Njemba ilikua ina kiwanda cha kutengeneza gobole

jmnamba

Senior Member
Mar 31, 2012
156
25
Njemba moja hiyo alikamatwa siku kadhaa zilizopita alikua ana kiwanda cha kutengeneza silaa za moto aina ya gobole ambazo baadhi alizotengeneza zilishatumika kwenye ujambazi sehemu kadha wa kadha...
Mhusika wa aina hii anapokamatwa ndio kinyume cha sheria lakini je kwa mfano angeendelezwa kwa fani aliyonayo kuna ubaya?
 
Badala yake twaagiza AK47 toka Russia wakati ukiwagroom watu kama hao tunaweza pata at Tz2012
 
Njemba moja hiyo alikamatwa siku kadhaa zilizopita alikua ana kiwanda cha kutengeneza silaa za moto aina ya gobole ambazo baadhi alizotengeneza zilishatumika kwenye ujambazi sehemu kadha wa kadha...
Mhusika wa aina hii anapokamatwa ndio kinyume cha sheria lakini je kwa mfano angeendelezwa kwa fani aliyonayo kuna ubaya?

Mimi pia nilipomsikia huyu jamaa,nilipata wazo kama la kwako! Kwa maelezo ya kamanda wa polisi,ni kwamba hizi Gobole zimetengenezwa kwa technologia ya kisasa na zinatumia risasi za kisasa! Niliposikia hilo,nikasema huyu jamaa angewezeshwa angetengeneza vitu mpaka tuka-export hata Marekani,badala ya ku-import!
 
Badala yake twaagiza AK47 toka Russia wakati ukiwagroom watu kama hao tunaweza pata at Tz2012

POINT!!
Magereza yetu yasitoe adhabu za kulima na kukata miti au kazi nyingine za suluba!
Skilled people lazima walelewe ili ku convert ujuzi wake toka njia mbaya kwenda kwenye njia itakayo boresha maisha yake na ya jamii kwa ujumla!
 
kwa ushujaa wa huyo jamaa mtengeneza gobole siwezi kumtofautisha na mtu anaeweza kunywa bia aina ya safari ya moto mchana wa saa 6...
 
Acheni masihali nyie. Mnataka tuwe kama rwanda nn? Kila mtu amiliki siraha, hivi itakuaje??

Afu mimi napinga sana huu mchezo wa kumiliki silaha. Naona umeshakuwa fashion kwa viongozi.. Siku hizi kila kiongozi ana silaha. Hii ina maanisha nn?

Dhamana tuliyowapa viongozi wetu kusimamia usalama wa nchi hii. Wenyewe wanatumia hiyo dhamana na kodi tunazowalipa kununua silaha za kujilinda wao kwanza... Hii ni tabia mbaya ya ubinafsi.... Kwanini wasiboreshe mfumo wa usalama nchini. Nini maana ya kuwa viongozi? Kujilinda mwenyewe kwanza?

Huwezi kukuta nchi makini kama marekani au uingereza, kiongozi anatembea na silaha mtaani...

Africa viongozi wetu hawako responsible na usalama wa nchi na raia. Ndo maana kila kiongozi anajilinda mwenyewe. Sasa ngoja kila mtu awe na bunduki ndo hapo tutapoona usalama wa nchi utavyokuwa

Na hao hao viongozi wakiwa bungeni eti utawasikia, "tulinde amani na usalama wa nchi yetu". Mbona wenyewe wanatembea na bunduki mfukoni kama nchi yetu ni ya amani???
 
Hii njemba ililfanya makosa. Ilipaswa kufanya ushirika na Adam Malima isingekamatwa. Maana Malima anafahamika kwa kupenda sana mitutu huenda angeweka ubia kiasi cha kutengeneza kombola la kutungulia ndege.
 
Wabunifu wa namna hiyo ni wengi sana nchini, sema sheria ndo zinawabana. Viwanda vya magobole na rifle vipo, kimoja kinaitwa Mzinga na kipo Mji kasoro Pwani. Huyu njema ilitakiwa apelekwe hapo Mzinga kwenda kufundwa ujuzi zaidi na si kuswekwa ndani. Wilayani Mbozi Mbeya, viwanda hivi vilishamiri sana miaka ya '90 kuja 2000, lakini Kova na Mwema kwa nyakati anuwai wakiwa makamanda wa polisi wa mkoa huo walivisambaratisha sana
 
Back
Top Bottom