Ukiwa kilaza basi unakuwa na chuki ,mchawi , mdhalimu , mshenzi , roho mbaya nk.Nyerere anauwamiza sana na kutaka kutangazwa mt.Waachie wakatoliki na mambo yao nyie mnaweza kuyafanya hayo muda wenu ukifika .Jadili hoja acheni vioja nyie wapuuzi .Mtu kafa kila siku kejeli angalikuwa dhuluma leo mnaliweza hata kusoma nyie ? Alichukua shule zetu akawapa hadi za kusoma wakati .............................wewe usiniudhi nikasema maneno ya kuwaudhi wengi kumbe uko mpuuzi peke yako .
Unazungumzia hizi shule zilijengwa na...
Viongozi wa Dini Wakiri Kuhusika Na Dawa za KulevyaViongozi sita wa madhehebu ya dini wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini, wamejitokeza mbele ya Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Dini na Haki za Jamii na kukiri kujihusisha na biashara hiyo kwa muda mrefu sasa.
Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa baada ya kuhojiwa, Viongozi hao waliiomba Kamati hiyo kutowataja hadharani majina ama madhehebu yao kwa kuhofia kubezwa kwa madhehebu wanayoyaongoza.
Akizungumza mwishoni mwa ziara yao Visiwani humo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekosti Tanzania, amesema kuwa orodha hiyo na nyingine ya watu 18 wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na Wanasiasa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu zote zitafikishwa kwa Mkuu wa kitengo cha Polisi cha Kupambana na dawa za kulevya nchi.
Mchungaji Mwamalanga amesema kuwa, tatizo la ongezeko la dawa za kulevya pia inazihusu nchi mbalimbali duniani na kwamba kamati hiyo itakutana na kamati nyingine kama hizo za nchi za Maziwa Makuu kwa maana ya Afrika ya Mashariki kuzungumzia ufumbuzi wa suala hilo.
Amesema mkutano huo pia utapendekeza kwa mabunge ya nchi hizo na Bunge la Afrika ya Mashariki kutunga sheria za kuwafilisi wale wote waliojilimbikizia mali kutokana na biasha za dawa za kulevya kwa nchi wanachama.