Njia rahisi ya kumaliza panya

Kireka1980

JF-Expert Member
Mar 18, 2008
302
43
Nadhani karibu wote mlishakumbwa na kero za panya na wengine bado mnasumbuliwa na hawa viumbe, mimi nilisumbuliwa sana lakini nilitumia hii mbinu na ndani ya siku mbili panya imekuwa historia, fanya yafuatayo;
- Nunua sumu ya panya ile ya rangi ya pink (mwambie muuzaji ni ya kukausha) ipo kama tambi inapatikana kwa wauzaji kirahisi sana (Tzs 1000 kama sikosei)
- Chukua samaki uwakaushe kwa mafuta hadi wakauke kiwango cha kuweza kusagika ila wasiungue, kisha wasage.
-Sumu ifunge kwenye gazeti na uisage kwa kutumia chupa au vyovyote.
-Changanya sumu na samaki kisha weka kwenye kipande cha box kama sehemu mbili au tatu kutegemeana na ukubwa wa nyumba.
ANGALIZO: hakikisha panya hawawi na access ya maji kwa usiku wote.
Hapo hawachomoki.... hakuna cha panya wa dar wala nini hapo.......
 
Kuna wachina wamemuuzia waifu lipira linamiguu kama ng'e wakasema ulipake mchuzi panya aking'ata ananata lakini wapi!... ila inaonekana panya wanaliogopa hilo pira maana sijawaona tangu linunuliwe K'Koo sh 500 tu.
 
Nna panya ameshindikana ni mpevu kwelix2 ana kg kama 1 hivi,nimeweka dawa kali lakini wapi! Ila ntajaribu mkuu dawa yako ila ikishindikana naenda kuchukua mzigo gongo la mboto si yapo yamezagaa tuu waungwana?
 
Mimi nawashauri badala ya sumu aliyoitaja changanya na dawa ya binadamu ya mifupa (indocid) sina uhakika kama ndio inavyoandikwa ila ndio inavyotamkwa. Nawashauri hili hasa wenye watoto, huwezi kujua siku ya bahati mbaya. Kwa kuhepusha hilo bora kutumia dawa ya binadamu kwani madhara yake hayatakuwa makubwa kama mtoto kwa bahati mbaya akilamba. Matokeo ni mazuri kama kutumia sumu tu, ila hawatakauka, hivyo ukiwaacha mpaka wafe watakunukia ndani. Ili wasinuke ndani ukishaweka usiku asubuhi ujaribu kuwasaka utakuta hawawezi kutembea, basi unawachukua na kuwaulia nje na ukipenda unaweza kuwa rafiki wa kunguru.
 
Unaweza fanya supu! Nyama yao nikama ya kuku
 
Na hawa narrow bee fly tunawafanyaje?
hawa nimefanikiwa kwa kuhakikisha nyavu za madirishani hazina matundu, pia nina mtindo wa kupuliza dawa kila jumamosi, nahakikisha mlango unafungwa ifikapo 12 jioni. ni ngumu but thats the only way
 
Nadhani karibu wote mlishakumbwa na kero za panya na wengine bado mnasumbuliwa na hawa viumbe, mimi nilisumbuliwa sana lakini nilitumia hii mbinu na ndani ya siku mbili panya imekuwa historia, fanya yafuatayo;
- Nunua sumu ya panya ile ya rangi ya pink (mwambie muuzaji ni ya kukausha) ipo kama tambi inapatikana kwa wauzaji kirahisi sana (Tzs 1000 kama sikosei)
- Chukua samaki uwakaushe kwa mafuta hadi wakauke kiwango cha kuweza kusagika ila wasiungue, kisha wasage.
-Sumu ifunge kwenye gazeti na uisage kwa kutumia chupa au vyovyote.
-Changanya sumu na samaki kisha weka kwenye kipande cha box kama sehemu mbili au tatu kutegemeana na ukubwa wa nyumba.
ANGALIZO: hakikisha panya hawawi na access ya maji kwa usiku wote.
Hapo hawachomoki.... hakuna cha panya wa dar wala nini hapo.......
panya ni tatizo kwa kweli kama hii itafanyakazi utakuwa msaada mkubwa sana kwangu! Aksante in advance! ila ni wajanja saaaana siku hizi!
 
Mkuu kwa hiyo mbinu hawana ujanja, jaribu then utashangaa, mimi ilikuwa issue mitego ya aina yote, paka nilikuwa nae wakahamia kwenye ceiling na makochi but kwa sasa nakula bata tuu....
 
Kuna wachina wamemuuzia waifu lipira linamiguu kama ng'e wakasema ulipake mchuzi panya aking'ata ananata lakini wapi!... ila inaonekana panya wanaliogopa hilo pira maana sijawaona tangu linunuliwe K'Koo sh 500 tu.

Ha haha....panya wamekimbia lipila linawatusha...na panya anaogopa ng'e vile vile unafikiri hajui hujuma zake....Mende ni kuhakikisha hakuna uchafu...nyumbani...au karibisha siafu kwa usiku mmoja...dah u will be amazed na turn around asubuhi.
 
mende tunawafanyaje mkuu? Tabu kweli wapuuzi hawa

dawa ya kuua mende nunua vidonge vya ngao (vile vinavyotumika kwenye vyandarua). Uweke kwenye maji kama maelekezo yaliyopo, halafu hayo maji unyunyuzie kwenye sakafu au maeneo mende wanapopita ni vizuri ufanye usiku wakati unaenda kulala na madirisha ufungue ili upate hewa safi, pia mikono yako uvae gloves ipo kwenye pakiti utayonunua, kesho yake asubuh mama apige deki kama kawaida. Mende wataokatiza hapo lazima wafe hata wiki ikipita watakuwa wanakufa
 
Back
Top Bottom