NMB Temeke yavamiwa kwa mabomu; mmoja auawa; msako mkali!

ni kweli majambazi hao wamevamia leo hii na kibaya zaidi wameua na kujeruhi. ujambazi wao ni wa hali ya juu maana wanatumia mabomu. ili kuona baadhi ya picha za tukio hilo angalieni blog ya full shangwe, issamichuzi nk.
 
Hizi benki kusogezwa karibu na wananchi inatakiwa na ulinzi pia kuongezwa. Ni risk kuweka benki Mbagala au Temeke
Huko ndio kwenye wateja wenyewe kitu cha msingi ni kuhakikisha usalama unakuwa sehemu zote
 
Ikiwa hawa wezi hawatakamatwa au walau sura zao kunaswa, basi majambazi ya nchi za jirani watahamishia kambi zao hapa Bongo.
 
Taarifa za kipolisi zinasema tukio hilo lilitokea mwendo was saa 5:30 asubuhi, na majambazi walitinga hapo na magari mawili Toyota Prado (SU) na Landrover Defender (STJ). Waliingia ndani na kujifanya wateja kabla ya kuanza kufyatua risasi. Mlinzi wa kampuni ya kujitegemea alitwangwa risasi na kufariki, polisi wawili walijeruhiwa vibaya. Kiasi cha fedha kilichoporwa bado hakijajulikana, lakini inakisiwa ni zaidi ya 150 milioni.
 
...inasikitisha ...mafanikio dhidi ya ujambazi ndio vita pekee aliyobaki anajivunia nayo kijana jk...kuwa amefanikiwa...sasa kama na hili litamshinda atabaki na nini...

tunasikitikia vifo kwanza vilivyotokea,vya askari wetu na wananchi ..hasa askari wanaolinda benki katika zama hizi kwenye mazingira magumu bila kupewa hata mavazi ya juu bullet prooof...wangekuwa nazo pengine wangeepuka kifo....

inashangaza tukio limetokea jirani na tukio la polisi changombe.....ni vigumu hata kufikiria kusema IGP afikirie upya mfumo wake au ajiuzulu.Si mnajuwa IGP ni semejiii kabisa wa KIKWETE ....yaani kaoa damu damu..baba moja!!!...sasa hapo itabidi tumeseme kishkaji..tu ...[eeh bwana IGP jitaidi bwana ...panga safu yajo na angalia formation na war strategies zako ,si unajuwa angekuwa mwenzangu na mimi ukizingatia na mauwaji ya tarime daily ungekuwa huna kazi???? usituangushe ...shemejiiiiiiii]
 
Ni siku ya majonzi na hasira; Wakati tunapiga vita uporaji mkubwa wa raslimali zetu wapo wengine ambao nao wanapora hata kile kidogo ambacho watu wameamua kujiwekea kwenye benki. Ni uhalifu ambao hauna uhalallisho wa aina yoyote na hakuna maelezo ya kutosha kuelezea umantiki wake. Ni uhalifu ambao ungeweza kutokea sehemu yoyote duniani na hausiani na kukosekana kwa CCTV, umaskini, jeshi kujipanga vibaya n.k Haya yote yanaweza kuchangia katika urahisi wake lakini ni wazi kuwa hawa watu walikuwa wamekusudia kufanikiwa.

Tutapiga kelele baadaye lakini wakati huu ni kuwatia hamasa polisi wetu na vyombo vyetu vya usalama kuhakikisha watu hawa wanatiwa mbaroni (mambo ya kukutana huko mitaani na kurushiana risasi halafu yaishe siyaungi mkono). Lakini Polisi wafanye kazi yao kwa nguvu zote kuhakikisha kuwa wahusika wote wanatiwa mbaroni na kushughulikiwa kisheria.
 
...inasikitisha ...mafanikio dhidi ya ujambazi ndio vita pekee aliyobaki anajivunia nayo kijana jk...kuwa amefanikiwa...sasa kama na hili litamshinda atabaki na nini...

tunasikitikia vifo kwanza vilivyotokea,vya askari wetu na wananchi ..hasa askari wanaolinda benki katika zama hizi kwenye mazingira magumu bila kupewa hata mavazi ya juu bullet prooof...wangekuwa nazo pengine wangeepuka kifo....

inashangaza tukio limetokea jirani na tukio la polisi changombe.....ni vigumu hata kufikiria kusema IGP afikirie upya mfumo wake au ajiuzulu.Si mnajuwa IGP ni semejiii kabisa wa KIKWETE ....yaani kaoa damu damu..baba moja!!!...sasa hapo itabidi tumeseme kishkaji..tu ...[eeh bwana IGP jitaidi bwana ...panga safu yajo na angalia formation na war strategies zako ,si unajuwa angekuwa mwenzangu na mimi ukizingatia na mauwaji ya tarime daily ungekuwa huna kazi???? usituangushe ...shemejiiiiiiii]
..
...Kaka unachangia Very low....Hivi kwanini usizungumzie Ubovu wa Jumla wa Jeshi la Polisi...Unaingiza weak Point ya Ushemeji...Ulitaka aolewe dada yako.......?

Back kwa Tukio....Yapasa lilaaniwe kwa nguvu zote na wahusike wakamatwe....Kuna Uzembe kwanza kwa Polisi na pia kwa NMB kudharau umuhim wa technologia.
 
Yoyo nadhani hauelewi ama haujui unachokiongea au you are out of your mind. Iweje risasi zinawaka wewe una unapiga video yako... Hiyo siyo kabumbu elewa ni risasi. Umeambiwa askari wenye silaha za moto wamelala chini ama wameuawa ama kujeruhiwa, iweje mtu ni kijicelular chacke?

Anyway unawapa hongera kwa kutenda maovu, inaelekea na wewe ni mwanachama
labda nimeongea kitu kigumu kukielewa......zile picha unazoziona kabul na baghdad unafikiria zinachukuliwaje? nenda kule liveleak.com uone clip za wanaojua kutumia simu za mkononi kurusha habari......
 
zuzu wewe
 
wengine wanaiba kwa kalamu (ufisadi/rushwa)
wengine wanaiba kwa silaha

mwizi wa silaha akikamatwa anatumia kalamu(rushwa) kutoka nje

kama tusipozuia wizi wa kalamu kamwe hatutoweza kuzuia wizi wa silaha kwa ajili mwenye silaha atatumia kalamu akikamatwa
 
Kitendo cha Ujambazi uliotoka leo Temeke ni lazima Ulaaniwe kwa nguvu zote.Imefika wakati sasa Jeshi la Polisi pia litazamwe upya,kuna polisi wengi wanashiriki katika Vitendo hivi vya Uizi.Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani/ Polisi kuna malalamiko Mengi kuhusu Polisi wanaoshiriki vitendo kinyume cha Maadili yao ya kazi.Viongozi wa Polisi wana majina ya Polisi hao.......Kuna Maelezo wazi kuwa Polisi wa Temeke mara nyingi wanashirikiana na Majambazi na wanawajua wahalifu hao.

Ni mwaka jana mwishoni Mkuu wa Kanda ya kipolisi Temeke Rpc.Edward Kinabo alikamatwa kwa tuhuma ya kupokea Hongo ya Tshs 30,000 katyika sakata la Nyumba za NHC,Sasa kama Mkuu wa Polisi anakuwa na tabia hiyo ni vipi Polisi wadogo wadogo ambao wana kipato kiduchu?Imefika wakati sasa Jeshi la Polisi liangaliwe Upya.....Kuna fununu kuwa Baadhi ya Majambazi wa leo walikuwa Polisi na wanaufahamu Vizuri mfumo wa Ulinzi wa Benki iliyovamiwa,kulikuwa kuna pesa nyingi ambazo zilikuwa zisafirishwe kupelekwa Makao makuu ya Benki hiyo.Ni wazi kuwa kuna Wafanyakazi pia walishiriki zoezi zima la Uizi.

Mwenyewzi mungu awalaze peponi waliofariki katika Tukio hilo...Na wale wote waliopata majeraha tunawatakia nafuu ya mapema.
 
Back
Top Bottom