Nondo na Cement za Dili zinahitajika haraka.

Acheni kujifanya wema sana,

Hii nchi bila kuiba kuendelea. Huyu jamaa sio wa kulaumiwa hata kidogo. Tumefika hapa sababu ya CCM. Hiyo bei anayoita ya dili kwa nchi zingine ndio bei halali. Ilitakiwa na kwetu owe hivyohivyo.

Jiulize Cement from Pakistani pamoja na faida ya Wapakistan
+ faida ya importer wa kibongo
+ usafiri
+ storage
+ kodi zote
Bado inauzwa 12,000/-, pungufu kuliko yetu ya hapo tegeta.

Nondo ndio usiseme, Mandela Road tu kuna viwanda vingi tu, wacha mikocheni.

Bado tunagongana bei za kuua. Halafu mnadai mna uchungu na mali kuibiwa, wakati wengi wetu nasi wezi tu. Tunaiba muda wa mwajiri kuja hapa JF na hatujioni.

Mkuu LBG, ukipata hivyo vifaa vikabaki nipasie kaka, achana na hawa wanaojifanya wana uchungu kumbe nao wamesomeshwa kwa hela ya dili!!
 
Umenikumbusha a desperate moment when i was soooo happy about the corrupt system in tz!
Iba baba, mie nikikutana na mtu anataka kuipa hela serikali namfundisha ninachojua kukwepa kulipa!
 
Hii nchi ina maajabu sana!!

Acha hizo mkuu, hili umeona na hili nalo ni ajabu?

Hii nchi tu yenyewe ni ajabu tosha.

Ndio nchi pekee ambayo wanafunzi wanafaulu STD 7 bila kujua kusoma wala kuandika.

Ndio nchi pekee ambayo Billioni ni vijisenti tu.

Ndio nchi pekee ambayo Muungano wa nchi mbili umezaa nchi mbili.


Ndio nchi pekee ambayo hata Rais wake hajui kwanin nchi yake ni maskini.
 
Bado sijamuelewa mleta huu uzi, msichukulie kiurahisi inawezekana anahitaji huduma za akili huyu.
 
Wabongo unafiki ndio unatuponza, ebu wote mliochangia na unayekuja kuchangia ebu nijibuni,
nani hajawahi nunua kitu kwa njia ya dili?
Nani hajawahi faulisha mzigo wake kastam kwa njia ya dili?
Nani ambaye hajawahi kutoa au kupokea rushwa?

mumewakia msela utafikiri nyinyi wenyewe ni wasafi!

vitu vya dili vimegawanyika kuna vya uwizi na halali vipo vingi!
mfano mabati ya dii mtu anaweza yapata ya dili yale ya uzio wakimaliza jenga ghorofa, mfano mtu anaweza pata mbao za dili zile zinazotumika kuweka makenchi ghorofa ikijengwa hiyo ni mifano michache
 
Inawezekana huyo jamaa anafanya kazi kwenye kiwanda mojawapo cha nondo au cement na labda kuna wizi ambao wameshindwa jinsi ya kubaini. Njia mojawapo ni kutangaza hichi kitu, then mtu anaweza kujitokeza na akamuuzia baadaye akakamatwa. Huo ni ujanja ujanja!
 
Inawezekana huyo jamaa anafanya kazi kwenye kiwanda mojawapo cha nondo au cement na labda kuna wizi ambao wameshindwa jinsi ya kubaini. Njia mojawapo ni kutangaza hichi kitu, then mtu anaweza kujitokeza na akamuuzia baadaye akakamatwa. Huo ni ujanja ujanja!
teh teh teh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom