NSSF kutumia Tsh 400 bil kuzalisha megawati 300: Yajitahidi kuchukua KIWIRA

..Ni mwendelezo tu wa Kumsaidia 'aliyeshindwa'..hatari tu ni kuwa katika kumsaidia hivyo..wanajisaidia wao kwa wao..na hivyo ni mwendelezo wa ufisadi mkubwa zaidi..naogopa sana vijana kama kina Zitto wanapoendelea kutumiwa katika 'deal' kama hizo kuzipigia chapuo n.k..poor my country Tanzania!..
 
Natanguliza heshima katika jukwaa hili. Tangu niingie JF sijawahi kuchangia katika jukwaa hili kwa sababu naliheshimu sana, kwa uhalisia wake...lakini naomba kutoa mchango kutokana na ushahidi wa kimazingira si tu juu ya NSSF na Kiwira bali NSSF na uwekezaji mkubwa ambao imekuwa ikijihusisha nao kwa kipindi hiki cha serikali ya awamu hii.

-Ujenzi wa Majengo ya UDOM. Uwekezaji mkubwa sana.
-Ujenzi wa Daraja la Kigamboni
-Ujenzi wa........
-Ujenzi wa........
-Ujenzi wa........

Kuna tetesi ambaz mimi binafsi naziamini kuwa kuna urafiki wa karibu kati ya JK na Dkt. Ramadhan Dau, MKUU wa NSSF. Sitaki kuwa moved na hisia zaidi badala ya reasoning lakini siwezi kuamini kama urafiki wa umejengeka katika 'Upwani' au vitu vingine, naomba kuamini ni urafiki basi...

Wakati fulani kulikuwa na move moja ambayo naona inaendelea chini chini, kumwondoa Hally Kitilya pale TRA. Wakati fulani move ilikuwa ikamilike kisha mamlka hiyo akabidhiwe Dkt. Dau, hoja za kuondolewa Kitilya hazikuwa kushindwa katika majukumu yake.....baadae ikawa kama vile imeshtukiwa lakini najua inaendelea chini chini, sasa kama bado atapewa Dau sina hakika.

Lakini kinachoonekana ni kuwa baada ya serikali ya JK kufeli katika mambo mengi, 'imeamuriwa' NSSF ndiyo imwokoe ili naye aonekane amefanya mambo fulani makubwa katika utawala wake. Ndiyo maana siwezi kushangaa kusikia Zitto akipingia chapuo sana NSSF ipewe mambo makubwa.

Lakini sina tatizo na NSSF kuwekeza kwa ajili ya maendeleo ya nchi, hata kama lengo ni kumsaidia zaidi 'rafiki' JK, MY CONCERN iko hapa; je NSSF wataweza kuendelea kujali wateja wao wakubwa, yaani WAFANYAKAZI wanaokatwa mafao yao kila mwezi, LAKINI INAPOFIKIA MAHALI PA KUYAPATA INAKUWA TATIZO KUBWA!!!!!!!

Mkuu,

Ijapokuwa sikatai maneno unayoyasema ila vile vile siamini hata kama wana urafiki wa karibu (JK na Dr Dau) hawakatazwi kufanya vitu vya maendeleo nchini. Mbona hujasema Harry Kitilya amefanya nini pale TRA zaidi ya kutafuna hela na kuwa billionaire kimya kimya? In fact anashindwa kuwaondoa makamishna wabovu kwasababu anaogopa kioo chake mwenyewe. Aondolewe awekwe mtu mwenye uwezo hizo conspiracy zitakuwa na zitaendelea kuwapo lakini maendeleo ndio mwananchi wa kawaida anayataka.

Kuhusu wasi wasi wako nikuulize PPF watu wanaiba na hela zinaenda mifukoni mwa watu je huna wasi wasi kule PPF maana ile hela ni kama imeenda kwa mganga hairudi tena!!!
 
Mkuu,

Wakijenga shule, Reli na ATCL hakuna faida as long as wanasiasa wana mkono wao. Project ya umeme ina faida na ni project ina uhakika wa kurejesha pesa kwani there is a monopolisation of market from Tanesco. Woga nilio nao ni akina Rostam (DOWANS) kutaka kumuangusha kwani MW 300 zinapunguza kama sio kuondoa kero ya umeme Tanzania (Gridi ya Taifa mahitaji ni MW 833 kadirio la juu na la kadirio la chini ni MW 701).

According to Tanesco kukiwa na ukame uzalishaji wa umeme kutokana na maji uko katika kiwango za MW 180 na Mafuta (Akina Dowans, IPTL, Songo Songo) ni kama MW 290 utaona kuwa kama NSSF wakijenga kinu cha makaa ya mawe umeme wa Taifa utakuwa wa kueleweka kwani kutakuwa na umeme wa jumla ya MW 770 (mahitaji ni 701 - 833 MW). Hiyo ni kwa kipindi cha ukame.

Kipindi cha mvua na maji yaani kukiwa hakuna ukame uzalishaji wa umeme wa maji hufikia kiwango cha MW 531 na ukiweka na vyanzo vyengine kama gesi, mafuta mazito ambao unazalisha umeme MW 290, wakijumlisha na NSSF MW 300 utakuta hatutakua na shida na umeme wa Dowans, IPTL ambao ni very very expensive. Tukibakia na umeme wa Songosongo, NSSF (Makaa ya mawe) na Maji mtera tutakuwa na jumla ya MW (530 + 230 + 300= 1060 MW). Umeme wa mgao unakuwa ni historia. Vile vile umeme wa makaa ya mawe ni bei rahisi sana kama ulivyo umeme wa gesi asilia kushinda umeme wa Dowans na nduguye IPTL wanaotukamua walalahoi.

Vile vile wakijenga kinu hicho wakaingiza katika gridi itasaidia hata kupunguza makali ya maisha kwa umeme umekuwa bei mbaya sana Tanzania.

Hii ni sababu ya kwanza faida ya project hii.

Mkuu umefafanua vizuri faida na umuhimu wa NSSF kuchukua mradi wa Kiwira. Ila tatizo linakuja kwenye madeni ambayo tunaambiwa NSSF watayarithi na kuyalipa. Kuna walionunua Kiwira kwa mil 70 na wakakopa ma billion bank ambayo yameenda kwingine. Hao nao jamani tuwalipe pesa zetu za NSSF hivihivi?
 
NSSF watarithi madeni na watarithi kudai madeni. Hata sasa NSSF wanadai madeni yao mengi tu, mmoja wa wadaiwa sugu wa NSSF ni Mbowe Hotels Limited, kampuni ya Mwenyekiti wa CHADEMA akishirikiana na Mkewe.
 
...................................

MY CONCERN iko hapa; je NSSF wataweza kuendelea kujali wateja wao wakubwa, yaani WAFANYAKAZI wanaokatwa mafao yao kila mwezi, LAKINI INAPOFIKIA MAHALI PA KUYAPATA INAKUWA TATIZO KUBWA!!!!!!!

Hii hata mimi huu ni wasi wasi wangu.

Kwangu binafsi naona Dr dau ni kichwa kiko missued kwa kuwekwa NSSF. May be alifaaa kupewa Benki FUlani hivi.

  • dhima y NSSF inatakiwa itofautishwe kuwa dhima ya Benki.
  • NSSF haitakikwi kuwekeza kwenye miradi yeneye mremngo wa faida zaidi. NSSF wanatkiwa wabalance faida na Social.
Mimi nitapenda kuona NSFF wajenge nyumba za bei nafuu kwa wafanyakazi japo 50 kila mkoa kila mwaka kwa mikoa mikubwa na nyumba japo 20 kwa mikoa kama kigoma.

Kuna watu wanafurahia tu kwa sababu NSSF inawekeza kwenye kutatua tatizo fulani sugu. But kila shirika au Taasisi wanatakiwa wa concetrate na MISSION na ViSSION zao.

Sina utaalam wa umeme wa mkaa (quality), lakini najua Kiwira Coal production ni dogo na HUTOA low quality coal - mkaa umejaa ash. Kuinua quality inabidi kuosha mkaa - ina maana ghali. Isije kesho NSSF wakaanza (I doubt kama watawekeza kweli) kuagiza mkaa toka Zimbabwe ama Zambia kama walivyofanya MBEYA CEMENT.

NSSF wangewekeza KUNUNUA mgodi na kukarabati power plant iliyopo hapo Kiwira kwanza (nadhani ni 10 MW) na kuwauzia TANESCO umeme. Baada ya hapo kama kuna faida ndo watajua wafanye nini. Halafu KIWIRA coal wanamatatizo ya uzalishaji na soko kiasi kwamba wafanyakazi hawajalipwa mishahara miaka mingi - NSSF itabidi kuwalipa hao kwanza (ghali) na ni wengi maana waliajiriwa wakati huo wa 'mali ya umma'.

Humu JF karibuni kumeongelewa mradi mwingine wa Liganga-Mchuchuma (NDC & *********) wa umeme wa makaa ya mawe bil 3 usd ambapo SICHUAN-HONGDA ya China - Sichuan wame-win tender. Sasa ni vizuri mradi mmoja ukawa ktk full swing ya ujenzi ndio kina Dau watuletee hizi hadithi za NSSF. CCM waache kutuchanganya ili kupata mianya ya kutufisadi, wafanye kazi ionekane.

Hivi jamani imeshatajwa miradi mingapi ya umeme toka tunazaliwa lakini mpaka sasa hakuna hata mmoja uliofanikiwa na kuendelea. Liganga na Stiers Gorge nimeanza kuisikia toka nipo nursery school!. Vipofu tunaongozana au?
 
Hii hata mimi huu ni wasi wasi wangu.

Kwangu binafsi naona Dr dau ni kichwa kiko missued kwa kuwekwa NSSF. May be alifaaa kupewa Benki FUlani hivi.

  • dhima y NSSF inatakiwa itofautishwe kuwa dhima ya Benki.
  • NSSF haitakikwi kuwekeza kwenye miradi yeneye mremngo wa faida zaidi. NSSF wanatkiwa wabalance faida na Social.

Mimi nitapenda kuona NSFF wajenge nyumba za bei nafuu kwa wafanyakazi japo 50 kila mkoa kila mwaka kwa mikoa mikubwa na nyumba japo 20 kwa mikoa kama kigoma.

Kuna watu wanafurahia tu kwa sababu NSSF inawekeza kwenye kutatua tatizo fulani sugu. But kila shirika au Taasisi wanatakiwa wa concetrate na MISSION na ViSSION zao.

Mkuu,

Naomba nitofautiane na wewe. Moja ya kazi za NSSF ni kuwekeza katika viable investments. Na uthibitisho wa hili soma NSSF Act ya 1997 inayosema hivi kipengele kimoja:-

53.-(1) There is established a Board or Trustees of the National
Social Security Fund.
Establishment
of
Board of
(2) The Board shall, in its corporate name be capable of-
(a) suing and being sued;
Trustees

(b) taking, purchasing or otherwise acquiring, holding, charging and
disposing of property, movable or immovable; and

(c) entering into contracts and performing all such other acts for the
proper performance of its functions under this Act which may
lawfully be performed by a body corporate.

Vile kuna kipengele hichi 62 na 63 kinasema hivi:-

62. Investment of money shall be done by the Board in any viable
venture as it may consider appropriate having regard to the economic
and commercial viability.
ment of
moneys in
the Fund

63. The Board may, subject to Provisions of section 67 utilize moneys
in the Fund for the acquisition of land, or aquisition or construction
of buildings and acquisition of equipment and other assets required for
the administration of the Board and the efficient performance by it of
its functions.

Hivyo nikuulize Dr Dau amekosea wapi?
 
Mdondoaji, kiasi gani kinahitajika kujenga bwawa la umeme wa kuzalisha 300MW?

Kiasi gani kinahitajika kufanyia matengenezo mabwawa yaliyopo ili kuweza kuyarudisha katika kiwango cha juu cha uzalishaji wa angalau 300MW?

hivi mwanakijiji bado tu unafkiria tuendelee na haya mabwawa yanayotegemea mvua.me naona ni vizuri tufanye diversification.tutafute vyazo vyengine zaidi.maana mvua ikigoma tu mgao huo.
 
Mkuu,

Kujenga a river damn project itagharimu taifa much cheaper than building a coal mine na binafsi naunga mkono tujenge river damn ila indirect cost za river damn kama environmental hazards ni kubwa ila kwashida tuliyonayo hatuna namna. Na kama river damn ya Mtera inauwezo wa kuzalisha MW 530 na Mtera ina capacity ndogo kulinganisha na mto Rufiji. Tatizo ni siasa zinatumika kwani river Rufiji plan zipo (Stiegler Gorge) kuna kampuni inaitwa Energerm walifanya utafiti wakasema ina uwezo wa kuzalisha 900MW!!!! (mahitaji yetu ni 833 kadirio la juu kabisa).

Home
 
NSSF watarithi madeni na watarithi kudai madeni. Hata sasa NSSF wanadai madeni yao mengi tu, mmoja wa wadaiwa sugu wa NSSF ni Mbowe Hotels Limited, kampuni ya Mwenyekiti wa CHADEMA akishirikiana na Mkewe.

NSSF kudai madeni halisi na ya ukweli kwa aliowakopesha ni jambo zuri na busara,lakini NSSF kuingia kichwakichwa kurithi deni la mkopo(afazali ingekuwa mishahara na arears za wavuja jasho wenzetu- wafanyakazi) huku ukielezwa na kufanya udaiwe madeni unlealistic naona kama si busara kabisa mkuu. Kumbuka pesa iliyonunua mgodi na madeni yatokanayo na pesa iliyokopwa fastafasta ambayo haijaendeleza chochote mpaka sasa!
 
Tatizo langu najiuliza inakuwaje NSSF wawe na ubavu wa kutumia pesa za wanachama jinsi wanavyopenda? Je wamepata ridhaa gani? Aidha mifuko hii ya "...social fund" inashindwa kuwahudumia wanachama wanapoondoka au kustaafu kazi. Kwa mfano investments zinazofanyika katika miradi mbali mbali, ni vipi mwanachama aliyekwisha kustaafu atafaidi matunda ya jasho lake? Hili ni jambo muhimu sana ama sivyo wafanyakazi waunde chombo chao tofauti.
 
NSSF watarithi madeni na watarithi kudai madeni. Hata sasa NSSF wanadai madeni yao mengi tu, mmoja wa wadaiwa sugu wa NSSF ni Mbowe Hotels Limited, kampuni ya Mwenyekiti wa CHADEMA akishirikiana na Mkewe.

Vyovyote iwavyo mzee,embu tujiulize mambo yafuatayo,kwa nini Kiwira wasipewe TANESCO na wakawezeshwa kwa mkopo??
Wenye hela zao namaanisha wafanyakazi wanaokatwa wameshirikishwa na kuridhia uwekezaji mkubwa kama huo?ambao ndani yake utarithi madeni?
 
Ningependa niwaambie NSSF wanigawie fungu langu walilonikata toka naanza kazi mpaka leo,nilitumie kwa maendeleo yangu na familia yangu wakati huu nikiwa na nguvu,kisha kama sheria itanibana niendelee kuwachangia michango yangu baadae tena kwa muda na mkataba maalum!. Mafao yao yote wanayatoa wakati mtu ni mzee hajiwezi anatarajiwa kufa baada ya mwaka mmoja. Tena baada ya kumaliza soli za viatu kufuatilia. What is the use of that!.UNANISAIDIA AU NAKUSAIDIA UENDELEZE UFISADI.Uliza kwa nini kampuni ya sigara (TCC) iliwaondoa wafanyakazi wake wote kwenye uanachama wa NSSF!. Ask urself and do research you will get true answers si porojo.
 
Wanachama wa NSSF twenda mahakamani kupinga hili....hizi ni fedha zetu ambazo zinaingizwa katika dili ambalo halieleweki eleweki kwanza wangehakikisha wanaimarisha hali za wanachama kwa kuwakopesha nyumba kabla ya kujitumbukiza katika biashara hiyo kichaa.
 
NSSF watarithi madeni na watarithi kudai madeni. Hata sasa NSSF wanadai madeni yao mengi tu, mmoja wa wadaiwa sugu wa NSSF ni Mbowe Hotels Limited, kampuni ya Mwenyekiti wa CHADEMA akishirikiana na Mkewe.

....At Last! Now I know You for what you really are.

Mhhh ukifuatilia mtiririko wa posts mbalimbali alizoweka MM Mwanakijiji, utaona kuna kitu kinafichwafichwa juu ya ukweli wa umiliki wa mradi wa Kiwira wa makaa ya mawe. Je ni NSSF kweli?? Ni Serikali au wachina???. Hapa naona NSSF wanataka kuingia ili kufidia pesa walizoikopesha zamani KIwira kwa udhamini wa serikali. Inavyoonekana NSSF walitoa pesa kwa Kiwira project, ambazo wameshindwa kuzilipa, na kwa kuwa Serikali ndo alikuwa/anakuwa ni mdhamini mkuu wa NSSF, ndio maana inajaribu kuonyesha kuwa NSSF wanataka kuumiliki mradi huo. Lakini ninachokiona hapa ni kama kiini macho tu, maana PESA hasa ishaliwa na nahisi nyingi ziliingia kwenye kampeni ya mwaka huu. TUSUBIRI WALA SI MBALI PICHA NYINGINE TITTLED UBADHIRIFU NSSF will be released (Launched) this weekend!!! MM Mwanakijiji please fuatilia kwa karibu utujpatie habari!!!!!!!!!!!!!
 
Wanachama wa NSSF twenda mahakamani kupinga hili....hizi ni fedha zetu ambazo zinaingizwa katika dili ambalo halieleweki eleweki kwanza wangehakikisha wanaimarisha hali za wanachama kwa kuwakopesha nyumba kabla ya kujitumbukiza katika biashara hiyo kichaa.

Utaandamana peke yako kwasababu watanzania tuna tabia moja sugu TUKIKOPESHWA HATULIPI!!!! Hivyo basi hilo tu ndio linalosababisha hilo unalolitaka lisifanikiwe mpaka serikali itakapostawisha miundo mbinu ya sheria na utekelezaji ndipo unachokisema venginevyo mie nawaunga mkono NSSF wanalolifanya. Biashara kichaa iko kule PPF wakurugenzi wanatafuna pesa za wafanyakazi wa umma hiyo ndio biashara kichaa ila sio hawa msiwaonee tu kwa sababu zenu nyengine.
 
Mkuuu ndio maana likatwa NSSF sio CRDB wala NMB. Mashirika kama haya hayatakiwi kuwa profit orinted sanaaaaa. yanaakiwa yaanagalie miradi inayowalenga zaidi wanachama. NSSF inatakiwa kuchukua risk kwa ajili ya miradi itakayowanafufahisha wanachama sio mradi utakaowanufaisha wao na serikali.

Hizi FFF F za nchi nyingine zinadhaminiwa na serikali kujenga nyumba za wafanyakazi na wakazi wa mikoani sio kuzalisha umeme au kujenga madaraja. Sio tu kujenga matower

NSSF haiko kwa ajili ya kuziba na kujaladia mapungufu ya serikali. Ndio maana hata shule na hospitali zingekuwa na faida bado ingekuwa ni miradi tata kwa NSSF

NSSF inatakiwa kuwekeza kwenye miradi inayowalenga wananchi. Mfano mradi kama ile ya

  • Hosteli ya mabibo, 100%
  • kujenga nyumba. hizi wamejenga nyumba tatzio wamejenga za wachache tena viongozi tu tena mkoa wa dar salaama pekee
Matatizo ya umeme yasifanye shirika kupoteza foucs yake halisi na sisi kuona sawa.

Ingawa siungi mkono miradi kama hii sometime najiuliza bora hawa wanatakakutupiga bao kwa kufaya kitu sasa sijui yale mashirika mengine yenye FFF yanatupigaje bao.

Halafu wanajipongeza kwa kulipa wastaafu 80,000/= kwa mwezi huku hela yote inaishia kwa wezi na matumbo yao... aibu tupu!!!
 
Mkuu,

Naomba nitofautiane na wewe. Moja ya kazi za NSSF ni kuwekeza katika viable investments. Na uthibitisho wa hili soma NSSF Act ya 1997 inayosema hivi kipengele kimoja:-

53.-(1) There is established a Board or Trustees of the National
Social Security Fund.
Establishment
of
Board of
(2) The Board shall, in its corporate name be capable of-
(a) suing and being sued;
Trustees

(b) taking, purchasing or otherwise acquiring, holding, charging and
disposing of property, movable or immovable; and

(c) entering into contracts and performing all such other acts for the
proper performance of its functions under this Act which may
lawfully be performed by a body corporate.

Vile kuna kipengele hichi 62 na 63 kinasema hivi:-

62. Investment of money shall be done by the Board in any viable
venture as it may consider appropriate having regard to the economic
and commercial viability.
ment of
moneys in
the Fund

63. The Board may, subject to Provisions of section 67 utilize moneys
in the Fund for the acquisition of land, or aquisition or construction
of buildings and acquisition of equipment and other assets required for
the administration of the Board and the efficient performance by it of
its functions.

Hivyo nikuulize Dr Dau amekosea wapi?

Kulipa 80,000/= kwa mwezi kwa wanachama wastaafu, kama kuna hela hivyo mpaka watu wanakopeshwa hovyo hovyo na matumizi mabovu (report ya CAG), kwanini hata wameshindwa kuboresha mafao hayo?
 
Back
Top Bottom