Njia wanazotumiaga kuiba kura na jinsi ya kukabiliana nazo

Kima mdogo, jitahidi kila unapoandika ukumbuke kuto-ziweka hizo "ga" kwenye neno. Utaeleweka vizuri tu bila hizo "ga", unatuharibia lugha yetu tamu, umesikia Kima?

shikamo dada FF...Vipi uko Igunga? au kati ya kata 20 Zinafanya uchaguzi wa madiwani..vipi mtatoka leo
 
wajemeni nimewai kukaa mahali nikasikia jinsi ccm walivyoiba kura kwenye uchaguzi mmoja wapo ambao ulishawai kufanywa hapo nyuma hakika nilichoka walitumia watu wa funguo za bandia kufungua chumba ambacho kilikuwa kimehifadhiwa kura na kilichofanyika ni kutoa baadhi ya masanduku na kuweka yale yaliyokuwa na kura za mgombea wa ccm hakika nilichoka sana na pia nashauri igunga chadema wawe makini na hii njia ccm wanaitumia sana

njia hii kwa sasa haitumiki kwa sababu kura zote zinahesabiwa vituo vya kupiga kura, hairuhusiwi kuhesabu kura toafauti na mahali zilikopigiwa na mgombea akikubali hilo imekula kwake. Kinachofanyika ni kufanya majumuisho wakitumia fomu za matokeo.
 
Duuh mkuu una strategies!! Ila sasa kumbuka kwamba vyama vyote visivyo na nguvu ni mateka wa CCM kwa hiyo si vya kutegemea saaaana!

Hiyo ya kupenyeza maneno na kuuma sikio si ndio mwanzo wa fujo!! Una maana hiyo strategy ndiyo iliyofanikisha CDM kunyakua majimbo ya Arusha na Mwanza. Sijui inaweza kuwa nzuri ama la. Lakini pia hujasema kama watakuwa wamejumlisha matokeo na kikuta wameshindwa iweje. Ningetegemea ungewashauri wawaambie pia makamanda wao kwamba tumeshindwa na tuondoke kwa amani.

Mkuu nakushukuru kwa gap. Chanzo cha vurugu hata kama chama kimeshindwa kihalali nikutoridhika na mchakato. Kwa hiyo makamanda wakishakijilizisha inabidi wakubali matokeo kwa sababu naimani lengo lao pia ni kujenga utamaduni wa kuheshimu demokrasia
 
CHADEMA ulinzi wa kura ni sharti ile ni mfululizo katika hatua zote za kura mpaka kutangazwa matokeo.
 
Kuhusu namna ya kulinda kura,cdm hutoa semina ya uhakika na ndio siri ya kushinda ubunge ubungo na kawe.tulipigwa semina na yote mnayoandika nimarudio muhim ni ni kuwa na moyo wa kujitolea tu.huchakachuliwa ktk kutangaza na ubadilishaji wa data katika ngazi ya juu ambako hakuna mawakala na mwenyeuamuzi wamwisho ni tume.
 
Wana JF.
Toka tuanze kuingia kwenye uchaguzi Mkuu wa vyama vingi mwaka 1995, tulianza kusikia kuwa kuna wizi wa kura ndiyo uliyoipitisha CCM.

Mwaka 2000 tulifanya tena uchaguzi Mkuu wa vyama vingi wapinzani wakalalamika tena tumeibiwa kura.

Mwaka 2005 tulifanya tena uchaguzi Mkuu wa vyama vingi wapinzani wakalalamika tena wameibiwa kura.

Mwaka 2010 tulifanya tena uchaguzi Mkuu wa vyama vingi wapinzani wakalalamika tena wameibiwa kura.

Hivi siku zote hizo mbinu za kuibiwa kura bado tu wapinzani hawazifahamu.

Na hizo kura zinazolalamikiwa kuwa zinaibiwa wanaiba vipi.
 
Kweli bora kudadavua hili,isijekuwa wanaisingizia ccm ya Nape kwamba inaiba kura,mbinu ni zipi? ukiachilia mbali hofu ya wasimamizi wa chaguzi(wakurugenzi) kuamrishwa na aliyewateua (rais) kutangaza anavotaka yeye?
 
Hii kitu imeishakuwa kama wimbo wa Taifa utakuta kiongozi wa chama anawaeleza wanachama wenzake kuwa tulikuwa tumeshinda ktk huu uchaguzi tatizo CCM wameiba kura.
 
Mwulize Kikwete. Kwenye ile press conference yake siku moja kabla ya uchaguzi wa 2010 alieleza jinsi kura zinavyoibiwa.
 
Wana JF.
Toka tuanze kuingia kwenye uchaguzi Mkuu wa vyama vingi mwaka 1995, tulianza kusikia kuwa kuna wizi wa kura ndiyo uliyoipitisha CCM.

Mwaka 2000 tulifanya tena uchaguzi Mkuu wa vyama vingi wapinzani wakalalamika tena tumeibiwa kura.

Mwaka 2005 tulifanya tena uchaguzi Mkuu wa vyama vingi wapinzani wakalalamika tena wameibiwa kura.

Mwaka 2010 tulifanya tena uchaguzi Mkuu wa vyama vingi wapinzani wakalalamika tena wameibiwa kura.

Hivi siku zote hizo mbinu za kuibiwa kura bado tu wapinzani hawazifahamu.

Na hizo kura zinazolalamikiwa kuwa zinaibiwa wanaiba vipi.
Yule mkurugenzi wa Tume alisema tatizo si kuhesabu kwenye vituo, bali ni Kujumulisha huko kujumulisha kidogo huwa si kwa kawaida ( Alisema haya ni mahesabu bwana , ni lazima watu wayafanye wakiwa wametulia ) huko kutulia ni pamoja na kufanya consultations na ......, ingelikuwa wanatumia tu hizi Summation tunazofundishwa madarasani mbona siku moja au mbili zilikuwa toha kabisa kutoa hali halisi ( Algorithm ya kujumulisha NEC iko complicated sana tu) lol
 
Wana CDM wana CUF wana NCCR Mageuzi wana TLP wana CCK, jitokezeni tujadili jinsi kura zinavyoibiwa na CCM kila siku mtakuwa mnalalamika tumeibiwa kura pasipo ushahidi.
 
Magamba ni ma'experts katika hako kamchezo! Rejao, Faiza fox , Malaria sugu etc wanajua!
 
Maalim Seif mwaka 2010 hakuibiwa kura, wewe c unaona sasahv full ving'ora.
 
Back
Top Bottom