Ndugu wana JamiiForums,
Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.
Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.
Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe Siri)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.
4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Nmb kwanini mnapenda kuona watu wamepanga mstali mrefu kwenye bank zenu kusubiria huduma?aisee uwajibikaji kwenu mm naona ni sifuri na Bahati yenu mna matawi mpaka vijijini isingekuwa ivyo hakika crdb wangewapita kwa kasi ya ajabu
nimefungua A/C ila sijapewa ATM Card,je naweza kuchua pesa? ikiwa tayari nina Account Number?
Mimi nilisumbuliwa kidogo niaibike .....
Haiwezekan kuchukua ela bila kadi ...
pole kwa yaliyokukuta,asante kwa kunipa taarifa muhimu.
Asante nimeshawishika kufungua account ya CRDB ila nataka nione kwanza huduma za NMB
CRDB wako poa sana.