Njia 8 za kupata ajira popote hata bila cheti (part 1.5 aka ufafanuzi)

Jun 8, 2016
83
648
Post ya kwanza nmeandika watu wengi sana wamepata cha kupata, wengine wame misunderstand my intentions za kuandika post in the first place, ngoja nirudi nyuma kidogo niweze jaribu kufunguka kwanini nmeandika na nani atae faidika sana akitumia hizi njia.

N.b This is part 1.5, najibu maswali ya wengine, hutoelewa kama hujasoma part 1, part 1 hii hapa Njia rahisi 8 za kupata ajira popote ukiwa umemaliza chuo hizi hapa

-The three main things to focus on ni vifuatavyo

1)Wafanyaji kazi vs. wajaza position (cogs)

Ukiisoma kampuni vizuri ipo hivi, kampuni succesful ni mashine ambayo inabidi iwe inafanya kazi mda wote, kila mashine ina replaceble cogs yaani kitu flani ambacho kikiharibika au ku malfunction unaweza kuki replace na kingine kipya ndani ya mda mdogo.. Ukifanya research kampuni yoyote utagundua hili... Na nafasi ikitangazwa ili mtu aijaze kwa specifications flani, that is a cog ili kampuni iweze kuendelea (a repleacable cog) anytime mtu mwenye cheti a b na c akitokea anaweza jaza hiyo nafasi we call them cogs... Watu wale ambao wapo tu ili kampuni iendelee kurun kawaida, cogs hawaifanyi kampuni iende juu hawaiongezei value yoyote kampuni all they can do is either wai bakishe vilevile ama wairudishe kampuni nyuma...

Being a cog is not a bad thing, wengi wanapenda kuwa cogs, hawapendi maisha yayumbe, hawapendi ku ji challenge, hawapendi taking risks, akipata kazi moja atakaa hapo miaka nenda miaka rudi akitegemea mshahara utaongezeka na kupandishwa cheo huku akisave kwenye pension yake, AMEFIKA! anachosubiri hapa ni kuoa, kupata watoto na mwisho wa siku ku rest in peace. This is not a bad thing, haya ni maamuzi.
(again most of this doesnt apply kwa kazi zote, this is for most middle class earning jobs, sio professions kama dakatari, wanasheria na wengine)

Cogs ni essential for a company lakini siyo wanaohitajika ili iweze survive miaka nenda miaka rudi, ofisi flani nilikua nimekaa nafanya kazi nikaangalia meza ya pembeni yangu namuona mtu ame fungua facebook anajibu message na kuchat, ilikua saa tisa hivi mchana, baada ya lunch. mi siwezi kaa mda mrefu sehemu moja so huwa nasimama natoka kidogo so nimesimama natembea nkapita watu kama watatu wote hakuna anaefanya kazi, yaani wameshafanya their fair share kuzungusha gurudumu kwa siku hiyo so wanaendelea na mambo yao, boss akaja akaingia tu, kila mtu akajifanya yupo busy. Wote wameingia kwa vyeti hawa, in the mean time mi nimesha anza kazi za kesho. How i wish the day na quit ninge rekodi tu jinsi gani huyu bosi aliniita ofisini na kunihoji kwa nini nataka acha hiyo kazi, for more than an hour kabla hajaniachia niende.

What im trying to point out ni kwamba the system is rigged, kampuni inahitaji wajaza position kama receptionist, marketer, manager na position zingine ili iendelee ku exist, lakini inahitaji wafanyaji kazi kama sisi ili iweze vuka matarijio yake na kuzidi kukua, kuteka market inayoishindania, kupata wateja zaidi, ku move forward na kadhalika. So most experienced companies zinajua kwamba zinatuhitaji, lakini kampuni mpya pia zinajifunza kuwa zinatuhitaji wafanyaji kazi kweli siyo wajaza position tu (cogs).

Any successful company inajifunza kwamba cheti cha chuo ni karatasi tu, mtu aki cheat successfully atapata cheti, ishu ni kwamba in real life huwezi ku cheat, unahitaji actual work ethic na uwezo wa ku adapt na situation yoyote, uwezo wa kujifunza haraka na kutatua matatizo yanayojitokeza kwenye kitengo chako au popote kwingine hata kama hujapangiwa.
Kazi yangu ya mwisho nilifanya kuanzia 2015 mwezi wa nne hadi wa nane, kampuni ilikua mpya ni kampuni ya mtu mkubwa sana hapa nchini kifedha (yaani ukiwaza wakubwa watatu mmoja wapo atakua ndio yeye) ambaye ana ventures nyingi sana, hii ndio moja wapo ameanzisha last year, what happened ni kwamba kabla kampuni haijaanza officially HR akatafuta watu wake wote yaani literally position zote zikawa filled na watu ambao wako referred by washauri na marafiki, mimi nikawa mmoja wapo. Nkasema what the hell ngoja niende nikacheki, nilipofika ilikua bonge la ofisi yaani sijawahi kufanya kazi sehemu kubwa kama hii, nkaonana na HR kama formal kujaza tu maelezo yangu etc etc, nikasema ngoja ni experience kufanya kazi ofisi kubwa for once. After position zote kuwa filled ndipo matangazo yakatoka kuwa wafanya kazi wanatafutwa kama formal tu, CV za wengine zikajaa kibao, nauhakika hadi leo zimekaa kwenye droo tu pale reception.

Qualifications for most positions ni kwa ajili ya ku filter watu, kampuni inaweza ikatangaza kazi moja, zikaja CV zaidi ya mia mikononi mwake, so ile experience "5 years" na mengine ni kwa ajili ya kupunguza lundo la watu, lakini people are looking for the most qualified person to do the job. So akitokea the most qualified person alafu ana cheti that is a bonus for a company, lakini most of the time, ukiweza onyesha kuwa you are the most qualified person for the job, utaipata hiyo kazi.

So kabla hujatafuta kazi jiulize kama unataka kufanya kazi ama kujaza position tu, kama unataka kujaza position basi jiangalie cheti ulichonacho na expirience uliyonayo afu ka apply kama watu elfu kadaa kwenye field wako wanaotaka kujaza position. kama untaka kufanya kazi, tafuta njia za kuongeza value yako, find new and faster ways to work, ongeza value yako kwa kujiongezea skills na mambo mengine, then apply kazi yoyote unayo ona utaiweza kuifanya usijali cheti wala nini.

2) Value, Value, Value

-This applies kwenye mambo mengi sana siyo kupata kazi tu, always provide as much value as you can kabla hujaomba upewe kitu chochote, if you are providing me value that is worth milioni 2 sioni shida ya kukulipa laki saba.
Hata kama kampuni ina uwezo wa kuingiza milioni 30 kila siku, bado ina hamu ya kuingiza hela zaidi. Na ukiweza prove kwamba utaweza iongezea value hiyo kampuni ipande kutoka milioni 30 hadi 33 kwa siku, hakuna mtu mwenye akili timamu ataeweza kataa kukupa kazi, japo kwa mwezi mmoja kujaribu kama utaweza kweli fanya kama unavyoongea.
Ukiweza Prove kwamba you are valuable na kweli unaweza hiko kitengo hakuna atae waza chochote kuhusu cheti gani ulicho nacho.

Value is more important than cheti, najua kuna baadhi ya watu mambo kama haya yanawakuta, mimi nipo kitengo cha I.T na nina ndugu mmoja ambae alikua I.T wizara ya fedha, i think ni maintainance or something, huyu ndugu kila akirudi nyumbani huwa alikua ananiomba mimi nimuelekeze vitu ambavyo yeye amesomea, i was basically doing her job for her, akipewa cha kufanya inamchukua more than 2 days kukamilisha, na kazi hii ameipata kwa ajili ya cheti chake.
Serikalini its harder to get a job bila cheti ila lets apply this same situation kwenye private sector (just to punguza malumbano) , mfano lets say huyu dada ameajiriwa na private company na computer ikiwa slow, kazi hazifanyiki for 2 days, which the company looses 4 million within hizo siku mbili then muajiri akaambiwa kuna mtu who can solve matatizo kama hayo kwa dakika 15 instead of 2 days ila hana cheti hata kimoja.... oh yeah na pia anatengeneza websites, ana uwezo wa ku edit picha pia, networking anaweza pia, ila hana cheti hata kimoja...
Muajiri ataesema ngoja nimuache huyuhuyu tu huyo hapati kazi hapa kisa hana cheti, hiyo kampuni haito last miaka mitano inayofuata.

Cheti pia kinadanganya watu wengi, wanaona kisa yeye anacho cheti basi ana deserve kupewa kazi, anajiona kuwa value yake ni kiasi flani kwa ajili ana cheti lakini the truth is very different. What is the value of kitu ambacho kila mtu anacho, well basically nothing, so watu hupata kazi kwa nepotism (upendeleaji wa kujuana) ama kwa njia ambayo wengi hawaijui which is Value. Ongeza value yako ten folds kazi inayohitaji nusu ya hiyo value utaipata kirahisi sana.

Value unaipata kwa expirience, adding more skills na kuwa na more connections.

3) Fanya kazi kwa malengo

Mimi nilikua nafanya kazi ili kujifunza as much as i can, kuhusu uendeshaji wa kampuni. nimefanya kazi kampuni ambazo zipo successfull na nimefanya ambazo zimefeli, so najifunza kote kipi wanachopatia na kukosea ili ninapokuja anzisha kampuni yangu nisirudie makosa na nifuate niliyoona yamefanywa sawa. Nikiona sina kipya cha kujifunza, akili yangu ina kwama haiwezi kuendelea kufanya kazi hiyo sehemu, ndiyo maana kuna kampuni nimefanya siku tatu na nyingine mieze sita.

The fact kwamba nimefanya kazi zaidi ya saba full time within the span of 3 years is me selling myself short, kuna za part time ambazo sijazi include kuna ambazo naingia tu then naacha bila hata kufikisha wiki sijazi include, i moved to doing freelance, then owning private companies baada ya kuona kwamba expirience na mafunzo niliyopata vinatosha.

So kama malengo yako ni kupata kazi moja tu utulie uendelee na maisha yako njia hizi sio za ku copy zote, chagua kitachofaa then apply, ila kama una tafuta expirience and connections na unataka kujiingizia kipato huku ukijifunza vyote utavyoweza jifunza kuhusu uendeshaji wa kampuni then by all means chukua and apply as much as you can from these methods ntazokua nazi jot down every once in a while.

Again ntatafuta mda nimalizie point nne za mwisho, kama bado kuna wataohitaji, kusuka mada itayokaa kwenye mpangilio mzuri inahitaji mda, siyo mda tu ila kichwa na chenyewe kiwe cheupe.

Narudia tena hii ni part 1.5, najibu maswali mengi yaliyoulizwa part 1 ambayo ina njia nne za kupata kazi popote hii hapa https://www.jamiiforums.com/threads/njia-rahisi-8-za-kupata-ajira-popote-ukiwa-umemaliza-chuo-hizi-hapa.1062090/ part 2 on its way
 
Wewe jamaa ni kichwa. Sijui kwa nini baadhi ya watu hawakuelewi. Unachoongea ni ukweli mtupu, yaani unapiga mule mule. Ila kwa mtu ambae amekuwa au anategemea kuwa part of the "rat race" hawezi kukuelewa asilani!! Watu ambao wamejitayarisha kuingia au wamebobea kwenye "rat race" hawawezi kuelewa maandishi yako kamwe!! Na kama ulivyosema, wala si kitu kibaya, its a choice ambayo wamechagua; ila sasa wasibishe kuwa "side B" pia ipo!!
 
Very inspiring writting
Nakuona wewe kama moja wa tu wachache sana wanaojitambua wawapo kazini. You are thinking first of the results and progress of the company than what your personal benefits.

Umeni-inspire sana pale uliposema kuwa wakati wengine wako bize na kuchati insta na facebook, tayari wewe ulishaanza kazi za kesho yake.

I wish to hear more from you.

Usiwe unapotea muda mrefu bila kurudi huku kwenye uzi wako kuona response na maswali ya watu
 
Post ya kwanza nmeandika watu wengi sana wamepata cha kupata, wengine wame misunderstand my intentions za kuandika post in the first place, ngoja nirudi nyuma kidogo niweze jaribu kufunguka kwanini nmeandika na nani atae faidika sana akitumia hizi njia.

