Niyaweke wapi maisha yangu jamani?

sonny

Member
Mar 12, 2012
8
1
Uwa nakaa nakujiuliza juu ya best yangu nakosa cha kumshauri,yeye ana miaka 26 anaishi Arusha lakini amezaa na mwanamke anamiaka 34 anaishi Dar es Salaam ni mfanya kazi,jamaa hana kazi bado ingawa amemaliza chuo kikuu pale Udom,lakini pia ana mpenzi mwingine ambae wanapendana sana na huyo mpenzi ana miaka 21 yuko chuo kikuu Arusha,shida inakuja kuwa jamaa anamtegemea yule mzazi mwenzie kwa kila kitu mpaka kodi ya nyumba na kwao na best yangu hawajui kama anamtoto na wanamtambua huyu msichana wake wa Arusha,juzi huyo mzazi mwenzake amesema jamaa aamie Dar ili wakaishi wote sa jamaa anakosa raha kabisa,ndo naomba ushauri ili nikamshauri best na tena ukizingatia huyo mzazi mwenzie alishawahi kuolewa halafu akaachika kwa hiyo ana watoto wawili pembeni,je best afanyaje jamani ndugu zangu naombeni mawazo nimsaidie best friend!Asante
 
huyo rafiki yako unayemsema mbona ni wewe? Wewe si ndo umezaa na binti huyo halaf hujapata kaz bado? Cha kwanza tafuta kazi kwanza
 
wazazi hawajui akakwambia wewe...kwa jinsi mazingira yalivyokaa...hii ishu ni yako.

achana na ilo limama wewe...dume zima unatunzwa hadi kodi na kidegree chako...hivi mmekuaje nyie??

apo unatofaut gani na mwanamke anaeomba ushauri wa aolewe na nani kati ya hao.........

we mwachie ilo litoto likipata akili litakutafuta.we kaa na machalii apo tafuta kazi hata ya tempo wewe..ivi kukaa kote apo huna conection japo ata ufundishe sec (maaana huwa ni rahisi kdg) upate izo lak 3 kwa mwezi........

unakaa kabisa unamuomba akutumie hela;........my foot!!!!

wanaume wameisha hapo bado kupungukiwa izo nguvu tu!!nakasirikaga sana yani
 
Watu wanachonga sana kuhusu degree za UDom, kwamba haziajiriki. Hapa utasababisha tuuamini uvumi huo.
 
yeye moyo wake unampenda mwanamke gani kati ya hao wawili?asikilize moyo wake bila kujali material things kama pesa na vingine eboo
 
acha kuzuga wewe hio inshu ni yako..na sijui unataka ushauri wa nini wakati unaonyesha unapenda kulelewa..hamia dar ukaolewe kabisa..kuna wimbo flani unaitwa wanaume kama mabinti..jalibu kuusikiliza plz..!
 
namshauri apambane kwanza na life yake,atafute kazi then mengine yafuate,bora abaki na huyo mwanafunzi while akifight maisha kuliko kwenda kwa jimama.kula kulala kwa men haipendezi,atajuta ....
 
Kila ajira ina masharti yake.....
Nenda kwa mwajiri wako kijana, sivyo utafutwa kazi.
 
pole sana mkuu,
huyo rafiki yako/kama sio ww mwambie achana na huyo limama mtu mzima , nafikir hata ukiwa nao hutakuwa confortable.

tafuta kaz ya kufanya ili ujitegemee, usiwe tegemezi hutakuwa na maamuzi.
 
pambaf sasa na hili nalo linaushauri tena? Waache wazee wachukuane wao kwa wao..ampige chini tu kwni ni nini?atalalamika mwanzoni but baadae utakua poa tu..after all life is not fair
 
Vijana wa kileo wapenda mtelemko mno ndo wanaoitwa marioo hao. Mwambie ajitume mwanamume si lazima kuajiriwa atafute kibarua hata cha kubeba zenge mwanamume ili siku moja aweze kuwahadithia wanae na wadogo zake maisha yalivyo tough. Sasa yeye anataka vya bure basi ndo matokeo yake hayo. Beba hata zege degree itafanya kazi baadae
 
Tamaa imemponza kupenda vya bure, kwani yeye kakwambia hampendi huyo mzazi mwenzake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom