Njia au kifaa cha ku-detect mafuta feki kwa watumiaji (cosumers)

Unadhani kuna haja ya meteja kuthibitishiwa ubora wa mafuta kabla ya kuamua kujaza mafuta?

  • HAPANA, haja hata hiyo michakato itachakachuliwa!

    Votes: 0 0.0%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    7

Maswala

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
560
225
Mwananchi Jumapli, 19 August 2012 00:17
"SHEHENA ya mafuta iliyopelekwa nchini Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imekataliwa katika nchi hizo kwa kukosa ubora na kurudishwa Tanzania ambapo sasa yameanza kuuzwa, Mwananchi Jumapili limebaini"

SIKU CHACHE ZILIZOPITA NILINUNUA PETROL KWA LITA 10 KWA AJILI YA GENERATOR YANGU MAANA UMEME ULIKUWA UMEKATIKA. KWA MSHANGAO, MASHINE ILIGOMA KUWAKA HADI NILIPOMUITA FUNDI, AKANAMBIA MAFUTA YAMECHAKACHULIWA. NDIPO TULIAMU KUTOA MAFUTA KUYAWEKA KATIKA NYUMBA TRANSPARENT NA KUYAONA KAMA YANAVYOONEKANA KATIKA PICHA NILIYOAMBATANISHA.

WAKATI HAYA YAKITOKEA NDO NASOMA HABARI HIZI KATIKA GAGESTI YA MWANANCHI JUMAPILI. MIMI NILIONA KUNA UHUSIANO MKUBWA.

JAMANI MTU HUHITAJI KUWA MTAALAM KUJUA HIYO HAPO SIO PETROL HALISI--BALI IMECHAKACHUHLIWA. KWANZA RANGI YAKE, PILI NI KUTOFAUTIANA RANGI JUU NA CHINI.

KAMA HIYO HAITOSHI, LEO NIKASEMA NGOJA TU NIENDE KITUO HICHO HICHO NIKIDHANI KUWA LABDA NAWEZA KUWA NIMEFANYA MAKOSA, NIKAWEKA LITA MOJA TUU KATIKA PIKIPIKI KUJARIBU KUONA KAMA YATALETA TOFAUTI. UKWELI NI KWAMBA, PIKIPIKI ILIKUWA INA MIS-MISES NYINGI! NILIPOYATOA NA KUWEKA MENGINE KUTOKA KITUO KINGINE, ILIWAKA NORMAL!

NA TATIZO LA GENERATOR YANGU NI LA MUDA MUREFU, KWANI MAFUTA HUNUNULIWA KUTUO HICHO HICHO KWA SABABU NDICHO KILICHOKO KARIBU. MAFUNDI HULA PESA YANGU MARA KADHAA BILA KUJUA KUWA TATIZO NI MAFUTA HADI NILIPOBADILI FUNDI.

HAMUONI KUWA KUNA HAJA YA KUWEPO NAMNA AU CHOMBO CHA KUPIMIA BIDHAA YA PETROL ILI KUMRIDHISHA MNUNUAJI KABLA YA KUWEKA MAFUTA KATIKA GARI?
Tazama Video hii pia
 

Attachments

  • Petra.jpg
    Petra.jpg
    274.8 KB · Views: 240
  • Petro.jpg
    Petro.jpg
    32.5 KB · Views: 72
Sema ni kituo gani hicho kifanyiwe ukaguzi wa kushtukiza usiku huu huu? watanzania tujifunze kuripoti matatizo kama haya mara moja bila kujali mhusika ni nani, hata kama ni miongoni mwa mafisadi nguli.
 
he yani ulijua tatizo ukaenda jaribia pikipiki ingekufa?au haina pump?da ingekua mimi nimejua hayo yoye mbona nengeneemeka na pesa ya kupeta weekend
 
Wacha uoga karipoti mapema na ikiwezekana uwadai fidia kubwa sana naona hii ishakuwa ni deal zao na wanajua Watanganyika wengi hutuna muda wa kupoteza muda mahakamani tundu lissu kasaidia kidogo kuwasema kuwa hawajui kitu...

Most ya vituo vyenye kuchakachua Mafuta ni Gapco haswa kile cha Samora Avenue yaani hayafai kabisa mimi nilikuwa naweka pale Gari basi huwa nashangaa miss za kufa mtu na kuna siku nikaenda na Motor bike Gapco ya Morogoro Road opp na Mtendeni pr school kidogo nipate Ajari kwa miss hadi Plug ikafa... Sasa hii picha ni aibu kubwa Kama hii imepita hadi TBS na Ewura tujue tunaibiwa na wezi tunaishi nao na tunawalipa Kodi zetu huwa nachukia sana pale ninaponunua kisha nikitizama Receipt kuna tozo lao dah!

Pole Sana Mkuu next time uombe na Receipt ukiwashtaki uwe na ushahidi wote... Haisaidii kureport kisha washitakiwe na Serikali Fidia zote wanapata Serikali wananchi ziiiiiiiiiii Poleni
 
he yani ulijua tatizo ukaenda jaribia pikipiki ingekufa?au haina pump?da ingekua mimi nimejua hayo yoye mbona nengeneemeka na pesa ya kupeta weekend
Dereva wangu juzi kidogo nimnyang'anye Gari niliona kinipa hasara kwani nikajua kanunua mafuta uchochoroni Basi lilizima Jangwani likavutwa pump imeharibika Nozel ikabidi nibadilishe Bulshait!!! nina hasira Tank limeshushwa a kulisafisha lote huu sasa ni ubazazi tuupinge wote tunarudishwa nyuma kimaendeleo...
 
Sisi bado ni wajinga ndo maana serikali yetu kwa kupitia Ewura kwa kushirikiana na wauza mafuta bado wanatuchezea
 
Dereva wangu juzi kidogo nimnyang'anye Gari niliona kinipa hasara kwani nikajua kanunua mafuta uchochoroni Basi lilizima Jangwani likavutwa pump imeharibika Nozel ikabidi nibadilishe Bulshait!!! nina hasira Tank limeshushwa a kulisafisha lote huu sasa ni ubazazi tuupinge wote tunarudishwa nyuma kimaendeleo...
Nina fahamu mtu ambaye aliwekewa mafuta p gari ikazima after few metres alishtaki mbona allipwa pesa ya maana.japo ndo kama ulivyosema watanzania hutataki usumbufu ndo mana tutaendelea tu kunyanyasika.Kma una mabasi wape sharti la kujaza mafuta kituo kimoja na kuchukua risiti likibuma unawashukia na gari na ewura juu
 
Pole sana. Bahati mbaya mafuta yalioingizwa kwa njia ya bulk procurement inasemekana yamechanganywa na ethanol. Sijui utakimbilia wapi ingawa wewe unasifia kwamba vituo vingine ni mazuri.
 
ktk taasisi nilizokosa nazo imani ya tatu ni hii ewura, tatizo hawa wafanyabiashara wakubwa ndio wamewaweka wanasiasa madarakani, wanasiasa nao wamewaweka ewura kwa maelekezo ya wafanyabiashara kwahiyo by default wanasiasa na ewura wanamtumikia mfanyabiashara mkubwa.

Mimi nikifika petrol station huwa nawaambia kbs gari ikipata matatizo huwa sina kawaida ya kwenda kushitaki polisi.. kuna station moja mwanza waliwahi kuniwekea mafuta machafu na kunilaza mapori ya ngudu, siku iliyofuata niliwarudia pale station hali ilioyoniplelekea kulala polisi kwa siku 2 kwa kosa la shambulizi la aibu na kusababisha maumivu makali kwa vijana wawili ..ilifikia kipindi wakiiona gari yangu walikuwa wanakataa kuniwekea mafuta kwa madai mzee mkorofi
 
Tutajieni hivyo vituo vinavyochakachua ili tuwakwepe-mimi nimeweka kawaida ya kujaza mafuta pale Bonjour mlimani sijawahi pata tatizo
 
Jamani asanteni kwa michango na mawazo yenu mazuri. Nimenunua risit ninayo, muda wa kufuatilia ndo sina. Ila nimepata somo. kuanzia sasa nitakuwa mwangalifu. sitaki ujinga tena.

Kinachonisangaza ni kuona EURA inaruhusu mafuta machafu ndani ya soko; hawa jamaa tunawalipa pesa zetu kila tukinunua bidhaa ya nishati. it is unfortunate! Hii inaashiria tunaelekea kubaya, kama taifa kama watanzania hatutafanya maaumuzi ya busara juu ya hali kama hii.
 
Back
Top Bottom