Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,710
Udini ni msamiati tata ulioanzishwa wakati wa Nyerere.Iwapo maana yake ni kuonesha imani ya mhusika katika utendaji wa jambo,basi udini mbaya upo Chadema na ni ule alionao mgombea wake dkt.Slaa.Huyu jamaa alipokuwa akijifanya msemaji sana bungeni,hakuwahi kutetea jambo lenye maslahi na nchi lililoutaja uislamu.Kinyume chake alikuwa ni mpinzani mkubwa wa chochote chenye nembo ya uislamu.
Wagombea wanaogombea kupitia Chadema ambao ni waislamu hawapati ushirikiano mzuri na wanapopatwa na matatizo hawashughulikiwi kichama.
Nimefurahi kuwa katika mdahalo wa star TV kati yake na Kinana wa CCM,Slaa ameshindwa vibaya na kaboronga katika suala la kutoa matibabu bure kwa wananchi.
Post kama zako haziwasaidii sana wagombea wa kiislamu bali zinawatenga na Watanzania wasio waislamu waliokuwa wanawapenda kwa sababu za vyama au itikadi au uwezo binafsi wa mtu. Hivi unadhani kura za waislamu peke yao zinaweza kumpa mgombea yeyote ushindi? Wagombea wote wana wafuasi wa dini zote, na unampunguzia mgombea umpendaye kura unapomnadi kwa ajenda ya dini ujue hilo.
Fahamu kuwa nchi hii waislamu ni raia kama wengine, na bungeni yanazungumzwa maslahi ya raia wote kwa pamoja. Kwani hoja zilizoibuliwa na Dr. Slaa zilikuwa zinatetea maslahi ya wakristo? EPA ina uhusiano gani na Dini? Twin tower ya BOT nayo ina dini gani? Richmond ina maslahi kwa nani?
Hebu AMI tutajie japo hoja moja tu ya Dr. Slaa ambayo imetetea maslahi ya dini moja peke yake na kuweka kando wengine.
Nawaona watu kama wewe hatari sana kwa nchi yetu. Naogopa kabisa.