NJAMA za Serikali, CCM & CUF, mikononi mwa Habari Leo, soma;

Kanawe uso urudie kusoma kisha uje na jibu hapahapa jukwaani!!
 
CUF walshachumbiwa long 2 mbona na mabwana zao CCMndoa yao naona imewadia. viva Chademaaaaa..........!
 
Siishangai CUF hata kidogo,namshangaa Lipumba!!!!
A%20S%2039.gif
 
Hiyo inaitwa mchakachaka watu wanatafuta pakujishika mwageni sera cuf wacheni wengine waendekeza vurugu na maandamano
 
Wakuu

Kile kinachoonekana kuwa ni mkakati maalum uliopangwa
kati ya CCM, CUF na baadhi ya viongozi wa serikali katika baadhi ya
mamlaka/ vyombo vya serikali dhidi ya CHADEMA, unaweza kukiona kwa uzuri
kwenye para kadhaa 1-5, kisha 14-mwisho, za stori ya Habari Leo,
iliyoandikwa Septemba 28, 2012, kama unavyoweza kuisoma hapa
chini.



CUF
yaitisha Chadema


Katika uandishi wa habari, hasa katika kufanya
kinachoitwa analytical reporting, mwandishi au mhariri asipokuwa
makini au kama hawezi kufanya aina hiyo ya uandishi kwa uzembe au kwa
kuzoea merely reporting (so and so said so, conveyer belt), ataishia
kuweka maoni yake au kuandika kile anachokitaka yeye. Hapa inakuwa ni
uhandisi wa habari, si uandishi wa habari tena.


Ukiisoma hiyo habari kwa umakini. Katikati ya maneno.
Ukafanya mahesabu ya kifikra, hasa katika kutafuta mantiki za hoja na
hatimaye kufikia hitimisho lililo sahihi na linaloaminika, utaona wazi
mchezo ambao baadhi yetu hapa mlishaanza kuuzungumza tangu jana.


Kwa uhakika mpaka leo asubuhi, vyanzo vya kuaminika vilikuwa vimeshatoa
mrejesho ulio kamili juu ya dokezo/angalizo la awali kabla hata ya
mkutano wa Jangwani ambapo ‘jamaa' walifanya mkutano wa hadhara, kisha
wakatangaza ‘copy and paste' ya kile ambacho CHADEMA walikuwa wanafanya.
Haikuwa dhambi.


Behind


Mapema sana, vyanzo vikaanza kutoa viashiria vya kuwepo kwa kitu kikubwa
zaidi nyuma ya V4C kilichokuwa nyuma ya pazia.


Inajulikana wazi kuwa CCM na serikali sasa hawawezi kufanya siasa tena.
Si bungeni, wala nje ya bunge. Kote huko wamechuja na hawawezi kujibu
hoja za CHADEMA tena. Kwa hiyo ilikuwa lazima itafutwe mbinu ya
kudhibiti watoa hoja. Kudhibiti wakosoaji. Kudhibiti upinzani usifanye
kazi yake ya kikatiba.


Njia nzingine haramu za kuwinda na kutaka kuua viongozi wa mabadiliko,
ikiwemo kumteka na kumtesa kutaka kumuua Ulimboka, kufungia Mwanahalisi
na kutaka kuwaua baadhi ya viongozi wa CHADEMA, hatutazijadili hapa kwa
sasa.


Njia ya kutumia vitisho, kwa kuua watu ili kuendeleza
propaganda kuwa CHADEMA ni chama cha vurugu na shughuli zake zinaendana
na vifo vya watu, ilikuwa futile. Hasa katika matukio mawili ya hivi
karibuni.


Pamoja na polisi kumuua kwa makusudi kijana Ally Zona pale Morogoro,
bado wakazi wa mji ule walikusanyika kwa wingi mno katika moja ya
mikutano mikubwa ya kihistoria ya CHADEMA, achilia kwa mkoa huo wenyewe.
Tukio la Polisi kumuua kwa makusudi Daudi Mwangosi likazamisha kabisa
mipango yao hiyo ya kutumia vyombo vya dola.


Sasa ilikuwa lazima mkakati mwingine ubuniwe na uanze kufanya kazi. V4C
ikawa moja ya fursa sahihi ambayo watu wengi wanaweza wasiione kwa
haraka na kwa uwazi.


Kwanza; kutaka kuonesha kuwa CHADEMA na CUF wako kwenye league moja.
Yaani vyama hivi vianze kujibishana. Automatically hapa focus ya
kuendelea kuipiga CCM na serikali yake inakuwa imepotezwa, hivyo wakati
vyama vya upinzani hivyo viwili vinajibishana, jamaa wanakatiza
katikati.


