Njia ya mwongo fupi. Sheria msumeno, unakata kote kote

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Mzee mmoja alikuwa na kijana wake ambaye alikuwa akisoma sekondari fulani ya bweni hapa nchini. Kijana huyo alikuwa ni mvivu na mtoro wa shule hivyo kusababisha yeye kushika nafasi ya mwisho darasani kila mtihani unapofanyika. Baba yake aligundua hili lakini kila alipomuuliza kijana alijigamba kuwa yeye ndiye anayeshika nafasi ya kwanza darasani.

Likizo nyingine ikawa imewadia na safari hii kabla ya kijana kurudi nyumbani baba yake alikuwa amenunua mtambo. Mtambo huu kazi yake kubwa ilikuwa ni kumkamata na kumtikisa mtu pindi anaposema uongo. Kijana akarudi nyumbani na baada ya salamu mazungimzo kati ya kijana na baba yake yalikuwa hivi:

Baba: Mwanangu safari hii umekuwa mtu wa ngapi?
Kijana: Kama kawaida baba, mtu wa kwanza. Limtambo likamdaka mikono.
Baba: Sema ukweli mwanangu.
Kijana: Nimekuwa wa pili baba. Limtambo likamdaka miguu. Wa tatu. Limtambo likamdaka mbavu....Mtambo ukaendelea kujiviringisha mwilini mwa kijana hadi alipokiri kuwa amekuwa mtu wa mwisho tangu aanze masomo yake.

Baba akaanza kumwasa kijana wake:
Mwanangu zingatia masomo kama mimi baba yako, nilikuwa nasoma na kila mtihani nikuwa mtu wa kwanza. Limtambo likamdaka baba mtu. Wa pili...likaendelea kumdaka...wa mwisho likaendelea kujiviringisha.... Likamdaka na kujiviringisha mwilini hadi dingi alipokiri kuwa hakuwahi kusoma shule.
 
Duuuuh!!! inafurahisha sana hii mkuu,
ndo maana wanasema ukiwa muongo usiwe msahaulifu.
 
Duuuuh!!! inafurahisha sana hii mkuu,
ndo maana wanasema ukiwa muongo usiwe msahaulifu.

Dingi alitaka kumtia nishai dogo wake, akajisahau kuwa limtambo halina cha dingi wala nani..!
 
Wazee pia mwache uongo! Ukipata div2 mzee anasema alpata div1 oooOH! "Mimi nlikuwa nashika namba moja darasani....!'' je wa mwisho alkuwa nani? Kama wote mlkuwa wakwanza.?
 
dingi ni nouma,,,vp limtambo lenyewe linajuaje kama unadanyanya? hii kali aisee
 
Dahhhh
Kungekuwa na kitu kama hii BUNGENI
............. ................. .................
 
Back
Top Bottom