Noti mpya zazua balaa Mbeya

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
UJIO wa noti mpya katika mzunguko wa fedha hapa nchini, umeleta hofu kwa baadhi ya wananchi na wafanyabiashara mkoani hapa kwa baadhi yao kufikia hatua ya kukataa kuzipokea.

Hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa baadhi ya watu ambao tayari wameanza kuzitumia.

Benki kuu ya Tanzania (BoT) iliruhusu kuingizwa kwenye mzunguko noti hizo mpya za viwango vya sh 500, 1000, 2000, 5,000 na 10,000 Januari mosi mwaka huu, huku ikitoa angalizo kwa wananchi kuwa noti za zamani bado ni fedha halali na zina thamani sawa na zile mpya.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida abiria mmoja aliyepanda gari ya abiria kutoka eneo la Mbalizi kuelekea Sokomatola jijini hapa jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kondakta wa daladala aliyefahamika kwa jina moja la Suleiman kugoma kupokea noti mpya ya sh 10, 000, aliyopewa na abiria huyo kama nauli.

Hali hiyo iliibua malumbano makali baina ya kondakta wa daladala na abiria huyo, jambo lililolazimisha abiria mwingine kuamua kumaliza sakata hilo kwa kumlipia nauli sh 300 abiria huyo.

Hata hivyo, baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya daladala hiyo wengi walionekana kuiona kwa mara ya kwanza noti hiyo hali iliyosababisha kila mmoja wao kutaka kuishika.

Mmoja alisikika akisema, “Kwa kweli noti hizi za viwango vya kimataifa maana ukiwa na sh 1,000,000 kwa namna zilivyo utadhani umebeba fedha kidogo sana,” alisikika mmoja wa abiria hao.

Mbali na kondakta huyo kuonekana kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya ujio huo mpya wa noti za Tanzania, baadhi ya wafanyabiashara wa mazao katika masoko ya Mbalizi na maeneo mengine wamekuwa wakisita kupokea fedha hizo mpya kwa kutokuwa na imani nazo.

Melezo ya elimu kwa umma yaliyotolewa na Benki kuu yalifafanua kuwa noti mpya zitaingia kwenye mzunguko sanjari na noti za zamani mpaka hapo zitakapotoweka taratibu na hatimaye kuisha kabisa kwenye mzunguko.
 
kwakweli ata me ningekuwa konda ningekataa kwani nirahisi kupigwa changa la macho me nipo dar nasijazitia machoni sembuse uko mkoa
 
kazi ipooo kuzikubali mi niliwahi kushinda njaa mahali kisa nina noti ambazo hawazitambui wanakijiji isee!!
 
Inaonekana huyo jamaa alikuwa amekwishaichakachua hiyo noti,kwa taarifa ni kuwa kuna matatizo ya kiufundi ndio maana noti zilichelewa kutoka na hata Dar hazijaanza kuwa katika mzunguko sembuse Mbeya!
 
UJIO wa noti mpya katika mzunguko wa fedha hapa nchini, umeleta hofu kwa baadhi ya wananchi na wafanyabiashara mkoani hapa kwa baadhi yao kufikia hatua ya kukataa kuzipokea.

Hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa baadhi ya watu ambao tayari wameanza kuzitumia.

Benki kuu ya Tanzania (BoT) iliruhusu kuingizwa kwenye mzunguko noti hizo mpya za viwango vya sh 500, 1000, 2000, 5,000 na 10,000 Januari mosi mwaka huu, huku ikitoa angalizo kwa wananchi kuwa noti za zamani bado ni fedha halali na zina thamani sawa na zile mpya.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida abiria mmoja aliyepanda gari ya abiria kutoka eneo la Mbalizi kuelekea Sokomatola jijini hapa jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kondakta wa daladala aliyefahamika kwa jina moja la Suleiman kugoma kupokea noti mpya ya sh 10, 000, aliyopewa na abiria huyo kama nauli.

Hali hiyo iliibua malumbano makali baina ya kondakta wa daladala na abiria huyo, jambo lililolazimisha abiria mwingine kuamua kumaliza sakata hilo kwa kumlipia nauli sh 300 abiria huyo.

Hata hivyo, baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya daladala hiyo wengi walionekana kuiona kwa mara ya kwanza noti hiyo hali iliyosababisha kila mmoja wao kutaka kuishika.

Mmoja alisikika akisema, "Kwa kweli noti hizi za viwango vya kimataifa maana ukiwa na sh 1,000,000 kwa namna zilivyo utadhani umebeba fedha kidogo sana," alisikika mmoja wa abiria hao.

Mbali na kondakta huyo kuonekana kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya ujio huo mpya wa noti za Tanzania, baadhi ya wafanyabiashara wa mazao katika masoko ya Mbalizi na maeneo mengine wamekuwa wakisita kupokea fedha hizo mpya kwa kutokuwa na imani nazo.

Melezo ya elimu kwa umma yaliyotolewa na Benki kuu yalifafanua kuwa noti mpya zitaingia kwenye mzunguko sanjari na noti za zamani mpaka hapo zitakapotoweka taratibu na hatimaye kuisha kabisa kwenye mzunguko.
kilimasera, asante kwa taarifa hii, somo pekee nililolipata hapa ni kuwa ileelimu kuhusu ujio wa noti mpya iliyotolewa na BOT, bado inahitajika kuendelea kutolewa mpaka noti hizo zizoeleke.
 
nafikiri BoT hawajafanya kazi ya kutosha katika kuwafahamisha watanzania juu ya ujio wa noti hizo mpya! Fikiria mi nipo hapa Dar, na nina access na vyanzo vyote vya habari na sijazitia machoni hizo noti mpya achilia mbali ujio wa noti zenyewe niliousikia kwenye TV ya channel 10 na picha kwenye blog moja Ndullu alipokuwa Ikulu akizitambulisha noti hizo kwa Rais! Sasa sembuse konda wa daladala mkoani mbeya! Ukiuliza kitengo cha PR - BoT kimetumia sh. ngapi kutoa elimu kwa umma, usishangae kuambiwa wametumia Tsh. 800 Milioni!! Wakati hata kariakoo kwenyewe jana watu walishtuka kwenda benki wanakuta wanapewa noti mpya! Hii ndo Tanzania anayoiongoza mbunge wa zamani wa Chalinze!
 
Noti mpya ziko mtaani toka jmnne.
nimeziona zapendeza ila ile pawasa aka elfu tano ni the best!
 
Brooklyn, mimi ni mfuatiliaji mzuri wa ujio wa noti hizi mpya, nimeona matangazo yao kila siku ITV, TBC, Star TV, Channel Ten, Mlimani TV na TVZ, pia nimeyasikia matangazo yao ya redio kwenye Radio Tanzania (TBC Taifa), Radio One, Radio Free Africa na Sautiya Tanzania Zanzibar.
Matangazo hayo yalitoka kila siku, sasa kama kote huko watu hawakusikia ama hayakuwafikia, BOT wawatangaziaje?, labda waendeshe kampeni kama makampuni ya simu, au makampuni ya vinywaji baridi na bia!.
 
Wakufoji wasije wakaanza kazi yao kabla hazijafika huku kijijini kwetu.
 
Noti mpya ziko mtaani toka jmnne.
nimeziona zapendeza ila ile pawasa aka elfu tano ni the best!
Ni kweli 5,000/= ina mvuto japokuwa 10,000/= haipendezi kutokana na kukolea sana rangi na kupewa naski nyingi. Ni nyepesi, nilijaribu kuwasiliana na wafanyakazi wa BOT wakanijuza wepesi ndiyo uimara na fedha hii kwa mujibu wa maelezo yao ina ubora kuliko hizi zinazatoka kwenye mzunguko.
Ngoja tone wachakachuaji wakishindwa nitawapa BIG UP serikali ya JK japokuwa najua muda si mrefu utasikia uchafu katika hizi note!!!!!
 
Back
Top Bottom