Notisi ya kuanzisha Mikoa na Wilaya

Tume wapo sahihi sana nadhani karibia majimbo yote mapya yametokana na wilaya mpya. Hiyo ipo powa, hatuwezi kuwa na wilaya isiyo na mbunge.
 
shule hazina madawati,maabara hakuna magamba yanaongeza majimbo 15 gharama za kuhudumia majimbo hayo kuanzia KILIMO KWANZA (ma-VX) wanayotumia waheshimiwa,pili posho na marupurupu wanayolipwa kwenye vikao mjengoni,tatu mifuko ya bunge.Hayo ni yale ambayo nayafahamu kwa upeo wangu.je pesa zote hizi ndani ya miaka 5 tungejenga zahanati ngapi vijijini.?
 
Kwa Kigoma ayatoll.a alisha fifisha upinzani...Ukipita utaliona kupitia bendera zao. Wamefanya hivyo baada kuona support wanayoweza kupata. Ushauri wangu kwa UKAWA...wavamie maeneo hayo kwa mikutano mingi ya ushawishi...uzuri kigona ni waelewa wa upinzani.


Ukawa( umoja wa katiba ya wahuni) hamna chenu tena Kigoma Bali nguvu zenu zielekezen kwingne maana mtapoteza mda wenu
 
Halafu wanapewa muda mfupi kuchangia hoja kisa wabunge ni wengi. Wachangie hoja kwa muda mfupi ili wachangie wengi
 
Tume ya uchaguzi haitendi haki kabisa katika kugawa majimbo ya uchaguzi. Inajulikana wazi kuwa Dar es salaam ndio jiji lenye watu wengi zaidi lakini ni mkoa wenye majimbo kidogo sana kulinganisha mikoa mingine ambayo ina watu wachache..
watu wa maeneo ya City Centre na Kariakoo ni jimbo kubwa na lina harakati nyingi zaidi za biashara na kiuchumi Ukweli linahitaji kuwa na mbunge wake.Lakini tume imekua kama haioni , pia maeneo ya msasani na peninsula sasa hivi ni makaazi ya watu wengi nao wanatakiwa kuwa na kuwa na mbunge wao.
pia eneo la mtoni , mbagala na kurasini litenganishwe na temeke ni eneo la harakati sana linahitaji mbunge wao.
jiji lenye watu million 5 huwezi kulipa majimbo kidogo na kilimanjaro lenye watu milion 1.6
tukisema kuna udini kupunguza idadi ya wabunge waislam maneno mengi yatasemwa lakini hakuna mantiki ya kuhalalisha upungufu huu, hali hii pia ipo MKOA WA Tanga WENYE watu zaidi ya million 2 .

NEC mna udini tu haiwezekani hali iendele hivi. Mohamed Said naku cc unalionaje hili ?
 
Last edited by a moderator:
Ni ujinga sana kutawaliwa na masikini mpumbavu /wapumbavu shenzi sana serikali ya maSikini! Ubaya wa maSikini hata akili yake inakuwa ya kimasikini Yaani anajiwazia yy tu na kwa wakati ule aliopo wala si wenzake na kesho yake
 
Tume wapo sahihi sana nadhani karibia majimbo yote mapya yametokana na wilaya mpya. Hiyo ipo powa, hatuwezi kuwa na wilaya isiyo na mbunge.

We unamanisha nini? Jimbo la kakonko ni wilaya mpya ya kakonko ambayo imetokana na wilaya ya kibondo kule kigoma.
kabla lilikuwa jimbo la buyungu lina Kata 13, kwa mpango huu wa tume, je wamegawa jimbo la buyungu lenye kata 13 ili kapata jimbo la buyungu na jimbo la kakonko?
Au wamelibatiza jimbo la buyungu jina jipya ambalo ni jimbo la kakonko, nini wamefanya tume?
 
Chemba ni wilaya mpya kutoka jimbo la Kondoa kusini. Je jimbo la Kondoa kusini litakuwepo?
 
Mlele sio Jimbo jipya mkoani Katavi,PM Pinda alichaguliwa 2010 kama Mbunge wa Mlele na katangaza hatagombea!Jimbo hili litaangukia UKAWA

Hata Jimbo ka Nyang'wale mkoani Geita siyo Jimbo jipya,Mbunge wa Jimbo hilo anaitwa Hussein Kasu na katangaza HATAGOMBEA!Jimbo hili ni UKAWA pick-up pia
 
duh hapo magoli yanapanuliwa ili kuongeza walaji. sitashangaa nao zanzibar wakiomba kuongeza majimbo wakati majimbo yao ni kama kata huku tanganyika. duh..
 
CCM mbona mnatuongezea mzigo wa walipa kodi tena!!!waliokuwepo tu ni kasheshe kuwahudumia na hawafanyi kazi pale bungeni…hao watahitaji ma VX, mishahara isiyokatwa kodi,kutibiwa ulaya nk…
Kwa nini msiongeze mahospitali mazuri na shule nzuri???

Halafu baadae tutakuja kukamatwa tuchangie maabara za shule za sekondari!! Yaani ningekuwa mimi ndo nafanya maamuzi ningeweka mbunge mmoja tu kila wilaya na kusingekuwa na viti maalumu!! Mimi huwa naamini kabisa kwamba zaidi ya nusu ya wabunge huwa hawafanyi kazi yao wawapo bungeni kwasababu tumeshuhudia wabunge ambao wanakaa miaka mitano bungeni halafu hajawahi hata kuuliza swali wala kuchangia mjadala wowote!!
 
MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI
1. Buhigwe—Kigoma
2. Uvinza — Kigoma
3. Kakonko—Kigoma
4. Butiama—Mara
5. Chemba— Dodoma
6. Ikungi— Singida
7. Itumila— Simiyu
8. Kaliua— Tabora
9. Mbogwe—Geita
10. Mkalama—Singida
11. Mlele— Katavi
12. Momba— Mbeya
13. Nyang'hwale— Geita
14. Nyasa— Ruvuma
15. Wanging'ombe—Njombe
Hili la butiama ni kwa ajili ya Makongoro Nyerere, na hapa ndoto za Urais hamna, it is just rumors that he is among the contesters
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom