Mantissa
JF-Expert Member
- Jul 24, 2010
- 876
- 166
Kufikia hatua ya kuteuliwa kugombea uraisi si kipimo cha ubora wa mgombea.Mara nyingi hatua hiyo hufikiwa kutokana na kubebwa na vyama tu, ambavyo navyo si kipimo cha akili za wananchi bali matakwa ya kimfumo unaotawala ulimwengu kwa sasa.
Mbali na kampeni za uchaguzi zinazoelekea ukingoni kutoa mielekeo ya nani anafaa zaidi kukabidhiwa uongozi wa nchi.Ufuatao ni uelewa wangu kuhusiana na wagombea watatu wa nafasi hizo.Hao ni Ibrahim Lipumba,Jakaya Kikwete na Wilbroad Slaa.
Mimi binafsi kwa nafasi hii namuamini zaidi Ibrahim Haruna Lipumba.Namuona ana elimu ya mambo ya kiuchumi ambalo ndilo tatizo sugu la watanzania.Ana uchangamfu wa kiuraisi na huzungumza kwa hekima.Wale wanaompinga si kutokana na kukosa sifa bali sababu nyengine ambazo ikibidi nitazitaja baadae.
Jakaya Mrisho Kikwete ni mkweli katika utekelezaji wa ahadi zake.Hata hivyo amezungukwa na wajanja wengi wa hapa ndani ya nchi na wale wa nje ambao mara nyingi huwa wanaingilia maslahi ya watanzania na hata kumzonga ili asitekeleze baadhi ya ahadi ambazo ziko ndani ya uwezo wake.
Wilbroad Slaa.Nitakayoyasema juu yake hapa, najuwa si pahala muafaka.Lakini ukweli wa moyoni mwangu unanifanya nisiwe na chaguo jengine isipokuwa nimueleze kama nimuonavyo.CHADEMA kwa makusudi au kwa bahati mbaya wametuletea chagua ambalo lisingepaswa kuwa hivyo kwa wakati huu.Hana sifa za kuwa raisi.Fani ya elimu yake hachaguliki kwa kundi kubwa la wapiga kura.Si muadilifu kwa nafsi yake na hawaheshimu watu wanaomzunguka.Ni mpayukaji.
Katika siasa kuna kudanganya huku kwa undani mtu anafanya vyengine kama alivyofanikiwa raisi wa mwanzo wa Tanzania;Julius Nyerere.Hilo ni gumu kufanikiwa kwa dkt Slaa.Zaidi ya ubunge aliokwishakuupata hastahiki kupata cheo cha juu na hata kurudia huo ubunge.
Chaguo linabaki kwa wagombea wawili,yaani Kikwete na Lipumba.Ili kuzuia hatari ya kushinda kwa dkt Slaa ambaye hana elimu wala sifa,nawashauri wapiga kura waangalie nani kati ya hawa wawili anafaa zaidi kupewa kura.
Wewekama rais ukipangiwa mambo ya kufanya na walio nje ya nchi yako, wewe ni *****. ushawishi unaotoa ni pumba tupu, njoo kwa mara nyingine.