N.b This is part 1.5, najibu maswali ya wengine, hutoelewa kama hujasoma part 1, part 1 hii hapa https://www.jamiiforums.com/threads/njia-rahisi-8-za-kupata-ajira-popote-ukiwa-umemaliza-chuo-hizi-hapa.1062090/

-The three main things to focus on ni vifuatavyo

1)Wafanyaji kazi vs. wajaza position (cogs)

Ukiisoma kampuni vizuri ipo hivi, kampuni succesful ni mashine ambayo inabidi iwe inafanya kazi mda wote, kila mashine ina replaceble cogs yaani kitu flani ambacho kikiharibika au ku malfunction unaweza kuki replace na kingine kipya ndani ya mda mdogo.. Ukifanya research kampuni yoyote utagundua hili... Na nafasi ikitangazwa ili mtu aijaze kwa specifications flani, that is a cog ili kampuni iweze kuendelea (a repleacable cog) anytime mtu mwenye cheti a b na c akitokea anaweza jaza hiyo nafasi we call them cogs... Watu wale ambao wapo tu ili kampuni iendelee kurun kawaida, cogs hawaifanyi kampuni iende juu hawaiongezei value yoyote kampuni all they can do is either wai bakishe vilevile ama wairudishe kampuni nyuma...

Being a cog is not a bad thing, wengi wanapenda kuwa cogs, hawapendi maisha yayumbe, hawapendi ku ji challenge, hawapendi taking risks, akipata kazi moja atakaa hapo miaka nenda miaka rudi akitegemea mshahara utaongezeka na kupandishwa cheo huku akisave kwenye pension yake, AMEFIKA! anachosubiri hapa ni kuoa, kupata watoto na mwisho wa siku ku rest in peace. This is not a bad thing, haya ni maamuzi.
(again most of this doesnt apply kwa kazi zote, this is for most middle class earning jobs, sio professions kama dakatari, wanasheria na wengine)

Cogs ni essential for a company lakini siyo wanaohitajika ili iweze survive miaka nenda miaka rudi, ofisi flani nilikua nimekaa nafanya kazi nikaangalia meza ya pembeni yangu namuona mtu ame fungua facebook anajibu message na kuchat, ilikua saa tisa hivi mchana, baada ya lunch. mi siwezi kaa mda mrefu sehemu moja so huwa nasimama natoka kidogo so nimesimama natembea nkapita watu kama watatu wote hakuna anaefanya kazi, yaani wameshafanya their fair share kuzungusha gurudumu kwa siku hiyo so wanaendelea na mambo yao, boss akaja akaingia tu, kila mtu akajifanya yupo busy. Wote wameingia kwa vyeti hawa, in the mean time mi nimesha anza kazi za kesho. How i wish the day na quit ninge rekodi tu jinsi gani huyu bosi aliniita ofisini na kunihoji kwa nini nataka acha hiyo kazi, for more than an hour kabla hajaniachia niende.

What im trying to point out ni kwamba the system is rigged, kampuni inahitaji wajaza position kama receptionist, marketer, manager na position zingine ili iendelee ku exist, lakini inahitaji wafanyaji kazi kama sisi ili iweze vuka matarijio yake na kuzidi kukua, kuteka market inayoishindania, kupata wateja zaidi, ku move forward na kadhalika. So most experienced companies zinajua kwamba zinatuhitaji, lakini kampuni mpya pia zinajifunza kuwa zinatuhitaji wafanyaji kazi kweli siyo wajaza position tu (cogs).

Any successful company inajifunza kwamba cheti cha chuo ni karatasi tu, mtu aki cheat successfully atapata cheti, ishu ni kwamba in real life huwezi ku cheat, unahitaji actual work ethic na uwezo wa ku adapt na situation yoyote, uwezo wa kujifunza haraka na kutatua matatizo yanayojitokeza kwenye kitengo chako au popote kwingine hata kama hujapangiwa.
Kazi yangu ya mwisho nilifanya kuanzia 2015 mwezi wa nne hadi wa nane, kampuni ilikua mpya ni kampuni ya mtu mkubwa sana hapa nchini kifedha (yaani ukiwaza wakubwa watatu mmoja wapo atakua ndio yeye) ambaye ana ventures nyingi sana, hii ndio moja wapo ameanzisha last year, what happened ni kwamba kabla kampuni haijaanza officially HR akatafuta watu wake wote yaani literally position zote zikawa filled na watu ambao wako referred by washauri na marafiki, mimi nikawa mmoja wapo. Nkasema what the hell ngoja niende nikacheki, nilipofika ilikua bonge la ofisi yaani sijawahi kufanya kazi sehemu kubwa kama hii, nkaonana na HR kama formal kujaza tu maelezo yangu etc etc, nikasema ngoja ni experience kufanya kazi ofisi kubwa for once. After position zote kuwa filled ndipo matangazo yakatoka kuwa wafanya kazi wanatafutwa kama formal tu, CV za wengine zikajaa kibao, nauhakika hadi leo zimekaa kwenye droo tu pale reception.

Qualifications for most positions ni kwa ajili ya ku filter watu, kampuni inaweza ikatangaza kazi moja, zikaja CV zaidi ya mia mikononi mwake, so ile experience "5 years" na mengine ni kwa ajili ya kupunguza lundo la watu, lakini people are looking for the most qualified person to do the job. So akitokea the most qualified person alafu ana cheti that is a bonus for a company, lakini most of the time, ukiweza onyesha kuwa you are the most qualified person for the job, utaipata hiyo kazi.

So kabla hujatafuta kazi jiulize kama unataka kufanya kazi ama kujaza position tu, kama unataka kujaza position basi jiangalie cheti ulichonacho na expirience uliyonayo afu ka apply kama watu elfu kadaa kwenye field wako wanaotaka kujaza position. kama untaka kufanya kazi, tafuta njia za kuongeza value yako, find new and faster ways to work, ongeza value yako kwa kujiongezea skills na mambo mengine, then apply kazi yoyote unayo ona utaiweza kuifanya usijali cheti wala nini.

2) Value, Value, Value

-This applies kwenye mambo mengi sana siyo kupata kazi tu, always provide as much value as you can kabla hujaomba upewe kitu chochote, if you are providing me value that is worth milioni 2 sioni shida ya kukulipa laki saba.
Hata kama kampuni ina uwezo wa kuingiza milioni 30 kila siku, bado ina hamu ya kuingiza hela zaidi. Na ukiweza prove kwamba utaweza iongezea value hiyo kampuni ipande kutoka milioni 30 hadi 33 kwa siku, hakuna mtu mwenye akili timamu ataeweza kataa kukupa kazi, japo kwa mwezi mmoja kujaribu kama utaweza kweli fanya kama unavyoongea.
Ukiweza Prove kwamba you are valuable na kweli unaweza hiko kitengo hakuna atae waza chochote kuhusu cheti gani ulicho nacho.

Value is more important than cheti, najua kuna baadhi ya watu mambo kama haya yanawakuta, mimi nipo kitengo cha I.T na nina ndugu mmoja ambae alikua I.T wizara ya fedha, i think ni maintainance or something, huyu ndugu kila akirudi nyumbani huwa alikua ananiomba mimi nimuelekeze vitu ambavyo yeye amesomea, i was basically doing her job for her, akipewa cha kufanya inamchukua more than 2 days kukamilisha, na kazi hii ameipata kwa ajili ya cheti chake.
Serikalini its harder to get a job bila cheti ila lets apply this same situation kwenye private sector (just to punguza malumbano) , mfano lets say huyu dada ameajiriwa na private company na computer ikiwa slow, kazi hazifanyiki for 2 days, which the company looses 4 million within hizo siku mbili then muajiri akaambiwa kuna mtu who can solve matatizo kama hayo kwa dakika 15 instead of 2 days ila hana cheti hata kimoja.... oh yeah na pia anatengeneza websites, ana uwezo wa ku edit picha pia, networking anaweza pia, ila hana cheti hata kimoja...
Muajiri ataesema ngoja nimuache huyuhuyu tu huyo hapati kazi hapa kisa hana cheti, hiyo kampuni haito last miaka mitano inayofuata.

Cheti pia kinadanganya watu wengi, wanaona kisa yeye anacho cheti basi ana deserve kupewa kazi, anajiona kuwa value yake ni kiasi flani kwa ajili ana cheti lakini the truth is very different. What is the value of kitu ambacho kila mtu anacho, well basically nothing, so watu hupata kazi kwa nepotism (upendeleaji wa kujuana) ama kwa njia ambayo wengi hawaijui which is Value. Ongeza value yako ten folds kazi inayohitaji nusu ya hiyo value utaipata kirahisi sana.

