NMB Temeke yavamiwa kwa mabomu; mmoja auawa; msako mkali!

kwani cctv shiling ngapi? yaani kama mtu kama mie nina cctv gheto iweje NMB washindwe?

hata haina gharama za kukaa kikao kirefu. Viduka (mini-supermarkets) vidogo tu hapo bongo vina cctv, bank wanashindwa nini?
 
Mkuu hii thread ipo tayari humu JF
__________________

si uunganishe...changia ...laah kimbia fasta
 
..
...kaka unachangia very low....hivi kwanini usizungumzie ubovu wa jumla wa jeshi la polisi...unaingiza weak point ya ushemeji...ulitaka aolewe dada yako.......?

.

..dada sina labda..uwe ..wewe!!!

..kwa nini hilo la ushemejii limekuuma...maana hakuna aliyelishangaa ati zaidi yako .....kwani si siri??

tukate ishuu..acha ku capitalize kwenye mambo yasiyo na kichwa wala miguu....kama mshkaji anachemka ..anachemka tu ....hata ukimpaka mafuta..atapauka upepo ukipita tu!!!

naendelea kutoa rambi rambi kwa waliopata msiba ...ni wetu wote!!
 
hakuna aja ya kuwasaka wakimbana vizuri

AFANDE KOVA...ATAWATAJIA WOTE.....HAWA WAHUNI MNAFIKIRI POLISI HAWAWAJUI...LOOOH....,
SHAME POLISI NA WANAJESHI...HAO LAZIMA KUNA WANAJESHI/MAPOLISI KWENYE HAO MAJAMBAZI..NA UKIONA WAMEFANIKIWA BASI UJUE HAPO MGAO WA WAZEE UPO AMA UMEELEWEKA..UKIONA WAMEKAMATWA JAMA WALIELEWANA KUTOELEWANA......KAZI KWELI KWELI
 
kwa mujibu wa taarifa ya habari ya itv inayoendelea,Waziri masha ''AMEFURAHIA SANA'' kuona askari wake walikuwepo eneo la tukio (let's take on time according to yeye)

WAKATI HUOHUO:imethibitika kwamba kuna mtu kapoteza uhai wake pale,na kuna majeruhi si chini ya kumi.
HABARI ZA KUTHIBITIKA ZINATUJUZA KWAMBA:askari walifika dk 15 baada ya tukio!........

LOL!huyu 'kijana' naona anatuona watanzania wote mabwege
 
Hali itakuwa shwari pengine baada ya uchaguzi kwisha

Such a fatalistic attitude. We are clueless and hopeless, "Hali itakuwa shwari pengine baada ya..." Why, kwa nini udhanie pengine tatizo litakwisha lenyewe, how, why?

Sisi kila kitu tunaombea na ku-wish na ku-hope na ku-guess, hatuna vitendo au mawazo tunasema tujaribu tufanye hivi na vile juu ya tatizo hili na lile. Kazi yetu ni kuombea na kusubiri tuuu... Pengine tatizo litakwisha!?!

Si wananchi, si polisi, hakuna mwenye clue au nia ya kutafuta pa kuanzia kutatua tatizo. Yule Kamanda Kova kazi yake kila siku yuko kwenye ma press conference kutoa news za uhalifu. I am like, when does he ever sit down and work, and think through these intractable deadly problems gripping the city, damn! Kova na Mwema wawajibishwe, na tuweke mapolisi kanzu ndani ya polisi.
 
Yaleyale...Toa basi mawazo ya nini kifanyike ili tatizo liishe
 
Such a fatalistic attitude. We are clueless and hopeless,

1. Ok.. wewe ni mmoja wao.. - so ur clueless and hopeless;

Sisi kila kitu tunaombea na ku-wish na ku-hope na ku-guess, hatuna vitendo au mawazo tunasema tujaribu tufanye hivi na vile juu ya tatizo hili na lile. Kazi
2. Ok.. wewe ni mmoja wao - hauna vitendo au mawazo..

Si wananchi, si polisi, hakuna mwenye clue au nia ya kutafuta pa kuanzia kutatua tatizo.
3. Ok.. wewe ni mmoja wa wananchi na hivyo huna "clue" wala nia..

Yule Kamanda Kova kazi yake kila siku yuko kwenye ma press conference kutoa news za uhalifu.
Ok.. hii ni ngumu kuthibitisha; kuwa "kila siku yuko" really?

I am like, when does he ever sit down and work, and think through these intractable deadly problems gripping the city,
unatafuta mahali pa kuanzia kutafuta suluhisho which IN FACT it negates all 3 premises you have created!
damn! Kova na Mwema wawajibishwe,
Still breaking your own 3 premises

na tuweke mapolisi kanzu ndani ya polisi.
you are trying to offer a plausible solution.. but should the people take it serious if they were to believe the three premises?

When you attempt to make an argument make sure u do not break one of enduring and fundamental rules of logic that is; to avoid internal contradiction. Something can not be or not be at the same time concerning the same thing as a whole not as a part!

So.. kama sisi sote hatuna clue wala nia wala vitendo vya kutafuta suluhisho la mamambo haya ya ujambazi na kama wewe ni mmoja wa sisi; then how come you have some ideas of how to deal with the problem?

this is logic 101.
 
Uchaguzi unakaribia tutasikia majambazi tena na ujinga mwingi .JK akisha aapishwa atasema acheni .JK kwenye kampeni atasema nimekaa madarakani muda wote ujambazio ulipungua nipeni muda zaidi nikawamalize kabisa .Hapa kuna swali kubwa sana .Je wewe huna la kujiulisha kutokana na hili ? Tulimsikia na tutamsikia tena .
 
Bado wapelekeni majeshi na polisi wote Pemba kuna fujo la uchafuzi, Mnashindwa hata kulinda mabenki na madini ya bara bado mnataka mafuta ya zenj. Pinda sema cha maana bungeni, onyesha kama unaweza kuweka ulinzi bara wa mabenki na ma-albino ndio utake madaraka ya zenj. huna na hutakua nayo sifa ya kuiongoza zenj.
 
Yaleyale...Toa basi mawazo ya nini kifanyike ili tatizo liishe

Ulinisoma ukamaliza aya nzima? Narudia, najinukuu:
Kova na Mwema wawajibishwe, na tuweke mapolisi kanzu ndani ya polisi.

Nakutafsiria, kama unataka twende pole pole sana: Ukiwabadilisha Mwema na Kova utatengeneza uwezekano wa uongozi mpya, na labda mawazo mapya na vitendo vipya.

Ukiweka makachero ndani ya Polisi unaweza kukamata majambazi walio infiltrate Polisi.
 
So.. kama sisi sote hatuna clue wala nia wala vitendo vya kutafuta suluhisho la mamambo haya ya ujambazi na kama wewe ni mmoja wa sisi; then how come you have some ideas of how to deal with the problem?

this is logic 101.
Patamu hapo!
 
Njia ya kukomesha wizi wa silaha kwenye mabenki ni hii ifuatayo:

(1) Kuwe na CCTV (closed circuit television) kwenye kila tawi. Hii inarekodi yote yanayoteokea. Milango iwe remotely controlled.

(2) Kuwe na control room ambayo ni secure and hidden from view.

(3) Afisa aliyeko control room anajifungia humo, anaona sehemu za milango na zenye fedha, na hatoki mtu bila yeye kubonyeza button ya kumfungulia.

(4) Lazima kila tawi liwe na backup power supply

Haya yanawezekana na gharama yake si ya kutisha. Ni mambo yanayofanywa na mabenki ya Ulimwengu wa Tatu vile vile, sio ya nchi zilizoendelea tu.
 
ni jambo la kusikitisha sana na pia natoa pole kwa wote wafiwa na majeruhi kutokana na tukio lililo tokea ikiwa police wote wamepelekwa pemba kulinda daftari la uchanguzi sasa unategemea nini hii ni yakulaumiwa ni serikali haiwezekani pahala hakuna wezi na kumetulia leo mnawapeleka police na mnaacha kupeleka askar kwa wingi kwenye matatizo wanapelekwa pemba ili walinde madaraka yao kutisha raia ambao hawana silaha wasiandikishwe kwenye daftari ili wapate kuiba kura unategemea nini mimi napenda waziri wa mambo ya ndani ajiuzulu wakati anajua kuwa majambazi siku hizi wamejitoa kafara wao wamepeleka askari pemba makubwa
 
Njia ya kukomesha wizi wa silaha kwenye mabenki ni hii ifuatayo:

(1) Kuwe na CCTV (closed circuit television) kwenye kila tawi. Hii inarekodi yote yanayoteokea. Milango iwe remotely controlled.

(2) Kuwe na control room ambayo ni secure and hidden from view.

(3) Afisa aliyeko control room anajifungia humo, anaona sehemu za milango na zenye fedha, na hatoki mtu bila yeye kubonyeza button ya kumfungulia.

(4) Lazima kila tawi liwe na backup power supply

Haya yanawezekana na gharama yake si ya kutisha. Ni mambo yanayofanywa na mabenki ya Ulimwengu wa Tatu vile vile, sio ya nchi zilizoendelea tu.

Nakubaliana na mapendekezo yako isipokuwa nilipo highlight red. Hivyo inamaanisha hata vyumba vya ATM havina cctv?
 
Ulinisoma ukamaliza aya nzima? Narudia, najinukuu:

Nakutafsiria, kama unataka twende pole pole sana: Ukiwabadilisha Mwema na Kova utatengeneza uwezekano wa uongozi mpya, na labda mawazo mapya na vitendo vipya.

Ukiweka makachero ndani ya Polisi unaweza kukamata majambazi walio infiltrate Polisi.

You can not do that!
 
Nakubaliana na mapendekezo yako isipokuwa nilipo highlight red. Hivyo inamaanisha hata vyumba vya ATM havina cctv?

Labda hujamwelewa anasema kwenye chumba hicho Control Room hawezi toka mpaka ajifungulie mwenyewe...sio mtu yuko nje amfungulie....
 
..dada sina labda..uwe ..wewe!!!

..kwa nini hilo la ushemejii limekuuma...maana hakuna aliyelishangaa ati zaidi yako .....kwani si siri??

tukate ishuu..acha ku capitalize kwenye mambo yasiyo na kichwa wala miguu....kama mshkaji anachemka ..anachemka tu ....hata ukimpaka mafuta..atapauka upepo ukipita tu!!!

naendelea kutoa rambi rambi kwa waliopata msiba ...ni wetu wote!!

Mtu mzima unachangia Pumba!!!...Wewe ndie uliekuja na mambo yasio na kichwa wala Miguu..eti Mambo ya Ushemeji...?Who cares....?
 
Tatizo la polisi wa Masha na wenzake wameku-trained kufocus kwa waandamanaji wasio na silaha wanaopinga matokeo ya uchaguzi tu. Hili linathibitishwa na kitendo cha kupeleka askari wa kuzuia ghasia (FFU) kupambana na majambazi, unatarajia nini?. Umefika wakati sasa watawala wajue kuwa kazi ya kwanza ya Polisi ni usalama wa raia kama ilivyokuwa madhumuni ya kuwa na jeshi la polisi na nembo yao inavyosomeka (USALAMA WA RAIA) na si usalama wa CCM kwenye uchaguzi. Tukiwa na mtazamo huo basi polisi watapewa vifaa vya kupambana na watu wenye silaha badala ya watu wasio na silaha (raia wema walionyang'anywa haki yao cha kuchagua viongozi)

Kwa madhumuni ya sasa ya polisi wa Masha na wenzake, linapokuja suala la wazee wa kazi (majambazi) inawabidi wasubiri kwanza jamaa wamalize kazi yao ndiyo wakawahoji victims, na kutangaza uharibifu uliopatikana. Yaani kutoka hapo NMB Temeke na Polisi Chang'ombe ni mwendo wa 30 seconds kwa gari lenye askari waliojidhatiti kwa kazi za kipolisi badala ya kulinda kura za watu fulani. Tatizo ni kwamba huwezi kupeleka askari kichwa kchwa kwenye defender liliwazi la kuonea raia wasio na silaha ukapambane na majambazi wenye silaha za kivita, mtauwawa kama sisimizi, na ndiyo maana jamaa waliogopa hilo, unakumbuka tukio la Kawe?.

Kama askari polisi wangekuwa trained kupambana na matukio kama haya badala ya wapiga kura wasio na silaha, wakapatiwa vifaa, kama bullet proof vehicles nina uhakika hawa majambazi wangekamatwa on spot.
 
Last edited:
Inasikitisha sana kuona serikali ambayo wananchi tunaumia kulipa kodi kuiweka madarakani ituhakikishie usalama haioni kama ni jukumu lake kuhakikisha tunakuwa salama. Hivi siku hizi kila ukienda benki huna uhakika kama utatoka salama. Na kinachosikitisha kuwa hawa watu hawakamatwi.

Hili ni tatizo lililomea mizizi katika jamii. Kosa la wizi ni lile lile moja, tatizo ni mazingira tu. Huyu aliyeiba BOT bila kufunguliwa mashtaka, labda kwa kuwa hakutumia silaha hatumchukulii kama ni mwizi. Kwa kuwa jamii yetu ni yenye kubariki vitendo visivyo halali kwa kuwakumbatia wahalifu hatuoni kama ni tatizo, mpaka pale damu inapomwagika.

Kuna watu wangapi mitaani wanaishi maisha ya kifahari wakati kazi wanazozifanya hazithibitishi kuwa wanaweza kuwa na vipato hivyo? Tunachoweza kukifanya mitaani ni kusifia tu, hili ghorofa ni la fulani, kama ni kijana ataitwa bosi mtoto, bila kuhoji alipataje fedha za kuweza kujenga jengo hilo tena kwa muda mfupi bila kusimama. Mifano ipo mingi, wananunua magari ya kifahari na vitu kama hivyo bila kueleweka wameupataje utajiri.

Rais alisema anayo orodha ya majambazi anawapa muda wajirekebishe!! Hapo tunajifunza nini? ni kama alivyowapa muda watu wa EPA kurudisha fedha, kwa hiyo ni suala la kuiba na kugawana tu!! hawaoni umuhimu wa kutulinda.

Ni lazima ifike wakati tuwe na maadili kama wanadamu tunaoishi kwenye jamii yenye sheria na kuheshimiana. Kila mtu akimthamini mwenzake kama binadamu ataheshimu hata haki yake ya kuishi. Mtu mmoja anapojisikia anahaki ya kutoa hata uhai wangu huko ni kukosa utu na maadili, na hii lazima tuifundishe hata kwa watoto wetu. Kuiba ni kosa, haijalishi kama umetumia silaha au mdomo ni kosa na watu wote lazima wawe chini ya sheria.
 
Back
Top Bottom