Njemba zinapotwangana kwa penzi la baamedi!

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
68,012
95,352
Hii kwangu ilikaa vibaya. Mwanzoni nilidhani masihara mpaka niliposhuhudia makonde na chupa zikirushwa. Kisa? bar maid.

Ni kwamba kuna ka baameid kamoja ka kimbulu kameleta zahma kwenye bar moja mitaa ya kwetu (lazima nikiri ni kazuri, kwakuwa hata mzee mzima nilikuwa napanga kukasarandia). Njemba moja kumbe ndio inakaweka mjini; imekapangia chumba na inakapa fedha za matumizi. Kumbe swahiba wake njemba ambaye anajua uhusiano ule akawa anakaiba kisirisiri. Siri ikafichuka jana, baada ya mabaameidi wenye wivu kumtonya mwenye mali.

Njemba yenye mali, ikapandisha na kushusha presha. Ikamsubiri swahiba wake anayemwibia. Kama masihara vile, njemba mwizi ilipotinga kaunta na kuagiza ka valeur kake ikashangaa inakwidwa kwa nyuma. Wadau kwakuwa tunaujua uswahiba wao, tukadhani masihara mpaka ulipoibuka mtiti wa kufa mtu.

Kibaya zaidi hizi njemba zote zimeoa, na zinaishi maeneo ya jirani. Nadhani mpaka mida hii, habari zitakuwa zimefika kwa wake zao. (Labda na kwa wife wangu pia, huwezi jua. Nasubiria nipigiwe simu kuulizwa kulikoni kwakuwa njemba zenyewe ni washkaji zangu pia.)

Kutandikana kwa sababu ya penzi la baameidi imenishangaza sana. Na kumgharamia baameidi kiasi kile wakati wale ni watu wa kumegwa na kila mtu atakaye ndilo limenishangaza zaidi. Ni mimi tu nimebakia, ni mimi tu kuwaletea habari.

Wasalaam.
 
chrispin kweli weye unajidhihirishan hujatulia

wanaume kwa nini mnafanya hivi mnatia aibu mmeoa ??? mnaacha wake zenu majumbani mnaenda kugombea baamed ,aibu baamedi anawafanya mpoteze heshima yenu
aibu sana ..ukitoka hapo ukakuta mkeo amekosea kidogo ugomvi unashindwa kumsamehe
aaah nasikia hasira
 
FL1 Nitake radhi. Mi sijatulia kivipi? Aliyepigana si mimi wajameni. Mimi nimebaki kuwaleteeni habari.
 
chrispin kweli weye unajidhihirishan hujatulia

wanaume kwa nini mnafanya hivi mnatia aibu mmeoa ??? mnaacha wake zenu majumbani mnaenda kugombea baamed ,aibu baamedi anawafanya mpoteze heshima yenu
aibu sana ..ukitoka hapo ukakuta mkeo amekosea kidogo ugomvi unashindwa kumsamehe
aaah nasikia hasira

na wewe mwenyewe hujatulia .si ndo juzi ulisema huyu ni mumeo wewe na umejisikia kumwambia kupitia JF kuwa unampenda.lol
 
na wewe mwenyewe hujatulia .si ndo juzi ulisema huyu ni mumeo wewe na umejisikia kumwambia kupitia JF kuwa unampenda.lol

Mkuu heshima mbele. Wivu wa kupigwa chini au? Hahahahah!
 
wewe umesema unamtamani baamed nakuomba radhi :)

Apology accepted. Lakini kuna ubaya wowote wa kumtamani baameid. Hujakaona hako ninakozungumzia, acha walume watwangane bana. Kana mvuto balaa.
 
Kutandikana kwa sababu ya penzi la baameidi imenishangaza sana. Na kumgharamia baameidi kiasi kile wakati wale ni watu wa kumegwa na kila mtu atakaye ndilo limenishangaza zaidi. Ni mimi tu nimebakia, ni mimi tu kuwaletea habari.

Wasalaam.
....................... Mh hii sifa hata si haki kuwapa wao mbona kuna wanawake na ndoa zao wanaomegwa ovyohovyo na si mabarmaid?....... watake radhi tafadhali!
 
Hapo sasa unajua nini mkubwa hako kamburu c kana kwamba ni kazuri ila itakuwa pia ni katamu kuliko wake wa hizo njemba na vilevile hata wewe pia ungemega angempita mkeo
 
....................... Mh hii sifa hata si haki kuwapa wao mbona kuna wanawake na ndoa zao wanaomegwa ovyohovyo na si mabarmaid?....... watake radhi tafadhali!

Nitajie wawili unaowajua, then ntaomba radhi.
 
Hapo sasa unajua nini mkubwa hako kamburu c kana kwamba ni kazuri ila itakuwa pia ni katamu kuliko wake wa hizo njemba na vilevile hata wewe pia ungemega angempita mkeo

Lol! Mkuu nakushauri uje ukaone. Ni kazuri kinoma. Ila kwamba ni katamu kuliko my wife wangu, hapo unashauriwa umtake radhi mke wangu kabla hujanitaka mimi radhi. You are crazy man/woman.
 
Ha ha ha aha aha hako sio tu kamburu ila ni kamburu meeee. Washa tu. Katamu ati
 
Hapo sasa unajua nini mkubwa hako kamburu c kana kwamba ni kazuri ila itakuwa pia ni katamu kuliko wake wa hizo njemba na vilevile hata wewe pia ungemega angempita mkeo

Wadau tatizo watu wanawafanya wanawake wa nje vitu ambavyo mkewe hawezi kumfanya hata siku moja. Hayo mambo ya utamu yanakuaja hapo.

Ingekuwa watu wako huru kuwafanyia wake zao yale wanayoyafanya huko nje,nawaambi haya mambo ya kutoka nje yangeisha.
 
Hii kwangu ilikaa vibaya. Mwanzoni nilidhani masihara mpaka niliposhuhudia makonde na chupa zikirushwa. Kisa? bar maid.

Ni kwamba kuna ka baameid kamoja ka kimbulu kameleta zahma kwenye bar moja mitaa ya kwetu (lazima nikiri ni kazuri, kwakuwa hata mzee mzima nilikuwa napanga kukasarandia)

Kutandikana kwa sababu ya penzi la baameidi imenishangaza sana. Na kumgharamia baameidi kiasi kile wakati wale ni watu wa kumegwa na kila mtu atakaye ndilo limenishangaza zaidi.

Wasalaam.

Chrispin una mambo weye,kauli zako zinanipa utata,ni kazuri nawe pia ulipanga kukasarandia, kwa nini ulipanga kukasarandia na unajua fika kuwa kanachukuliwa na rafiki yako? yaani hapa inaonyesha kabisa wewe na rafiki zako kazi yenu ni kusaliti tu wake zenu.

Kingine umesema unashangaa jamaa kutandikana kwa sababu ya barmaid,unachoshangaa ni nini wakti nawe ulikuwa kwenye mkakati wa kukafata hako kambulu? Isije ikawa ni wewe ndo mlitandikana na jamaa halafu unakuja kutubadilishia hapa mada kuwa kuna majamaa kumbe mhusika mkuu ni wewe.
 
Back
Top Bottom