NSSF kujenga daraja la Kigamboni, ni uwekezaji au kusaidia kutekeleza ahadi za CCM?

Dullo

JF-Expert Member
Oct 24, 2009
251
64
Katika mchakato wa ujenzi wa daraja la Kigamboni ambapo wadau wakubwa katika ujenzi huo ni NSSF kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania.

Hapa ni kigugumizi kwa sababu naona wanachofanya ni kutekeleza ahadi za CCM kwa kutumia fedha za watanzania wanaotegemea fedha hizo kuwasaidia baadae. Hivi kwanini NSSF isitumie fedha hizo kwa kuwakopesha wanachama wake? Jamani mwenye mawazo mbadala atujuze!
 
kweli mkuu NSSF wanakula tu faida kuuubwa sisi wanachama hatunufaiki na lolote, Vitega uchumi wanavyo vingi sana kwa nini wasikopeshe wanachama wake? inaniudhi sana hii iisue
 
Halafu hao serikali wenyewe wanamifuko yao hawachangii NSSF hata senti moja, kwani hawatumii mifuko yao ya LAPF,PSPF na mingine mingi wanakimbilia NSSF tu.
 
Nchi hii ishauzwa, Kama hujui fahamu leo.Thibitisha Maneno yangu baada ya miak kumi.
Kigamboni si Tanzania, kigamboni ni Singapore.


Shortly, Hakuna mwafrika atakayeweza kuishi Kigamboni.
 
Wewe unachotaka nini? Si maendeleo tuu? Hata nyinyi magwanda kama munaweza jengeni.......Kumbe hampendi maendeleo ya nchi hii.........
 
Mr.NSSF yupo humu JF amejaa tele, natumai atakuja na majibu kabambe kukidhi maswali yako yote... behold!!!
 
Hili swala linanichefua sana. Ukifuatilia mafao yako utapigwa kalenda kama kalenda!!! Ooh faili lako bado mara ah! Lazima uwe na smart card nawakati wanajua wazi uwezo wakutengeneza smart kwa wateja wake hasa mikoani hawana!!!!!!
 
mimi binafsi kinacho niacha hoi ni jinsi watakavyorudisha hizi pesa.......maana investiment kama hizi zina social na indirect economic returns lakini halina financial returns........no return of capital na return on capital........kwa ujumla kukokotoa payback period ni ngumu.....labda watu wa investiment analysis watusaidie katika hili....
 
Magari yatawekewa gate toll, asiyetaka kulipia atakua free kuzunguka njia ya mbagala, kongowe, tua ngoma ndio aipate kigamboni.
 
Sisi kama shirika hatuna makuu. Unlike PPF, PSPF, na wengine

Tunafanza investments ambazo zinawagusa wanachi moja kwa moja. Alitekuwa anatuchelewesha. Hazupo tena na serikali ishaji toa kauli kilichobaki ni kuleta maandishi ili watu wajimwage site. Kwa kuonzesha how serious we are. Tayari tenda zishatangaywa na walau tunaweza kupunguza unemplozment kwa muda, na serikali ikafaidia na taxes na baada za mradi kuisha mlio na mashamba vijibweni na kibugumo mtakuwa hamuna haja za kuzunguka
 
Kwani Serikali inaongozwa na chama kipi kwa sasa? Na hiyo NSSF ni ya nani?

Mambo mengine yote yanayofanywa na Serikali si yako katika kutimiza sera za chama?

Swali la mtoa mada lina walakin.
 
Ni matumizi mabaya ya michango ya watu kwenye mifuko hiyo, aliyechangia atapewa riba kiasi gani kwenye mradi huo
 
Sisi kama shirika hatuna makuu. Unlike PPF, PSPF, na wengine

Tunafanza investments ambazo zinawagusa wanachi moja kwa moja. Alitekuwa anatuchelewesha. Hazupo tena na serikali ishaji toa kauli kilichobaki ni kuleta maandishi ili watu wajimwage site. Kwa kuonzesha how serious we are. Tayari tenda zishatangaywa na walau tunaweza kupunguza unemplozment kwa muda, na serikali ikafaidia na taxes na baada za mradi kuisha mlio na mashamba vijibweni na kibugumo mtakuwa hamuna haja za kuzunguka

Eeebana eh! kwani unatumia keyboard ya aina gani mbona lugha gonga sana?
 
Back
Top Bottom