NMB Bank

Darwin

JF-Expert Member
May 14, 2008
908
56
Kama kuna waajiriwa au wakubwa wa NMB hapa, sio kwamba nataka kuiua biashara yenu ila nataka kuuliza.

Nipeni sababu yakuwa mteja wenu?

ATM foleni tena sio foleni ya watu kumi
Banking foleni hivyo hivyo
Card zenu huwezi kuchukua kwenye bank nyingine.
Ukitaka kwenda NMB umeshaanza kupata uvivu hata kabla hujaliona jengo la NMB

Kiufupi nikwamba NMB service zao ni poor kama nini.
Nashangaa watu wengi wanaipenda hii Bank wakati inajulikana kama bank ya karaha.
 
wengi ni walimu ndugu yangu.....sijui walilazimishwa wawe na ac kule
 
wengi ni walimu ndugu yangu.....sijui walilazimishwa wawe na ac kule

NMB Imetokana na NBC ya Zamani ambayo iligawanyika kwensa NBC na NMB, kutokanana Historia ya NBC ya Zamani ilikuwa ni benk yenye matawi karibu kila wilaya ya Tanzania, kumbuka kuwa wakati serikali inafanya zoezi la utambuzi wa GHOST workers walitoa agizo la mishahara yote kupitia Benki tofauti na ilivyokuwa mwanzo wakati tunachukua mishahara madirishani, Hivyo katika kufikia huko NBC kwa kuwa ina coverage kubwa ndiyo benki iliyotumiwa sana na ndiyo inayotumiwa kuwafikia watu wengi Vijijini.
 
Ukitaka kuona faida ya NMB safiri kwenda wilayani...lakini kama uko dar,Arusha,mwanza hutaona faida ya kuwa na account NMB
 
Sio tu huduma zao ni mbaya; wafanya kazi wao ni jeuri kwa wateja hawajui kabisa mambo ya customer care; ukitaka kujionea wafanyakazi wa benki jeuri we nenda pale tawi lao la Mwenge lililopo nyumba moja na TRA!! Ujeuri wao umenifanya nifunge account yangu hata nikauza hata hisa zao kwani nilijua uzembe wao utaathiri thamani ya hisa zao ambazo kweli zimeshuka kwenye soko la hisa!!
 
Kamanda wewe kama mimi.
 
wengi ni walimu ndugu yangu.....sijui walilazimishwa wawe na ac kule

mama me si mwalimu ila nina account kule kunachosha ka nini ...jtatu mpaka jmos foleni
si ATM or ndani ya bank yenyewe .
ni vyema kuwa na account nyingi ili ukikwama hapa unahamia pale .naipenda CRDB bank .
 
Hamia Benki nyingine. Hii ndiyo moja ya faida kiduchu za utandawazi. Kma huduma mbovu basi unaenda Benki nyingine zeney huduma bora zaidi. JARIBU CRDB Bank!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hamia Benki nyingine. Hii ndiyo moja ya faida kiduchu za utandawazi. Kma huduma mbovu basi unaenda Benki nyingine zeney huduma bora zaidi. JARIBU CRDB Bank!!!!!!!!!!!!!!!

Benki zote bwana ni yale yale. CRDB wana tawi pale banana utakoma...linapoteza network kishenzi
 
Back
Top Bottom