Novel gani ilikuvutia enzi uko secondary?

Za skuli? Hapana hazikutuvutia kabisa, hao kina chinua Achebe na wenzake kama Ngungi wa Thiong'o tulikuwa tunawapitia kwa sababu ya Marks za darasani. Lakini bila ya kusoma zile za James Hardley Chase basi wewe ulionekana siyo Mkali. Kwa kwa za kibongo nilipenda sana ile ya "Kitanda cha Mauti" ya Hamie Rajabu kama sikosei,na zote tatu za Mzee Musiba (RIP) muhusika wake mkuu akiwa ni Willy Gamba. Kuna za mtu anaitwa Agatha Christie hizo nazo nilizipitia sana!!

musiba namkubali sana hasa kitabu chake cha hofu
 
Back
Top Bottom