Lakini pia mkakati huu ulidhaniwa kuwa ni njia nzuri ya kuirudisha CUF
kwenye forum ya walau kuanza kujadiliwa kila siku. Maana kujibishana na
CHADEMA kungewapatia jukwaa la bure. Ndiyo maana tangu siku ya kwanza,
neon CHADEMA lilikuwa ndiyo kibwagizo kwa hoja za wazungumzaji wengi
pale Jangwani. Huo mkakati ulishaonekana mapema.


Pili; ndiyo hiyo unayoiona kwenye Habari Leo. Kwamba zianzishwe vurugu
kwenye mikutano au mikusanyiko inayoihusu CUF kisha lawama zielekezwe
kwa CHADEMA. Kwa nguvu zote. Kwa kutumia kila njia inayowezekana. Si
ajabu gazti hilo lilianza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi. Soma vizuri
kuanzia para ya kwanza ya stori hiyo mpaka ya tano. Ukishasoma uzushi wa
Kambaya, soma tena kwa makini para ya 14 mpaka mwisho. Katika para hizo
unaona vyema kisichoonekana kwa akili ya kawaida hivi!


Sasa kwa nini hii namba mbili; simple. Inatafutwa hila ya kuzuia kazi za
kisiasa zinazofanywa na CHADEMA. Kama ilivyoandikwa hapo juu,
zitaanzishwa vurugu makusudi, watu wanaweza kupigwa/kupigana kwa
makusudi. Watu wataumia. Kutakuwa na tension ya kutengenezwa.


CUF watatoka na kudai waliofanya hivyo ni CHADEMA. Hivyo nao wanajipanga
kulipiza kisasi katika maeneo mengine kwa kisingizio eti wamefanyiwa
fujo na CHADEMA blah blah blah! Hili tayari limefanyika hivi majuzi,
ambapo CUF wamepita sokoni, wamefanyiwa fujo na watu wachache
wasiojulikana, mbele ya Askari Polisi, muda mfupi kiongozi wa chama
hicho anakurupuka kuhitimisha waliofanya hivyo ni CHADEMA.


Hizo ni hisia zako tu!
 
Huku Mwanza ili wafanikishe mambo yao,shalti waanze na salaam ya PEOPLES.......kama alivoambiwa PINDA.
 
Wanakwenda kinyume na malengo ya chama cha upinzani. Chama chochote cha upinzani lengo lake kuu ni kushika dola/ madaraka kwa kuonyesha madhaifu ya serikali na kuomba ridhaa ya wananchi kuongoza. KWA HILI, CUF WAMECHEMKA
 
Mwisho kabisa shetani atashindwa na wokovu utatamalaki kwa Wanaomtegemea Mungu. Wenye mbinu za kishetani wote watashindwa b'se God is always superior!
 
Mungu atawalipa stahiki awanayohitaji, njaa mbaya sana, wao CUF walifanyiwa mengi mabaya lakini CDM haikuwa kuiunga mkono serikali na CDM wamewaunga mkono sana CUF katika chaguzi mbalimbali tangu 1995, mpaka mwaka 2005 walipoamua kujitegemea baada ya kuona CUF hawako tayari kuwaunga mkono CDM...

CUF Wanajiua wenyewe kwakupambana na CDM badala ya kupambana na watawala wa CCM. Lakini yanamwisho na mwisho Watajulikana tu na mipango yao michafu ya kutumika.

Hawajiulizi ni kwanini ccm imeshindwa mpaka sasa inaamua kuwatumia wao? Inavyoonekana CUF kwa sasa wao wakipewa fedha hata na NCCR, TLP, ADC au chama kingine chochote wako tayari kutumiwa ilimradi tu wao wapate fedha. Kinachomuweka Prof. Lipumba CUF mimi nadhani ni ruzuku ya chama anayopokea kutoka serikalini tu, akipoteza nusu ya wabunge ktk uchaguzi ujao hawezi tena kuendelea kubaki CUF kwani kinachomuweka hapo kitakuwa kimetoweka.
 
CUF na CCM ni kitu kimoja hatudanyiki
Kijana niseme kama umekurupuka. Wengi wa wenu wana cdm mumekuwa mukisema kwamba ccm na cuf wana ndoa moja. Nataka mutoe ushahidi wenu. Je? Ni wazir gani au naibu waziri au nafasi gani ya uongozi katik SMT aliyetoka cuf.
 
Back
Top Bottom