NRA kupiga kambi mikoa ya Kusini

hassan kisabya

Senior Member
Jun 14, 2014
165
109
Viongozi wa kitaifa wa NRA watafanya ziara ya kikazi katika mikoa ya kusini Kwa lengo la kukagua Kazi za chama,baadhi ya viongozi watakaokuwa katika ziara hiyo ni Mhe Rashid Mtuta -Mwenyekiti TAIFA(ambaye pia ni MBUNGE BUNGE MAALUM LA KATIBA),mhe HASSAN KISABYA(N/Katibu Mkuu Taifa na KATIBU MKUU BODI YA WADHAMINI),mhe BAKARI MAANJE(mkurugrnzi Makao makuu Mazingira) na mhe Peter Chipunga(mjumbe bodi ya chama),ziara hii itaanza tarehe 24/06 hadi 29/06/2014.
Ikumbukwe NRA Ndio chama cha kwanza kuonyesha Upinzani wa dhati ktk miaka ya 1994-95, kabla ya kifo cha mmoja wa viongozi wake mashuhuri Hayati Prof.Kighoma Ali Malima,NRA ni miongoni mwa vyama vya kwanza kusajiliwa baada tu ya kuruhusiwa Kwa mfumo wa vyama vingi,kilisajiliwa mwaka 1993,NRA inaamini katika siasa za kistaarabu,siasa zenye tija na siasa za masuluhisho na sio siasa za lawama,fujo ama siasa za chuki,SERA YETU NI "TAIFA KWANZA ,VYAMA BAADAE"
Kwa taarifa hii tunawataka wakazi wa mikoa ya kusini kujipanga kupokea sera nzuri Kwa ustawi wao na kudumisha
amani
 
Viongozi wa kitaifa wa NRA watafanya ziara ya kikazi katika mikoa ya kusini Kwa lengo la kukagua Kazi za chama,baadhi ya viongozi watakaokuwa katika ziara hiyo ni Mhe Rashid Mtuta -Mwenyekiti TAIFA(ambaye pia ni MBUNGE BUNGE MAALUM LA KATIBA),mhe HASSAN KISABYA(N/Katibu Mkuu Taifa na KATIBU MKUU BODI YA WADHAMINI),mhe BAKARI MAANJE(mkurugrnzi Makao makuu Mazingira) na mhe Peter Chipunga(mjumbe bodi ya chama),ziara hii itaanza tarehe 24/06 hadi 29/06/2014.
Ikumbukwe NRA Ndio chama cha kwanza kuonyesha Upinzani wa dhati ktk miaka ya 1994-95, kabla ya kifo cha mmoja wa viongozi wake mashuhuri Hayati Prof.Kighoma Ali Malima,NRA ni miongoni mwa vyama vya kwanza kusajiliwa baada tu ya kuruhusiwa Kwa mfumo wa vyama vingi,kilisajiliwa mwaka 1993,NRA inaamini katika siasa za kistaarabu,siasa zenye tija na siasa za masuluhisho na sio siasa za lawama,fujo ama siasa za chuki,SERA YETU NI "TAIFA KWANZA ,VYAMA BAADAE"
Kwa taarifa hii tunawataka wakazi wa mikoa ya kusini kujipanga kupokea sera nzuri Kwa Israel wao na kudumisha
amani

Mna patikana wapi kiofisi?
 
Hawa Wanaenda huko kuhalalisha ziara za Nnape kuwa hata upinzani walifanya mikutano ..........so wait .....
 
Haki sawa"hizo ni changamoto ndani ya siasa za kiafrika,hatutakiwi kuhofia wengine nao kufanya Kazi za nchi,sidhani kama yupo mtanzania mwenye hati milki ya kufanya siasa,kila chama chenye usajili wa kudumu Tanzania,kitafanya siasa Tanzania na sio China wala Kenya,hivyo tupeane fursa ili watanzania waamue! karibu NRA
 
Last edited by a moderator:

Naona hapa:

MAHOJIANO MAALUMU NA NAIBU KATIBU MKUU WA NRA

Ndugu wana-Mzizima 24, mtakumbuka kuwa nchi yetu iliingia katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 wakati wa utawala wa awamu ya pili ya Mzee wetu, Al-Haj Ali Hassani Mwinyi.Ni katika kipindi hicho ambapo mabadiliko kadhaa yalifanyika kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuruhusu urejeshwaji wa mfumo huo. Ni hapo ndipo vyama kadhaa vilisajiliwa na mwaka 1995 Tanzania ikafanya uchaguzi mkuu chini ya mfumo huu mpya.

Mpaka sasa Tanzania imefanya uchaguzi mara nne chini ya mfumo huu mpya, na inakadiriwa kuwepo kwa vyama vya kisiasa visivyopungua 22.
Miongoni mwa vyama vya mwanzo kabisa baada ya kutambulishwa kwa mfumo huu, ni chama cha NATIONAL RECONSTRUCTION ALLIANCE (NRA), kilichoasisiwa mwaka 1992 chini ya mwenyekiti wake wa kwanza, hayati ndugu Aboubakar Ulotu, na baadaye chini ya hayati ndugu Kighoma Ali Malima.
Katika kujadili historia, hatima, sera na miongozo ya chama hiki kikongwe na siasa cha nchi yetu kwa ujumla tumemualika ulingoni NAIBU KATIBU MKUU wa chama hiki kwa upande wa Tanzania Bara, ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini wa Chama hiki, ndugu Hassan Kisabya Almas.

Ndugu Kisabya ni miongoni mwa viongozi vijana katika nafasi za juu za kisiasa hapa nchini akiwa na
umri wa miaka 29, nafasi inayomfanya awe kielelezo cha uwezo wa vijana kisiasa.

Tunawakaribisha wasomaji wetu katika mahojiano haya maalumu na mnaruhusiwa kumuuliza ndugu Kisabya naye atakuwa tayari kuwajibu.

https://sw-ke.facebook.com/mzizima24/posts/535871183163797
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom