Elections 2010 Niwaonavyo wagombea watatu wa urais

Mbali na kampeni za uchaguzi zinazoelekea ukingoni kutoa mielekeo ya nani anafaa zaidi kukabidhiwa uongozi wa nchi.Ufuatao ni uelewa wangu kuhusiana na wagombea watatu wa nafasi hizo.Hao ni Ibrahim Lipumba,Jakaya Kikwete na Wilbroad Slaa.
Mimi binafsi kwa nafasi hii namuamini zaidi Ibrahim Haruna Lipumba.Namuona ana elimu ya mambo ya kiuchumi ambalo ndilo tatizo sugu la watanzania.Ana uchangamfu wa kiuraisi na huzungumza kwa hekima.Wale wanaompinga si kutokana na kukosa sifa bali sababu nyengine ambazo ikibidi nitazitaja baadae.
Jakaya Mrisho Kikwete ni mkweli katika utekelezaji wa ahadi zake.Hata hivyo amezungukwa na wajanja wengi wa hapa ndani ya nchi na wale wa nje ambao mara nyingi huwa wanaingilia maslahi ya watanzania na hata kumzonga ili asitekeleze baadhi ya ahadi ambazo ziko ndani ya uwezo wake.
Wilbroad Slaa.Nitakayoyasema juu yake hapa, najuwa si pahala muafaka.Lakini ukweli wa moyoni mwangu unanifanya nisiwe na chaguo jengine isipokuwa nimueleze kama nimuonavyo.
CHADEMA kwa makusudi au kwa bahati mbaya wametuletea chagua ambalo lisingepaswa kuwa hivyo kwa wakati huu.Kwa upande mmoja ni dalili za ulegelege wa chama chenyewe.Mgombea wao hana sifa za kuwa raisi.Fani ya elimu yake hachaguliki kwa kundi kubwa la wapiga kura.Si muadilifu kwa nafsi yake na hawaheshimu watu wanaomzunguka.Ni mpayukaji.
Katika siasa kuna kudanganya huku kwa undani mtu anafanya vyengine kama alivyofanikiwa raisi wa mwanzo wa Tanzania;Julius Nyerere.Hilo ni gumu kufanikiwa kwa dkt Slaa.Zaidi ya ubunge aliokwishakuupata hastahiki kupata cheo cha juu na hata kurudia huo ubunge.Ukifuatilia kampeni zinavyoendelea hali yake ni mbaya.Katika baadhi ya maeneo amekuwa akipata mahudhurio makubwa,ukweli unabaki kuwa wapiga kura walio wengi hawamjui kwa hivyo huenda huko kumuona tu.Kampeni za CCM na CUF zimetangulia, hivyo maamuzi ya wapiga kura nayo pia yametangulia kampeni.
Kibaya zaidi kwa Dkt.Slaa amekumbwa na kashfa nzito kipindi hiki cha kampeni.Amalize tu lakini hatoweza kujisafisha.
Chaguo linabaki kwa wagombea wawili,yaani Kikwete na Lipumba.Ili kuzuia hatari ya kushinda kwa dkt Slaa ambaye hana elimu wala sifa,nawashauri wapiga kura waangalie nani kati ya hawa wawili anafaa zaidi kupewa kura.
Asante kwa uchambuzi wako wa kina. Ama kweli kuna watu wamesoma, na ni vyema kusikiliza watu waliosoma na kuelimika na kuitumia elimu yao ktk kusaidi wananchi wote bureeeee.

Sasa msiposikia ya mkuu mtavunjika guu. Ushauri ni wa buree.

UCHAGUZI NI KATI YA KIKWETE NA LIPUMBA, YAANI 'K' na 'L'
 
Mkuu tofauti yetu na wewe ni kubwa sana, huwezi kuiona kwa mtizamo ulionao.
Ukitaka shule za Serikali zilingane na status ya Seminari wambie hao viongozi wako waache ufisadi na wawekeze kwenye elimu ya kweli na sio shule za kata. Sitaki kuongea mengi kwa kuwa unaujua ubovu wa system yenu na nakushangaa unapomshambulia mtu kwa dini yake. Wewe upo uislaam kwa matakwa yako au umejikuta upo huko baada ya kuzaliwa na wazazi waislaamu? Fikiri zaidi ya dini, ni ushauri wa bure tu. Ningependa nikufahamishe zaidi lakini kwa mtizamo wa machapisho yako haupo tayari kujifunza ya wengine, nafikiri sitokujibu tena manake kuendelea kufanya hivyo ni sawa na kupoteza muda wangu.

Kutokuweza kuendelea kujibu ni kuwa huna hoja na huna jipya.
Jibu swali:
Huo ujanja wa seminari kuwa bora mumeupata wapi?.Kwanini hutaki huo ubora uhamie serikalini na sisi waislamu pia tuwe nao?
Jibu ikiwa huna ni kuwa ujanja wenu mara zote ni katika kudhulumu na kujipendelea.
 
Mnaweza kubishana bureeee kumbe jamaa ni mdini tu,wala msihangaike?kikubwa tar 31.10.2010 pale ndo tutajua kama Dr. Slaa hana elimu kama dr. Kikwete
 
Udini ni msamiati tata ulioanzishwa wakati wa Nyerere.Iwapo maana yake ni kuonesha imani ya mhusika katika utendaji wa jambo,basi udini mbaya upo Chadema na ni ule alionao mgombea wake dkt.Slaa.Huyu jamaa alipokuwa akijifanya msemaji sana bungeni,hakuwahi kutetea jambo lenye maslahi na nchi lililoutaja uislamu.Kinyume chake alikuwa ni mpinzani mkubwa wa chochote chenye nembo ya uislamu.
Wagombea wanaogombea kupitia Chadema ambao ni waislamu hawapati ushirikiano mzuri na wanapopatwa na matatizo hawashughulikiwi kichama.
Nimefurahi kuwa katika mdahalo wa star TV kati yake na Kinana wa CCM,Slaa ameshindwa vibaya na kaboronga katika suala la kutoa matibabu bure kwa wananchi.
 
yaani we ndo mdebweeedo kwelikweli!
 
Watanzania wameshaamua kumpandisha cheo Dr. Slaa kutoka mbunge aliyetukuka na kuwa rais wa nchi. Msiompenda katafuteni kamba mjinyonge.

Kaazi kweli kweli. Ina maana Mkuu Jasusi Slaa akishindwa UTAJINYONGA. Siasa ni ushindani, mnashindana anayeshinda mnaungana kulisukuma mbele Taifa. Huu utofauti wakati wa kampeni usituvunjie Taifa letu.
 
TAIFA HALIVUNJIKI WALA HALITAVUNJIKA KWA KUWA SIASA HAZIKUANZA LEO.
Wanaofanya fujo ni wachache wasio na uelewa wa mambo fulani especially "TANZANIA NI MOJA NA RAIA WAKE NI NDUGU".

Mungu ameilinda Tanzania na anaendelea kuilinda.
Amani ya Tz haijawahi kutokana na siasa na wala haitatokana na siasa.
 
Hiyo ni sawa kabisa.
 
Udini ni msamiati tata ulioanzishwa wakati wa Nyerere.Iwapo maana yake ni kuonesha imani ya mhusika katika utendaji wa jambo,basi udini mbaya upo Chadema na ni ule alionao mgombea wake dkt.Slaa.Huyu jamaa alipokuwa akijifanya msemaji sana bungeni,hakuwahi kutetea jambo lenye maslahi na nchi lililoutaja uislamu.Kinyume chake alikuwa ni mpinzani mkubwa wa chochote chenye nembo ya uislamu.
Wagombea wanaogombea kupitia Chadema ambao ni waislamu hawapati ushirikiano mzuri na wanapopatwa na matatizo hawashughulikiwi kichama.
Nimefurahi kuwa katika mdahalo wa star TV kati yake na Kinana wa CCM,Slaa ameshindwa vibaya na kaboronga katika suala la kutoa matibabu bure kwa wananchi.
hahahahaaaa! kampikie Kinana chai bana! kisha ukamburudishe makamba ......usisahau kuvaa shanga
 
duu ndo walewaleee elimu yake duni na mawazo yake finyu upeo ndo empty tarehe 2 akiapishwa hama nchi asikuongoze dr.wa ukweli mkristo.
 
Tatizo ni nini kwa sisi watanzania?mbona watu wanashindwa kujua nini tunataka?haya bana wajinga ndio waliwao ujinga tutakaoufanya tarehe 31/10/2010 utatucost maisha,sitaki baadae nisikie hawa wajinga wakilia njaa na kusaga meno.itwabidi wasubiri miaka mitano ijayo.Mungu ibariki Tanzania
 
Mbali na kampeni za uchaguzi zinazoelekea ukingoni kutoa mielekeo ya nani anafaa zaidi kukabidhiwa uongozi wa nchi.Ufuatao ni uelewa wangu kuhusiana na wagombea watatu wa nafasi hizo.Hao ni Ibrahim Lipumba,Jakaya Kikwete na Wilbroad Slaa.
Mimi binafsi kwa nafasi hii namuamini zaidi Ibrahim Haruna Lipumba.Namuona ana elimu ya mambo ya kiuchumi ambalo ndilo tatizo sugu la watanzania.Ana uchangamfu wa kiuraisi na huzungumza kwa hekima.Wale wanaompinga si kutokana na kukosa sifa bali zaidi ni kutokana na chuki zao za kidini.
Pamoja na hivyo ikiwa umesalia muda mfupi kabla ya uchaguzi wenyewe,mpambano unaonekana upo zaidi kati ya Slaa na Kikwete.
Waislamu kwa kiwango kikubwa wanaonekana kumuunga mkono Kikwete,si kwamba wanamuona bora bali ili kumpinga Slaa ambaye wametoa takwimu nyingi kuonesha hisia zao dhidi yake.
Mbali na kuwa ana historia ya kupinga ajenda za waislamu bali anaonekana ni mtu muovu wa tabia hasa kutokana na kosa la kumnadi mke wa mtu kuwa ni mchumba wake.Wanahisi pindi akishika uraisi atakuwa ni mtu wa nuhsi moja baada ya nyengine.
Hisia hizo unaweza kuzipata wazi wazi kupitia redio kadhaa za kiislamu na magazeti yao hasa An-nuur na ALhuda.
Kutokana na kupigwa pande na kundi kubwa la wapiga kura na kampeni za kawaida za CCM, ni dhahiri kuwa dkt.Slaa hatoweza kupita katika uchaguzi huu hata.

tutajie jina la first lady tukimpa urais lipumba!!!!!
 
Avatar yako imeisha nipa jibu kwa nini umeandika hivyo. Ondoa udini wako hapa sisi ni watanzania wa kitanganyika na kizanzibar na uislamu ni wa kiarabu na ukristu ni wa kimagharibi sasa kwa nini tugombane kwa hili?
 
Mbali na kampeni za uchaguzi zinazoelekea ukingoni kutoa mielekeo ya nani anafaa zaidi kukabidhiwa uongozi wa nchi.Ufuatao ni uelewa wangu kuhusiana na wagombea watatu wa nafasi hizo.Hao ni Ibrahim Lipumba,Jakaya Kikwete na Wilbroad Slaa.
Mimi binafsi kwa nafasi hii namuamini zaidi Ibrahim Haruna Lipumba.Namuona ana elimu ya mambo ya kiuchumi ambalo ndilo tatizo sugu la watanzania.Ana uchangamfu wa kiuraisi na huzungumza kwa hekima.Wale wanaompinga si kutokana na kukosa sifa bali zaidi ni kutokana na chuki zao za kidini.
Pamoja na hivyo ikiwa umesalia muda mfupi kabla ya uchaguzi wenyewe,mpambano unaonekana upo zaidi kati ya Slaa na Kikwete.
Waislamu kwa kiwango kikubwa wanaonekana kumuunga mkono Kikwete,si kwamba wanamuona bora bali ili kumpinga Slaa ambaye wametoa takwimu nyingi kuonesha hisia zao dhidi yake.
Mbali na kuwa ana historia ya kupinga ajenda za waislamu bali anaonekana ni mtu muovu wa tabia hasa kutokana na kosa la kumnadi mke wa mtu kuwa ni mchumba wake.Wanahisi pindi akishika uraisi atakuwa ni mtu wa nuhsi moja baada ya nyengine.
Hisia hizo unaweza kuzipata wazi wazi kupitia redio kadhaa za kiislamu na magazeti yao hasa An-nuur na ALhuda.
Kutokana na kupigwa pande na kundi kubwa la wapiga kura na kampeni za kawaida za CCM, ni dhahiri kuwa dkt.Slaa hatoweza kupita katika uchaguzi huu hata.

lipumba alisha kuwa mshauri kwa serikali ya ccm, si tu kwamba hatukufanya vizuri kiuchumi, bado dhahabu yetu haikulindwa, msijitume kufikiri lipumba anaweza kuisaidia tz.
 
Usidanganyike na wingi wa watu kwenye mikutano.Unajua Dkt Slaa ana mtandao mkubwa wa mavuvuzela wanaompigia debe kama wewe hapo.Hivyo watu huamua kwenda kumuona tu si kwamba wanampenda.Mwishowe wengi huishia kama mimi baada ya kumsikia porojo zake za ufisadi kumbe fisadi ni yeye mwenyewe.
Lazima nikose usingizi.Najiuliza mtu kama huyu akiingia ikulu itakuwaje.Ni balaa tupu baada ya balaa!.

Tumekuelewa vizuri. Wewe unataka mtu yeyote wa dini yako na unamkataa yeyote asiye wa dini yako. Kwako wewe hakuna sifa ya uongozi zaidi ya hiyo. Huo ndio UDINI, na ni mbaya sana kwa nchi yetu.

Wewe ni mtu hatari.
 
Back
Top Bottom