Njia za matangazo kwa mtandao

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Biashara ya matangazo kwa njia ya mtandao imetoka mbali na mara nyingi imebadilika kutokana na watu kuja na njia bora zaidi za kutangaza , vifaa vya kuangalilia kurasa za mitandao kama simu za mikono na hata programu nyingine za kufunga au kuzuia baadhi ya matangazo yasitokee au kuonekana mtu anapofungua kurasa fulani fulani .

Mfano zamani kidogo hakukuwa na tekinologia za kuruhusu tangazo fulani lisiweze kuangaliwa baadhi ya maeneo au kufunga aina hiyo ya matangazo kwenye maeneo fulani , kwa sasa mtu unaweza kutangaza huduma yako na google na kuamua ni wapi unataka tangazo lako lionekane na kwa muda gani kutokana na malipo yako .

Kitu muhimu cha kuzingatia kwenye matangazo ya mtandao , ili kuweza kuonekana vizuri ni vizuri komputa yako au kifaa kinachotumika kuangalia kurasa za mtandao kuwa na program za ziada na zilizoimara kwa kufanyiwa updates , mfano utapata tabu sana kutembelea African Union kama komputa yako au simu yako haina flashplayer ya kisasa kuweza kucheza matangazo hayo na kuona vilivyomo pia kuna maswala mengine kama Kasi ya komputa yako au simu au Huduma yako ya Internet na Programu za ziada kama JAVA nanyingine nyingi kutegemeana na matangazo .

Pamoja na maelezo marefu niliyotoa hapo juu kitu muhimu ni kujua kwamba muoekano wa matangazo na jinsi watu wanavyoweza kuangalia matangazo hayo pia inahusiana sana na wepesi wa komputa hizo katika utendaji wa kazi na pia uhakikishe Programu yako unayotumia kutembelea mtandao imeruhusu baadhi ya progamu .

KUZUIA /DISABLE PROGRAMU
Hili ni suala pata kidogo linahusiana na sheria na taratibu za kazi za baadhi ya kampuni na mashirika kama unaangalia mtandao kutumia vifaa vya maofisini , kuna baadhi ya kampuni haziruhusu utumiaji wa Flashplayer kwa mfano kutokana na sababu zao binafsi kwahiyo unakuta imefungiwa programu hiyo , kama ukiingia kwenye kurasa ya namna hiyo unaweza kulazimisha kuingiza kwenye komputa yako ili kuweza kuona unachotaka kuona lakini sheria za kazi haziruhusu .

KWANINI KUZUIA /DISABLE PROGRAMU
Ni kwa sababu baadhi ya kampuni haswa za matangazo zinatumia matangazo katika kukusanya taarifa kuhusu wateja wao na wengine wanaotembelea kwenye tovuti hizo kwa ajili ya kufanyia kazi pia baadhi ya tovuti haswa za wahalifu wanaweza kutumia mfumo wa matangazo hayo kulaghai watu kuingiza taarifa au kuonyesha picha chafu na mengine yanayohusiana na hayo , unaweza kujifunza zaidi ukisoma vyanzo mbalimbali vya mtandao kuweza kujua jinsi inavyokuwa .

NJIA ZA MATANGAZO .
Kwa sababu watu wengi na kampuni nyingi hazijui ni vipi zitangaze kazi zao au shuguli zao kwa njia ya mtandao ndio maana kuna hizi njia chache ambazo unaweza kujifunza zaidi na kuzifanyia kazi mbeleni .
Kitu muhimu kujua ni kwamba matangazo haya yana gharama zake na gharama hizo zinategemea kati ya kampuni na kampuni na kati ya aina ya tangazo na kati ya aina ya sehemu unazotaka tangazo fulani lionekane , muda wa kuweka tangazo hilo hewani na jinsi linalovyolipiwa

Mfano kuna matangazo mengine yanalipiwa pale mtu anavyo click Tangazo hilo na kupelekwa kwenye Tovuti iliyotangaza au huduma , nyingine wanalipa pale mtu anavyoona tangazo hilo mara nyingi ni idadi ya watu mara nyingi ni watu zaidi ya 500 au 1000 kwahiyo ni vizuri ukajua wateja wako na bajeti yako ili kuweza kutengeneza faida unavyotangaza .

BARUA PEPE .
Kama ilivyo wanabidii.net kwenye wanachama zaidi ya 6000 au mtandao mwingine unaotumia barua pepe kwa ajili ya mawasiliano ya wanachama wao mtu anaweza kutengeneza tangazo lake na kulisambaza au tangazo hilo likawa ndani ya kurasa ya mada fulani au kijarida mtandao ambacho kinaweza kusambazwa kwa maelfu , watu wengi huita aina hii ya matangazo kama uhalifu fulani .
Kutokana na baadhi ya watu kuhusisha hiyo na uhalifu au uharamia wa mtandao baadhi ya nchi kwenye sheria zake za mtandao zina vipengele vinavyoelezea aina hiyo ya matangazo na jinsi yanavyoweza kushugulikiwa .

Shida yake
Shida yake kubwa ni moja , ukishatuma tangazo lako kwa kundi la watu hao utakuwa labda umepoteza haki zako zingine mtu anaweza kuedit kazi hiyo au tangazo hilo kwa kutumia program nyingine na kupotosha kama anataka kufanya hiyo kwenye mtandao mengine mfano hai ni wakati wa Kampeni ambapo baadhi ya watu walichukuwa picha za Pweza Paul zilizopigwa Afrika ya kusini na kuweka Bendera za Vyama vya siasa .

MATANGAZO RAMANI
Kama wewe ni mtumiaji wa Google Earth , Google Maps na Galileo inayotarajia kuja siku za karibuni utakuwa umeona unavyotafuta kitu haswa nchi Za ulaya na miji mikubwa duniani mfano ukitafuta Moshi Eneo lilaloitwa Soweto kutumia Google Earth ulitakiwa kukuta matangazo kwenye sehemu hiyo yanayohusu Vitu vya Soweto kama maduka na ofisi za huduma mbalimbali .

Kama ni Google Maps unavyotafuta Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania utaona ramani ya eneo ambalo Ubalozi upo na majina ya Mitaa kuelekea hapo , sehemu hiyo kampuni kama ZANTEL ilitakiwa kuweka Matangazo yake , au AirTel ilitakuwa kuwa na matangazo yake kwenye mtaa wake .

Mtu mwingine anaweza akawa yuko Uwanja wa Ndege ni Mgeni anataka kwenda Chuo kikuu ch Dar es salaam akiingia kwenye Google Earth au Maps kutafuta njia alitakiwa akute matangazo na huduma mbalimbali njiani kuelekea Mlimani .

MATANGAZO VIDEO
Ukitembelea tovuti kama Yahoo.com sehemu ya Movies mara nyingi utakuta matangazo ya Movie mpya na sehemu unayoweza kuona video hiyo , ndani ya video hizo kuwa kampuni huwa zinatangaza bidhaa zao na huduma mbalimbali , aina hii ya matangazo ni nzuri sana kutumiwa na watu wanaotangaza filamu haswa nchini Tanzania kuweza kukuza soko lao liende mbali zaidi .

TRICK BANNER
Mara nyingi umewahi kutembelea baadhi ya tovuti na kukuta ujumbe kama You Have Won 5 Million Usd , au unapata ujumbe kwenye komputa yako kama vile Kuna tatizo na unaonyeshwa Programu ya kutengeneza Tatizo hilo hiyo ni Trick Banner lakini unapoona matangazo ya aina hiyo sio lazima Kugonga huwezi Juwa unaelekea wapi .

TANGAZO LINALOKUA – EXPANDING ADS
Haya ni matangazo yanayokuwa na kubadilika rangi na ukubwa na yanaweza kubadilisha baadhi ya vitu kwenye kurasa za tovuti fulani kwa kuficha vitu .

TANGAZO ELEA
Kama umewahi kuangalia baadhi ya Kurasa za tovuti na kukuta matangazo yanayoelea juu ya Maandishi ndio kitu kinachoongelewa hapo mathara yake ni sawa na Tangazo Linalokuwa kwa sababu linaficha baadhi ya vitu chini .

Hizo ni njia fupi na maelezo ambayo mtu au kampuni inaweza kutumia kama inataka kutangaza kwa njia ya mtandao , kama unataka kutangaza unaweza kumwambia mwenye tovuti nahitaji aina hii ya tangazo tangazo hilo liwe hivi na vile .

NENO LA MWISHO
Hayo ni maelezo mafupi kuhusu Njia za Matangazo , mengi zaidi unaweza kujifunza kwa kusoma vyanzo mbalimbali vya majarida au makala kwa njia ya mtandao na kujua jinsi gani unavyoweza kufaidika na njia mbalimbali za matangazo kwa njia ya mtandao kama unatovuti yako , blogu , vitabu vyako na nyingine nyingi sana .

Jambo la muhimu ni mtu kutokata tamaa , mtu anatakiwa ajifunze sana , asome sana kujua jinsi hivi vitu vunavyofanya kazi na jinsi watu wanavyofaidika usichoke kuuliza wala usisite kujiunga katika makundi au majukwaa mbalimbali ya mtandao yanayojadili masuala hayo ili kuweza kuuliza hoji na kujifunza vitu kadhaa .

Ingawa matangazo Kwa njia ya Mtandao yamesaidia kupunguza Uchafu wa matangazo ya kawaida barabarani na kwenye mabango , bado kuna shida ya Uchafu uliokwepo kwenye mtandao unahusishwa na Nyaraka zinazohifadhiwa na kazi mbalimbali zinazotakiwa kufutwa au kuharibiwa ili kuleta usalama hii ni changamoto kubwa kwa wanaharakani wa Mazingira kwa sasa

YONA F MARO
+255786 806028
 
.............

NENO LA MWISHO
Hayo ni maelezo mafupi kuhusu Njia za Matangazo , mengi zaidi unaweza kujifunza kwa kusoma vyanzo mbalimbali vya majarida au makala kwa njia ya mtandao na kujua jinsi gani unavyoweza kufaidika na njia mbalimbali za matangazo kwa njia ya mtandao kama unatovuti yako , blogu , vitabu vyako na nyingine nyingi sana .

Tatizo lako ni moja umefanya kazi nzuri ya kutuelimisha lakini hutuki kusema vyanzo hivyo unavyosema.

Kutoa link hakukufanyi wewe kutokuwa mtaalam. Na wala haiwezekani hya wewe uliyajua darasani au chuoni. Jaribu kuwa unafanya reference japo moja kwenye makala zako
.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom