Ambassador
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 933
- 75
Leo shemeji/wifi yenu kaenda tawi moja la NMB jijini kuuliza taratibu za kufungua akaunti kwa ajili ya watoto akaambiwa apeleke fomu toka serikali za mitaa zenye picha ya kila mtoto na mama, pamoja na kopi za vyeti vya kuzaliwa. Wife akahangaika kupata docs na kuziwasilisha NMB akaambiwa vinatakiwa vyeti original pamoja na copy. Aliporudi na hizo original akaambiwa picha yake kwenye fomu masikio hayaonekani akapige nyingine!
Kilichofuata? Wife alikasirika na akaelekea CRDB. Huko akapewa fomu na kuambiwa apate sahihi za wadhamini wawili wenye akaunti CRDB, alete kopi za vyeti vya kuzaliwa na kitambulisho chake na mchezo ukaisha!
La kujiuliza hapa, kwa nini NMB hawakukagua vema hizo fomu na kutambua makosa yote ili wife asirudi mara mbilimbili? Na kwa nini hawakumpa maelezo ya kutosha mwanzoni kwamba waltaka original? Kwa kupoteza wateja watarajiwa wanne kwa wakati mmoja hii kwao sio issue kwa kuwa ni watoto na hawana pesa ya kuweka benki? Ofcourse kama wazazi wanojali tumeamua kuwafungulia akaunti ili kuwawekea akiba itakayowasaidia hapo baadae na lazima akaunti zao ziwe operational.
Kwa ndugu zangu wa NMB, wekeni taratibu zinazoeleweka na rahisi kwa wateja wenu ili kuepuka usumbufu na kujipotezea wateja. Onyesheni kwamba ninyi ni benki ya wananchi kweli. Au ndo mmebweteka? Shauri lenu...!!