Nitapataje nembo ya tbs?

Mapujds

JF-Expert Member
May 12, 2011
1,286
127
Ndugu wana jf namba mtu yeyote mwenye ufahamu ni hatua gani au ninawezaje kupata nembo ya tbs kutoka shirika la viwango.nataka kuwa mjasilia mali wa kutengeneza bidhaa za mafuta ya kupikia yatokanayo na mbegu kama alizeti,karanga na nyonyo.nimehangaika sana na advance diploma yangu ya computer naona hainisaidii kupata ajira.naomba mnijuze tafadhali.
 
masharti na vigezo kuzingatiwa je utatumiaje nembo ya watu bila makubaliano.je elimu uliyosoma imekusaidia nini?kama vitu hivi hujui unajua ni dharau sana kuuliza swali kama hili then unasema una ADVANCE DIPLOMA KWELIKWELI!!!!!!!!!!!
 
Mkuu fika ofisini kwao utapewa fomu za kujaza, na kupewa gharama, kisha baada ya kulipia gharama ambazo ni za ukaguzi na testing, wakaguzi watakuja kwenye site yako na baada ya kulidhika utapewa namba na nembo. Nafikiri umeelewa
 
masharti na vigezo kuzingatiwa je utatumiaje nembo ya watu bila makubaliano.je elimu uliyosoma imekusaidia nini?kama vitu hivi hujui unajua ni dharau sana kuuliza swali kama hili then unasema una ADVANCE DIPLOMA KWELIKWELI!!!!!!!!!!!

read between the lines,hujamuelewa mdau unataka tu kujidai wewe ni fundi wa maneno...
 
Unahitaji nembo ya TBS ya nini,wewe uza bidhaa zako vuzuri tu maana hizo zenye nembo ya TBS ndo zimechakachuliwa na zisizo na nembo ya TBS ndo za ukweli,vipi hujui kama Tanzania siku hizi tunakwenda kinyumenyume
 
read between the lines,hujamuelewa mdau unataka tu kujidai wewe ni fundi wa maneno...
Unajua mijitu mingine kazi yao ni kukurupuka tu kama imefumaniwa haijui ustaarabu ili mradi ijionyeshe kuwa nayo inajua kila kitu kumbe badala ya kuelewa mwenzake anataka nini kazi yake ni kulewa ujuvi mwingi.
 
KUNA wataalamu wanasaidia watu kama wewe. kwa makubaliano anakuchongea hiyo nembo ili ujigongee mwenyewe maana hao TBS wakileta nembo yao watakudai pesa nyingi zaidi ya gharama za kuandaa bidhaa yako
 
KUNA wataalamu wanasaidia watu kama wewe. kwa makubaliano anakuchongea hiyo nembo ili ujigongee mwenyewe maana hao TBS wakileta nembo yao watakudai pesa nyingi zaidi ya gharama za kuandaa bidhaa yako

Siku akikamatwa Mkuu sijui utasemaje?

Mpe Ushauri mzuri mwenzio siyo huu wa kuchakachua na mwisho wa siku ni kukamatwa na kutozwa faini kubwa au pengine kifungo. Ndugu mleta mada usijaribu hii kitu ni hatari!
 
Back
Top Bottom