Njama za kummaliza Dk. Slaa, CHADEMA zabainika

washwa washwa

JF-Expert Member
Jul 21, 2012
1,613
717
amka2.gif
IMEBAINIKA kuwa mwenendo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika mikutano na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni mkakati wa makusudi uliosukwa na watawala ili kukivuruga chama hicho, na kuwatisha wananchi kwamba ni chama cha fujo.
Hii si mara ya kwanza kwa watawala kufanya njama hizi dhidi ya wapinzani. Mara ya mwisho, waliofanyiwa hivyo ni Chama cha Wananchi (CUF), kilipokuwa chama kikuu cha upinzani.

Njama hizo zilikiangusha chama hicho, hadi kikajisalimisha kwa kufunga ndoa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, huku kikipoteza mvuto Tanzania Bara.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameliambia gazeti hili kuwa, CHADEMA inapaswa kuwa macho na njama hizi, kwani CCM imegundua kwamba inazidi kudhoofika na CHADEMA kinazidi kuimarika katika jamii; hivyo walio madarakani wanafanya kila njama kuua wapinzani ili wabaki madarakani.

Siku chache zilizopita, polisi walimuua kijana Ally Zona wakati wakitawanya waandamanaji wa CHADEMA mjini Morogoro. Jumapili iliyopita wameua mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi, mkoani Iringa na kuleta sokomoko la kitaifa, ambalo limelichafua mno Jeshi la Polisi na Tanzania mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Utetezi wa polisi na jitihada zake kuwasingizia CHADEMA, waandishi na wananchi wengine kuwa ndio walifanya mauaji hayo, umegonga mwamba kwa sababu katika matukio yote haya, wapo mashahidi waliokuwapo pale pale.

Matukio haya yanatokea wakati ambapo vita ya kisiasa baina ya chama kilichoko madarakani na CHADEMA ikizidi kuongezeka kutokana na uungwaji mkono mkubwa unaopata chama hicho cha upinzani kwa sasa kuliko historia ya wakati mwingine wowote.

Kasi ya kukua kwa CHADEMA katika miaka ya karibuni inatishia madaraka ya watawala ambao wamekuwa madarakani kwa miaka ipatayo 50, na ambao chama chao, CCM, kimepoteza mvuto kwa umma, na hakiaminiki kutokana na kuzongwa na tuhuma nyingi za ufisadi, na kukumbatia makundi hasimu yanayotafuta madaraka na masilahi mengine, huku yakiendelea kudhoofisha uongozi wa CCM uliokwisha nyong’onyea.

Wakati CHADEMA kikipambana kukumbatia mapenzi ya umma unaokiunga mkono, huku kikifungua misingi na matawi vijijini, CCM inahaha kukidhibiti kwa propaganda na nguvu za polisi.
Kwa muda mrefu, CCM imejaribu kukipaka CHADEMA matope ya ukanda, ukabila na udini, kama ilivyofanya kwa CUF miaka ya nyuma; lakini baada ya kuona mbinu hizo zimeshindikana, sasa imeamua kutumia jeshi kutisha viongozi wake na wananchi kwa visingizo mbalimbali.

Hata hivyo, CHADEMA kinasema kimejiandaa vema kukabililiana na propaganda zote na vitisho vya watawala; na kwamba kimejifunza kwa makosa waliyofanya wengine katika NCCR-Mageuzi na CUF.
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, anazo tafsiri tatu za matukio ya mauaji yanayofanywa na polisi katika mikutano ya CHADEMA.
Anasema: “Hawana majibu na matatizo ya wananchi, hawana majibu na tatizo la maji, elimu, matibabu ya uhakika na kero kadha wa kadha zinazowakabili wananchi. Kwa sababu hawana jibu, wanatumia nguvu. Sasa hawatumii vitisho tu, wanatumia nguvu.
“Hii ni taswira ya ‘system’ (mfumo) inayojua inaondoka. System imara haitumii nguvu, inatumia vitisho, kama kupeleka watu mahakamani. Sasa huko tumekwishapita, tumeingia katika hatua ya kuuawa.”

Tafsiri ya pili ya Lissu, ambayo ina uhusiano na ile ya kwanza, ni kwamba kwa vile watawala wanaona wako hatarini kuondoka, wanatafuta namna ya kuwachafua CHADEMA kwa wananchi ili wawaogope.
“Ikishindikana kutuchafua kwa propaganda wanaua. Wanaua watu kwenye mikutano na hadharani. Maana yake ni nini? Ni kwamba wanatuma ujumbe kwa jamii kwamba ukienda kwenye maandamano ya CHADEMA utakufa. Tafsiri yake ni kwamba watu waogope,” anasema Lissu.