Value unaipata kwa expirience, adding more skills na kuwa na more connections.

3) Fanya kazi kwa malengo

Mimi nilikua nafanya kazi ili kujifunza as much as i can, kuhusu uendeshaji wa kampuni. nimefanya kazi kampuni ambazo zipo successfull na nimefanya ambazo zimefeli, so najifunza kote kipi wanachopatia na kukosea ili ninapokuja anzisha kampuni yangu nisirudie makosa na nifuate niliyoona yamefanywa sawa. Nikiona sina kipya cha kujifunza, akili yangu ina kwama haiwezi kuendelea kufanya kazi hiyo sehemu, ndiyo maana kuna kampuni nimefanya siku tatu na nyingine mieze sita.

The fact kwamba nimefanya kazi zaidi ya saba full time within the span of 3 years is me selling myself short, kuna za part time ambazo sijazi include kuna ambazo naingia tu then naacha bila hata kufikisha wiki sijazi include, i moved to doing freelance, then owning private companies baada ya kuona kwamba expirience na mafunzo niliyopata vinatosha.

So kama malengo yako ni kupata kazi moja tu utulie uendelee na maisha yako njia hizi sio za ku copy zote, chagua kitachofaa then apply, ila kama una tafuta expirience and connections na unataka kujiingizia kipato huku ukijifunza vyote utavyoweza jifunza kuhusu uendeshaji wa kampuni then by all means chukua and apply as much as you can from these methods ntazokua nazi jot down every once in a while.

Again ntatafuta mda nimalizie point nne za mwisho, kama bado kuna wataohitaji, kusuka mada itayokaa kwenye mpangilio mzuri inahitaji mda, siyo mda tu ila kichwa na chenyewe kiwe cheupe.

narudia tena hii ni part 1.5, najibu maswali mengi yaliyoulizwa part 1 ambayo ina njia nne za kupata kazi popote hii hapa https://www.jamiiforums.com/threads/njia-rahisi-8-za-kupata-ajira-popote-ukiwa-umemaliza-chuo-hizi-hapa.1062090/ part 2 on its way
Nashkuru bro umeniongezea kitu
 
Daah pongez saana mkuu unaonekana we si mbinafsi kutokana na tabia yako ndio maana mungu anakusaidia ktk kila njia unazopitia
 
Very inspiring writting
Nakuona wewe kama moja wa tu wachache sana wanaojitambua wawapo kazini. You are thinking first of the results and progress of the company than what your personal benefits.

Umeni-inspire sana pale uliposema kuwa wakati wengine wako bize na kuchati insta na facebook, tayari wewe ulishaanza kazi za kesho yake.

I wish to hear more from you.

Usiwe unapotea muda mrefu bila kurudi huku kwenye uzi wako kuona response na maswali ya watu

asante sana kaka.. najitahidi kuwa nachangia zaidi, kuna mambo mengi nafanyia kazi ningependa kushare zaidi as time goes, ntatafuta the best way to do so.
 
Ubarikiwe sana mkuu! Thread nzuri sana sana.. japokuwa mimi sio 'mtafuta ajira' lakini kuna kitu kikubwa sana sana nimejifunza na naamini kitanisaidia kwenye mishe zangu.. Natamani urudi tena uweke muendelezo..
 
Daaaah, nisipokupongeza nitakuwa mchoyo, PONGEZI NYINGI SANA KWAKO MKUU, kiukweli umetufungua macho broo, vijana tulio wengi huwa tunapenda pindi tumalizapo vyuo tupate kazi hapo hapo na mshahara mzuri tu, kinyume na hapo wengi hukata tamaa, kwa hili acha tukajitolee tu kuliko kukaa kitaa tukisubiria simu za interview miaka nenda rudi, mwisho wa siku tunaweza tukajikuta tushakuwa waganga wa kienyeji bila kutegemea! tunaomba upatapo muda endelea kutupa madini zaidi na zaidi... JF buana
 
Hongera sana, kumbe kwenye haya company inakuwa ni geresho kutuma MAOMBI kumbe watu wameshachaguliwa Muda unatuma maombi uwitwi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom