NSSF kutatua tatizo la umeme Tanzania

This is the best news na naomba wawezeshwe maana to be honest its impressive na inatia moyo kuona kuwa kuna watu pamoja na matatizo yoote tulionayo kama taifa, bado tunao ma PATRIOTS

Good idea but not right for NSSF!
Wasiwasi wangu mkubwa ni malimbikizo ya malipo kwa wastaafu wanaoidai NSSF, je hii haitaongeza malimbikizo as lot of shillings may be taken for the project!
[/QUOTE]
 
Ok sasa nimeelewa

The issue hapa people are not interested (apart from the few) na either NSSF wainvest kwenye power generation, ila tatizo la wengi humu ni kuwa investment inafanyika chini ya Dr RAMADHANI dau.

So I get it now. Duh ! I was so misguided kudhani kuwa kwenye hili tutaangalia mambo based on National Interest kumbee nimesahau ileeee angle nyingine. Na no one was interested kutaka kujaua Mewatts Ngapi NSSG wataproduce etc...

No wonder wako kimya on ERIO na PPF pamoja na uozo uliojaaa kule.


That said, nawapa hongera walioamua kujadili hii mada kwa kufocus on the issue in hand.
 
People criticize without merit, that is the problem with this forum and the ultimate downfall of JF will be brought about by the fact that most contributors know absolutely nothing about what they are talking about. Have any of you ****** tried to consider whether similar projects have been attempted in other countries especially developing economies. Here's a lil homework for all you critics, check out the Malaysian Pensions action on energy under the instruction of Dr. Mahatya Mohamed. Kazi yenu kunyea tuu.. Morons.
 
wa concentrate katika akiba zaidi na real estate investment sio power generation utility
 

NSSF kufua umeme wa megawati 300 Desemba

Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha; Tarehe: 2nd February 2011 @ 23:57

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umeanza mchakato wa kuzalisha umeme wa megawati 300 ifikapo Desemba mwaka huu, ili kusaidia kuondoa kero iliyopo nchini sasa.

Hayo yalisemwa jana mkoani hapa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Dk. Ramadhani Dau, kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa wadau wa NSSF.

Dau alisema pamoja na kuzalisha umeme huo pia wanaangalia uwezekano wa kutandaza bomba la gesi kutoka Mnazi Bay hadi Dar es Salaam na Mwanza, lengo likiwa ni kusambaza gesi inayozalishwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema shirika hilo limeshateua mshauri ili kusaidia kufikia azma hiyo na kupunguza kero ya kukatika kwa umeme ambayo husababisha shughuli za jamii kusimama kwa muda.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano, shirika hilo limeongeza idadi ya wanachama kutoka 380,693 mwaka 2005/06 hadi 506,216 mwaka 2009/10 sawa na ongezeko la asilimia 33, na ifikapo Juni mwaka huu, wanachama wa shirika hilo wanatarajiwa kufikia 518,410.

Aliongeza kuwa kwa upande wa wanachama makusanyo yameongezeka kutoka Sh. bilioni 126,96 hadi Sh. bilioni 315.31 sawa na ongezeko la asilimia 148, matazamio yao ni kukusanya Sh bilioni 404.58 ifikapo Juni mwaka huu.

Aidha, mwaka 2005/ 6 hadi 2009/10 shirika hilo liliongeza uwekezaji kutoka Sh bilioni 424.89 hadi Sh trilioni 1.03 sawa na ongezeko la asilimia 144, pia katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kwa kushirikiana na Serikali NSSF imewekeza kwenye miradi mbalimbali ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), nyumba za Polisi na nyumba za Jeshi la Wananchi.

Alisema miradi mingine imegharimu Sh bilioni 340.5 ambazo ni mkopo kwa Serikali na uwekezaji katika maeneo mbalimbali na kuongezeka kutoka Sh bilioni 477.76 mwaka 2005/06 hadi Sh trilioni 1.136 mwaka 2009/10 na Oktoba mwaka jana, NSSF ilipandisha
pensheni kwa asilimia 52 na hivyo wastaafu kuongezwa pensheni kutoka Sh.52,000 hadi Sh.80,000 kwa mwezi.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, malipo ya wanachama yaliongezeka kutoka Sh bilioni 40.18 mwaka 2005/06 hadi Sh. bilioni 102.82 mwaka 2009/10 sawa na ongezeko la asilimia 156.

"Nawasihi waajiri kulipa michango ya wafanyakazi kwa wakati ili wanufaike na shirika letu pia tunajitahidi kukamilisha miradi ya ujenzi wa daraja la Kigamboni na kujenga upya makazi kuanzia Mchikichini, lengo likiwa ni kubomoa nyumba mbovu na kujenga mji wa kisasa unaojitegemea - Satellite City".

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alilipongeza shirika hilo kwa kujenga majengo mbalimbali likiwamo la makazi na UDOM, daraja la Kigamboni na mpango wa kuzalisha umeme nchini, ili kuondoa kero kwa
wananchi.

Alisema wananchi watafarijika kusikia daraja la Kigamboni litajengwa wakati wowote lengo ni kurahisisha shughuli za maendeleo na alitoa angalizo kwa shirika hilo kutafiti sekta isiyo rasmi ambayo mchango wake ni mkubwa kwenye uchumi wa Taifa na kutoa angalizo kwa waajiri kupeleka michango ya wafanyakazi kwa wakati, ili kuepusha usumbufu baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Katika mkutano huo wanachama saba na wastaafu wawili waliotekeleza sheria za NSSF na kupeleka makato ya wafanyakazi kwa wakati walizawadiwa.

Wanachama hao ni Kampuni ya Madini ya Bulyanhulu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Kampuni ya simu ya Vodacom, Chuo Kikuu cha St. Augustine, Mwanza; Sekta Binafsi, Said Salum Barkhresa, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Kiwanda cha Tobacco Alliance,
Morogoro; hospitali ya Lugoda, Mufindi na wastaafu Joram Elirai na Joseph Sikira.



J
 
Kero kuhusu NSSF ni kuwa mambo yao hayawekwi mezani.........haitoshi kuweka mipango kijuujuu tu unafaa wateja wao kujua undani wa mipango na matumizi husika..............................
 
At last wamekuja na Investment ideas za maana.
Mi sipendi kuona shirika kubwa linawekeza kwenye nyumba za kuishi, We need big investments kama Power Production, Construction of EPZs, Large Scale farming etc. sio kujenga vigorofa posta na vibanda vya kuishi kule mbagala
 
Isije ikawa Dowans/EPA zinahamia kwenye mashirika ya umma. Hawa waungwana hawana la maana hata kidogo. Ila kama ni mradi ulioanzishwa in good faith utakuwa mzuri provided kwamba uko viable financially
 
Kufua umeme kunahitaji hela nyingi na ni risk, hao NSSF nani kawaruhusu kutumia pesa zetu? tena wana invest kwa faida ya soko lakini cha ajabu wanachama tunaambulia 2% tu, huu si ni wizi jamani.

Policies za hii mifuko ya jamii hizi lazima ziwe reviewed, kuna harufu ya ufisadi ufisadi. Kwanza lazima waweke hadharani mkataba wenyewe ili sisi wanachama tuuone, siyo kutupeleka peleka tu wanavyotaka wao wenyewe wakati pesa ni zetu.
 
Kufua umeme kunahitaji hela nyingi na ni risk, hao NSSF nani kawaruhusu kutumia pesa zetu? tena wana invest kwa faida ya soko lakini cha ajabu wanachama tunaambulia 2% tu, huu si ni wizi jamani.

Policies za hii mifuko ya jamii hizi lazima ziwe reviewed, kuna harufu ya ufisadi ufisadi. Kwanza lazima waweke hadharani mkataba wenyewe ili sisi wanachama tuuone, siyo kutupeleka peleka tu wanavyotaka wao wenyewe wakati pesa ni zetu.

na isije ikawa white elephant kama ilivyo miradi mingi ya public institutions..... the likes of machinga complex ni wale wale NSSF.... hivi kwanini.? ...investment appraisal zao zinakua na kasoro gani...?.au hawafanyi kabisa au hao wachumi wao hawana uwezo
 
Hivi wachangiaji wa mfuko huo ambao hata kupata madai yao wanapohitaji hadi wahonge na kubembeleza sana sana wanafaidika nini na investment za NSSF?
  • Shirika ambalo lina wafanyakazi wengi mno kupita mahitaji yake (pesa zetu hizo!) hebu wafanyiwe tathmini ya idadi ya wafanyakazi na majukumu ya kila mfanyakazi aliyeajiriwa
  • shirika ambalo linaendeshwa kwa udini mkubwa (ukiwa mfanyakazi wa dini fulani mambo poa kwako)
  • NSSF waachane na mambo yasiyowahusu wajali vision na mission yao - Social Security, wapunguze overheads zisizo na lazima na waige mifano ya wenzetu wanaoona mbali........
  • Watoe mikopo kwa wachangiaji kwa kutumia faida wanayopata kwenye investment zinazotokana na hizo hizo pesa zetu - eti miaka 50 tunaweza kujiendesha bila kutegemea michango, hiyo pesa mmeipata wapi? Si michango yetu, nini mmerudisha kwetu?
  • Kwani nani asiyejua kuna ufisadi mkubwa ndani ya NSSF? Ule mpango wa mfumo wa kompyuta India mliopoteza fedha nyingi bila mafanikio mliwaambia wachangiaji wa pesa zao? Si mlificha na mabilioni yakapotea? Mliwafanya nini wahusika?
 
Ok sasa nimeelewa

The issue hapa people are not interested (apart from the few) na either NSSF wainvest kwenye power generation, ila tatizo la wengi humu ni kuwa investment inafanyika chini ya Dr RAMADHANI dau.

So I get it now. Duh ! I was so misguided kudhani kuwa kwenye hili tutaangalia mambo based on National Interest kumbee nimesahau ileeee angle nyingine. Na no one was interested kutaka kujaua Mewatts Ngapi NSSG wataproduce etc...

No wonder wako kimya on ERIO na PPF pamoja na uozo uliojaaa kule.



That said, nawapa hongera walioamua kujadili hii mada kwa kufocus on the issue in hand.

Ina maana ile thread ya PPF huisomi mkuu? mbona uanenda personal sana mazee?

haya daraja letu liko wapi? au bado mnachanganua upembuzi yakinifu na kuangalia EIA ili kucheki kama ROI iko safi na namna ya kufaidi 10% bila kugusa mfupa siyo?
 
Eti wajenge nyumba zakuuzia polisi na waalimu..lol That is BS and those are not even investments, pensioners will die bila sumni

Hahaha eti BS unless hujui ni kwa namna gani NSFF, PPF na hayo mashirika yenye FF yainatakiwa kuwa tofauti na CRDB, au NMB. Mbona wamejnge nyumba zaviongozi wachache. kwa nini scope ya miradi yao isilenge watu wa kawaida. Serikali inaweza kuwa gurantee just as serikali inakuwa guranteee kwenye miardi yao mingine.
 
hivi dau( kijana wa yusuf manji, kimbisa na madabida) bado anapelekwa TRA na mngwana? maanake Kitilya kashaaaga makamishna wenzake kwamba anaondoka kabla ya mwezi wa sita... hatari kabisa
 
Back
Top Bottom