Nmeipenda sana kauli ya kiongozi huyu wa dini

MELODY

Member
Apr 6, 2012
23
11
Katika maadhimisho ya Ijumaa kuu Askofu Mkuu kanisa Katholiki Jimbo la Arusha Josephat Lebulu alisema"...Matumizi ya mabavu ambayo hufanya makundi ya watu kukaa kwa siri na kupanga mbinu za kumwangamiza mtu asiye na hatia na wakati mwingine hata kuhonga mahakama zipotoshe hukumu dhidi ya wanyonge"Mwananchi 7th april 2012.
Hukumu ya Lema haikuwa ya haki.

ASANTE BABA KWA KUWA MKWELI NA MTETEZI WA HAKI KWA WANAKONDOO WAKO
 
Mkuu mbona unamuita mama wakati huyo aliyetoa hiyo kauli ni baba askofu?
 
Katika maadhimisho ya Ijumaa kuu Askofu Mkuu kanisa Katholiki Jimbo la Arusha Josephat Lebulu alisema"...Matumizi ya mabavu ambayo hufanya makundi ya watu kukaa kwa siri na kupanga mbinu za kumwangamiza mtu asiye na hatia na wakati mwingine hata kuhonga mahakama zipotoshe hukumu dhidi ya wanyonge"Mwananchi 7th april 2012.
Hukumu ya Lema haikuwa ya haki.

ASANTE MAMA KWA KUWA MKWELI NA MTETEZI WA HAKI KWA WANAKONDOO WAKO

Hapo ndipo viongozi wa dini wanapo kuwa wanapotoka. Akiulizwa atoe ushahidi wa haya aliyosema atasema Hana, ila wao wakiambiwa wanauza dawa za kulevya utasikia wanasema lalamika. Hiki ni chombo huru cha maamuzi wasikiingilie hata chembe.
 
Alishawahi muombea Fisadi kuwa kaonewa alipoangushwa katika U-PM so huwa siamini sana kauli zake. Ni uzao wa Mafisadi tu huyo
 
Askofu huyo, ni mkweli hataki unafiki, maaskofu wote wangesimamia ukweli nchi ingekombolewa haraka.
 
Hapo ndipo viongozi wa dini wanapo kuwa wanapotoka. Akiulizwa atoe ushahidi wa haya aliyosema atasema Hana, ila wao wakiambiwa wanauza dawa za kulevya utasikia wanasema lalamika. Hiki ni chombo huru cha maamuzi wasikiingilie hata chembe.

Atakuambia yeye mchungaji wa kondoo wa bwana anachunga kondoo popote.
 
Hapo ndipo viongozi wa dini wanapo kuwa wanapotoka. Akiulizwa atoe ushahidi wa haya aliyosema atasema Hana, ila wao wakiambiwa wanauza dawa za kulevya utasikia wanasema lalamika. Hiki ni chombo huru cha maamuzi wasikiingilie hata chembe.

In theory mahakama ni chombo huru lakini in practice mahakama zetu zinaingiliwa na serikali kulazimisha maamuzi fulani. Ukweli huu ulisemwa majuzi na jaji mkuu mstaafu (akaondolewa na stahili zake ikiwemo ulinzi). Kuna jaji alitoa injunction saa 2 usiku ili kumruhusu Kitwana Kondo agombee umeya, kuna mwingine alimnyima Mtikila nafasi ya kujitetea na akamfunga kwa maelezo ya upande wa mashtaka pekee. Mifano ni mingi.
 
Me sipendi watu wa makanisa na misikiti kuingilia mambo ya kisiasa hadharani kiasi hiki. Tunajua wana mapenzi na vyama vya siasa, lakini Askofu anaposimama hadharani au Shekh kuzungumzia kitu ambacho kinaonesha bias uupande mmoja, tunagawanyika kwa misingi ya dini ilihali lengo letu ni kutaka ukombozi wa nchi yetu. Wakristo wanapenda na kuyaunga mkono matamko ya maaskofu, waislamu wanapenda na kuyaunga mkono matamko ya mashekh...tukiendekeza matamko ya maaskofu na mashekh, tunazidi kugawanyika kwa misingi ya dini na adui yetu CCM anazidi kushamiri na kujiimarisha zaidi. Kitu ambacho kinachelewesha mabadiliko tunayoyataka.