Tafsiri yake ya tatu ni kwamba, watawala wanatengeneza mazingira ya kisiasa ili CHADEMA kionekane chama cha vurugu, ili utafutwe msingi wa kukifutia usajili.
“Ukishafanya mauaji kwenye mkutano unajenga mazingira ya kusema hiki chama hakina sifa, unamtengenezea mazingira msajili wa vyama vya siasa akiondoe…ukikiondoa CHADEMA maana yake umeondoa mgogoro na bungeni…utawaondoa akina Lissu, akina nani kule… Hivyo, nasema wanatafuta sababu ya kuendelea kutawala kupitia kuua raia,” anasema Lissu.
Anasisitiza kwamba kwa mantiki hiyo, Jeshi la Polisi limeacha kazi yao ya msingi ya kulinda raia na mali zao, na sasa limegeuka jeshi la kulinda walio madarakani ili waendelee kutawala.

“Jeshi limegeuzwa chombo cha ulinzi wa watawala. Hilo la kusema kwamba kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao ni siasa, lakini the primary function (kazi yao ya msingi) ambayo hawaisemi ni hii ya kulinda watawala ili waendee kuwepo,” anasema Lissu.
Aidha, wachambuzi wanasema kinachotokea sasa ni kwamba watawala wanaanza kuhamanika, na wanaweza kutumia polisi kutenda mambo ambayo hatima yake itakuwa mbaya kwao, kama ilivyokuwa kwa watawala wa mataifa mengine waliofikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu, The Hague, Uholanzi.

Taratibu, kwa sababu ya matumizi mabaya ya Jeshi la Polisi, hata sifa ya Tanzania katika jamii ya kimataifa inaanza kuchafuka.
 
Mimi nakubaliana na hoja, anayewindwa kuuwawa ni dr, Slaa. Mtindo huu wa mabomu utakuja kutumika kwa viongozi wa CDM ikiaminika kuwa kulitokea fujo na ikabidi kutumia mabomu; kumbe bomu moja litatumika kama lile lililomuua Mwangosi kwa viogozi wa cdm.
 
Hiyo ni mbinu ya kuwatisha wananchi.robert Mugabe alitumia mbinu hiyo kule Zimbabwe hadi Morgan Tsavangirai akasusia duru ya pili ya uchaguzi kwa kuwa kila mkutano wananchi walikuwa wakiuwaawa na kuteswa.Hapa haturudi nyuma

Nilishangaa watu wengine wanakurupuka na kutoa maneno ya kufuta chama cha siasa bila kufikiria mwenendo wa vyombo vya diola katika kukwaza demokrasia.Kama watajaribu kufuta usajili wa CHADEMA kwa hila yoyote watakiona cha moto.Hawa makamnda wote watapelekwa wapi?Hatutavua kombati ....Tutaenda mbele zaidi,extreme measures!
 
Story za kutunga. Kuuana wanasisa upinzani umepitwa na wakati na kamwe sio awamu ya JMK.
 
Kuua mtu ni jambo rahisi sana kuliko tunavyofikiri, unaweza kumpiga mtu ngumi moja tu kichwani akafa, lakini ukisikia kuwa mtu ameua unaweza pata picha kuwa ilichukua juhudi nyingi kuua, vivyo hivyo nchi kuingia kwenye machafuko na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ni rahisi mno kuliko watawala wanavyofikiria. Kama wakiendelea na mambo haya wanayoyafanya, wasahau hata hayo madaraka wanayoyaota.
 
Aluta continua CDM!!! Nguvu ya Wananchi itasema tu 2015. Watu hatuangalii mtu, hata akiondoka Dr. Slaa bado CDM ni Viva forever!!
 
Hiyo ni mbinu ya kuwatisha wananchi.robert Mugabe alitumia mbinu hiyo kule Zimbabwe hadi Morgan Tsavangirai akasusia duru ya pili ya uchaguzi kwa kuwa kila mkutano wananchi walikuwa wakiuwaawa na kuteswa.Hapa haturudi nyuma

Nilishangaa watu wengine wanakurupuka na kutoa maneno ya kufuta chama cha siasa bila kufikiria mwenendo wa vyombo vya diola katika kukwaza demokrasia.Kama watajaribu kufuta usajili wa CHADEMA kwa hila yoyote watakiona cha moto.Hawa makamnda wote watapelekwa wapi?Hatutavua kombati ....Tutaenda mbele zaidi,extreme measures!

A Very good comment, Ben. Tendwa jana alinikumbusha ndugu yangu mmoja ambaye aliwahi kuugua cerebral malaria kisha akapona. Kwa kitu kama mwezi hivi, hakuna mtu alikuwa anamwelewa anachokizungumza.
 
dah!! ama kwa kweli ccm MAONGO/MAJAMBAZI/MAFISADI/WAUAJI wanaichungulia kambi ya upinzani live. wameona wamebanana, hawana uhakika wa kuwashawishi wananchi kwa hoja, njia pekeee waliyochagua ni kucheza rafu mbaya. hiki kikundi cha ccm hakina maana tena.


Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waliong'oe madarakani hili li serikali la ccm MAONGO/MAJAMBAZI/MAFISADI/WAUAJI.
 
2 015 napaona mbali sana inamaana hatuna njia nyingine ya kumtoa huyu nduli ccm ?
 
Back
Top Bottom