Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,534
- 8,619
NImeanza kuangalia hapa (ndani ya siku hizi chache zilizopita) na ninaanza kuona tatizo mahali fulani; japo kwa juu inaonekana vizuri sana lakini naanza kuhofia na ninashindwa kuelewa kwanini NSSF inawekeza fedha za wafanyakazi wake kwenye miradi hii mikubwa ya Umeme, Ujenzi wa Madaraja na sasa Ujenzi wa Barabara.
Kuna kitu hakiko sahihi; nia yaweza kuwa nzuri lakini kuna kitu hakiko sahihi... sijui ni kitu gani bado.. lakini something is very very wrong somewhere..
Miradi mingine wanayobuni NSSF ni mizuri lakini kama watategemea kwa asilimia 100% serikali katika uwekezaji wake ...ikishindwa kuwalipa basi pesa za wafanyakazi zitakuwa hatarini..mfano mashirika haya yamewekeza sana UDOM ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa inayalipa haya mashirika marejesho kwa wakati...
Nashauri miradi ya barabara ...ie interchanges ,flyovers etc...NSSF Wakishirikiana na mashirika mengine yafanye hivi....
- Yapewe na wizara ya ardhi maeno makubwa ..amabayo watayaendeleza kama satelite cities....na hizo bara bara wajenge kuhakikisha maeneo watakayowekeza kwa makazi na viwanda....yana miondo mbinu ya uhakika.....wakaazi watakao chagua kuishi kwenye maeno hayo ..they have to pay road toll...au watakaopenda kutumia .....ni biashara ya uhakika...lakini kujenga na kuwapa serikali itakuwa haina impact.....we need have TOLL ROAD AUTHORITY...
-Njia nyingine ni kuwekeza kwenye highways ...mfano tumegundua we have only one road exit in north from dar..and another ipo south[kilwa road]...tutakuwa na nyingine bagamoyo karibuni.......that has to be under toll road ---PPP.
NSSF wanaweza kujenga njia nyingine alternative ya kutoka AIRPORT hadi MBEZI....HADI chalinze ..inayojitegemea hiyo iwe EXPRESS CARRIAGE HIGHWAY....mtu ambaye ana pesa yake na anaona njia ya ubungo inamchelewesha kuingia au kutoka dar.....simply anaingia kwenye NSSF carriage way...analipa anaambaa zake ..simple....
Mradi wa umeme hauwafai NSSF ...kwani sheria bado inaweka wazi muendeshaji ni TANESCO ...isitoshe hao TANESCO walipewa 100 bilioni..syndicate loans na mabenki na wakashindwa kulipa...so ni risk kuingiza pesa za wafanyakazi kwenye mradi wa umeme ..pia sababu kubwa ni kuwa NSSF Ni wazuri kwenye uwekezaji wa properties na ndio maana hata barabara wakiwekeza kwa mfumo huo hakuna neno....kujipeleka kwenye umeme ni kwenda mbali sana nje ya uwekezaji wao wa kawaida ...hawana uzoefu..kabisa!!..na sio vizuri kwenda nje sana na uzoefu kwenye biashara!!