NMB Temeke yavamiwa kwa mabomu; mmoja auawa; msako mkali!

Shukuru

JF-Expert Member
Sep 3, 2007
748
15
Jamani kuna mtu kanipigia simu kuwa bank NMB ya tawi la temeke maeneo ya Mwembeyanga limevamiwa..

je kuna ukweli kuhusu hili na kama kuna mtu aliye karibu na eneo la tukio Plz bring news to us maana nasikia mapambano kati ya polisi na majambazi bado yanaendelea
 
Last edited by a moderator:
Km ndio hivyo we are at risk, hawa majambazi kuelekea kwenye chaguzi isije kuwa hivi vyama vyetu vya kisiasa ni njia yao mbadala ya kujipatia kipato.
 
Title nadhani imekosewa, ni NMB na si MNB... Tumerekebisha hilo.

Naona mwisho wa mwezi umefika na watu wanachukua chao mapema...!
 
Ni kweli, ndugu yangu alikuwemo humo ndani ya benki yeye amejeruhiwa na watu walikuwa wakigombania mlango kutoka baada ya majambazi hao kutoka. Ameniambia majambazi hao wamefanikiwa kutoroka na fedha nyingi kutoka benki na wateja wa benki hiyo. Walinzi na askari ama wameuawa au kujeruhiwa takriban walinzi watatu walikuwa wamelala chini ama wakufa au kujeruhiwa. Tukio lilikuwa kama mchezo wa filamu.
 
Mambo haya yataendelea sana kutokea kadri hali ya uchumi inavyozidi kuzama.Ajira hakuna ,Walinzi yaani polisi wamekata tamaa,wananchi wana hasira na serikali yao,Kwani haijakidhi matarajio yao.Maisha bora kwa kila Mtanzania.Sasa majambazi wameamua kujitwalia maisha bora mkononi.Nani alaumiwe????
 
Hizi benki kusogezwa karibu na wananchi inatakiwa na ulinzi pia kuongezwa. Ni risk kuweka benki Mbagala au Temeke
 
Hawa si wale majambazi Mkuu wa Polisi juzi alisema wameingia Dar toka Kenya?

Wako wengi na silaha kibao- tuwe macho!

Huu ndo ujirani mwema??
 
Hizi benki kusogezwa karibu na wananchi inatakiwa na ulinzi pia kuongezwa. Ni risk kuweka benki Mbagala au Temeke

haya maeneo unayafahamu Mkuu? inawezekana uliiona Temeke kwa mara ya mwisho siku nyingi sana. Temeke ni ndani ya City aise.
 
Hawa si wale majambazi Mkuu wa Polisi juzi alisema wameingia Dar toka Kenya?

Wako wengi na silaha kibao- tuwe macho!

Huu ndo ujirani mwema??

Sasa kwa nini wasiwakamate kama wamewaona wameingia nchini na wanawajua!? Au wanasubiri wafanye matukio ndio wawakamate!?
 
Ni pale ambapo mtu mmoja alipokuwa anapeleka fedha ndani ya bank alivamiwa gafla na majamazi hayo wakiwa wawili ndipo walipotokea polisi wawili kuanza kupamabana kwa risasi haliyopelekea polisi wawili kupata majeraha mabaya sana na mauututi
 
Tujulishane ukweli wa Wizi kwa kutumia silaha za kivita (mabomu) ktk bank ya NMB temeke na kusababisha kifo cha mtu mmoja
 
Jeshi la polisi lilitoa tahadhari kwa mabenki mwezi ulopita juu ya majambazi yenye silaha kujiandaa kwa uporaji katika taasisi za fedha,binafsi niliwasifu kuwa inteligensia yao inaenda na wakati,lakini kwa hili kama kweli majambazi yamevamia benki na kupora na kutokomea kiulaini namna hii basi kuna mahala ndani ya jeshi la polisi kuna ubovu,haiwezekani uwaambie watu wachukue tahadhari huku mtoa tahadhari ukiendelea kulala...Labda kama na wao wanahusika otherwise nasubiri taarifa ya hayo majambazi kukamatwa au kuuawa,ni imani yangu jeshi lilikuwa katika tahadhari ya juu sana.
 
Ni kweli wizi umetokea, inasemekana ni vijana wadogo tu walikuwa na bunduki pamoja na vitu vinavyodhaniwa ni mabomu ambapo mashuhuda wanasema vilikuwa mithili ya simu za mkononi ambavyo walikuwa wakirusha wakati wanaondoka.

Jamaa hao walikuwa na Toyota Land Cruiser ya Kijani na walitoroka kuelekea njia ya Tandika. Kweli wamechota mihela maana inasemekana walikuwa na begi
"Rack Sack" kubwa tu lililokuwa limejaa mihela. Mhanga mmoja alisalimisha fedha zake TZS 2,000,000 alizokuwa akimtumia Baba Yake.

Majeruhi ni wengi, na inasemekana Askari Polisi wawili walipigwa risasi kabla jamaa hawajaingia ndani.

Polisi walifika eneo la tukio kama baada ya dakika kumi na tano.

Kweli ilikuwa kama action movie.
 
Back
Top Bottom