaji yao pale nakukubaliana na Risk za Biashara, Makampuni Makubwa ya Ulaya na USA yaliyofirisika mwaka Jana na Juzi Sharers walikubali kwasababu ndio biashara, wao kwa utashi wao waliwekeza mitaji yao kwa ajili ya biashara, sasa hapa Risk yote ya Biashara inabebeshwa Umma, kwa maana ya Wafanyakazi kama hizo fedha zikipotelea huko watakaoteseka ni Umma pengine Umma wa wanyonge peke yako, Kwahiyo Kitaalaam tunashauri Risk kama hiyo ingelibebeshwa Makampuni ya Ushafirishaji na Watumiaji wa Barabara kwa maana wao ndio Malory yao yanaaribu barabara na pengine labda watakuwa na uchungu na Barabara wasi-overload kwasababu ni fedha zao; ukishaona kitu kinafanywa kwa fedha za Umma alafu kikapewa jina Investment huo ni Uongo, hamna Investment hapo utaperi mkubwa, Investment maana yake kuna -analysis ya kitaalam imefanywa na biashara imeoneka inalipa kweli kweli utaona wanakuja wawekeza wanawekeza Mitaji yao hiyo ndio investment, mbona hawakupewa kuchimba madini ambacho nadhani kila mwanachama angerukaruka juu kama angesikia hivyo.
  • Uchumi wa Tanzania bado haujaruhusu Barabara kuwa kitega uchumi (Investment), watu wameandika nadharia nyingi humu bila kuja kila nadharai ina-sehemu na wakati wake, Bado hatujawa na Uchumi wa barabara za kulipia sasa hivi tunapoogea hapa EU na UK wanafikia kuzipunguza mara dufu hadi zisiwepo kabisa kwasababu ya kuyumba kwa uchumi, hatazinapolipiwa hakuna mahala popote hizo fedha zimewai kukidhi gharama za mradi na matengenezo duniani kote hakuna, sasa hivi wenzetu wanakuja na malipo mengine Slaili siyo kupita tu kwenye barabara ulipie, Kama barabara ingeliwa ni Kitega Uchumi tokea zimeanza kujengwa sasa tungeliwa tumekusanya fedha nyingi sana, tafiti zinaonyesha reli inaweza kurudisha fedha ya Ujenzi baada ya miaka 30 hadi 40 siyo barabara, hazijawai kurudisha.
  • Nadhalia ya kuwekeza kupitia Private Partner imejikita katika wafanyabiasha wakubwa ambao biashara zao zinategemea miradi husika, mfano Barabara hapa Tanzania Parner mzuri sasa hivi alipaswa kuwa Barrick na wachimbaji wa madini maana usafirishaji wao mkubwa wa mizigo nk unategemea barabara, siyo Umma, kuchukua fedha NSSF kujengea Daraja haina tofauti na kuchukua fedha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi kujengea barabara eti kwakuwa labda mwaka huo hawajakopesha wanafunzi wengi, hiyo hairuhusiwi hata kidogo maana hilo sio jukumu lao, kama sijasahau hicho ndicho kilicho uwa mashika yote ya Umma kama UFI, MWATEX, URAFIKI by then nk, huwezi kushindwa huku badala ya kuboresha unaficha mapungufu, NSSF wao wanatakiwa kuhakikisha wanachama wananeemeka kama fedha zipo; Mara mia hiyo kazi ingefanywa na Mabenki
  • Hayo mashirika yakiruhusu hivyo ndio chanzo cha kuanza kunyanyasa wanachama na kuwawekea sheria ngumu za michango na mlolongo mrefu wa kulipwa Pensheni ili waandelee kuwa na fedha za kutosha kufanyia biashara, tutakapoona huo mkataba tutajua mwanachama wakawaida ameshirikiswa vipi, lakini kitaalam NSSF walipaswa kujikita katika miradi ya maendeleo ya wanachama wake kielimu, kiafya, kimakazi, kiuchumi nk, kuna Road Fund wanafanya nini au aina wataalam wao ndio wanajukunu la kutafuta fedha za Barabara si NSSF; Tanzania kuna kuna source nyingi ya fedha za Barabara mpaka nashaangaa wanipe hiyo Road Fund Miaka Mitano fedha za Barabara zitakuwa historia, huwezi kujenga nchni na fedha ambazo hazipo kwenye bajeti ukapata uchumi imara hamna, hakuna strategy ndio maana mambo shangla bagla.

Njia za kupata fedha za barabara ni nyingi sana, Road Fund sijui anayo nani huyo yeye haoni haibu kubebesha NSSF mzigo wa bomu ili-ife.
 
How? You'd better tell us specifically and in a detailed manner why you think this particular document is relevant to this discussion.

specifically naweza in detail nitakuwa naandika thesis; Pension Watch inahusiana na mipango ya nchi mbalimbali zilizoendelea kutumia social security funds kuwekeza katika miradi mikubwa ya miundo mbinu. NSSF ni social security fund na inataka kuwekeza katika miradi mikubwa ya miundombinu katika nchi isiyoendelea kama ya kwetu.
 
MMKJJ: Mimi nimtaalam katika nyanja ya Investments tena katika miradi mikubwa ya maendeleo, tume-outsource na ku-plan miradi mikubwa sana EU, Middle east na UK kwa kifupi hapa umegusa eneo langu la kujidai.



Arafat asante sana maana hapa umechangia mawazo muhimu sana na umenisaidia sana kufikiri maana nilikuwa naona hiki kitu kama instinct zangu tu bila kuwa na rational argument either way. Ngoja tuone kama tunaweza kupata taarifa zaidi nitaweka kwenye post ya kwanza.
 
Arafat asante sana maana hapa umechangia mawazo muhimu sana na umenisaidia sana kufikiri maana nilikuwa naona hiki kitu kama instinct zangu tu bila kuwa na rational argument either way. Ngoja tuone kama tunaweza kupata taarifa zaidi nitaweka kwenye post ya kwanza.

Jitahidi uipate mi najua barabara haziwezi kurudisha fedha, sijui kama ipo report kama hiyo, We jaribu kufanya utafiti mdogo sijui kama watakupa data, angalia barabara zote zilizojengwa kati ya miaka miwili na mitano iliyopita, hata kama wewe siyo mtaalam angalia zina hali gani (Kwa maana ya uchakavu), alafu tafuta gharama za ukarabati (Maintenance costs) ambazo zimewai kutumika mara baada ya ujenzi mpaka sasa utapata jibu rahisi MMKJJ; alafu jiulize maswali madogo wewe mwenye ukiwa palepale barabarani mara baada ya kupita magari kama kumi, jiulize kama kuna kitu hiyo barabara imechangia kwenye uchumi wetu alafu kitafutie thamani yake then pili jiulize hivi kweli hiyo barabara ita-dumu miaka 3 ijayo? utapata picha kuwa haziwezi kuwa-reliable investment na mara nyingi ni Service inayotakiwa itolewe na Serikali na michango ya wafanyabiashara kama barabara husika sio equitable kwa Umma bali kwa ajili yao wao wafanyabiashara, ndipo dhana ya PPP inapokuja.
 
Arafat.. umenifanya nijiulize.. wakishajenga hizo barabara za kulipia, watu hawatatafuta njia za mkato?
 
NSSF wameshindwa kulipa watu wao mpaka leo, my mother ambae amefanyia kazi serikali for over 20 years hajapata cheki tangu 2008 kisa file limepotea.

Badala ya hawa kuwekeza kwenye hizi big projects ambazo hakuna true analysis ambayo inayoonyesha how they will get their money back, why wasiwekeze kwenye system ambayo itawezesha smooth payments?

Ujenzi wa Daraja la kigamboni unategemea kurudisha pesa through toll payments, ambazo hakuna feasible analysis ambayo inaonyesha ni kwa muda gani NSSF wata brake even? This are massive Capex investments, na ni bora ukawekwa mchakato wa kukutengeza pesa. Kama kuongeza kodi za majengo kwa kila jengo litakalo jengwa Kigamobi kwa muda fulani. Huwezi kutegemea toll payments wakati over 80% ya wananchi wako ni masikini wa kufa. The only way forward ni kuzi tax massively business ambazo zitawekeza kigamboni area, madhara yake ni kwamba business hizo zitakimbia. So, the best approach kwa hili daraja ni serikali kuwekeza na sio vinginevyo. Au uwepo mchakato mzima wa kushare cost katika swala zima la ujenzi.

Mimi ninacho hofia ni kwa NSSF kujiingiza kwenye plan ambazo ni controversial, Tanesco is a dying organization jee ni kwa nini mnaingia mkataba na kampuni inayokufa? Who guarantee stakeholders hapa? Serikali will pick slacks kama Tanesco itashindwa kusuport mkataba mzima?
 
bado tungoje tu utasikia shirika la Ndege linataka kuchukuliwa na NSSF, another CCM tricks to 2015 uchaguzi...Subirini na hapo utasikia UFISADI umetokea... mtakuja niambia jamni...
 
Wakiwakopesha serikali ni wazo zuri ila wakiendesha wao wenyewe mh nadhani ni akili za unazi una hakika na hizi taarifa maana navyojua mie NSSF wanawajengea serikali hivyo ni mkopo wa masharti nafuu kwa serikali. Maana sijui wanacharge bei gani maana wakicharge 10,000 kwa kila gari nadhani nitaliweka limkweche wangu ndani na kutembea kwa miguu ninakotaka kuenda haina maana.

Mkuu, kauli ya serikal kwamba daraja la Kigamboni litalipiwa na wenye magari lipo kwenye hansard ya bunge na halijatolewa lingine tofauti. Kwa nini wenye magari wanaoishi Kigamboni pekee katika hii nchi ndio walipie daraja. Lile la BMkapa mbona halilipiwi? Lile la salenda mbona halilipiwi? Madaraja yote nchini mbona hayakipiwi?

Kila mwenye gari nchi hii analipa kodi. Kwenye mafuta, vipuri, leseni ya barabara, kuandikisha gari, kodi ya kuagiza gari nje ya nchi, kodi ya kuuziana gari, n.k. Pia wanalipa faini mbalimbali za usalama barabarani. Tunaambiwa hizi pesa zote ni kwa ajili ya kujenga na kutunza miundombinu. Kwa nini wakazi wa kigamboni walipie daraja?

Kwa mujibu wa hansard, serikali ya Uholanzi walitoa walichangia mbili ya tatu ya ujenzi wa daraja la Kigamboni. Hizi pesa zilikpelekwa wapi? Kuna wakati serikali ya uholanzi walilalamikia serikali kwamba wanachelewesha mambo. Nani alichelewesha na kwa nini? Kwa nini serikali haikutumia pesa za msaada za uholanzi badala yake wanasukumia hili jambo NSSF na kulazimisha wananchi walipe?

Kama wananchi watalipa hili daraja maana yake ni wao ndio wamelijenga, ni Mali yao siyo serikali. Kwa mantiki hiyo wenye mali hawa ndio wanaotakiwa kukaa na kuamua usanifu na gharama ya kujenga daraja lao, siyo serikali. Kwa nini serikali ndo inayofanya hiyo kazi? Na kwa nini serikali imeweka mizengwe na ukiritimba? Hakuna rushwa na ufisadi?

Mwisho, gharama ya kujenga hili daraja ni bilioni 91, kwa mujibu wa tathmini ya NSSF Kama ilivotolewa na serikali bungeni. Malipo ya tuzo ya Dowani ni bilioni 95. Serikali imekuwa ikitudanganya kwamba inakusudia kujenga daraja hili tangu 2000. Daraja litatumika na watz na litakuza uchumi wa tz. Tuzo ya Dowani siyo ya watz na haitakuza uchumi wa tz. Ni vigezo gani vilivyotumika kuamua malipo ya Dowani ni muhimu kuliko maisha na uchumi wa watz wa Kigamboni?
 
Mnajua kuna mambo mengine yakitamkwa kwa mbwembwe mara nyingi, watu huamini. Hebu fikiria practical aspect ya ada ya daraja la Kigamboni.

Kwanza magari yote ya serikali yatakuwa yanapita bure. Matajiri wote watapata kibali cha kupita bure kutoka kwa mkubwa huko juu. Magari binafsi ya wanasiasa wengi watakuwa wanapora bure. Asilimia kubwa ya wenye magari Kigamboni inajumuisha maafisa wa serikali, wanajeshi, polisi, usalama wa taifa, wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa. Kumbe mzigo wa kujenga daraja utakuwa mabegani mwa watu wa kawaida ambao siyo wengi sana. Hii ni haki? Watamaliza kulipa Hilo deni lini? Kwa nini wasipewe wao wajenge na kusimamia mapato ya hilo daraja? Ndiyo, kwa mantiki wao ndio wanaostahili kulimiliki!

Sasa hivi wananchi wakiuliza mapato na matumizi ya kivuli hawapewi. Wanakusanya mania ya milioni kila siku lakini hawatujengei daraja? Watupe mapato na matumizi ya kivuko kwanza. Pengine mapato ya kivuko kwa mwezi pekee yanatosha kujenga daraja la Kigamboni!

Haya, historia imewahi kubadilika? Nipeni majibu kuhusu ukusanyaji mapato ya Soko la kariakoo, ubungo bus terminal, magogoni international ferry market, machinga complex, n.k. Wananchi wana sauti kiasi gani? Ufisadi kiasi gani? Je, faini za usalama barabarani zinakusanywa stahili? Polisi wana vitabu vyao vya risiti, wanachukua rushwa badala ya kutoza fauni. TRA wanakusanyia kodi mifukoni mwao badala ya mfuko wa hazina.

Bottom line, huu ni mkakati kifisadi na kwa mantiki ya maelezo yangu hapo juu, hili daraja halitawahi kumaliza kurudisha gharama kutokana na bridge toll. Maisha!
 
naona unaelekea kile kilicho nyuma ya swali langu.. thanks.. Kwanini NSSF ionakane kuwa itaweza kufanya yale ambayo Serikali ya CCM imeshindwa kufanya? Hivi NSSF ikipewa Bandari, ATCL, Tanesco.. itashangaza..? Something is not right.. ! Tatizo siyo NSSF kuwekeza tatizo ni kwanini wanaamini NSSF itafanikiwa pale ambapo TANROADS imeshindwa, pale ambapo TANESCO imeshindwa n.k Yawezekana NSSF ina fedha zaidi kuliko serikali?

MMKJ labda maswali mengine ya msingi ya kujiuliza ni kuwa:

Ni nini hasa jukumu la msingi la NSSF na pension funds nyingine?

Je wamefanikiwa kwa kiwango gani kutimiza kwa ufanisi majukumu yao ya msingi waliyoanzishwa kuyatekeleza kisheria? Yaani kuwalipa wastaafu pension inayokidhi ongezeko la gharama za maisha linalotokana na mfumko wa bei.

Je ujenzi wa miundombinu utachangia vipi ama kufanikisha au kuzorotesha uwezo wa NSSF kutimiza majukumu yake ya msingi?

Je ni kweli kuwa NSSF wana uwezo wa kitaalamu wa kubuni, kujenga na kusimamia miradi mikubwa ya miundombinu ambayo wanapanga kuijenga kuliko vyombo ambavyo tayari vipo kwa ajili hiyo? yaani TANROADS, TPDC etc.
 
Tunatakiwa kuamini kuwa NSSF itakuwa na good governance muda wote? Ni kitu gani kitazuia wanasiasa kuingilia kati mambo ya NSSF either kwa uteuzi unaofanywa na Rais au teuzi zinazofanywa na Waziri?

Bado tunakumbuka kashfa ya Manji na NSSF kwenye jengo la Quality Plaza. Kwa bahati mbaya hawahawa wanaotuambia habari za miradi mikubwa inayokuja ndiyo walewale walioshiriki kwenye kashfa ya Quality Plaza. Ni nini kitakachowazuia safari hii wasiingie kwenye ufisadi mwingine?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom