Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,407
- 31,388
Labda una maana hatujaamua kumuondoa! kuweza kumuondoa tunaweza kabisa. Wakati wa kampeni katiba yetu ilielekeza kuwa wagombea waende kwa wananchi waombe ridhaa. Ridhaa maana yake waombe ajira!Back to square one.
Hatujamwajiri rais wetu. Katiba yetu haituwezeshi sisi kumwajiri rais.Hatuwezi hata kumwondoa, the same system ipo kwenye vyama mbadala, kuna watawala na wengineo ni watwana. Hata ukiamua kugombea nafasi fulani huruhusiwi kwa sababu wewe ni mtwana. Sasa hiyo ndiyo tuiondoe.
Tunapenda kujiaminisha kuwa tumewaajiri hawa wanasiasa ilhali hao ndio wametuajiri tuwafanyie kazi na kuwatajirisha. Dah!! aliyegundua pilau ana akili kuliko Einstein.
Kumbu kumbu zangu zinaonyesha orange revolution kule Ukraine(kama nipo sahihi) ni matokeo ya waajiri kuiweka kando katiba kwanza ili washughulike na tatizo halafu walirudi kutengeneza katiba.
Kuna kitu kinaitwa 'radical therapy' hasa pale 'conventional therapy' inaposhindwa. Je, si wakati sasa wa kuwa na radical therapy!
Tatizo la Watanzania ni kutojiamini na kuamini kuwa hawawezi. Hapo wajanja wanatumia udhaifu wetu kuleta hadithi, ngano na mashairi. Ndiyo maana tunadanganywa na maneno mchakato, linazungumzika, amani na utulivu, wasikivu,wazee wa Dar n.k.