NONSENSE: Madaktari Wamelipwa na Kundi fulani ili Wagome ILI Nchi isitawalike!

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,442
5,953
Bunge letu limeendelea kuwa la VITUKO kila uchao! Leo tena Mbunge wa Chama tawala Mh. Martha Mlata kaja na mpya kuwa Mgomo unaoendelea wa madaktari unadhaminiwa na kundi fulani. Hili hakika ni TUSI kubwa kwa madaktari wetu na ni vema AOMBE RADHI. Hivi kweli tumefikia kiwango cha kuwa-underrate madaktari wetu kwa kiwango hiki kwa kuwahusisha na malpractise ya aina hii. Anataka kutuaminisha kuwa wanachodai Madktari sio cha kweli bali wako influenced?

Tunakumbuka jinsi wabunge walivyozua tafrani wakati serikali hii inaingia madarakani wakidai POSHO ZAIDI NA KUPIGIWA SALUTI, hivi kipindi hicho walilipwa na nani? Wao hivi sasa wamepandishiwa stahili zao kwa 100% hadi 10,000,000/= hili kwao limewezekanaje? Kwa nini kwa madktari, na watumishi wengine, iwe nongwa?

Au ndio ule msemo wa ''Kunya anakunya kuku, bata anaharisha?''

IT IS MORE THAN PAIN
 
daah so sad..ulivyosema MIL 10 nimeumia sana kwakweli..huku sisi wengine tunatoil mbaya na bado hakuna posho..
 
Achana nao hawa ndio wale wabunge wanaofikiria kwa udhaifu hawataki kutafuta suluhu na madokta wamekazana kutafuta mchawi.yeye kila mwezi ana zaidi ya 10m anashida gani? kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
 
Hii ni kashfa, mlata umewatusi madaktari, waombe radhi ama umetangaza vita na madktari,
 
Hivi ni kwanini wabunge wa CCM wanaona watanzania hawana akili na utashi wa kudai chochote bila ya 'watu fulani'? Na kwa nini Spika hakumtaka Mlata athibitishe madai yake kuwa madaktari wanalipwa ili kufanya nchi isitawalike?

Katiba mpya ije haraka maana wabunge wa viti maalum CCM ni mzigo kwa walipa kodi.
 
Sasa hivi wasikilize wabunge wanabwabwaja . Jimboni mwangu hatuna Daktari tunaomba Ofisi ya Waziri Mkuu ituletee Daktari ,
Sikia Sasa Waziri Mkuu "Liwalo na liwe " Nchi hii ina laana
 
Huyu halikuwa hana cha kuongea....kuna wabunge wengine ni heri warudi makwao tu wakalee wajukuu...kweli TZ kichwa cha mwendawazimu !
 
"ama kweli the beautiful ones are not yet born" mnataka kumdelete dr. ulimboka kisa anatetea haki za madaktari. shame on you CHAMA CHA MAJAMBAZI
 
jamani viti maalum lazima uoneshe kitu flani hivi,sio makosa yake ni makosa ya kiti anachoitiwa.
 
Hiyo ni kweli, kundi la madaktari linaloanzia na g..... likishirikiana na dr. majeruhi wamechukua fwedha kuendesha harakati za mgomo kutoka chama kioja cha siasa tanzania na NGO nitaitaja baadaye ili kutoa madai yasiyotekelezeka. Hii ni aibu kubwa, eti kuendeleza maslahi ya chama hicho. ukilitazama kwa undani suala hili ni la kisiasa sana kwani daktari anayeanza kazi alipwe 3.5m huyo ambaye ni specialist alipwe ngapi? haya walimu wenye degree zinazofanana na za madaktari wanalipwa tshs ngapi? mshahara wa kuanzaia tshs 1,100,000 eti ni mdogo? acheni udwanzi sisi walimu tunalipwa 420,000 mnatofauti gani na sisi? hizo ni siasa chafu
 
Mheshimiwa Mlata ahujiwe na Police kwani inaonyesha anajua mengi so ni shahidi muhimu hahahahah!
 
Back
Top Bottom