Hawa watu wa dini wazidi kuwaombea waumini wao wamche mungu na waache ufisadi na siyo kutoa matamko ambayo hayana mashiko kwa taifa. Na kama ni muhimu kufanya hivyo, basi wakutane wote Maaskofu na Mashekh watoe matamko kwa pamoja na siyo kupingana hadharani kama ilivyokuwa kipindi cha Mauaji ya Arusha February 2011.

Mambo ya siasa watuachie waamini wao ili tuendeleze jitihada za ukombozi, kama wanawashwa na wanahamu sana ya kujiunga, wavue majoho na kanzu waingie kwenye siasa tufahamu si watu wa makanisa au misikiti tena. Tukiendeleza mambo ya udini, TANZANIA TUNAYOITAKA IKO MBALI SANA, PENGINE HATA SIYO KIZAZI CHETU....ASANTENI.
 
Askofu huyo, ni mkweli hataki unafiki, maaskofu wote wangesimamia ukweli nchi ingekombolewa haraka.
siyo maaskofu wote tu...ni viongozi wote dini zote wanatakiwa wafanye hivyo...cha kushangaza wengine dhulma kama hizi hautasikia wakizipgia kelele , wenyewe wanasubiri matokeo ya form iv na vi ndiyo waanze kulalamika kuwa wanafanyiwa dhulma kumbe ni uzembe wao wenyewe...ukombozi wa kifikra utachukua muda mrefu sana tanzania mpaka tuupate...!
 
Hapo ndipo viongozi wa dini wanapo kuwa wanapotoka. Akiulizwa atoe ushahidi wa haya aliyosema atasema Hana, ila wao wakiambiwa wanauza dawa za kulevya utasikia wanasema lalamika. Hiki ni chombo huru cha maamuzi wasikiingilie hata chembe.
Maamuzi ya kihuni ya kushurutishwa na wenye hela nayo unayaita maamuzi huru ya mahakama, hata Yuda alimsaliti Yesu lakini akaishia kujinyonga kwa tamaa ya hizi fedha, Na hata hawa wadhalimu wa haki hatutawasubiri wajinyonge bali ipo siku watakosa hata kuomba msamaha mbele yetu maana hawatakuwa na nafasi hiyo
 
Hapo ndipo viongozi wa dini wanapo kuwa wanapotoka. Akiulizwa atoe ushahidi wa haya aliyosema atasema Hana, ila wao wakiambiwa wanauza dawa za kulevya utasikia wanasema lalamika. Hiki ni chombo huru cha maamuzi wasikiingilie hata chembe.

Hoja za kitoto wauzaj dawa za kulevya unawafahamu kupeleka mahakaman unasubir nn?achen kutawala kwa ndoto na kauli za kulialia za nn?kama huwez kuongea kaa kimya.
 
Hapo ndipo viongozi wa dini wanapo kuwa wanapotoka. Akiulizwa atoe ushahidi wa haya aliyosema atasema Hana, ila wao wakiambiwa wanauza dawa za kulevya utasikia wanasema lalamika. Hiki ni chombo huru cha maamuzi wasikiingilie hata chembe.
Ha ha ha te te te ! Mkuu ni kweli makundi ya watu hukaa kwa siri na kupanga njama za kupindisha haki. Kuna thread humu inasema usalama wa taifa huko singida pia wamekaa kwa siri na viongozi wa ccm kumvua mh Lissu ubunge. Kuanzia mlingotini bagamoyo hadi kwa shehe yahya magomeni da slam kila mtu anajua ccm ni chama cha mashetani
 
Hapo ndipo viongozi wa dini wanapo kuwa wanapotoka. Akiulizwa atoe ushahidi wa haya aliyosema atasema Hana, ila wao wakiambiwa wanauza dawa za kulevya utasikia wanasema lalamika. Hiki ni chombo huru cha maamuzi wasikiingilie hata chembe.

Alipata kusema Bw. Yesu kwamba, wana masikio, lakini hawatasikia, na kwamba wana macho lakini hawataona.
Mkuu, sijui jina lako ni Dumela Mbegu au ni Dume la Mbegu? kama ni mswahili utajaza mwenyewe.
Je, wewe ni mgeni sana katika siasa za Tz hata usijue nini kinazungumziwa hususan maamuzi ya jaji katika kesi ya kuupinga ubunge wa mh. Lema?
Yawezekana unajua ila umejifunika blanketi la gamba lililokufanya usione wala kusikia.
Pole sana.
 
Back
Top Bottom